CHADEMA yawapa raha watanzania: Taifa Lazizima

Safi sana Chadema Mungu mkubwa,aibu yao CCM inayogandamiza haki na utu wa mwanadamu! Mungu mkubwa,Viva Chadema.
 
Pamoja na wabunge wote wa CHADEMA na wananchi walalahoi wa Tanzania walioamua bila kujali vitisho kuungana na wabunge wazalendo toka CHADEMA, naomba kwa namna ya peke kabisa kuwashukuru wananchi wa Singida Mashariki kwa kutuletea Lissu bungeni. Kwa mara ya kwanza watanzania tumeona kwa vitendo nini maana ya kusimamia hoja. Hata CCM waliotumia bunge lililopita kumtukana Lissu "personally wamekubali kuwa Lissu ana uwezo mkubwa wa kuchambua sheria. Anasoma neno kwa neno, anatoa tafsiri pana na madhara/faida zake. Hii ndio kazi ya mbunge kama mwakilishi wa wananchi katika chombo cha kutunga sheria.

Wale waliokimbilia kwenye vyombo vya habari wakisema kuwa Lissu alikuwa anajidai anajua sheria na kwamba eti wao wanao watu waliobobea kwenye sheria wanasemaje?

Tuombe uzima na ulinzi wa mwenyezi mungu maana bunge la bajeti mwezi June/July laweza kuwa kivutio tosha!
Lissu mungu akulinde.
 
Kwa kuongezea tu, baba Riz1 itapendeza sana kama walau mara moja kwa mwezi mkakutana na watu wenye mawazo ya kujenga ambao hawaogopi kukuambia ukweli pale unapokosea ili kujenga taifa lao kuliko kuwasikiliza hao wanaokulisha pumba na kasa kila uchao, ili wajaze matumbo yao kama Anna M. Ondoa washauri wasiojielewa kama MKPP, mawaziri wasio na msaada kama WN, Mp, Maig n.k. Watanzania milioni 40 ni mtaji tosha kwako achana na ushauri wa wachumia tumbo.
Nachukizwa sana na uandishi wa aina hii katika sehemu nilizokuwekea RED, kumbuka hapa hatupo katika kitendawili tega.
 
Safi sana, ila tusimsahau marehemu REGIA MTEMA ALIYETOA WAZO LA KWENDA IKULU, bravo chadema umenikumbusha nikalipe hela ya uanachama...maana hapo ndio naona hela yangu ikitumika vizuri...

Kitu kimoja tu ambacho JK atakumbukwa nacho ni katiba basiiiiiii, ila kama atasimamia vizuri na kuondoa uchama huku akiweka maslahi ya taifa.

Kwa hili hongera JK. Naanza kuona TZ mpya yenye mafanikio kwa mbali sana...
 
Watanzania wenzangu! mimi nimsomaji tu humu na sijawahi kuchangia sana ila naomba na mimi kwa hili niingie kwenye historia ya wawakilishi wachache wataopata fursa ya kupongeza viongozi wetu makini waliofanikisha marekebisho haya kupita kwa ajili tu ya masilahi ya Watanzania..

Kwanza kabisa napenda kwa dhati kumshukuru na kumpongeza RAIS wetu J M Kikwete kwa ujasiri na pengine moyo wa usaliti aliouonyesha kwa chama chake na kuweka maslahi na uzalendo mbele kuridhia mawazo na mapendekezo yaliyowasilishwa kweke na CHADEMA. Ni ukomavu wa hali ya juu sana katika ulimwengu wa waliostaarabika.

Ni dhahiri siasa za dunia ya tatu ni tete mbovu hasa kwenye masuala ya msingi kitaifa kama hili. Ni historia Rais na utaishi na raha hiyo milelePili Nachukua fursa hii kuwapongeza CHADEMA NA WANA CHADEMA kwa kazi nzuri inayofanywa kuinua taifa letu changa linaloelekea kupotoshwa na kuyumbishwa na walafi wachache!

Ni hatua ya hali ya juu iliyotukuka inayokifanya CHADEMA kuimarika kila kukicha pale inapokumbatia Utaifa na uzalendo wa kweli kwa kila wazo au jambo linalofanywa. Nawapongeza sana na ninawahakikishia historia itachukua mkondo wake pale muda utakapotimia.MUNGU IBARIKI TANZANIA.[

YOTE YAWEZEKANA UKITAKULIZA TAFAKARI KABLA YA KUTENDA,WALIOZOMEA SASA WAMETAMBUA FAIDA YA KUELEWA JAMBO KABLA YA KULICHANGIA.UKIWA KIONGOZI FANYA KAZI ULOTUMWA NA UNAOWAONGOZA NDO MSINGI WA WALIOKUCHAGUA.
VIVA CHADEMA,WAJF NA WATANZANIA KWA UVUMILIVU WAO.
 
daaah maneno safi kweli haya..hebu tukutane mtekenyo pub nkupe bia mbili mdogo wangu...
 
Wenye akili za kuona karibu wanaweza kukubaliana na mawazo finyu kama ya kwako yenye ushabiki tu
na siyo analysis.
Watanzania wanajua sana kwamba, analysis kama hizo ni za kivuvuzela tu na lengo lake ni ili baadaye wapite mitaani kwamba wao ndiyo chimbuko la kisiasa. Nashukuru kwamba umetambua mawazo ya watu walichangia kupita kwa muswada wa katiba kuwa ni Pamoja na ROJEPH WARYOBA, SALIM AHAMED SALIMU ila ukaharibu kwa kuchomekea mavuvuzela eti kisa walitoka nje ya ukumbi wa bunge, kuzunguka nchini kuwashawishi wananchi wasijihusishe na shughuli za maendeleo huku ukidanganya kwa walikuwa wanatoa elimu ya uraia. Ndugu hukumbuki kilichotokea katika jimbo la Engineer STELAA MANYANYA? huko kulikuwa ni kutoa elimu ya uraia kuhusu katiba mpya?

Wasomi wote na watanzania wenye mapenzi mema na nchi yao hawatawasahau akina Prof. ISSA SHIVJI, MWAITAMA, JENERALI ULIMWENGU na wengine wengi. Nakumbuka siku moja katika kongamano la katiba mpya pale UDSM, Tindu Lissu aliumbuliwa na Prof. Shivji kwa jinsi alivyokuwa akichangia kisiasa siasa tu leo nae unamtaka kwenye list yako ya mavuvuzela. Nakumbuka ambavyo wasomi walisimama kidete kuhakikisha Wanasiasa wasiteke mjadala wa Katiba mpya, leo unanitajia mzee wa Bilkana kama mwasisi na Baba Josephine Mshumbuzi. Kweli watanzania tumelala. Umeshindwa angalau kumtaka Mabere Marando? Pole.

Total crap
 
naomba nimpongeze JK, kwa kuwa ndo mtu pekee kukubali mabadiliko wengine woote siwapongezi sababu bado tunakazi ngumu na tupo upande mmoja!
 
Wenye akili za kuona karibu wanaweza kukubaliana na mawazo finyu kama ya kwako yenye ushabiki tu na siyo analysis.
Watanzania wanajua sana kwamba, analysis kama hizo ni za kivuvuzela tu na lengo lake ni ili baadaye wapite mitaani kwamba wao ndiyo chimbuko la kisiasa. Nashukuru kwamba umetambua mawazo ya watu walichangia kupita kwa muswada wa katiba kuwa ni Pamoja na ROJEPH WARYOBA, SALIM AHAMED SALIMU ila ukaharibu kwa kuchomekea mavuvuzela eti kisa walitoka nje ya ukumbi wa bunge, kuzunguka nchini kuwashawishi wananchi wasijihusishe na shughuli za maendeleo huku ukidanganya kwa walikuwa wanatoa elimu ya uraia. Ndugu hukumbuki kilichotokea katika jimbo la Engineer STELAA MANYANYA? huko kulikuwa ni kutoa elimu ya uraia kuhusu katiba mpya?

Wasomi wote na watanzania wenye mapenzi mema na nchi yao hawatawasahau akina Prof. ISSA SHIVJI, MWAITAMA, JENERALI ULIMWENGU na wengine wengi. Nakumbuka siku moja katika kongamano la katiba mpya pale UDSM, Tindu Lissu aliumbuliwa na Prof. Shivji kwa jinsi alivyokuwa akichangia kisiasa siasa tu leo nae unamtaka kwenye list yako ya mavuvuzela. Nakumbuka ambavyo wasomi walisimama kidete kuhakikisha Wanasiasa wasiteke mjadala wa Katiba mpya, leo unanitajia mzee wa Bilkana kama mwasisi na Baba Josephine Mshumbuzi. Kweli watanzania tumelala. Umeshindwa angalau kumtaka Mabere Marando? Pole.
kinachokusumbua wewe si ushabiki tu, bali ni kukosa umakini hasa unapokuwa kwenye siku zako
 
PINDI USIKIAPO 'MTU KUSIMAMIA KILE ANACHOKIAMINI NA KUTHAMINI' SANAA MOYONI HAKIKA MAANA YAKE HALISI NI MAAGANO KATI YA MOYO WAKE NA AKILI JUU YA KITU 'KIFO'

Wakuu,

Hata siku moja usiombe kukutana uso kwa uso na
MTU ANAYESIMAMIA KILE ANACHOKIAMINI NA KUTHAMINI SANA MOYONI maana kwake yeye mtu kama huyu ni kama vile akilini mwake keshaagana na roho yake kwamba HATA IWEJE, liwalo na liwe.

Hongereni sana Prof Baregu katika haya yote, Dr Slaa, Dr Kitila Mkumbo, Wana-Chama wetu CDM Zanzibar kwa jinsi mnavotutia moyo katika vipindi vigumu kama hivi, hongereni BAVICHA, BAWACHA na CHADEMA Pupies mlioko katika vyuo na vyuo vikuu mbalimbali nchini.

Nasema bila ya walalahoi wamachinga wanaodharaulika nchi hii, waalimu waliosahaulika kwa kila kitu, wakulima waliokopwa mazao ya kwa zaidi ya karne nne bila malipo yoyote, bil ya uungwaji mkono wa viongozi wetu wa dini zote nchini pamoja na kazi mzito ya Jumuia za Kimataifa nyuma ya pazia, je sisi CHADEMA tu ni nani katika nchi hii hata tukayafikia mafanikio yote haya bila ya ushirikiano wenu wa karibu pamoja na sala??

Hadi hapo ndipo sasa haja ya kuwatwangeni salama zangu za kizalendo za 'UTAIFA MBEEEEEELE KAMA TAI' katika masuala yote ya kitaifa na kwa manufaa na maslahi ya Umma wa Tanzania.

Mheshimiwa Kikwete, ukiendeleza kiwango hichi cha uzalendo na kuweka Itikadi za U-CCM pembeni kidogo basi nakuhakikishia kwamba utaweza kuachia taifa hili kumbukumbu ya karne kuliko hata ile ya Mzee Mkapa na Uwanja wa Michezo wa Taifa - nayo itakua ni KATIBA MPYA ILIOUNDWA NA WANANCHI WENYEWE TUKIWA TUMESHIKA USUKANI.

Hakika hilo likitendeka ipasavyo basi huenda tusilazimike huko mbele ya safari KUPIGA CHINI KATIBA kwenye kura ya maoni ya taifa / referendum itakapoitishwa mwisho wa siku juu ya hilo.

Pamoja na wabunge wote wa CHADEMA na wananchi walalahoi wa Tanzania walioamua bila kujali vitisho kuungana na wabunge wazalendo toka CHADEMA, naomba kwa namna ya peke kabisa kuwashukuru wananchi wa Singida Mashariki kwa kutuletea Lissu bungeni.

Kwa mara ya kwanza watanzania tumeona kwa vitendo nini maana ya kusimamia hoja. Hata CCM waliotumia bunge lililopita kumtukana Lissu "personally wamekubali kuwa Lissu ana uwezo mkubwa wa kuchambua sheria.

Anasoma neno kwa neno, anatoa tafsiri pana na madhara/faida zake. Hii ndio kazi ya mbunge kama mwakilishi wa wananchi katika chombo cha kutunga sheria.

Wale waliokimbilia kwenye vyombo vya habari wakisema kuwa Lissu alikuwa anajidai anajua sheria na kwamba eti wao wanao watu waliobobea kwenye sheria wanasemaje?

Tuombe uzima na ulinzi wa mwenyezi mungu maana bunge la bajeti mwezi June/July laweza kuwa kivutio tosha!
Lissu mungu akulinde.
 
Hakika wanastahili pongezi sana,na huu ndo uzalendo wa kweli wameuonyesha,big up viva chadema na timu yoote ya wanamapambano,pia jf ni darasa tosha kwa watu wote,mwanga tunaoupata humu jamvini hakika hata chembe ya magazeti hakuna.ila wananchi wengi wamesikitishwa sana na hoja ya mh zitto kutokuungwa mkono
 
Wakuu zangu,

Kwanza kabisa ningependa kutoa shukran kwa uongozi wa Chadema na watu wote walioshiriki ktk mchakato wa katiba mpya. Nachopenda kufahamu ni kwamba muswada uliopita unakubalika na wananchi?.. Je, marekebisho yaliyofanywa yamefanywa kwa kuzingatia hoja za wananchi na kwa kiasi gani tunakubaliana na sheria itakayopitishwa.
 
naomba nimpongeze JK, kwa kuwa ndo mtu pekee kukubali mabadiliko wengine woote siwapongezi sababu bado tunakazi ngumu na tupo upande mmoja!

lakini angeheshimika zaidi endapo angesoma mswada na bila kusaini arudishe ujadiliwe upya maana kusaini kitu ni kukikubali anaonekana hana msimamo anataka kuridhisha wote ccm kwa kusaini cdm kwa kurudisha sheria ifanyiwe marekebisho.
 
Huyu jamaan ni noma kweli.
Alisema watanzania mta mkumbuka,...atleast kafanya moja zuri la
kukumbukwa.
 
Back
Top Bottom