CHADEMA yawapa raha watanzania: Taifa Lazizima

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
WanaJF,
Tutakuwa hatutendi haki kama hatutasimama kama Watanzania kutoa pongezi za dhati kabisa kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) kwa kusimamia kidete suala la Katiba mpya mpaka sasa marekebisho ya sheria ya Katiba mpya yakapitishwa na bunge leo.Ni wazi watu mbalimbali akiwemo Rais Kikwete wamechangia hili lakini bila kumung'unya maneno niseme kama si CHADEMA kusingekuwa na hoja hii ya Katiba mpya leo.

Kwanini?
  • CHADEMA iliweka suala la Katiba mpya kwenye ilani yake ya Uchaguzi mwaka 2010
  • Wabunge wa CHADEMA walitoka nje ya bunge siku Rais alipolifungua bunge pamoja na mambo mengine kudai katiba mpya itakayotoa fursa ya kuwa na tume huru ya uchaguzi
  • Mwaka mzima wa 2011 CHADEMA iliongoza maandamano nchi nzima kutoa elimu ya uraia na kutaka kuungwa mkono na UMMA juu ya kupata katiba mpya
  • Wabunge wa CHADEMA walitoka nje ya bunge mwezi Novemba 2011 kupinga mswada wa Katiba mpya uliokuwa na Mapungufu mengi na ya kimsingi
  • Kamati kuu ya CHADEMA ilinyoosha Mkono wa mapatano na serikali kwa kukutana na Rais Kikwete kupinga mswada uliokuwa mbovu uliopitishwa kiushabiki na wabubge wa CCM na CUF
  • Rais aliridhia mapendeklezo yote ya CHADEMA na kuamuru mabadiliko ya sheria iliyokuwa imepitishwa kishabiki na wabubge wa CCM na CUF
  • Hatimaye marekebisho ya sheria yakapitishwa na bunge na kufungua rasmi mlango wa kutengeneza katiba mpya ya Tanzania.
Ni wazi kwa yote yaliyotajwa hapo juu yanatufanya tuamini CHADEMA imesimama imara katika kupigania Katiba ya nchi.Watanzania wengi walikata tamaa na kudhani baada ya mswada mbovu kupitishwa mwaka jana CHADEMA ingesusia moja kwa moja zoezi zima.Lakini CHADEMA imejenga taswira tofauti kwa Watanzania kwa kupigana kwa hali yoyote kuhakikisha Katiba mpya inapatikana.

Wafuatao wanastahili heshima ya pekee:

Pamoja na CHADEMA kama taasisi kuonekana kukomaa na kusimamia agenda zake,ni lazima tuwatambue baadhi ya watu walioongoza mpambano huu kwa Amani na utulivu na siku moja wataingia katika vitabu vya historia


  • Dr Wilbroad P. Slaa-Ni kiongozi makini,madhubuti na anayeweza kuyasimamia maneno yake kwa kuinadi ilani ya CHADEMA nchi nzima wakati wa kugombea urais mwaka 2010 na watu wakaamini na kuona umuhimu wa Katiba mpya.Lakini Pia ni Katibu mkuu ambaye ni mtendaji mkuu wa chama anayeongoza sekretariati ya chama inayopanga agenda za chama na kusimamia mikakati yote ya chama,suala la Katiba mpya likiwa mojawapo ya mkakati.
  • Freeman A.Mbowe-Huyu ni kiongozi wa upinzani bungeni na muda wote ameiongoza vema kambi ya upinzani bungeni kusimamia agenda hii ya katiba mpya.Hakutetereka na amekuwa akisimamia uwajibikaji wa pamoja wa kambi yake bungeni.Kwa jinsi leo alivyohitimisha mswada huu wa katiba mpya hawezi kusahaulika kirahisi.Amewafanya watanzania sasa kutambua ni nini maana ya kambi ya upinzani bungeni.
  • Zitto Z.Kabwe-Huyu ni Naibu kiongozi wa upinzani bungeni na siku zote amekuwa msaidizi muhimu na wa kuaminiwa wa kiongozi wa upinzani bungeni.Ni wazi amesaidia sana kuifanya kambi ya upinzani kuwa kama jinsi ilivyo na anastahili kufurahia matunda ya kupigania katiba mpya ndani ya bunge.
  • Tundu A.Lissu-Ni mnadhimu mkuu wa upinzani bungeni.Huyu ukitaja jina lake kwa sasa hata mtoto mdogo anamjua.Hili ni jembe kweli kweli.Alipinga kwa nguvu zote mswada mbovu wa mwaka jana.Kutokana na upinzani wake kwa mswada wabunge wa CCM na CUF walimshambulia kwa kila neno baya ili kumchafua mbele ya jamii.Lakini alisimama kidete kupambana ndani na nje ya bunge mpaka leo hii walau watanzania wanafurahia mabadiliko ya sheria ile.
  • Wabunge wote wa CHADEMA-Hawa kwa ujumla wao wamesimama kidete kwa umoja ndani na nje ya bunge kuhakikisha katiba mpya inapatikana.Kila walichokifanya kuhusu katiba ni msimamo wa chama chao.Wote walinena lugha moja.Hakika huu ni mfano wa kuigwa kwa vyama vingie pale kunapokuwa na jambo la msingi la kuwatetea watanzania.Iliwashangaza wengi pale hata mbunge wa Maswa John Shibuda alipoungana na wenzake mwaka jana kutoka nje ya bunge kususia mswada mbovu uliowasilishwa.

  • Rais Jakaya Kikwete-Kwa heshima ya Pekee anastahili pongezi za dhati kabisa kwa uamuzi wake wa kukubali mwito wa kukaa na CHADEMA.Ni wazi Rais alikubali kuweka pembeni itikadi ya chama chake na kuamua kuwasikiliza CHADEMA na hatimaye kuyakubali madai yao yote.Ilihitaji moyo mkuu kufanya hivi.Aliipuuza kelele za wana CCM wenzake waliokuwa hawataki akubaliane na CHADEMA.Aliwapuuza na kuwadharau wabunge wa chama chake waliotishia kupiga kura ya kutokuwa na Imani na Rais kisa eti amekubali mapendekezo ya CHADEMA ili kupata katiba bora kwa Taifa letu.Wana CCM wengine wakadiriki kusema Rais anafanya haya kwa vile anamaliza muda wake wa urais kwa hiyo anajiandalia mwisho mwema,lakini hata hawa pia Rais aliwapuuza kwa maslahi ya Katiba bora.Kwa hili hakika Jakaya Kikwete amejiandikia historia ambayo haitafutika kirahisi.
Kwa ufupi kabisa niseme waliyoyafanya CHADEMA yameingia kwenye historia mpya.Yatasimuliwa vizazi na vizazivijavyo na ni mfano kwa wanasiasa na vyama vingine vyote.Hakika wameonyesha ukomavu wa hali ya juu.Na labda niseme lakini msiniite mtabiri! Kwamba ikipatikana Katiba mpya ya watu,ambayo itatoa tume huru kabisa ya uchaguzi itakayotenda haki kwa vyama vyote mwaka 2015,basi watanzania msishangae kumuona Michael Satta wa Tanzania akimrithi Jakaya Kikwete.Na tusubiri tuone.

Mungu awatangulie watanzania katika kupata katiba bora mpya ya Tanzania.Alilolipanga Mungu mwanadamu kamwe hawezi kulipangua.

WanaJF,Nawasilisha kwenu!
 
Excellent analysis.Huu ndio ukweli mtupu.Mungu azidi kuwaongoza CDM.Hakika umenifurahisha na Heading yako-CDM yatupa raha watanzania
 
bila kumsahau Shibuda pamoja na umbumbu wake ambao wabunge wa CDM wameamua kupampatiliza lakini akaongeza kiasi cha Ruzuku inayoliamsha Taifa Tanzania
 
watu mliopo field ya computer typing tabu tupu kila muda mnaandika hata yasiyoeleweka
 
CCM wataendelea kutia akili na wataamkakaribia 2015 na hapo watakuwa too late .Chadema onyesheni Utanzania na kwa ninimnaitwa Chadema na mie ninawafagilia sananyie watu .
 
Na juu ya yote, watanzania wanastahili pongezi sana kwa kuonyesha moyo wa imani kwa chadema.

Tangu suala la shgeria ya katiba mpya lilipoanza, na hasa pale wabunge wa chadema walipotoka nje kupinga muswada ule, wananchi wa kada mbali mbali na kutoka kila kona ya nchi walionekana kuwaunga mkono, na hatimaye sasa angalau yale mapungufu mengi ya msingi katika sheria ile yameweza kurekebishwa kwa maslahi ya watanzania wote ili hatimaye tupate katiba ya watanzania wenyewe.

Bila shaka chadema itaendelea kusimamia na kuongoza utoaji wa elimu kwa wananchi ili waweze kushiriki vizuri na kikamilifu katika kutoa maoni yao juu ya katiba mpya.

Viva Chadema, Viva Watanzania.
 
Pongezi zangu zawaendea WAZEE WETU WA HESHIMA SANA ndani ya nchi Wazee Joseph Sinde Warioba na Salim Ahmed Salim kwa kufanikisha hili.

Aidha pongezi za pekee ziwaendee vijana kote nchini pamoja na JF kwa kusimama kidete muda wote katika hili. Hata hivo vijana tusilale bado mapambano.

Kwa mara ya kwanza nawapongeza pia Rais Kikwete, Dr Kashillila, Kichaa wetu Ndugai pamoja na wabunge wa CCM kwa kuonyesha uzalendo katika hili na kubwa zaidi ni kule kutambua kwamba yote juu ya yote, TAIFA KWANZA!!!!!!!
 
fmpiganaji,

Bravo. Huo ni ukweli na ukweli mtupu. CHADEMA wanastahili pongezi za dhati kabisa. Frankly speaking CHADEMA ndiyo kioo cha Uongozi katika Taifa hili mabalo kwa sasa limepoteza mwelekeo kutokana na uongozi MBOVU wa Chama cha Magamba.
Kwa heshima na Taadhima napenda nami kuwapa pongezi nyingi Viongozi waandamizi wa CDM,Wabunge,Wanachama na Wapenzi wa CDM.

Sitakuwa nimetenda haki pasipo kumtaja Marehemu, dada yetu mpenzi Bi Regia Mtema(RIP) kwa mchango na mawazo yake kwenye mchakato huu kabla hajatutoka mapema mwezi uliopita.
 
Hongera mleta Mada,ni analysis nzuri yenye sura ya uhalisia wa mchakato mzima hadi leo,kweli ulikuwa ni mpambano mkali sana na hata wabunge mashabiki wa CCM NA CUF mara nyingi huwa wanashabikia vitu tu.
cha msingi tuungane pamoja kueneza elimu ya uraia na watu wenye mapenzi mema tushirikiane kukijenga chama kwa moyo mmoja na tuwe kitu kimoja hadi tujikomboe
 
Pomoja na CDM; pia natambua uwepo wa:-

MOSI: (Narudia) Natambua uwepo wa Mkuu wa kaya kuungana na sisi wanyonge; akaamua kuiweka CCM yake kando na kuuva uzalendo wa Tanzania na kusema YATOSHA wana CCM wenzangu, Ya kaisali basi mpeni kaisali ...Hongera Mkuu wa kaya kwa usikivu wako: kwa kitendo hili cha kizalendo kwa niamba ya CDM POKEA TANO:

PILI: Hata JF inabidi tujipongeze wenyewe , kuna watu wamechangia hoja nzito sana humu kuhusu katiba, na hilo lilisaidia kufungua maskio kwa baadhi ya wabunge na wana CCM ambao walifikiri bado tunaandika katiba ya CCM kumbe sisi tunaandika katiba ya Tanzania ambayo inahitaji makundi yote kushirikiswa asilimia mia. hongera wana JF -- Makofi kwenu Tafadhali.. kwa kitendo hiki na nyie POKEENI TANO:

TATU: Wapenzi na wanachama wa CDM; tupo pamoja kuimalizia hii project yetu ili 2015 tuikabidhi nchi hii kwa wenyewe ambao ndiyo sisi walala hoi, kwa uvumilivu wenu wa ajabu tangu kupokea matokeo ya uchaguzi mpaka sasa na nyie kwa kitendo hiki POKEENI TANO:

NNE: na mwsho inakuja kwako wewe mleta hoja, kweli ulijipanga vilivyo -- kwa kitendo hiki na wewe POKEA TANO:
 
Hongera sana ziwaendee Watanzania wote wanao endelea kuiamini sana Chadema na Viongozi wake bila kuwasahau wanachama wake kwa kufanya hivyo wamewatia moyo na nguvu kubwa viongozi ili kuonesha wazi kuwa wanacho kifanya ni sahihi kabisa
 
Haujamtendea haki Baba Mwanaasha kwa ushirikiano aliouonyesha wa kufumba macho na masikio na kukubali kuonekana kigeugeu kwa kukubali kufanyia marekebisho kitu ambacho ametoka kukubalina nacho mia kwa mia masaa machache tu yaliyopita.

Kweli mkuu maana jamaa wanataka kumtenga lakini aliona taifa mbele !
 
85 Reactions
Reply
Back
Top Bottom