Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 575
- 2,559
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeshuku mauaji yaliyofanywa na Jeshi la Polisi dhidi ya majambazi wilayani Serengeti, Mkoa wa Mara, kikitoa hoja nne kuthibitisha mashaka yake.
Mashaka hayo yanaibuka ikiwa ni karibu wiki moja tangu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mara, Longinus Tibishuana aliporipoti kuwauwa watu watatu waliodaiwa kuwa majambazi na mmoja kutokomea kusikojulikana.
Leo Jumanne Septemba 27, 2022, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bara, Benson Kigaila akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya Chadema, Kinondoni jijini Dar es Salaam amesema, idadi ya watu wanaodaiwa kukamatwa katika oparesheni ya Polisi iliyohusisha mauaji hayo ni zaidi ya wanne.
"Tumefanya uchunguzi wetu kwa kuwahoji wanakijiji na uongozi wa Kijiji na tumepata taarifa kwamba waliokamatwa hawakuwa wanne kama inavyosema Polisi ni zaidi ya hao," amesema.
Amefafanua watu wengine waliachiwa baada ya kulipa fedha kati ya Sh1 milioni hadi Sh2.5 milioni walizotozwa na jeshi hilo baada ya kuwekwa kuzuizini.
Hata hivyo, amesema inatia shaka mtuhumiwa wa ujambazi wa kutumia silaha kuachwa bila kufungwa pingu.
"Wanasema waliwajeruhi baada ya kutaka kukimbia walipofika porini kuonyesha walipokuwa majambazi wenzao na silaha, ina maana hawakuwa na Pingu," amehoji.
Hata mauaji, Kigaila amesema Mwenyekiti wa Kijiji (David Mugendi) ameeleza yamefanyika saa 9 alfajiri eneo lilipo rambo la kunyweshea mifugo, sio porini kama inavyoelezwa na Polisi.
Kutokana na mashaka hayo, Kigaila ametaka Rais Samia Suluhu Hassan kumfuta kazi Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Camilius Wambura, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Ramadhan Kingai na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Massauni.
Wengine aliotaka wafutwe kazi ni uongozi wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Mara, ili kuimarisha utendaji wa Jeshi hilo.
Pia, amemtaka Rais Samia kuunda tume ya majaji kufanya uchunguzi wa tukio hilo, akisema wanakijiji wapo tayari kutoa ushahidi.
Chanzo: Mwananchi