CHADEMA yashinda uchaguzi Mbeya Vijijini

walio sema CDM ni chama cha watu wa Kaskazini waseme sasa je huku ni kaskazini

Lakini hii propaganda imesha kufa tunasubiri nyingine

HONGERA SANA CHADEMA wakuu kumbukeni kuwa huku ni kwa Shitambala

Mkuu hizo zilikuwa ni kauli za wafa maji.
 
Hilo tumesha limaliza la siasa za kaskazini. MTAJI wa chama cha majambazi (CCM) ulikua vijijini ebu angalia uchaguzi wa 2010 miji mikubwa yote na majimbo muhimu vitovu vya majiji yote 4 Mwanza, Mbeya Dar na Arusha yaliwekwa mikononi mwa CDM hii inatia raha sana kuona tumeanza kuvamia Vijijini ambako propaganda zilikua zikifanya kazi mapambano yanaendeleaaaaaaaa!!!! Tuendelee kutoa elimu kwa watanzania
 
Mkuu hizo zilikuwa ni kauli za wafa maji.
ngoja waendelee kufa taratibu kufikia 2015 watakuwawameshakufa kabisaaa. Mbeya hakuna mchezo chama kimejipanga sawasawa kuanzia ngazi ya kata kina viongozi wa idara zote sasa tunaelekea ngazi ya shina lengo ni kuwa na "mabalozi au wajumbe wa kila nyuma 10"

Wanao tuangusha ni DAR tu sijui wakoje
 
Mkuu unayemwambia ni mpambanaji mwenzako.

Dah anisamehe mkuu,nilijua ni gamba,kumbe mkuu LAT kaiweka hii ktk mfumo wa joke!nisamehe mkuu Lat,nilijua ni gamba maana mtu wa gamba angemaanisha hiyo kwa jinsi uerevu wao ulivyo duni
 
Hongereni sana wananchi wa mbeya vijijini naomba na vijiji vingine viige mfano huo hata sisi tunaokaa dar sasa tubadilike tuchague wachapa kazi hasa 2015 wabunge wote dar watoke cdm
 
Ni ushindi mkubwa sana huu kwa magwanda na wanahitaji kila pongezi, Mwenyekiti wa kijiji ni mtu muhimu sana. Hongera CHADEMA.

Ngoja tuone Arumeru, mtaweza?
Yale magari manne ya maji ya ***** na hao policcm mliowatoa Dodoma, Singida, Dar n.k, hawatoshi. Ombeni na msaada wa jeshi la Rwanda, Burundi, na lile la .... muongeze na vifaru vya WW II, bado mtabwagwa tu. Magamba!!!!
 
shida bado iko kyela na rungwe tu.....which is surprising kwani kila mtu angetegemea ndiko kuwe chimbuko la mabadiliko!

Mkuu siasa za Kyela na Rungwe zinajulikana.Kuna majabali Mwandosya na Mwakyembe.Watu wanawapenda hao wawili na hawaipendi CCM.Siku watakapoondoka hao wawili ndio kifo cha CCM huko.
 
Mbeya ni turning point ya political revolution kwa sasa hapa TZ. Mungu awe nanyi daima.
 
Mkiambiwa wafuasi wa magamba ni malumpen mnaona mmetukanwa,wakati wenzenu wanakwenda shule nyie mlikua wapi?nani kakuambia Ndola ipo Malawi?rudi darasani mkuu!hata kufuta ujinga kidogo itatosha

Inawezekana wewe hujaelewa kabisa, LAT amefanya kuchombeza tu, ila namini wewe unadhani inaongelewa Ndola ya Zambia.
Mbeya kuna vijiji viwili vinaitwa Ndola, kimoja Mbeya vijijini na kingine kipo Tukuyu maeneo ya Katusyo ukiwa unaelekea Masoko na Mbambo.
 
WANANCHI wa Kijiji cha Ndola, Kata ya Nsalala wilaya ya Mbeya Vijijini, wamekikataa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kutomchagua mwenyekiti wa kijiji hicho aliyesimamishwa na chama hicho.

Hali hiyo ilijidhihirisha juzi wakati wa uchaguzi wa viongozi wa kijiji hicho ambapo mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Difasi Mwakisale, alitangazwa kuwa mshindi wa nafasi hiyo.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi msaidizi wa uchaguzi huo, Malongo Sumuni, ambaye pia ni Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Mbalizi, alisema kuwa Mwakisale alipata kura 513 dhidi ya mgombea mwenzake wa CCM Gilbert Mwanjela ambaye alipata kura 292.

Awali uchaguzi ulipofanyika Desemba 11 mwaka jana, Mwakisale alipata kura 405 na Mwanjela alipata kura 288, hivyo serikali ikapata kigugumizi kumtangaza na kuitisha uchaguzi upya ambao umefanyika baada ya wananchi hao kutishia kuandamana.

Wakizungumza na Tanzania Daima, wananchi wa Kijiji cha Ndola walisema kuwa uchaguzi huo ulifanyika kutokana na kugawika kwa Kata ya Utengule Usongwe baada ya serikali kuongeza kata katika wilaya hiyo.

Walisema katika uchaguzi huo wagombea wote kutoka CHADEMA walishinda katika nafasi zao ambapo ilimlazimu msimamizi msaidizi wa uchaguzi huo ambaye ni Kaimu Ofisa Mtendaji wa kata hiyo, John Mwanampasi, kukataa kumtangaza mgombea wa nafasi ya uenyekiti kutoka chama hicho.

Source:Tanzania Daima
Nimeongea na Difas Mwakisale kanithibitishia kuwa ni kweli tena kasema karibu vitongoji vyote vya kata ya Nsalala vinashikiliwa na CDM. Inasemekana Polisi CCM walitinga Mbalizi wakati wa uchaguzi kuwatisha wananchi wasiitumie demokrasia yao vizuri. Sasa naamini kuwa Shitambala aliuza kura za wananchi wa Mbeya vijijini kwa magamba.com, haiwezekani chama kilichojikita hadi kwenye vitongoji kikose ubunge kirahisi
 
Nimeongea na Difas Mwakisale kanithibitishia kuwa ni kweli tena kasema karibu vitongoji vyote vya kata ya Nsalala vinashikiliwa na CDM. Inasemekana Polisi CCM walitinga Mbalizi wakati wa uchaguzi kuwatisha wananchi wasiitumie demokrasia yao vizuri. Sasa naamini kuwa Shitambala aliuza kura za wananchi wa Mbeya vijijini kwa magamba.com, haiwezekani chama kilichojikita hadi kwenye vitongoji kikose ubunge kirahisi

Mkuu kwa sasa Mbeya hali inavyokwenda si ajabu uchaguzi mkuu ujao majimbo yote yakaenda CDM
 
Inawezekana wewe hujaelewa kabisa, LAT amefanya kuchombeza tu, ila namini wewe unadhani inaongelewa Ndola ya Zambia.
Mbeya kuna vijiji viwili vinaitwa Ndola, kimoja Mbeya vijijini na kingine kipo Tukuyu maeneo ya Katusyo ukiwa unaelekea Masoko na Mbambo.

Ni kweli mkuu,nilikua sijamuelewa LAT ila kiongozi Molemo alinielewesha nikajua Lat alirushia kibwagizo tu!naomba LAT anisamehe kwa ilo!
 
safi sana mbeya c jui Dar tumekunywa maji ya bendera?

Dar wacheza bao na zuna ni wengi, ushabiki wa kijinga wakati kila siku wanaomba omba.. tena mtu anakuja kukuomba mia tano juu kapiga tshirt yake ya kijani.. upuuzi umejaa sana ndio maana ukienda kwenye sehemu zenye waelewa ccm haipati kitu angalia ubungo,kawe, segerea then angalia sehemu zenye uswahili kama ilala,kinondoni,kigamboni,temeke
 
Mkuu unayemwambia ni mpambanaji mwenzako.

bora umemwambia kamanda bkoz unatakiwa usome comment kwa umakini nd then uijibu na so kuponda 2 kwan kamanda aliposema hadi malawi alimaanisha kuwa CDM imepanuka sana nchini but alitumia lugha fulani so as kuelezea ukuaji wa CDM.
 
si nasikiaga cdm imejijenga mijini tu, au hicho kijiji kimekua na kuwa mji!?
 
Back
Top Bottom