CHADEMA yasambaratika mkoani Kigoma

Wenye itikadi kamwe mmoja hawezi kuajiri kikundi cha watu kumdhuru mwingine. Kumshushia credibility, uaminifu wake kwa mambo ya kutunga. Slaa itikadi yake sio iliyokatika makaratasi ya chadema ambayo zito ndio anasimamia itikadi hiyo. Zitto amekuwa mtu wa busara na asiemnafiki. Umesahau kuwa slaa amemuunga mkono kagame dhidi ya nchi?
Umesahau jinsi anavyopinga kila jambo linaloanzishwa au kufanywa na ccm hata ikitokea nila muhimu kiasi gani kwa taifa?

Nani kakwambia Zitto na Dr Slaa ni maadui? Kama huna hoja ya kuchangia kaa kimya au kanywe kiroba original ulale. Zitto mwenyewe kashasema hana tatizo lolote na Slaa nyie CCM inawwauma nini? Nenda hospitali kapime yawezekana malalia imekupanda kicchwani au una kipandauso.
 
Kigoma ninayoijua mimi, ni Kigoma ambayo CCM ndicho chama kisichopendwa.

Sababu za Kutopendwa CCM Kigoma

Kuthamini Wenye fedha.

Hili lilijitokeza tangu mwanzo kabisa wa siasa za vyama vingi. Wakati huo Kigoma kulikuwa na watu wanaopendwa, waungwana na walio na karama za uongozi. Mfano ni Amaan Walid Kabourou na Rajab Kakolwa Mbano, ambaye kaka yake Marehemu Rajab Omar Mbano aliwahi kuwa mbunge kabla ya vyama vingi. CCM kwa kuthamini wenye fedha iliwaweka kando hawa na kumteua Azim Suleiman Premji kuwa mgombea wa CCM Kigoma mjini. Huyu hakuwa na mvuto kwa watu zaidi ya kuwa alikuwa tajiri. Alikuwa anamiliki Gereji ya Magari (Kigoma Auto Garage) na alikuwa anaendesha kwa kukodi Hotel ya kitalii iliyokuwa inamilikiwa na Railways (Kigoma Railways Hotel - Kwa sasa Lake Tanganyika Beach Hotel). Yaani alikuwa na uwezo wa kununua maamuzi ya vigogo wa CCM. Matokeo yake ni kuwa watu wa Kigoma wakasema EKAYEEE! (=NO). Wakamwambia Kabourou ajiunge na CHADEMA na wakamchagua Kabourou miongoni mbunge wa kwanza wa CHADEMA, na kati ya wabunge wachache sana wa upinzani 1995. Premji baadaye alikuwa Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Kigoma.

Kama hiyo haitoshi akajitokeza tajiri mwingine Kigoma. Huyu ni mmiliki wa Kigoma Hilltop Hotel, na Sheni's Commercial Ltd inayojishugulisha na uwindaji wa kitalii (tembo wetu). Huyu habari zake zimeandikwa sana mitandaoni na kwinginepo.
Muhsin Abdullah (Shen) Ameinunua This Country?


MOHSIN "SHENI" ABDALLAH AT IT AGAIN ; Where Have All the Elephants Gone?


Huyu Kada anaitwa Mohsin Abdallah, kuna yeyote mwana JF atupe Background yake ?


Mjue Kada wa CCM Mohsin Abdallah

Tanzania/Kenya - Where Have All the Elephants Gone? - Foreign Correspondent - ABC

Huyu pia alitaka kuingia kwenye siasa. Japo alikuwa hakubaliki kwa wanachama alikingiwa kifua na makao makuu, na kuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa. Huyu Kada yumo katika list ya matajiri wahusika wa madawa ya kulevya. Kwa sasa amemaliza muda wake wa ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa. Analalamika kuwa yeye na Premji wamebaguliwa kwa rangi yao.

Kuna kada mwingine wa CCM wilayani kibondo kwa jina la Jamal Tamim. Huyu anatoka kijiji cha Mabamba wilayani Kibondo katika jimbo la uchaguzi la Muhambwe. Pale Mabamba shughuli anazofanya Jamal hazijulikani, lakini Jamal ni tajiri kupindukia. Mwaka 2007 walipafanya kura za maoni za kufichua wanaofanya biashara za viungo vya albino, Jamal aliongoza kwa kutajwa na wengi wilaya ya Kibondo. Licha ya hayo, Jamal anatuhumiwa kuwa na kikundi cha ujambazi ambacho pamoja na mambo mengine, huteka mabasi, na kufanya matukio mengine ya wizi wa kutumia nguvu. Pamoja na shutuma zote hizi kuwa wazi, CCM ilimpitisha Jamal kuwa mgombea ubunge kiti cha Muhambwe. Pingamizi la kwanza lilitoka mkoani Kigoma kwenye kamati ya Maadili ya CCM. Simbakalia na Kastico walionyesha wazi kuwa huyu Jamal hauziki, lakini kwa influence ya Rostam Aziz na JK, alipitishwa. Kastico (Katibu wa CCM Mkoa wakati huo) aliondolewa Kigoma Oktoba 2010 wakati wa kampeni kwa sababu aliweka pingamizi, na aliondolewa na JK mwenyewe alipofanya ziara ya dharura Kigoma Oktoba 2010.

Matokeo yake wana CCM wengi Kigoma walivunjika nguvu hata kupiga debe kwa wagombea wao. Uchaguzi uliopita, CCM ilishinda kiti cha Kigoma Mjini (kwa kuchakachua), Manyovu na Buyungu. Kati ya viti hivyo vyote Buyungu tu ndio wanaweza kusema kuwa waliwekewa mgombea wanayemtaka (Waziri Christopher Chiza) - ambaye hata mimi namkubali. Ni viti vitatu kati ya vinane. Ni mkoa wa bara ambao asilimia ya wawakilishi (wabunge) wa CCM ni ndogo kuliko popote Tanzania.

mkigoma, Shelui, Simiyu yetu, CHAMVIGA, utaifakwanza, Lizaboni, SONGEA ONE, njoni na hoja zinazoonesha mnaijua vizuri Kigoma na siasa zake.

Sisi watu wa Kigoma tuna mpango wa kuendelea kuikataa CCM na hatujali anayeingiea ni CHADEMA, CUF au NCCR, sisi hatuitaki CCM.

Muha akishasema NTIBHISHOBHOKA, harudi nyuma. Nyie endeleeni kupiga propaganda.
Mkuu umemaliza kabisa. Naona waliozoea propaganda za uongo wakipewa facts wanajificha.
 
Akili za magamba utazijua tu wote hata kama wamesoma wanafanana na gaidi wao Mkuu migulu
 
akigombea tu ndiyo basi tena hamtamuona tena.....................

uploadfromtaptalk1377697548073.jpg
 
Hakuna zito kabwe nje ya chadema! Wengi walishahama vyama vyao na kurudi kwa magamba na wakaishia kusikojulikana! Yupo wapi masumbuko lamwai, wasira amekuja kuokolewa na jk kwa sbabu za uswahiba tu otherwise alishafulia zamani, kabour yupo wapi, hiza tambwe je n.k! Kama zitto anadhani ana umaarufu sana nje ya chadema na atoke aone!. Hata yeye analitambua hilo ndio maana hawezi kuondoka chadema ingawa magamba at one time walijaribu kumtumia kukisambaratisha chadema lakini wakashindwa na chadema wanasonga mbele.

Zitto anasumbuliwa na jambo moja tu kwamba anataka kuwa mkwe wa ccm sasa kuwaponda wakwe zake laivu inakuwa ngumu kwake ndio maana anajifanya yupo neutral na wasiojua hili wanadhani katengwa ndani ya chadema! Kama ni ukabila mbona kuna vijana wengi tu ma makabila tofauti na wana vyeo vikubwa tu ndani ya chadema? Huo ukabila unamwandama zitto kabwe tu? That's shit!

Zitto asirubuniwe zito leo yupo hapo alipo leo kwa sababu ya chadema na kama anaona kweli ameshindwa kukaa ndani ya chadema na awe huru kutoka hakuna mtu atakeyemlazimisha kukaa humo!

Asanteni kwa kunifuatilia!
 
kaaazi kweli kweli....!

Hivi ni nani asiyejua umuhimu wa Zitto ndani ya CDM? nani asiyejua mamlaka aliyokuwa nayo zitto PAC? amebaguliwa na wewe siyo?

achaga u-mbulula, zitto kajenga sana chama na usitake leta porojo zisizo za maana hapa, kashasema yuko pamoja ktk kampeni za M4C na hata mikutano ya kupokea maoni ya wanachama kuhusu rasimu ya katiba mpya na alishindwa kuudhuria kutokana na vikao vya kamati za Bunge ambayo yeye ni mwenyekiti wa kamati hiyo ya PAC 1.

uletapo uzi humu angalieni leteni uzi za kujenga na kuelimisha taifa na si kubaguana na kupenyeza mitafaruku kwenye mshikamano.
 
Chadema ni zaidi ya Zitto. Hakuna mtu ambaye ni mpinzai wa dhati atahama CDM unless ni kibaraka
 
dhambi ya ubaguzi haitaishia hapo, watazidi kusigishana sana tu.

Sijui udhaifu wako wa kujua Ubaguzi ndio unadhoofisha ufahamu wako wa mambo ..... jinsi ulivyo siamini km unamaanisha UCHAGA ...., je wewe na wenzio mnaoamini nchi hii raia wa kwanza ni MwanaCCM na siyo wengine ndio UMOJA mnaotaka.....Nyerere mwasisi wa CCM hakuwahi kusema watanzania tuangaliane kwa UKABILA wetu....alisisitiza Watanzania tuangaliane kwa hulka na maudhui yetu na siyo huo upuuzi mnaoushikilia hata km Wanyakyusa ndiyo walioongoza BIMA ikumbukwe haikua maudhui ya UKABILA iliyotumika bali hulka ya utendaji wa kazi ndio kigezo kwanza haidhuru hata km wote watakua wasukuma.... Hauwezi kuwa Mtanzania km wewe Siyo Mchagga, Msukuma, Mndengeleko nk. Kinacho kukera wewe ni nini ?
 
Hiyo ni hali ya kawaida katika ukuaji na maendeleo ya taasisi yeyote ile. Misuguano ni njia moja wapo ya kuelekea ukomavu zaidi. Wasipopata uzoefu wa ku-handle misuguano sasa hivi, itawapa shida sana baadaye watakaposhika utawala wa nchi, maana watakuwa hawakuandaliwa vema katika kukabiliana na hali hiyo. Hiyo ni dalili kwamba chama kinakua na kinasonga mbele. Waingereza wanasema, "where there is friction, there is movement", yaani pale paliopo na msuguano pana mwendo (kwa maana ya mwendo wa kusonga mbele), na waswahili nao wanasema, "huwezi kula mua bila kukuta fundo", Hivyo hali hii ni ya kawaida na isiwatishe hata kidogo. Kikubwa ni wajifunze kutokana na hali hii kitu ambacho kitasaidia zaidi wakati wa utawala. Peopleeeeeees Poweeeeeeer!!!!!!
 
WanaCCM Wanao mpamba Zitto km mhanga wa Ukabila ndani ya CDM ndio wanavyomdhoofisha .... hawajui kwa kung'ang'ana na hoja ya UKABILA ndio wanavyoonyesha walivyowaongo ... Binafsi naanza kuona umuhimu wa hawa watu wenye ufikiri huu ndio wanaokijenga CDM
 
Kuna tetesi kuwa Zitto atagombea Tabora mjini kwani CCM imepoteza muelekeo na CUF ni kama wamekufa vile.
 
kwani mh zitto kuijenga chadema kigoma anahitaji ridhaa ya makao makuu ?mbona akina msigwa,sugu, na wingine wanakijenga chama maeneo yao ?au wao wanafanyaje ndio zitto ashindwe kigoma?Tuache siasa hizi tumsaidie zitto unless we ant-CDM
 
Kutokana na mvutano unaoendelea ndani ya Chama cha demokrasia na maendeleo na Chadema imesababisha Chama hicho kusambaratika na kupoteza mvuto mkoani kigoma, sababu hasa inaonekana ni kutengwa kwa kijana wao zitto kabwe ndani ya chama hicho, na hata tetesi zinazoongelewa katika vijiwe vya siasa mkoani kigoma, aliye kuwa mgombea wa chama cha chadema Mwaka 2010 Ally mlee akakihama Chama muda wowote kuanzia sasa. Hali ni mbaya mkoani hapa, kila kijiwe kinaongelea ubaguzi ndani ya chama hicho.

kumbe ni habari za kijiweni..peleka kwa shigongo bana.hapa tunaitaji habari zenye fact..sio mambo ya kistoni wewe Gamba .
 
Back
Top Bottom