CHADEMA yakimbiwa Kilosa

RICH OIL SHEIKH

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
883
167
Katibu mwenezi wa CDM Kilosa Bw. Ramond Mlama na Mjumbe wa Wilaya ya Kilosa Penfold Chimola wamekitosa CDM na kujiunga na CCM kwa kuwa CDM haina sera madhubuti, na CCM si chama cha wabaguzi na wababaishaji. Ameongezea kuwa washabiki wa CDM hawajui ubaguzi uliokitanda chama hicho ila yeye kama kiongozi ameona. Hii imetokea juzi. Poleni sana.

Source Mwananchi la leo
 
asante gamba naona tangu jana mumeamua mulianzia arusha mwanza na sasa huko bado kidogo mumalize mikoa ya tz.huo ni unafiki na kukosa sera ila pia itambulike kua sera na matendo yako wazi huwezi linganisha matendo ya ccm na chadema hata kidogo.angalia hata huko mwanza ccm wamewatekeza wa tz huko.na mengine mengi wanayofanya ccm.tueleze aina gani ya ubaguzi wanaofanya chadema huko.
 
wangeeleza nani kabaguliwa wapi, wange site sera wanayodai kuwa legelege na kukosa umadhubuti, waseme pia kuwa walichukua hatua zipi kuboresha hizo sera, na chadema kama chama kimebabaisha nini. mimi nawatuhumu hawa jamaa kumuiga yuda iskariote.
 
Huyo akili yake haiko sawa, kwani kabla ya CDM alikuwa wapi si huko huko? Huyo hatutishi tuliofanya kabla ya kutenda.
 
No wonder boss wa BAKWATA alikuwa huko.......kwa baraka za Mkullo

MUFTI+KUTOA+HOTUBA-1.JPG
 
CDM ni kwa watu makini tu hao wachumia tumbo ni lazima wakimbie na warudi huko huko kwa wenzao Magamba maana ndio kunawafaa!!
 
Katibu mwenezi wa CDM Kilosa Bw. Ramond Mlama na Mjumbe wa Wilaya ya Kilosa Penfold Chimola wamekitosa CDM na kujiunga na CCM kwa kuwa CDM haina sera madhubuti, na CCM si chama cha wabaguzi na wababaishaji. Ameongezea kuwa washabiki wa CDM hawajui ubaguzi uliokitanda chama hicho ila yeye kama kiongozi ameona. Hii imetokea juzi. Poleni sana.

Source Mwananchi la leo
Sasa anadhani huko ccm ndiko salama? Kwa kuwa haijui ccm anadhani mambo ni shwari ccm, nao pia wanatapatapa tu. Amuulize Mwakyembe ndo atajua kuwa hata ccm sio salama, ni heri hata angekaa tu bila chama ningemuona mwenye busara. Nadhani hao jamaa wana njaa tu ambao nadhani walipata mgao wa Nape katika mkakati wake wa kununua wanachadema.
 
Nyani akivaa suti kali akaingia kwenye kundi la binadamu hata akijikaza vipi hataweza maana itakua vigumu kuiga kila kitu ambacho si asili yake,watu wakifurahi watacheka na kupiga makofi wakati yeye atapiga kelele na kutikisa mkia wakati kauficha kwenye suti!atahis kagundulika na ataondoka mwenyewe.hao ni manyani,magamba hao,wameshindwa kuhimili mikiki ya makamanda na sasa wanarudi kwenye asili yao.
 
Jamani baadhi ya waislam uwezo wao wa kufikiri ni zaidi ya Rejao, Ritz, malaria sugu na Bibiye FF
 
Dah,
hiyo ndo kazi aliyoendea mufti huko hiyo juzi tarehe 05.02.2012 siku ya maulidi. na huyu mkullo anaendekeza sana udini. eti sherehe za maulidi kitaifa zinafanyika kilosa..duh, mbona mnazi mmoja ndo ilionekana kama kitaifa vile!

Halafu muulizeni mkullo hivi ule mradi wa maji wa kanali ghadaff umeishia wapi? mana aliahidi kutandaza maji kwa msaada wa ghadaff katika mji huo wa kilosa.

Yote kwa yote, nimeongea na diwani wa kata ya magomeni huko kilosa anasema hata kama wakiondoka hao jamaa hawana influence yoyote katika chama ngazi ya wilaya.
 
Back
Top Bottom