CHADEMA Yaanza Operesheni PAMOJA DAIMA: Helkopta tatu Kutumika!

Mtanke

JF-Expert Member
Nov 19, 2011
726
1,800
M/Kiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mh. Freeman Mbowe ametangaza kuanza kwa Operesheni Pamoja Daima yenye lengo la Kuwaandaa Wananchi kushiriki kikamilifu kwenye Mchakato wa Katiba ikiwa ni pamoja na kujiandikisha katika Daftari la Wapiga Kura wakati ukifika.

Mh. Mbowe amyasema wakati akizungumza na Waadishi wa Habari jijini Dar es Salaam Mkao kuu ya CHADEMA leo. Ziara hiyo itaongozwa na timu tatu zitakazoanzia mikoa Mwaza, Ruvuma na Tanga. Mbowe asema pia kuwa ziara hiyo itakuwa ni ya wiki mbili na siku zinaweza kuongezeka kadiri itakavyohitajika.

Pia ameongeza kwa kusema "Katiba Mpya ni lazima na kama haitapatikana kwa utaratibu uliowekwa kwa mapenzi tu ya Rais na Wabunge wachache wa CCM watanzania wataitafuta Katiba Mpya kwa utaratibu mwigine".

Kwa ufupi
· Ziara hiyoinaanzia katika mikoa ya Tanga, Mwanza na Ruvuma, huku viongozi wa chama hichowakijigawa katika makundi sita; matatu yakitumia helkopta na matatu yatawafikiawananchi kwa kutumia usafiri wa magari.

Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)kuanzia leo, kinarusha helkopta tatu kwa siku 14 mfululizo, katika kutekelezakampeni iliyopewa jina la Operesheni Pamoja Daima (ODB) itakayoendeshwa katikamikoa yote nchini.

· Ziara hiyoinaanzia katika mikoa ya Tanga, Mwanza na Ruvuma, huku viongozi wa chama hichowakijigawa katika makundi sita; matatu yakitumia helkopta na matatu yatawafikiawananchi kwa kutumia usafiri wa magari.

· Mwenyekiti waChadema, Freeman Mbowe alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa, lengo laoperesheni hiyo ni kukiimarisha chama hicho na kuwafumbua macho wananchi kuhusumchakato wa Katiba Mpya.

· "Tumejigawakatika makundi sita na makundi matatu kati ya hayo yatatumia helikopta kilamoja, makundi mengine yatawafikia wananchi kwa misafara ya ardhini," alisemaMbowe na kuongeza;

· "Viongozi wakuuwa chama, wabunge, wenyeviti wa mikoa, wilaya, majimbo na kanda kila mmojaatashiriki kwa nafasi yake katika operesheni hii. Tutafanya mikutano kwa wikimbili, ila tunaweza kuongeza wiki nyingine moja."

· Alisema chamahicho kimejipanga kuwafikia wananchi wengi kadri itakavyowezekana, ikiwa nisehemu ya maandalizi ya uchaguzi wake wa ndani kuanzia ngazi ya mashina,uchaguzi mdogo wa madiwani katika Kata 27 nchini utakaofanyika Februari 9,mwaka huu pamoja na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

· "Naombatueleweke, katika hili hatufanyi kampeni hata kidogo, huu ni mwendelezo wamaandalizi ya chaguzi mbalimbali. Kama mnakumbuka tulianza kujiandaa nauchaguzi wa mwaka 2015 baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa 2010," alisemaMbowe na kuongeza;

· "Kwa sasatunachokifanya ni kuongeza nguvu na umakini zaidi. Makundi yataanzia katikamikoa ya Tanga, Mwanza na Ruvuma, tutapita kila Kata ambazo utafanyika uchaguziwa madiwani."

· Mbowe alisemaoperesheni hiyo itapiga kambi katika Jimbo la Kalenga ambalo kwa sasa lipo wazibaada ya mbunge wake ambaye pia alikuwa Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk WilliamMgimwa kufariki dunia Januari 1, mwaka huu nchini Afrika Kusini.

· "Tume ya Taifaya Uchaguzi (Nec) haijatangaza kufanyika uchaguzi katika jimbo hilo, Chadematutafika Kalenga na tutafanya mkutano maalumu na kutoa pole kwa wakazi wa jimbohilo kutokana na msiba mkubwa wa mbunge wao," alisema Mbowe.

· Operesheni hiyoinafanyika siku chache tangu chama hicho kikuu cha upinzani nchini kipitekatika mgogoro ambao ulisababisha aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wake, Zitto Kabwekukimbilia mahakamani ili kunusuru uanachama wake.

· Wakati Zittoakinusurika kufukuzwa kutokana na zuio la mahakama, aliyekuwa Mwenyekiti waChadema mkoani Arusha, Samson Mwigamba na Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk KitilaMkumbo walifukuzwa uanachama, likiwa ni hitimisho la mchakato ulioanza kwakuwavua nyadhifa zao pamoja na Zitto.

· Daftari lawapigakura
· Mbowe alisemamsimamo wa chama chake ni kutaka daftari la kudumu la wapigakura lifanyiwemarekebisho kabla ya kupigwa kwa kura za maoni kwa ajili ya kupitisha KatibaMpya.

· "Tutagomeaupigaji wa kura na tutawahamasisha wananchi kugomea kupiga kura. Serikali yaCCM isijidanganye kwa kuweka mikakati ya kukwamisha zoezi hili," alisema Mbowe.

· Alisema kamaSerikali inataka amani iendelee kuwepo isifanye mzaha katika mchakato wa KatibaMpya kwa maelezo kuwa Katiba siyo mali ya vyama vya siasa, bali ni mali yawananchi.

· "Katiba siyo yaChadema, CUF wala NCCR-Mageuzi. Sheria inaeleza wazi kwamba daftari lawapigakura ni lazima lifanyiwe marekebisho mara mbili baada ya Uchaguzi Mkuu nakabla ya kuanza Uchaguzi Mkuu mwingine lakini hilo halijafanyika mpaka sasalicha ya Uchaguzi Mkuu kufanyika miaka minne iliyopita," alisema Mbowe.

· Alisema wapoWatanzania waliohama maeneo yao ya awali, waliopoteza vitambulisho,waliofikisha umri wa kupiga kura na kusisitiza kuwa kuwaacha watu hao nje yamfumo wa kupiga kura ni kuwanyima haki yao ya Kikatiba.

· "Kwa mujibu wautafiti tulioufanya tumebaini kuwa wapo watu zaidi ya milioni 5 wanaohitajikuingizwa katika daftari la wapigakura," alisema Mbowe na kuongeza;

· "Kama Katibahaitapita kwa sababu ya kutokuboreshwa kwa daftari la wapigakura hatutarudikatika Katiba ya sasa hiyo ni ndoto."

Chanzo: Mwananchi
 
Nice kamanda wa anga maccm kifo chao kimefika katiba ni ya watanzania wote milioni 46
 
Suala sio kuwa na katiba mpya tu, zaidi ni maudhui ya katiba hiyo mpya!
 
M/Kiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mh. Freeman Mbowe ametangaza kuanza kwa Operesheni Pamoja Daima yenye lengo la Kuwaandaa Wananchi kushiriki kikamilifu kwenye Mchakato wa Katiba ikiwa ni pamoja na kujiandikisha katika Daftari la Wapiga Kura wakati ukifika.

Mh. Mbowe amyasema wakati akizungumza na Waadishi wa Habari jijini Dar es Salaam Mkao kuu ya CHADEMA leo. Ziara hiyo itaongozwa na timu tatu zitakazoanzia mikoa Mwaza, Ruvuma na Tanga. Mbowe asema pia kuwa ziara hiyo itakuwa ni ya wiki mbili na siku zinaweza kuongezeka kadiri itakavyohitajika.

Pia ameongeza kwa kusema "Katiba Mpya ni lazima na kama haitapatikana kwa utaratibu uliowekwa kwa mapenzi tu ya Rais na Wabunge wachache wa CCM watanzania wataitafuta Katiba Mpya kwa utaratibu mwigine".

Muda wa fedha za chama kuliwa na wajanja wachache umefika tena, MBOWE kishajikodishia helikopta , wakati mikoani hata mishahara kwa watendaji wa chama hakuna wanavaa suaruali zimetoboka kwenye makalio.
 
1. Operesheni Sangara.

2. M4C.

3. Chadema ni Msingi.

4. Pamoja Daima.

Zote zimefeli....
 
Back
Top Bottom