Bibi Ntilie
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 245
- 8
Mtoto, Mimi si mwanachama wa Chadema, lakini naona huenda CHADEMA kikawa ndio tegemeo la Watanzania. Ndio maana ningependa kuona Chadema ikiwa na clarity ya hali ya juu.
Wako Watanzania wengi nje na ndani ya nchi ambao wanadhani CHADEMA ndio inapashwa kuchaguliwa kungoza nchi kuanzia 2010. Wanataka waone umakini unaoonyeshwa na viongozi wa CHADEMA unaonekana hata kwenye tovuti yao.
In a way, you are what you write.
Naam, Watanzania wengi walitegemea kwamba huenda CHADEMA kitatoa changamoto inayostahili kwa Chama cha Mapinduzi, kumbe wapi! Tatizo ni kwamba viongozi hawana mshikamano unaotakiwa. Mbowe ni Mwenyekiti anayesikika kwenye chaguzi zaidi kuliko kwenye kukijenga na kukiimarisha Chama chake. Viongozi wengine kila mmoja anaonekana kutafuta umaarufu binafsi.
Yuko wapi Tundu Lissu? Hasikiki sana siku hizi. Zitto ambaye alikuwa ndio tunategemea ataendelea kugombea ubunge na wakati huo huo kujifunza kuwa kiongozi shupavu kwa kukosea na kujisahihisha, tumeambiwa hataki kugombea tena ubunge. Hata Mbowe naye aliondoka mapema mno kwenye siasa za Ubunge na kutaka kuwa Mwenyekiti wa Chama. Angeliwaachia wale wazee - Mzee Makani na Mzee Mtei waendelee kushika wadhifa wa Mwenyekiti na wakati huo huo wakawa washauri wakuu kwa kuwa wazee hao ni watu makini na siasa za nchi hii wanazielewa vizuri sana.
Mjadala wa 'mrengo na mirengo' unafurahisha! Hivi kweli tunaweza kuiletea Tanzania maendeleo kwa kuiga mambo ya mirengo ya kushoto, kulia na kati? Bado tunahitaji kuendesha siasa za nchi yetu kwa kuzingatia hali halisi. Kama walivyosema baadhi humu, utaenda kwa 'wananchi wa kawaida' wa vijijini hata mijini ukawaambia chama changu kinafuata siasa/itikadi ya 'mrengo wa kati' nani atakuelewa. Ukija na maelezo kwamba kuna Liberals and Conservatives etc etc pia sie akina Bibi Ntilie wauza pilau na maandazi mjini tutatoka kapa na kura zetu hutapata!
Wenye kuponda waendelee, lakini wahenga waliokuwa na 'fikra sahihi' walipotamka "Tutafuata/tunafuata Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea' ilikuwa "simpo" sana kuielezea kwa wananchi wa kawaida wakaelewa. Utata uliokuwepo na utaendelea kuwepo ni kwenye utekelezaji. Mpaka pale Watanzania tutakapoona mwanga na kuamua kuondoa 'fikra za kifisadi' za katika vichwa vyetu.
Zidumu Fikra Sahihi! Enyi waungwana, msikasirike!