CHADEMA Wazindua Matawi vyuo Vikuu: St Johns, DIT, CBE, IFM na Mipango-Dodoma

Regia Mtema

R I P
Nov 21, 2009
2,970
864
Wakuu habari.

Jana siku ya Jumamosi tarehe 12 Februari 2011 kwa nyakati tofauti Wabunge wa CHADEMA wamezindua matawi ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Vya Mt Johns na Mipango.Kabla ya Uzinduzi kulitanguliwa na hotuba fupi fupi za wabunge hao. Mikutano yote ilikuwa ni mizuri sana.

Wabunge waliowakilisha Chama ni

1. Prof Kahigi- Bukombe
2.Halima Mdee- Kawe
3.John Mnyika-Ubungo
4.Godbless Lema-Arusha Mjini
5.Rebecca Mgodo-Viti Maalum Arusha
6.Regia Mtema- Vitimaalum Kilombero

Wanafunzi zaidi ya 200 wa Chuo Cha Mt John wamejiunga na CHADEMA sambamba na ufunguzi wa ofisi ya tawi hilo.

Zaidi ya wanafunzi 1000 wa Vyuo vya Mipango na UDOM wamejiunga na CHADEMA Sambamba na ufunguzi wa Tawi.


Wabunge hawa walipokelewa kwa nderemo na vifijo na wanafunzi hao.

Mapambano yanaendelea,Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke.


N.B: Picha za matukio yote mawili baadaye kidogo.

Zoezi hili linaendelea leo viwanja via Sabasaba jijini Dar es Salaam kwa vyuo vya DIT, IFM, CBE n.k

From Dodoma.

Aluta Continua
 
kazi nzuri mnaifanya ...hawa vijana nao wataufikisha ujumbe kwenye jamii zao
 
Asante sana Regia

Naomba zoezi hili liwe endelevu kwa kila kijiji katika Tanzania bara na makao makuu ya chama kwa kila kijiji kuwa makao makuu ya kata, mfungue na kuweka viongozi wanaokubariki na jamii nzima inayozuguka kijiji husika, nyuma yenu kuna kundi kubwa linawasubiria kwa jili ya kuichukua nchii hii kutoka mikononi mwa wanyanganyi
 
God Regia kwa kutuhabarisha inatiamoyo nivema kila wakati kuyatembelea haya matawi na kuyaimarisha kwani kufungua tawi ni jambo moja na tawi kukuwa ni jambo lingine so nivema mkaweka mikakati ya kuyapitia mara kwa mara
Pia wikiend hii nilitembelea maeneo ya bangamoyo pana vyuo kadhaa pale na pia kunavijana nilifanya nao mazunguzo walitaka kujua ikiwa bagamoyo pana uongozi wa chadema kwani wanataka wawe na tawi lao la waendesha pikipiki na kama upo naomba mawasiliano ya hao viongozi niwaunganishenao

Natanguliza shukurani zangu.
 
Wakuu ndio tunaelekea kuzindua tawi la CDM kwa vyuo vya DIT, IFM, CBE nk. Kweny viwanja vya Sabasaba. Peoples power........
 
Tupo pamoja kufuatilia kitakachojiri huku, tumefurahi kupata kwayaliyojiri Jana Chuo cha mipango, st. John , madini ya UDOM zaidi ya watu 1200 walijiunga na chadema, kwakweli inatia moyo sana.
 
Regia nianze kwa kukupongeza wewe binafsi kwa hatua hii ya Cdm kufungua matawi sehemu za makusanyiko ya vijana, maana vijana ni chachu ya mabadiliko...Hata atakapomaliza vyuo hivyo, wataenda vijijini au mijini kuchachusha wale wawazungukao.
Lakini pia nikupongeze kwa kutuhabarisha juu ya jambo hili, maana ni faraja hii, na kwangu binafsi umenitengenezea siku!

Huu uwe ni mwendelezo, na msichague maeneo...
 
hiz ni habari nzuri sana,
keep going CDM
mpaka kieleweke:coffee::coffee::roll:
 
Regia nashukuru kwa taarifa yako. Nimeona mara kadhaa umekuwa ukituhabarisha kuhusu matukio mbalimbali yanayohusu shughuli za Chadema humu jamvini.

Ninapendekeza suala hili lisiwe kama bahati tu. kutupasha liwe suala endelevu na liwe chini ya mwongozo wa Chadema. Chadema itambue kuwa habari kama hizi ni muhimu kwa wapenzi wa Chadema na wananchi kwa ujumla. Hivyo ni vizuri vyanzo vya habari rasmi za Chama vikidhibitiwa itawasaidia kuepusha upotoshaji wa habari.
 
Mu-sir anaomba radhi kwani hana access ya Internet tena kutoka viwanja vya Sabasaba, thread(s) zimeunganishwa na ya Regia
 
Hilo ndiyo neno - Hakuna kulala mpaka kieleweke! Ahsante sana dada Regia,ahsante sana
chadema
 
Hapa ndio umuhimu wa CDM kuwa na combo chake cha habari Kama Radio au Tv unapoonekana,habri Kama hizi zilitakiwa zisambae Kama kimbunga nchi nzima ili mwamko uwe juu zaidi maana vyombo vingine vya habari sio vya kutegemea sana kutoa uzito kwa mambo Kama haya pamoja na umuhimu wake
 
Back
Top Bottom