CHADEMA: Watanzania puuzeni propaganda za udini...

Wakati Cuf ilipokuwa imevuma sana na kuwa na wafuasi wengi ilichafuliwa na kutangazwa kuwa ni chama cha waislam, na wakristo wakapandikizwa chuki dhidi ya CUF, na sasa wakati huu CHADEMA imepata nguvu na kuwa na wafuasi wengi, imejengewa chuki kuwa ni chama cha wakatoliki(wakristo) Je watanzania tumekuwa mbumbu kiasi cha kushindwa kuutambua fitina hizi?
 
Mkuu lilikuwa fumbo hilo hawa wanajulikana sana humu !hawa pro chadema hapa JF ndiye wadini wakubwa wana kejeli Waislam sana hapa JF mara ooh hawajaenda shule,wala ubwawa, nk nk sasa sijui hawa amabo hawajenda shule au wala ubwabwa hawapigi kura?

Nilisha eleza kwenye thread nyingine kuwa kuna viongozi wengi wakuu wa chadema wana pita humu lakini hakuna hata mmoja wao amejaribu kukumea hizi dharau na dhihaka wanazo zifanya hawa wanachadema hapa JF,wakielezwa wadini chama chao kina dhihaki Waislam wanasema hizo propaganda za CCM,mwenye macho haambiwi ona , kejeli zote wanazo zifanya wanachadema hapa JF kwa Waislaam.

Hili halina mjadala Chadema waliyo wengi wana chuki sana na Waislam na Uislam mfano halisi unaanzia hapa JF tena si ajabu wengine wanajulikana wanajificha wanaona waelezee hisia zao hapa JF,lakini yule mchungaji mbunge wa Iringa ameshajiweka hadaharani kuwa yeye ni ant-Islam,

Hivi Mie siwaelewi hawa Chadema na haswa hawa wa JF hivi kama mna ndoto ya kutawala Tanzania hivi kwa akili yenu mtaweza kuwatawala bila ushirikiano wa Waislaam?

Hata kama mnadhani Waislaam, wapo minority nchini unafikiri uchache wao itawapa amani?Angalieni Waislam wapo minority nchi nyingi kwa mfano India kuna wakati kulikuwa na vita vikubwa kati ya Waislam na Wahindu,Phillipines,Burma,kuna kipindi huko Trinadan na Tobago Waislam waliteka bunge nzima kwa bunduki zote hizi choko choko za kidini.

Hivi nyie pro-chadema mliopo hapa JF wabaya wenu waamue kuanika hizi kejeli zenu kwa waislam wa kawaida waliopo huko mitaani mnadhani chama chenu kitajengeka?

Hizo kejeli zenu mnazo Wafanyia Waislaam CCM wanazipenda sana wanajua mnajikaanga kwa mafuta yenu wenyewe hamuwapi tabu za kuwamiliza mnajimaliza wenyewe.

Msijidanganye hata kidogo ya kuwa hiyo mikutano ya hadhara na watu wanaokuja kwenye mikutano ndiye ushindi wenu hao sio wapiga kura pekee kuna mamilioni ya wapiga kura ambao hawaji kwenye mikutano yenu ambao wapo mitaani na majumbani mwao ambao wengine mnawa kejeli na kuwadhihaki dini yao!

TIme will tell!Pro-Chadema mliopo hapa JF mnahitaji kujirekebisha kama mwakipenda chama chenu kama ni kweli nyie wafuasi wa ukweli wa chadema unless nyie mashabiki tu!
Hawakukemea kwa kuwa na wao walijua watatumia hii propaganda ya udini
 
Back
Top Bottom