Chadema wataka uchaguzi mpya wa madiwani

baraka boki

Senior Member
Sep 20, 2010
181
80
urudani

Maoni ya mhariri

Safu



source;Nipashe
Na Richard Makore
6th June 2011







Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kama serikali imebaini uelewa mdogo kwa Madiwani ni kikwazo katika usimamizi wa matumizi ya fedha katika halmashauri, kuna haja ya kuweka vigezo vya elimu pamoja na kuitisha uchaguzi mkuu haraka ili kupata watu wenye uwezo wa kufanya kazi hiyo.

Ushauri huo ulitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Chadema, Erasto Tumbo, alipozungumza na NIAPSHE na kuongeza kuwa kama hilo halitafanyika fedha za walipa kodi zitaendelea kupotea.

Hatua hiyo ya Chadema imekuja siku mbili baada ya wiki iliyopita, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), George Mkuchika, kuweka bayana kwamba Madiwani wengi katika halmashauri mbalimbali nchini wanashindwa kumudu kusimamia fedha za serikali kutokana na elimu ndogo waliyonayo.

Aidha, Tumbo alisema Chadema kinaoongoza halmashauri saba hapa nchini na kwamba zote hazina ubadhirifu ikilinganishwa na zile zinazoongozwa na Madiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Alisema kama ni “umbumbumbu’Madiwani wa CCM ndiyo wanaoongoza kwa kuwa wao halmashauri wanazoziongoza ndizo zenye matatizo makubwa tofauti na zile za zinazosimamiwa na Chadema.”

Alisema kama serikali imekiri na kuliona tatizo hilo, kuna haja ya kuchukua hatua za haraka katika kulitatua ikiwemo kuitisha Uchaguzi Mkuu kwa ajili ya kuwapata Madiwani wenye sifa hususani kwa kuzingatia kigezo cha elimu.

Mkuchika akizungumza na wabunge wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Sheria, Katiba na Utawala wiki iliyopita, alisema watendaji wengi wa halmashauri nyingi nchini wanatumia udhaifu wa Madiwani kufuja fedha.

Suala la ubadhirifu lilijotokeza katika vikao vya Kamati za Bunge vilivyomalizika wiki iliyopita jijini Dar es Salaam baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Augustino Mrema, kutoa takwimu kuwa kwa mwaka mmoja Sh. bilioni 5.3 zimebainika kutafunwa na watendaji wa halmashauri mbalimbali hapa nc
 
Back
Top Bottom