Feedback
JF-Expert Member
- Mar 14, 2011
- 7,988
- 4,507
Katiba si ya Kikwete, nimeusoma muswada umempa rais madaraka makubwa mno, yeye ndiye anateua na kuwathibitisha wajumbe wa tume, yeye anaanda hadidu za rejea anapokea mapendekezo ya tume na kuyakubali au kuyakataa.
Kwenye bunge la katiba ukiacha wabunge na wawakilishi ambao ni wajumbe yeye atayathibitisha majina mengine 116,
baadae yeye ndiye anaitisha bunge la katiba ambalo litawajibika kwake.
Walichoongeza kwenye huu mswada mpya ni kwamba kila wakati atashauriana na rais wa Zanzibar. Namwambia kwamba hii katiba ni ya watanzania si ya ukoo wa Mrisho muda wake ukiisha ataondoka na kuiacha, kwa hiyo atuache tuamue wenyewe.