CHADEMA wamesema hawatoshiriki katika uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Muhambwe

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,281
Chama cha CHADEMA kimesema hakitashiriki uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Muhambwe lililopo wilayani Kibondo Mkoa wa Kigoma.

Jimbo la Muhambwe liko wazi baada ya aliyekuwa mbunge Atashasta Nditiye kufariki dunia Februari 12, 2021 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa mkoani Dodoma alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kupata ajali ya gari iliyotokea Februari 10, 2021 eneo la Nane Nane, mkoani humo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Aprili mosi, 2021 naibu katibu mkuu wa CHADEMA, Benson Kigaila amesema baada ya kikao cha kamati kuu kilichofanyika Machi 31, 2021 kwa njia ya mtandao wameazimia kutoshiriki uchaguzi huo kutokana na mazingira ya tume ya uchaguzi kutotenda haki.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeshatangaza kuwa uchaguzi katika jimbo hilo utafanyika Mei 2, 2021.

Tayari Chama cha Mapinduzi (CCM) kimemteua Florence Samizi kuwa mgombea wa nafasi ya ubunge katika jimbo hilo.

Chanzo: Mwananchi
 
Nawaunga mkono.

CCM ni ile ile na Tume ni ile ile huku Mama akiwa bado kazungukwa na watu wenye mentalily za Magu.

Kingine: Katika hizi chaguzi ndogo, wanaweza kuwaacha wapinzani washinde/demokrasia itawale ili wawapumbaze waamini sasa Tume inatenda haki chini ya Mama Samia,halafu waje wawageuzie kibao kwenye uchaguzi mkuu wa 2025.

Ogopa nyoka na CCM.

Tuendelee kudai Katiba Mpya/Tume Huru ya Uchaguzi
 
Nawaunga mkono.

CCM ni ile ile na Tume ni ile ile huku Mama akiwa bado kazungukwa na watu wenye mentalily za Magu.

We unatakaje?
Yan tuache kufanya mambo ya msingi tuwe busy kutaka kuwaridhisha chadema?

Wakina mnyika na Mbowe walikuwa wabunge kwa tume gani?

Mbona kipindi huko hawakugomea?
 
Hata wakishiriki watagalagazwa tu kama walivyogalagazwa mwenyekiti wao na makamu mwenyekiti ktk uchaguzi mkuu uliyofanyika mwaka jana. Ikiwa mwenyekiti aligalagazwa ni nani mungine anaweza kushinda nafasi ya ubunge ktk chama chao. Big up chadema kwa kusoma alama za nyakati
 
We unatakaje?
Yan tuache kufanya mambo ya msingi tuwe busy kutaka kuwaridhisha chadema?

Wakina mnyika na Mbowe walikuwa wabunge kwa tume gani?

Mbona kipindi huko hawakugomea?
Halafu mnashangaa kwanini watu wanafurahia watu wengine wanapopatwa na matatizo kumbe kisa ni kauli na matendo yenu na ya viongozi wenu
 
Nawaunga mkono.

CCM ni ile ile na Tume ni ile ile huku Mama akiwa bado kazungukwa na watu wenye mentalily za Magu.

Kingine:Katika hizi chaguzi ndogo, wanaweza kuwaacha wapinzani washinde/demokrasia itawale ili wawapumbaze waamini sasa Tume inatenda haki chini ya Mama Samia,halafu waje wawageuzie kibao kwenye uchaguzi mkuu wa 2025.

Ogopa nyoka na CCM.
Hatutashiri
 
Chademwa watazame upande mwingine, wakati wao wakisusa wengine wanashiriki hivyo kama kuna picha mbaya inaondoka kwa wapinzani wachache.
 
Nawapongeza sana kwa kuona mbali. Maana wangeambulia Aibu ingine kubwa sana. Wananchi watapiga kura za kumuhenzi Rais Magufuli Kipenzi chao.

Na swaga za tumeibiwa kura zisinge wasaidia wazee wa sinema hawa.

Napenda tu kuwaambia waachane na siasa maana Ndugu yetu Magufuli Ametupandia mbegu ya Uzalendo na hatudanganyiki tena na sinema zao.

CCM imezidi kuwa imara na ndio chama chenye nia yakweli ya kutuletea Watanzania maendeleo.

Leo tuichague chadema nchi iuzwe kwa Mabeberu? Maana Viongozi wote wamekimbilia Ubeberuni wametuacha kwenye mataa.
 
Back
Top Bottom