CHADEMA wamebanwa katikati ya 'A rock and a hard place'

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,282
12,818
Yaani wakisimama nshale, wakikaa nshale.

Inaonekana CDM wanaoptions mbili kubwa. Maandamano au maridhiano. Zote ni options ngumu kwao zenye nafasi ndogo sana ya kufanikiwa.

1. Watu hawawezi kuandamana kama hujawapa sababu ya kufanya hivyo. Waanzania hawaandamani si sababu ni waoga, bali hawajaona sababu ya kuandamana. Mkulima Lindi hajui chochote kuhusu habari ya katiba mpya na faida zake hadi aiandamanie, lakini anaweza kuandamana akiambiwa ataacha kupunjwa bei ya Korosho. So, CHADEMA katika harakati zao hawawezi itisha maandamano yakafanikiwa kwa sababau hawajawapa watu sababu ya kuandamana nao.

2. Maridhiano, huwezi kuridhiana na mwenye nguvu. Kwanza atakupa terms mbovu. Na hata mkifikia makubaliano na wote mkaridhika, kesho tu anabadilika na kuachana nayo akiona hayamfaidishi na huna cha kumfanya. Mtu dhaifu na mwenye nguvu hawawezi kuridhiana, hasa kama maridhiano hayo yanaweza mpunguzia nguvu zake.

Nashauri warudi mezani, wachunguze hatua zao waone wapi walipoteza nguvu ya umma waliyowahi kuwa nayo hapo zamani. Nguvu ya wananchi ndiyo itawasaidia kwenye maridhiano na maandamano. Bila hiyo, katika options walizo nazo hakuna itakayofanikiwa.
 
CHADEMA kwenye hayo maongezi ya kinafiki. CCM wanabadilika kila uchwao na wao Wana serikali wakiamua kwenda kinyume na majadiliano utawafanyaje?.
 
Naona wengi mnailaumu Chadema bila kushauri nini kifanyike. Walipokaza wameshukiwa na mabavu ya vyombo vya dola wengi kupoteza maisha,kuishia jela na wengine kubaki vilema.Hizi lawama ambazo haziji na plan B maana yake vyama vingi vife ibaki CCM tu ituburuze.
 
CDM ni walamba asali tu. CCM ipo vizuri licha ya upungufu mdogo ilionao, acha iendelee kutawala.
 
Naona wengi mnailaumu Chadema bila kushauri nini kifanyike. Walipokaza wameshukiwa na mabavu ya vyombo vya dola wengi kupoteza maisha,kuishia jela na wengine kubaki vilema.Hizi lawama ambazo haziji na plan B maana yake vyama vingi vife ibaki CCM tu ituburuze.
Inamaana hujaona ushauri?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom