CHADEMA waingia mtegoni kirahisi, itawagharimu

Wanabodi,

Kama mlivyoona reaction ya viongozi wengi wa CHADEMA kutokana na mkutano wa viongozi wa dini pale ikulu na mkuu wa nchi. Zimetumika lugha za ajabu kidogo kubeza viongozi wale kwasababu tu hawakusema waliyotaka wasikie.

Naomba nitoe tahadhari kwa CHADEMA na hasa baraza la wazee. Mnatakiwa mrudishe nidhamu ya matamko yanayoweza kukichafua chama. Acheni mashabiki na wanamtandao waseme wanayotaka lakini viongozi wa chama lazima kuwe na utaratibu wa kutoa maoni ambao utakuwa msimamo rasmi wa chama bila kwenda kinyume na sera, itakadi na katiba yake.

Mchango wa viongozi wa dini kwa upinzani na hasa CHADEMA ni mkubwa mno. Msikubali mihemuko ya baadhi ya viongozi kuwafarakanisha. Tukio kama lile la ikulu si la viongozi kukurupuka na matusi huko twita bila kwanza kukutana na kujadili na kupata azimio la pamoja ambalo lina hekima na misingi ya kuheshimu mawazo ya wengine kama CHADEMA inavyopenda kuhubiri.

CHADEMA hakuna tena nidhamu kama zamani ambapo tulipata misimamo ya chama kwa utaratibu kupitia Tumaini Makene, Katibu mkuu na viongozi wengine lakini kwa utaratibu.

Naona viongozi wa CHADEMA wasio wakristo wamekuwa na hekima kwa kukaa kimya kuheshimu viongozi wao wa imani na kuwaacha wenzao wa kikristo wakiwakosea adabu viongozi wao.

Baraza la wazee CHADEMA jadilini mrudishe nidhamu kabla hawa vijana wenye mihemuko hawajafarakanisha chama na kila taasisi.

Sasa kupitia uzi huu ndio mtajua kati ya JPM na CHADEMA nani asiyependa kukosolewa. #uhuruwamawazo #practicewhatyoupreach

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi hawa vijana waliojaa kwenye mitandao ya kijamii wakiporomosha matusi ya nguoni kwa watu wanaokosoa CCM na serikali yake huku wakiisifia CCM na serikali ndio msimamo wa CCM na serikali yake kuporomosha matusi ya nguoni ama?! labda sijakuelewa vizuri unachomaanisha ndugu.
 
Ilikufa cuf uliwahi kusikia ccm au mwanaccm anaishi maisha mazur au uchumi wetu umeupita wa marekani? Unafaidika na nini?
faida na furaha yangu ni kuona chadema kinafutika kwenye uso wa siasa za Tanzania kwa sababu wababaishaji wengi,that's it.
 
Sasa huo ufisadi magufuli anaopambana nao umesababishwa na chadema wababaishaji hili taifa lina wajinga wengi sana
 
Wanabodi,

Kama mlivyoona reaction ya viongozi wengi wa CHADEMA kutokana na mkutano wa viongozi wa dini pale ikulu na mkuu wa nchi. Zimetumika lugha za ajabu kidogo kubeza viongozi wale kwasababu tu hawakusema waliyotaka wasikie.

Naomba nitoe tahadhari kwa CHADEMA na hasa baraza la wazee. Mnatakiwa mrudishe nidhamu ya matamko yanayoweza kukichafua chama. Acheni mashabiki na wanamtandao waseme wanayotaka lakini viongozi wa chama lazima kuwe na utaratibu wa kutoa maoni ambao utakuwa msimamo rasmi wa chama bila kwenda kinyume na sera, itakadi na katiba yake.

Mchango wa viongozi wa dini kwa upinzani na hasa CHADEMA ni mkubwa mno. Msikubali mihemuko ya baadhi ya viongozi kuwafarakanisha. Tukio kama lile la ikulu si la viongozi kukurupuka na matusi huko twita bila kwanza kukutana na kujadili na kupata azimio la pamoja ambalo lina hekima na misingi ya kuheshimu mawazo ya wengine kama CHADEMA inavyopenda kuhubiri.

CHADEMA hakuna tena nidhamu kama zamani ambapo tulipata misimamo ya chama kwa utaratibu kupitia Tumaini Makene, Katibu mkuu na viongozi wengine lakini kwa utaratibu.

Naona viongozi wa CHADEMA wasio wakristo wamekuwa na hekima kwa kukaa kimya kuheshimu viongozi wao wa imani na kuwaacha wenzao wa kikristo wakiwakosea adabu viongozi wao.

Baraza la wazee CHADEMA jadilini mrudishe nidhamu kabla hawa vijana wenye mihemuko hawajafarakanisha chama na kila taasisi.

Sasa kupitia uzi huu ndio mtajua kati ya JPM na CHADEMA nani asiyependa kukosolewa. #uhuruwamawazo #practicewhatyoupreach

Sent using Jamii Forums mobile app
Tangu Mbowe aende Jela, nidham imeshuka chadema.
Kila mtu ni muongeaji
 
Hivi hawa vijana waliojaa kwenye mitandao ya kijamii wakiporomosha matusi ya nguoni kwa watu wanaokosoa CCM na serikali yake huku wakiisifia CCM na serikali ndio msimamo wa CCM na serikali yake kuporomosha matusi ya nguoni ama?! labda sijakuelewa vizuri unachomaanisha ndugu.
Hujanielewa mkuu, nisome tena

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulipotoka Waraka wa KKKT na TEC vijana wa CCM mliwatukana viongozi wa dini matusi ya nguoni leo mnajifanya eti wema kwao kama sio unafiki ni nini.

Subirini waraka wa pasaka utoke akili ndipo zitakapowarudi.
Nasimama upande wako mkuu
 
Waraka wa pasaka ya mwaka huu utauona, utasifia na kuunga mkono jitihada pamoja na maombi tele na baraka

Back
Top Bottom