CHADEMA waanzishe na kumiliki News Media zao

Mi nadhani hoja imeungwa mkono, sasa tuangalie utekelezaji, tumeshaongea vya kutosha. Humu ndani namuona dada Regina, mbunge, viongozi wengine CDM kama wapo wayafanyie kazi haya ya kuanzisha mfuko, mimi binafsi niko tayari si tu nkuchanga bali kuhamasisha wadau kufanya hivyo pia.

Mh Regina njooni na utaratibu pliiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiz, tuanze hata kesho. cdm hatutaki kusikia mmeshindwa kufanya jambo kwa sababu ya fedha, wachangiaji tupo.

Ningependa kusikia toka kwa viongozi.


PIPOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOZ!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Mie naitwa potokaz nachangia buku ! isaidie familia yako kwanza iko hali mbaya
 
Wakati watu wanaongea mambo ya msingi kuhusu ukombozi wewe unaongelea ushoga. hakika pesa za nape zitawapa ujauzito hata mkitumiwa kwa nyuma.

safi sana. Mi nilitaka kumjibu nikaona naikimbilia ban kwa escaping velocity
 
Mie naitwa potokaz nachangia buku ! isaidie familia yako kwanza iko hali mbaya

wamekaa kulia njaa halafu wanakuja na stori za mchango, hapa kuna dili ninaunganishwa. Chapombe anachekelea tu saizi.
 
Mod uunganisha ile thread ya "Hii ni Kwa wanachadema tu" na hii maana ni kitu kimoja.
 
halafu wawekeze kwa mabalozi.ccm hawalipi mabalozi.chadema ianzishe sera ya kulipa mabalozi.hiyo ita leta ushindani ndani ya vijiji kwani walio wengi watajitokeza kugombea kwa upande wa chadema tofauti na sasa ambapo ubalozi ni wito.hali ya kufanya kampeni za kupata nafasi ya ubalozi vijijini itasaidia kuitangaza chadema.mia
Mkuu hapo umenena!
 
we uliotoa wazo sikuzote kwanini usitoe inamaana mlikuwa hamjui kama CDM NA CUF, NCCR NA UDP hawana nguvu vijijini. Kama ulikuwa huna taarifa vyama hivi vyote hata TLP vijulikana huku vijijini kama huamini tembelea kijijini kama hutapata wajumbe na wenyeviti wa serikali za mitaa hasa Wa CUF niwengi sana tu tembelea uone. Sasa aanzisheni huo mchango sisi tu bwie au tuongeze mitaji ktk makampuni yetu kwa sisi vidagaa huo mchango utatusaidia hata kwenye vikao pombe kwa sana kama zitakuwa nyingi tutaingiza kwa bilcans group. Hata twaweza kuiboost free media kwa kuwahonga wana habari wazidi kutupamba CDM. Kumbe chini kuna tundu.
 
Mi ni mwanachama wa CHADEMA lakini hili la kuchangia siwezi fanya labda nione effort za kupeleka chama vijijini then nitachangia tena kijijini kwetu,


sababu ni hii,

chama kinapokea mamilion ya shilingi na zinaishia kugawana wao kwa wao ndani ya chama badala ya kuweka matawi vijijini afu mnaanza kusema tuchangie, anzisheni mfuko wa kuwasaidia wasio jiweza hapo ndo tutafanya jambo.


watu wengine hata jf wameshindwa kuchangia hata buku 5 sasa hivi ndo wanaanzisha sred ya kuchangia chama, HUU NI UNAFKI. mi nikirudi bongo ntachangia jf na kuchangia wasio jiweza yaani wale wasio weza fanya kazi wakaingiza kipato but not chama.


I hop mmnenisoma.
 
Ni hoja nzuri sana ila kabla ya kwenda vijijini kuwe na mkakati mahususi wa kufungua Matawi Mijini especially katika miji mikuu ya Wilaya na mikoa w
Maana hao wanaosema ni wapenzi au mashabiki wachama hawajulikani katika maeneo yao,wengi ni macoward kujionyesha na kutoa mawazo yao,ni wakati wa kujua kwamba pamoja na katiba kutokidhi matakwa ya wananchi kwa ajili ya kuwa na chaguzi huru bado inakupa wewe mwananchi haki ya kushiriki katika kutoa mawazo yako na ushiriki katika vyama mbalimbali.

Vipi kuhusu takwimu za majimbo ya mjini kuwa ya chadema kama kweli tunakubalika? vipi kuhusu madiwani? Ni lazima tuweke mtandao wa uhakika kwa wenye uwelewa ili sumu isambae vijijini.

Shalom!
 
Makao Makuu CHADEMA, tunaomba mwongo juu ya utekelezaji wa haraka wa wazo hili zuri kutoka kwa mfurukutwa wetu mojawapo. Katika hili tayari nimeikea mapendekezo yako tiki na ninasubiri to indiketa ya kila kitu kuanza mara moja.

Ndugu wana JF

wote mnajua kuwa CDM inakubalika mijini zaidi kwa sababu zifuatazo
1.mjini kuna wasomi wengi ambao ni wepesi wa kuchambua mambo
2. upatikanaji wa Vyombo vya habari vingi
3.Kampeni nyingi huwa zinaishia mijini hasa kwa sababu ya ufinyu wa budget

Ili CDM iweze kuchukua dola 2015 in wazi kuwa ni lazima iweke mkakati wa kwenda vijijini kwa muda huu ili kiweze kuweka mizizi huko kama ilivyo kwa CCM. Kazi hii ni ngumu na inaitaji fedha nyingi.
Napendekeza uongozi wa CDM waanzishe mfuko maalumu ambao wanachama na watanzania wote wenye mapenzi mema na wanaopenda kulikomboa taifa hill 2015 wachangie ili kufanikisha CDM kuenea vijijini. Pia mfuko huo uwezeshe CDM kuanzisha TV na Radio yake ili kiweze kunadi sera zake zaidi. katika kurahisisha uchangiaji utaratibu wa M-Pesa, Tigo pesa nk, etc utakua mzuri sana kutumika.

nawasilisha
 
wazo lako nzuri kabisa, kwani CDM ikiweza kupata mabalozi wa shina kama ilivyokua wakati wa nyerere yani kila nyumba kumi ikawa na balozi mwanachama wa chadema tunaweza kuongeza wanachama kama ifuatavyo, Tanzania inakadiriwa kuwa na watu 45million, hii ni sawa na kaya million 9 kwa wastani wa watu watano katika kila kaya, that means kaya kumi zikitoa balozi mmoja ina maana tutakua na mabalozi 900,000 nchi nzima. hizo ni kura 900,000, bado wake zao au waume zao marafiki nk. Hivyo hinyo ngazi ya kijiji, kata, tarafa n,k tukiwa na safu za uongozi ngazi zote hizo utajikuta tuna wanachama wakutosha kuibwaga CCM

pumbaaaaaaaaaaaaa tupu
 
Nilishawahi kuongelea hili jambo hapa ila watu hawakulitilia maanani. Ni jambo zuri kwa hoja zifuatazo:
Ili nchi iendelee kunahitajika ushindani wa itikadi za kisiasa, na ushindani wa kisiasa ndio unaowazindua wanaojisahau katika utumishi wa umma kuwajibika.

Wingi wa vyama vya siasa sio ukuzaji demokrasi, bali tunahitaji vyama viwili vyenye nguvu ili kujenga nguvu za kiitikadi kama ilivyo CCM kutetea wenye nacho na Chadema kutetea wafanyakazi na wakulima.

CCM ina vyombo vya habari walivyovitaifisha kutoka vyombo vya umma kama gazeti la uhuru na mzalendo, na kuwa na Radio Uhuru. Chadema nao kwa kuwa ndicho chama kinachoinukia na kukubalika zaidi na umma na kupokeleka kutokana na kutetea maslahi ya taifa na wananchi, chama hiki kinahitaji kuwa na vyombo vya habari vya kujitangaza na kuwa huru kueleza sera na itikadi zake ili kuleta ufanisi katika jitihada zao za kuelimisha umma elimu ya uraia.

Binafsi nimefurahishwa na ushindani wa uchaguzi ilivyotokea Igunga, ni ishara ya kukua zaidi demokrasi na sasa Chadema wanatakiwa kujizatiti zaidi katika nyanja za media communication ili kuwe na ushindani wenye kuwiana na CCM.
 
Hizo pesa si mchange kwa ajili ya maendeleo ya watu vijijini na si kwa ajili ya kutafutia madaraka?
 
Ndugu wana JF

wote mnajua kuwa CDM inakubalika mijini zaidi kwa sababu zifuatazo
1.mjini kuna wasomi wengi ambao ni wepesi wa kuchambua mambo
2. upatikanaji wa Vyombo vya habari vingi
3.Kampeni nyingi huwa zinaishia mijini hasa kwa sababu ya ufinyu wa budget

Ili CDM iweze kuchukua dola 2015 in wazi kuwa ni lazima iweke mkakati wa kwenda vijijini kwa muda huu ili kiweze kuweka mizizi huko kama ilivyo kwa CCM. Kazi hii ni ngumu na inaitaji fedha nyingi.
Napendekeza uongozi wa CDM waanzishe mfuko maalumu ambao wanachama na watanzania wote wenye mapenzi mema na wanaopenda kulikomboa taifa hill 2015 wachangie ili kufanikisha CDM kuenea vijijini. Pia mfuko huo uwezeshe CDM kuanzisha TV na Radio yake ili kiweze kunadi sera zake zaidi. katika kurahisisha uchangiaji utaratibu wa M-Pesa, Tigo pesa nk, etc utakua mzuri sana kutumika.

nawasilisha

Wazo lako limeenda shule kama wewe mwenyewe. Kwanza naunga mkono ila nna maswali..hiyo tv au radio tutegemee ipewe leseni na mamlaka zetu au
Wenzetu wa kule shamba wanasikiliza radio kupata miziki na udaku sio wengi wanafuatilia kwa nia ya kujua nchi inaendeshwa kivipi..
Kwa maana hiyo mi naona mtaji mkubwa wa mageuzi ni sisi wenyewe kuchukua jukumu na kuwa na mazoea ya kuwatembelea ndugu zetu na kuwapa elimu kwanza kisha mawazo mengine itakuwa ni rahisi kufuata..
Ni mawazo tangy
 
CHADEMA 'THINK-TANK' MAKAO MAKUU HUSIKENI MOJA KWA MOJA NA MAWAZO YETU SISI WENYE CHAMA CHETU ILI KUNAWIRISHA ZAIDI AZMA YETU YA KUWAKABIDHINI DOLA 2015.

Tulia mtoto DubiousBrain, acha kupiga mayowe bure hapo chini!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Wana-CDM msihangaike naye sana huyu kwani kila soko kuna kichaa wake na sisi hapa JF tunao wendawazimu 9 ambao mmoja wao ni huyu na yule Nape. Twende nao hivo hivo maana nao wana haki ya maoni hata kama ni upupu.

Wewe mtani DubiousBrain, sasa naanza na SERIOUS BUSINESS kwa wana-CDM, kwako wewe subiri kidogo utaona utamu wa chama kupendwa; hakuna kugasi wafanyabiashara kupitia siasa za TRA bali hapa ni sisi wenyewe wananchi ndio tunakiomba CHADEMA tukichangie kwa ajili ya kupatikana vituo vya kweli vya televisheni ya TAIFA pamoja na radio.

Kuendeleza elimu ya uraia kote nchini hasa vijijini maana CCM huwa wamewekeza zaidi katika umbumbumbu wetu wananchi.

Na kwa kuwa tumegundua siri kubwa ya CCM ni kutumia mabalozi wa nyumba kumi kama nguzo kuu ya KUCHAKACHUA KURA kama walivyokamatwa wakifanya kule Igunga, lengo letu vijana sasa ligeukie kunyakua viti vya utawala vyote vijijini vikiwa ni pamoja na kiti cha:


1. Mwenyekiti wa Kijiji,

2. Kiti cha Udiwani,

3. Kiti cha Balozi wa Nyumba Kumi

4. Mashina ya Chama katika kila kata na kijiji (kuwepo watu wa kuhiari kutumikia chama na wa wa kuhiari kufadhili uendeshaji wa ofisi husika).

5. Benchi la Matawi ya CDM katika vyuo vikuu kote nchini.

6. Kuwaomba wenzetu walioko huko ughaibuni nao kufungua matawi huko huko.

7. Matawi yanayoratibu Maendeleo ya akina Mama CHADEMA vijijini.

8. Kubadilisha haraka USIMAMIZI WA UCHAGUZI usifanywe na wakurugenzi wa halmashauri za miji ambao siku zote makada wa CCM, badala ya kazi ifanywe na taasisi huru kabisa kama vile NGO.

9. CHADEMA kianzishe mfumo wa kepembua vijana maalum (Young Turks - wasichana kwa wavulana) katika ngzi ya kila Kata na waandaliwe vizuri sana kuwa MA-KADA watarajiwa wa chama n waunganishwe ndani ya BAVICHA.

10. Mawasiliano rasmi nazisizo rasmi kati ya makao makuu ya chama na mashina na vyombo vyote vya CDM bila kusubiri ha siku za uchaguzi tu.

Da Regia, ni vema kutumike teknolojia za kisasa zaidi, zenye tija zaidi, haraka zaidi, na yenye kuleta uwepo wa maafisa wa juu CDM kuwa karibu zaidi na waongozwa mashinani. Kwani tujue kwamba kujenga mtandao mzito kama hivi sasa CDM ni jambo moja na kulihudumia huo mtandao kuendeleza uhai wake ni jambo lingine kabisa.

Mpaka leo hii kila mmoja anaju ni mchangu muhimu kiasi gani kilichofanywa na viongozi wetu BAVICHA kule Igunga - kweli BAVICHA ni mashine kubwa mnooo!!!!!!!!!!!!!!!

Huu ndio wakati mwafaka wa kukipa CHADEMA nguvu kweli kweli ILI KIENDELEE KUPAA zaidi na zaidi. Hakika maeneo hayo saba yakitekelezwa vizuri basi nawahakikishieni kwamba watu tutaona moto mkubwa ajabu wa mabadiliko nchini. Siku zote vita bila mikakati endelevu ni kazi bure twende sasa!!!!!!!!!!!!

NB: kwa kuwa umemaliza kusoma mawazo yetu haya hapa hebu sasa malizi kwa kusema maneno haya hapa:

'MABADILIKO YA KWELI NCHINI KUPITIA CHADEMA SIKU ZOTE YANAANZA NA MIMI NA NI JUKUMU LANGU KUWA SEHEMU NA CHACHU WA MABADILIKO HAYO NINAYOYATAMANI.'

Craaaap baada ya pesa yote kuimaliza igunga chama akaunti zake zote zipo nyeupeee ! msiwe mnaingia kwenye vitu msivyo viweza. Ushauri wangu sasa ni huu, ni bora chama kisiwe kinashiriki hizi chaguzi ndogo ili hiyo pesa itumike kuimarisha chama vijijini. Kama hili la igunga pesa mmepoteza na hamkupata kitu km mlivyotarajia
 
Washabiki wote wa CDM ni majobless sasa hizo hela zitatoka wapi? Bora mfateni RA awasaidie.
Mtumwa wa mawazo utamjua tuu,we unadhani kwa vile JK na chama chake mnalamba miguu ya RA unaona hiyo ni fahari
 
Back
Top Bottom