Ni jambo lililo wazi kuwa watanzania tumebadilika sana kimitazamo na kuwa forums zilizopo na hasa TV na radio kwa mtazamo wangu zinashindwa kukidhi kiwango cha upevu wa kimawazo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Ukiangalia TV karibu zote TZ na hata radio zetu nyingi zina muelekeo wa entertainment zaidi na kama ni siasa basi ni za kiwango cha uelewa wa chini sana na au ushabiki ambao unakosa uhalisia wa mambo hivyo kutengeneza ombwe katika nyanja hii.
Ukiangalia kwa mfano radio zetu za FM ambazo nilitegemea zingekuwa na coverage kubwa sana ya siasa na uchumi, nyingi zina vijana ambao elimu na uelewa wao ni wa chini sana (si nia yangu kudharau) na hivyo hata mazungumzo ni ya level ya chini sana.
Kenya kwa mfano FM radio stations kama Capital FM, zina vijana waliosoma degree ya Mass Communication na hata vyuo vikuu vingine na hivyo kuwa na mijadala yenye mantiki, ya kisomi na yenye kuvutia hasa.
Sasa ili tuweze kukidhi haja ya wasikilizaji wengi wanaopenda indepth discussions katika nyanya muhimu nashauri CHADEMA tuwe na mkakati wa kuongeza visibility yetu na pia kushiriki katika kuwapa elimu ya uraia wananchi wetu kwa kuanzisha TV station na Radio.
Nna imani vijana wengi wasomi watapata ajira na wengi tutapata nafasi ya kushiriki, kusikiliza na kuangalia vipindi vyenye mitazamo ya kimaendeleo kuliko ilivyo sasa.
Naomba kuwasilisha.
========
Oktoba 05, 2011

Agosti 27, 2012Ndugu wana JF
Wote mnajua kuwa CDM inakubalika mijini zaidi kwa sababu zifuatazo:
1. Mjini kuna wasomi wengi ambao ni wepesi wa kuchambua mambo
2. Upatikanaji wa Vyombo vya habari vingi
3. Kampeni nyingi huwa zinaishia mijini hasa kwa sababu ya ufinyu wa budget
Ili CDM iweze kuchukua dola 2015 in wazi kuwa ni lazima iweke mkakati wa kwenda vijijini kwa muda huu ili kiweze kuweka mizizi huko kama ilivyo kwa CCM. Kazi hii ni ngumu na inaitaji fedha nyingi.
Napendekeza uongozi wa CHADEMA waanzishe mfuko maalumu ambao wanachama na watanzania wote wenye mapenzi mema na wanaopenda kulikomboa taifa hill 2015 wachangie ili kufanikisha CHADEMA kuenea vijijini. Pia mfuko huo uwezeshe CHADEMA kuanzisha TV na Radio yake ili kiweze kunadi sera zake zaidi. Katika kurahisisha uchangiaji utaratibu wa M-Pesa, Tigo pesa nk, etc utakua mzuri sana kutumika.
Nawasilisha
Oktoba 11, 2012Ndg wana JF napata taabu kuona CHADEMA chama kikuu cha upinzani nchini, chama tarajiwa kuongoza serikali mwaka 2015, chama chenye mikakati ya uhakika na viongozi makini na shupavu lakini hakina hata chombo kimoja cha habari ktk kurahisisha upatikanaji wa habari za chama na taarifa mbalimali.
Hivi ktk vuguvugu hili la M4C vyombo vya habari kama gazeti, radio au hata televion si ingetufaa kabisa! Nguvu ya umma tuko tayari kuchangia ktk kuanzisha na kuendesha vyombo hivyo au labda kama TCRA watakuwa wametunyima vibari kwa maelekezo ya CCM.
Naomba kufahamishwa kwanini hatuweki nguvu ktk kumiliki vyombo vya habari sie kama chama?
Naomba kuwasilisha.
Wakuu, nadhani kila mtu anaelewa na kutambua umuhimu wa CHADEMA kuwa na television na radio yake hasa katika kipindi hiki cha kuelekea 2015.
Tunajua namna vyombo vya habari vya CCM vinavyoeneza propaganda chafu dhidi ya vyama vya upinzani hususani CHADEMA.
Uwepo wa CHADEMA TV na Radio utarahisisha sana kueneza sera na taarifa mbalimbali zinazoihusu CHADEMA kwa wananchi hususani wale waliopo vijijini ambapo chama hakijaenea sana. Naamini kabisa muda unaofaa kuanzishwa kwa vyombo hivi ni sasa na wala sio kesho.
Je CHADEMA hawalitambui hili?