CHADEMA vunjeni UKAWA

Unaweza kuyataja hayo majimbo mkuu, ili na sisi tupate mwanga.

mfano majimbo ya bukoba mjini. shinyanga mjini. kibaha. Igunga kt marudio. iyo ni mifano tu.
For sure bila ukawa Tutarudi kule kule. naamini nguvu pia mziki wa ukawa ccm kwaheri. Jaman bila ukawa basi maccm yatatesa tena sana bila shaka
 
Kisendi

Mimi nilidhani lengo la Chadema ni kuchukuwa dola kumbe lengo ni kushinda majimbo mengi kuongeza ruzuku.

Kumbe Chadema mnaichukilia Zanzibar kama Mkoa siyo daah!!!

Salum Mwalimu umewasikia jamaa zako lakini wanasema Zanzibar ni mkoa.
 
Last edited by a moderator:
Kisendi

CUF inakubalika Tanga Mjini tu na sio Tanga nzima.Kusema CHADEMA itakosa kura Tanga ni ufinyu wa fikra.Tanga kuna majimbo kumi na mbili.

Tukisema CHADEMA inakubalika Arusha akili zote zinapelekwa Arusha Mjini,tunasahau Monduli na Ngorongoro ambapo CCM inatamba.
 
Last edited by a moderator:
Segerea Mpendazoe alikosa kwasababu Wapinzani waligawana kura. i.e Jumla ya kura za Wapinzani zilikuwa zaidi ya CCM. Tarime CDM walikosa lakini kura za CDM + CUF zilikuwa zaidi ya CCM. The same scenerio kwa majimbo mengine. Je, nini kinachokufanya uamini kwamba 2015 hali kama hiyo haitatokea tena?

Lakini pia, lengo kuu la UKAWA ni kumuondoa mkoloni mweusi CCM madarakani, sio CDM kupata viti vingi vya ubunge. CDM ime sacrifice hayo kwa masilahi mapana ya Watanzania.

Bobuk umeongea vyema.
 
Mi lalamiko langu sio mgao wa majimbo bali ni wana UKAWA wengine kutokuwekeza majimboni,vijana wao wapo ofisini tu,wazee kama Prof.Lipumba na Dr.Slaa kutwa kuwatafutia kura
 
Kinachosikitisha ni baadhi ya vyama kung'ang'ania majimbo ambayo hawajawekeza kabisa. Wakati CHADEMA wanafanya mikutano na kuhamasisha wananchi kujiandikisha, wao wapo majumbani kwao tu.

Hatuwezi kuota kwenda ikulu huku wenzetu wamekaa tu na hiyo nia dalili ya kugawa majimbo bure kabisa kwa CCM.
Huu umoja ni muhimu, lakini chadema wameungana na vyama dhaifu vilivyo jichokea, mi nashangaa chama kama NCCR kinavyojitutumua uraisi, wakati ina wabunge wanne tu. Na vyote havijafanya harakati zozote za kuhamasisha, wapo maofisini tu wanasoma magazeti wanasubiri chadema wafanye mikutano nchi nzima bila kulala. Ngoja tuwabebe mwaka huu tuone out come yake
 
Kwa majimbo kama segerea, ukonga, kigamboni, Serengeti, morogoro mjini na kilosa chadema ina nguvu Sana ukilinganisha na vyama vingine ndani ya ukawa...mi naona Ni bora hayo majimbo vyama vingine vikakubari kugawana hayo mengine yaliyobaki..
 
United we stand divide we fall
kwa kweli,mleta uzi ana pointi ya msingi sana lakini ngoja tu tuseme kuwa un apoungana unasacrifce baadhi ya tunu zako.kwa mafano jimbo la serengeti,katibu mkuu wa nccr mh.mosena nyambabe analing'ang'ania lakini ukiangalia,nccr haina hazina yoyote ktk hilo jimbo,haina hata ofisi moja ya tawi jimbo zima.

Na huyu mh.amekuwa akigombea ktk hili jimbo miaka nenda rudi lkn hajawahi kuwa tishio kwa ccm hata siku moja.leo hii cdm imeimarika serengeti,viongozi wa cdm vitongoji,vijiji na kata kila kona ya jimbo,vijana wa boda boda pale stendi ya mugumu mjini kila wakilala wakiamka ni cdm leo unaenda kuwambia eti nccr ambayo hata hawajawahi kuujua huo msamiati hapo kabla.
 
Huu umoja ni muhimu, lakini chadema wameungana na vyama dhaifu vilivyo jichokea, mi nashangaa chama kama NCCR kinavyojitutumua uraisi, wakati ina wabunge wanne tu. Na vyote havijafanya harakati zozote za kuhamasisha, wapo maofisini tu wanasoma magazeti wanasubiri chadema wafanye mikutano nchi nzima bila kulala. Ngoja tuwabebe mwaka huu tuone out come yake

Kama NCCR na CUF ni vyama DHAIFU, hebu nitajie hivyo vyama VYENYE NGUVU ambavyo ungependa CDM iungane navyo?

Inaelekea napoteza muda wangu kumjibu mtu ambaye has no iota of political landscape of Tanzania.
 
SAMAHANI ZANZIBAR SIO MKOA....mistypo

Nadhani Chadema wawape tu hayo majimbo halafu baadaye tutafanya analysisi tuone peefomance imekuwaje. Sidhani km ni busara sasa hivi kufanya jambo lolote la kuwakatisha tamaa wananchi. Huu muunguno ni mtego tumeingia kosa moja tu tutahaeibu kila kitu.

Huwez kuvunja ukawa kipibdi sensitive hiki. Itakuwa suicidal. Turapoteza majimbo mengi sana! Tumekuwa tukigawaba sana kura na kuwaidisha ccm. Na mtoa mada hili halielewi kabisa!
 
Kama NCCR na CUF ni vyama DHAIFU, hebu nitajie hivyo vyama VYENYE NGUVU ambavyo ungependa CDM iungane navyo?

Inaelekea napoteza muda wangu kumjibu mtu ambaye has no iota of political landscape of Tanzania.

CUF sio chama dhaifu kama wanavyodhani chadema, mwaka huu kitawashangaza sana wao.
 
Kusema kweli nilitamani kushuhudia muungano kati ya CUF na CHADEMA, ungekuwa bora zaidi.Sasa hawa NCCR-Mageuzi nao dah.Halafu wanayang'ang'ania yale majimbo ambayo CHADEMA wana nguvu na ushawishi kwasababu ya uwekezaji mkubwa walioufanya huko.Hawataki kwenda maeneo mengine ambayo vyama vingine havina nguvu na ushawishi ili nacho kikajenge huko.

Kina njia ya mkato,kwakweli CHADEMA wawe makini maamuzi yoyote yatakayolenga kuwanyima nafasi nafasi watu ambao walitumia rasilimali zao binafsi,juhudi na muda wao kujenga ngome huko majimboni kisha kuwapa watu wengine ambao hawakushiriki kufanya harakati zozote huko kwa mgongo wa UKAWA,hawa watu wanaweza kwenda ACT na kushinda au kusababisha kura kugawanyika na kutoa mwanya CCM kushinda kirahisi.
 
Mleta mada ana hoja ya msingi lakini sikubaliani na hitimisho lake kwamba ufumbuzi wa sintofahamu hii ni kuvunja UKAWA.Ukweli wa mambo ni kwamba CHADEMA wamefanya uwekezaji mkubwa kote nchini tangu mwaka 2010.Sasa katika hatua hii ya mgawanyo wa majimbo na kata hali halisi ni lazima izingatiwe.Itakuwa ni upuuzi ku sacrifice jimbo lolote eti kwa kigezo tu cha kutaka kuridhisha chama mshirika.Kigezo kikuu cha ni chama gani kisimamishe mgombea mahali flani itakuwa ni kukubalika kwa chama husika na si vinginevyo.Kwa mfano jimbo la segerea sote tunajua ni kiasi gani CHADEMA wamewekeza vilivyo leo hii ukilitoa jimbo hili kwa CUF au NCCR itakuwa ni kulitoa sadaka kwa CCM.
 
Sayansi ya siasa au Political Science ndiyo muanzisha uzi anafanya. Kutaka kujenga mazingira yote kuonyesha kuwa Kuna mtafaruku au aanzishe mtafaruku.

UKAWA imejipanga hachonganishiki mtu. Lengo kuu la UKAWA ni kuwaondoa wakoloni hawa weusi.
 
Back
Top Bottom