Tumekuwa na mihemko na hasira muda mrefu na vitu vilivyokkuwa vikitoke kwenye chama chetu, sasa naona ni muda muafaka kumsamehe huyu bwana na tusonge mbele. Shibuda huwa tunakuwa tumemsamehe kabla hata hajasema kitu wala hajafanya kitu, mimi kwa mapendekezo yagu naona hata Zitto asamehewe hata kabla hajawaza kitu!
Tumsamehe tuu pamoja na kauwa sidhani kama atakuwa tayari kuomba msamaha, Tumsamehe na tujenge chama kwa upya kwa spidi isiyo ya kawaida.
Mkuu hili sio sahihi mfano mdogo tu.
1. Kikwete nimewasamehe wezi wa rada - wezi wa kuku wanafungwa
2. CCM magamba hayajavuliwa wamesameheana kimya kimya
Maswali
1. kama zito atasamehewa nini itakuwa tofauti ya cdm na ccm
2. Kama zito atasamehewa je nini nafasi ya wale akina shonza na wenzake
3. Je kumsamehe zito kunaashiria nini hapo baadae?
a. uwezo wa kufanya maamuzi magumu na kuyasimamia
b. Ubutu na udhaifu wa kufanya maamuzi magumu na kutoweza yasimamia?
Zito lazima afukuzwe na kunyang'anywa uanachama kabisa ilikujenga discpline, na kufanya maamuzi ambayo
watanzania wengi wanayataraji kwa afya ya Taifa kwa ujumla wake. Kugeuka nyuma cdm itakuwa jiwe la chumnvi