CHADEMA Sumbawanga Mjini yakanusha upotoshaji uliofanywa na Stella Manyanya na CCM mkoa wa Rukwa

USHAURI>
Naomba ufanye yafuatayo kama wewe kweli ni kiongozi wa Wanasumbawanga na kuwa unapenda CDM iendelee kuwa rohoni mwa jamii hiyo:-

1. Ita vyombo vya Habari vyote vya hapo Sumbawanga, waeleze ukweli kama ulivyoeleza humu ndani ya JF
2. Kama UNAUHAKIKA na USHAHIDI wa hayo aliyoyatenda Bw Shayo akiwa CDM yamwage hadharani ili watu wajue kuwa hajafanya kosa kujiunga na CCM maanake, amerudi kundini kwa wenzake
3. Hebu waeleze wanasumbawanga waelewe makosa ambayo CCM inayafanya ya kufanya sherehe ya kumkaribisha mtu mmoja ktk chama kwa pesa za Watanzania. Najua CCM haina pesa itakua imechukua pesa aidha toka Halmashauri au Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kufanya ujinga huo. Fedha hizo ni za Wananchi WOTE bila kujali itikadi.
4. Mkuu wa Mkoa huyo Mama, anafanya makosa (najua yeye ni kada wa CCM) lakini angetenda mambo ya kiserikali zaidi kwa ajili ya Sumbawanga na hiyo kazi akamwachia M/kiti wa CCM wilaya manake hata M/kiti CCM Mkoa ni mkubwa hatakiwi kwenda kumpokea huyo NYANG'AU!

Kwaheri kwa sasa.[/QUOT

Big up mkuu, nakuunga mkono 100%

Mkuu sahizi viongozi wa BAVICHA wilaya Ya Sumbawanga wako live Sumbawanga tv wakijibu shutuma na kukanusha upotoshaji uliofanywa pamoja na mengine mtangazaji anawahoji pia hoja nyingine za kitaifa zikiwepo za maandamano. Nadhani sasa utakubaliana na mimi kuwa ushauri unafanyiwa kazi na wanasumbawanga wanapiga simu na kupongeza kukanusha upotoshaji
 
Kweli CCM Wamechoka Kufikiri!! Hata MWIZI ANAFANYIWA SHEREHE YA MAPOKEZI!! KWELI UKOMBOZI UPO KARIBU SANA
 
Mkuu sahizi viongozi wa BAVICHA wilaya Ya Sumbawanga wako live Sumbawanga tv wakijibu shutuma na kukanusha upotoshaji uliofanywa pamoja na mengine mtangazaji anawahoji pia hoja nyingine za kitaifa zikiwepo za maandamano. Nadhani sasa utakubaliana na mimi kuwa ushauri unafanyiwa kazi na wanasumbawanga wanapiga simu na kupongeza kukanusha upotoshaji


Asante mkuu kwa updates! Hiyo ndo njia sahihii ya kuumbua huo upotoshaji uliofanywa na ccm na watendaji wa serikali kwa kutumia rasilimali zitokanazo na kodi zetu!
Endelea kutujuza yanayojiri baada ya uongo wao kutengwa na ukweli!
 
Safi sana.......mapinduzi yataanzia kwa watanzania wanaonyanyasika na kukosa huduma muhimu. Kwa sasa watanzania wanaelewa kuwa si kwamba nchi ni maskini bali ni ufisadi wa CCM. Wananchi ikataeni ccm.
 
magamba kwa sasa hawana jipya sumbawanga, kilichobaki ni propaganda tu na kuendekeza majungu wakiwadanganya wananchi kwa propaganda zao. huyo fisadi shayo mwache tu aende huko huko kwa mafisadi wenzie
 
Kama ni kweli hii kitu imekuwa kete nzuri kwa wana CDM-Swanga. Na mbaya zaidi wamem corner arac bila yeye kujijua. Hali ya kisiasa haiko upande wa sisiem kiviile, You will tell me... Ntarudi siku hii sakata ikianza kuwagharimu sisiem.
 
Nimegunduaa kuwa unaweza kitapeli ccm hela za kufa mtu iwapo tu utajitangaza kuwa wewe ulikuwa mwanachadema na sasa unajiunga na ccm, hata mimi ninakampango ka kwenda kufanya uhuni huu ccm ila naomba ushauri wenu wanajf niende nikajitangaze nilikuwa kiongozi gani chadema ili wanifanyie sherehe kubwa kuliko ya Shayo
 
Back
Top Bottom