CHADEMA sasa Tishio GEITA

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
MIKUTANO ya vuguvugu la mabadiliko (M4C) inayoongozwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), imetikisa Jimbo la Busanda, wilayani Geita, mkoani Geita, baada ya wanachama 18,670 wakiwamo wazee na makada wa siku nyingi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutimkia CHADEMA.
Mbali na kuzoa maelfu ya wanachama, pia chama hicho kimeunda uongozi kwa kuteua wenyeviti, makatibu, na wahazini wa chama kwenye kila kata zilizokuwa hazina uongozi ngazi ya tawi.
Viongozi waliosimikwa ni wenyeviti, makatibu, wenezi na wahazini wa matawi pamoja na wale wa jumuiya mbalimbali za chama hicho hususan wazee (BAWAWACHA), Vijana (BAVICHA) na Wanawake (BAWACHA), lengo likiwa ni kukiimarisha chama kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara yake kwenye jimbo hilo juzi, Kiongozi wa M4C mkoani Geita, Alphonce Mawazo, alisema wana CCM waliojiunga na chama hicho ni kutoka kata 13 kati ya 16 za jimbo hilo.
Alisema kati yao 11,235 ni wanachama wapya na 7,435 ni waliovua gamba na kuvaa gwanda, ili kuhakikisha CHADEMA kinaibwaga CCM kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na kuingia Ikulu.
Aliwataja miongoni mwa wazee na makada wa siku nyingi wa CCM waliorudisha kadi za CCM ni Thereza Lugembe (79) mkazi wa Kijiji cha Nyabulolo, Kwando Maduhu (109) mkazi wa Kijiji cha Nyarugusu na Shija Mihambo (87) mkazi wa Bugogo Bukoli ambaye alikuwa mwanachama wa CCM tangu Julai 7, mwaka 1979 kwa kadi namba C.812836.
“Kazi hii si ndogo…tunapambana na chama ambacho kina mizizi kila kona…tumezoea kuona vijana ndio wanajiunga na CHADEMA…lakini unapoona wazee nao wameanza kukimbia ujue saa ya ukombozi imekaribia,” alisema Mawazo.

Source:Tanzania Daima
 
CHADEMA wanatembeza kipigo cha mbwa mwizi kwa ccm bila huruma........................

Tanzania ya 2015 itakuwa hivi:
178901_218352028281589_1224983986_n.jpg
R.I.P. My dear CCM
attachment.php
 
chadema ni kama moto wa petrol hauzimiki kirahisi sana. Kila la heri makamanda kandamizeni vya ukweli wakuu. Mawazo big up, bananga twende kazi.
 
Turufu ya mwisho waliyo nayo ccm kwa sasa juu ya kuzimisha moto wa M4C ni kumtumia Tendwa kuifuta CHADEMA! Vinginevyo ccm hawana ubavu wa kuuzimisha moto wa M4C ndani ya Magwanda.
 
MIKUTANO ya vuguvugu la mabadiliko (M4C) inayoongozwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), imetikisa Jimbo la Busanda, wilayani Geita, mkoani Geita, baada ya wanachama 18,670 wakiwamo wazee na makada wa siku nyingi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutimkia CHADEMA.
Mbali na kuzoa maelfu ya wanachama, pia chama hicho kimeunda uongozi kwa kuteua wenyeviti, makatibu, na wahazini wa chama kwenye kila kata zilizokuwa hazina uongozi ngazi ya tawi.
Viongozi waliosimikwa ni wenyeviti, makatibu, wenezi na wahazini wa matawi pamoja na wale wa jumuiya mbalimbali za chama hicho hususan wazee (BAWAWACHA), Vijana (BAVICHA) na Wanawake (BAWACHA), lengo likiwa ni kukiimarisha chama kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara yake kwenye jimbo hilo juzi, Kiongozi wa M4C mkoani Geita, Alphonce Mawazo, alisema wana CCM waliojiunga na chama hicho ni kutoka kata 13 kati ya 16 za jimbo hilo.
Alisema kati yao 11,235 ni wanachama wapya na 7,435 ni waliovua gamba na kuvaa gwanda, ili kuhakikisha CHADEMA kinaibwaga CCM kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na kuingia Ikulu.
Aliwataja miongoni mwa wazee na makada wa siku nyingi wa CCM waliorudisha kadi za CCM ni Thereza Lugembe (79) mkazi wa Kijiji cha Nyabulolo, Kwando Maduhu (109) mkazi wa Kijiji cha Nyarugusu na Shija Mihambo (87) mkazi wa Bugogo Bukoli ambaye alikuwa mwanachama wa CCM tangu Julai 7, mwaka 1979 kwa kadi namba C.812836.
"Kazi hii si ndogo…tunapambana na chama ambacho kina mizizi kila kona…tumezoea kuona vijana ndio wanajiunga na CHADEMA…lakini unapoona wazee nao wameanza kukimbia ujue saa ya ukombozi imekaribia," alisema Mawazo.

Source:Tanzania Daima
Duh, naona wamekula chumvi nyingi hapo wamekubali mabadiliko, CCM should leave the country silencely.
 
Back
Top Bottom