CHADEMA rekebisheni tatizo hili kwenye kipengele cha Dua/Sala za kufungua mikutano na kufunga

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,505
51,101
Mikutano yenu huwa mnaianza kwa sala. Hilo ni jambo zuri sana. Maana mnamtanguliza Mwenyezi Mungu mbele.

Lakini wakati mkianza kwa sala, Wale ambao huwa mnawaita kufanya sala kwa niaba ya Wakiristo huwa ni watu ambao kwa namna moja huwa ni watu wenye authority katika taasisi zao za imani, wanaelewa protokali za maombi, yaani ni profeshno. Huwa ama ni wachungaji, mapadri au hata maaskofu.

Lakini inapokuja katika Kuomba dua kwa niaba ya waislamu, huwa ni kama hamjajiandaa kwa nukta hiyo ya mkutano, huwa mnakurupuka na kuita yeyote bora liende.

Matokeo yake, Huyo mtu anakuja kuomba vitu ambavyo kwa mujibu wa Imani ya kiislamu ni makosa makubwa sana, tena makosa yanayokulazimu kutubu baada ya kufanya hayo.

Kwa mfano Juzi katika mkutano wenu pale Bulyaga, mlimuita Askofu Mwamakula kuombea mkutano. Huyo ni profeshno , ana hekima zake, na anajua aombe nini.

Ilipokuja muda wa Muislamu kuomba dua, Mkajichukulia kamanda tu aliyevaa kombati za chama, Dua yake anachanganya maombi, Wakati mwingine anamuomba Mungu na wakati huohuo anamuomba Mtume. Kwenye Uislamu kumuomba Mtume ni kosa kubwa sana. Anayepaswa kuombwa ni Mwenyezi Mungu tu.

Na pia mambo anayoomba mengine ni mabaya, yamekaa kisiasa, hayaendani na hekima za maombi ya Waislamu yaliyofundishwa na mtume.

Sasa vitu kama hivi vinafanya Waislamu waone chama chenu ni Insensitive kwa Imani yao. Kwamba chama hakichukui muda kuwapa heshima stahiki kama ambavyo kinafanya kwa wakiristo. Na hivyo bila kujua kujikuta kinaingia katika mtego wa Propaganda kinaotengenezewa na mahasimu wao wa kisiasa yaani CCM.

Nafahamu, CHADEMA ni taasisi ya kisiasa na si kidini. Ila pale mtakapoamua kuinvolve watu wa dini basi pelekeni watu wanaostahiki kutoka pande hizo.Siyo upande mmoja unamleta baba mchungaji aombe dua, halafu upande wa pili unafanya zimamoto ilimradi bora liende.

Hili tatizo nimelishuhudia katika mikutano yenu mingi huko mikoani, Hamjajiandaa vizuri kwenye nukta ya waomba dua kwa niaba ya Waislamu. Huwa mnafanya tia maji tia maji. Sasa hii inawaput off Waislamu vibaya sana.

Rekebisheni hii kitu, mnaweza kudhani siyo issue ila nakuhakikishieni ni issue kubwa kwa waislamu nchini wanaofuatilia mikutano yenu.
 
Maoni yangu juu ya hili, CHADEMA waachane moja kwa moja na huu unafiki ulioanzishwa na CCM; waachane kabisa na mambo ya dini katika siasa.

Huu ni unafiki mtupu, hakuna la zaidi ya hapo.

Acha watu waombe kwa Mungu wao wanayemwamini majumbani mwao na kwenye nyumba zao za ibada.

Huyu Mungu wa maonyesho katika matamasha ya siasa ni utapeli mtupu.

Mungu anayeipenda Tanzania, hana makundi ya watu wenye kuhimiza tofauti zao kwa Mungu huyo huyo mmoja anayeipenda nchi yao na watu wake wote.
 
Basi ni kweli nakumbuka Ile 2015 nlienda kwenye kampeni zao (ndo last time ) wakamuita muhuni mmoja alivaa kanzu alipewa Mic ila arap
Alivomaliza wakasema wafungue mkutano kwa maombi
Mc; Chadema hata maostaz tunao
Ostaz njoo utupe dua

Jamaa hata suratul fatiha hakuweza kuimaliza akachanganya na salam assalam aleikum wakaitikia amin
 
CHADEMA wawe neutral bila kuhusisha dini. Kwa hali ilivyo wanazidi kujichafua na kuwapa wasiwasi watu wa imani zingine kwamba CHADEMA wakishika madaraka itakuwaje? Wapige siasa kama siasa. Au waamue CHADEMA iwe taasisi ya kidini kwasababu tayari wana Nabii Lema.
Upotofu wanaouiga toka CCM ni kuwa waTanzania watakipenda chama kwa kuwa karibu na dini yao. Huu ni ujinga.

WaTanzania watapenda chama kinachofanya shughuli zake kwa haki kwa kila mtu bila ya upendeleo unaohusisha tofauti za kidini au tofauti nyingine zozote.

CHADEMA wamefanya kila juhudi kuvuta waislam ndani ya chama chao kwa mafanikio hafifu sana, na ndio maana wanaokoteza yeyote aliye karibu kuwa kama mvuto kwa wengine.

Hii siyo njia sahihi. Waondokane na kujiweka karibu na dini yoyote ile, anayependa wanayosimamia aingie kama mTanzania yeyote bila kujali anasali wapi.
 
Basi ni kweli nakumbuka Ile 2015 nlienda kwenye kampeni zao (ndo last time ) wakamuita muhuni mmoja alivaa kanzu alipewa Mic ila arap
Alivomaliza wakasema wafungue mkutano kwa maombi
Mc; Chadema hata maostaz tunao
Ostaz njoo utupe dua

Jamaa hata suratul fatiha hakuweza kuimaliza akachanganya na salam assalam aleikum wakaitikia amin
Kumbe huwa mnawafuatilia kwa umakini Ila kinyemela?🤔
 
Mikutano yenu huwa mnaianza kwa sala. Hilo ni jambo zuri sana. Maana mnamtanguliza Mwenyezi Mungu mbele.

Lakini wakati mkianza kwa sala, Wale ambao huwa mnawaita kufanya sala kwa niaba ya Wakiristo huwa ni watu ambao kwa namna moja huwa ni watu wenye...
Chadema haina mamlaka ya kuamua nani ni muislamu wa kweli na nani wa uongo, pia mashehe wengi hujipendekeza CCM ili wajengewe misikiti na kupewa hela za kwenda Hija, na hili hutokana na waumini kutotaka kutoa sadaka stahiki na jata wakitoa misikiti haina mifumo ya kitaasisi kwenye utunzaji wa pesa na mali za misikiti.

Waislamu wajipange waache kuendesha mambo kiholela kwani hata kwenye maziko tunashuhudia mtu yeyote anaazima kanzu na barakhashia kisha anaongoza sala!
 
Mama samia alipoanzisha salamu kwa jina la jamhuri watu walimbeza mama aliona mbali. Dini na siasa havichangamani
Alifanya jambo jema.
Maana unakuta kiongozi labda muislam anasimama anasema tumsifu yesu kristu, huo ni unafiki wa hali ya juu.
Au mkristu aseme salam aleykum yaani unaona kabisa haikutoka moyoni.
 
Chadema haina mamlaka ya kuamua nani ni muislamu wa kweli na nani wa uongo, pia mashehe wengi hujipendekeza CCM ili wajengewe misikiti na kupewa hela za kwenda Hija...
Hata kama ulisemalo lingekuwa ni kweli, unfortunately kisiasa lina consequences.

Sasa chama makini inabidi kilifanyie kazi, kisijenge barrier kwa watu wengi au la kishupaze shingo kwa hoja kama ulizotoa kiendelee kuwa marginalised .
 
Au mkristu aseme salam aleykum yaani unaona kabisa haikutoka moyoni.
Hakuna ubaya wowote kwa Mkristo kutamka salama leko, hayo ni maneno ya Nabii Issa mwenyewe yenye kumaanisha Amani iwe nawe kwa lugha ya Kiarabu. Japo Yesu ni Myahudi, ila alikulia nchi ya Misri barani Afrika hadi alipotimiza miaka 30, hivyo lugha yake ni Kiarabu!.
P
 
Hoja ipi! Kwa waislamu mtu yeyote anaweza kuongoza sala mradi awe muislamu.
Hata kwa Wakristo mtu yoyote anaweza kuongoza sala, hoja ya mleta mada ni hoja ya msingi sana, maandalizi!. Mtoa dua wa upande mmoja anaandaliwa analetwa mtu mwenye darja, upande wa pili ni anafanywa kuokotwa!. Mleta mada anawatakia mema Chadema ili mlivue lile koti lenu la...
P
 
Back
Top Bottom