CHADEMA, punguzeni minyukano mjenge chama

Lukolo

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
5,143
3,196
Ukifuatilia kwa karibu mijadala inayoendelea ndani na nje ya Jamii forums, utagundua kwamba ndani ya CHADEMA hakupo shwari. Nimeona mara kadhaa Miss parliament na Marytina wakiamua kujifanya Polisi na mahakama wenyewe na kuwashutumu wenzao, kuwarushia maneno makali na kuwaonya waache tabia kadha wa kadha.

Lakini kuna jambo linanifikirisha hapa, hiki chama ni kichanga, na kinapitia changamoto ya kupoteza wanachama wake wengi ambao wanaamua kurudi CCM, wakati huu kinahitaji mshikamano zaidi wa wanachama na viongozi wake kwa ajili ya kujijenga badala ya kila mmoja ndani ya chama kumuona mwenzake ndiyo mbaya au yeye ndiyo bora kumshinda mwingine. Ni kawaida kwamba wakati wa uchaguzi huwa zinajitokeza tofauti, lakini mnatakiwa mzizike tofauti hizi mara tu baada ya uchaguzi kuisha. Habari za bavicha, viti maalumu, sijui kamati kuu nk, hivi sasa zimeshapita, hakuna kitakachobadilika tena. Sasa tugeukie kwenye kujenga chama.

Inawezekana ni kweli kwamba kundi la akina Ben na Zitto lina shida, na inawezekana kwamba zimeshindwa kutatulika katika njia ya kawaida, lakini ni sahihi kuja kuanika mapungufu ya chama hapa JF? Nakumbuka jana Gaijin alipendekeza kwamba CHADEMA wafanye seminar elekezi kwa viongozi na wabunge wake juu ya maadili na miiko ya uongozi. Mimi pia naungana naye, maana kama mambo yataachwa yaendelee hivi basi kuna hatari ya hiki chama kufa badala ya kustawi.

Kumbukeni hii minyukano ndiyo iliyoiua NCCR mageuzi (Chief Mkwawa alisema juzi), na pia hii minyukano ndiyo inayoimaliza CCM hivi sasa. Kama CHADEMA hamtakaa chini mziangalie tofauti zenu kwa jicho pana, basi 2015 tutakuwa na chama kingine kikuu cha upinzani bungeni.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom