CHADEMA pelekeni hoja binafsi kuomba vote of no confidence!

Lukolo

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
5,143
3,196
Tangu jana nasikiliza bunge nikitarajia CHADEMA watafikia hatua ya kutoa tamko la kupeleka hoja binafsi inayomtaka Kikwete ajiuzulu, badala yake naona wanaendeleza tu siasa, na kutoa kauli ambazo zinaruhusu mhusika ajifanyies self assessment. Hapa ilitakiwa CHADEMA watumie lungu la wabunge wengi kuipinga serikali, kama tiketi yao ya kuiondoa serikali madarakani. sasa wanalalamika tu, na hawafikii uamuzi.
 
pigeni kura wabunge ya kutokuwa na imani na serekali mtupe urahisi zanzibar kuchukua chetu.....nchi gani hii wizi mtupu kila pahali. na litote tugawane mbao
 
pigeni kura wabunge ya kutokuwa na imani na serekali mtupe urahisi zanzibar kuchukua chetu.....nchi gani hii wizi mtupu kila pahali. na litote tugawane mbao
Haha, sema ipigwe kura ya kutokuwa na imani na Rais, pamoja na kutokuwa na imani na muungano.
 
Ahsante kwa ushauri wako wa kizalendo,ila ukweli wake ni kuwa wabunge wa ccm hawatakubali,asilimia kubwa ya wabunge wa ccm wanategemea siasa na mfumo mzima wa ccm ulikuwa sio kuwatumikia wananchi ila ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi ili wafanye mambo yao ya kudhalilisha wananchi na kuwafanyia utumwa,hivi wanavyoongea ni sababu wameona kama chadema kinaweza shinda 2015 sasa watakosa ulaji,mfa maji hakosi kutapatapa!
Ila ni vizuri chadema wapeleke hoja binafsi ya vote of no confidence,ili hata ccm ikiwageuka wao watapata nguvu ya wananchi na maandalizi mema ya kuchukua nchi 2015.

CHADEMA walianzishe liungwe mkono na wabunge wote

Hii motion ni muhimu ikawepo, hata kama wabunge wa CCM watapiga kura ya kuwa na imani na serikali. Strategically ni suala zuri kwani upepo wake utawafikia viongozi serikalini na wapiga kura majimboni wataingiwa na imani kuwa serikali inaweza kuwajibishwa kwa matakwa yao pale ambapo watawachagua wabunge watakaosimamia maslahi yao ni si ya vyama vyao
 
Ahsante kwa ushauri wako wa kizalendo,ila ukweli wake ni kuwa wabunge wa ccm hawatakubali,asilimia kubwa ya wabunge wa ccm wanategemea siasa na mfumo mzima wa ccm ulikuwa sio kuwatumikia wananchi ila ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi ili wafanye mambo yao ya kudhalilisha wananchi na kuwafanyia utumwa,hivi wanavyoongea ni sababu wameona kama chadema kinaweza shinda 2015 sasa watakosa ulaji,mfa maji hakosi kutapatapa!
Ila ni vizuri chadema wapeleke hoja binafsi ya vote of no confidence,ili hata ccm ikiwageuka wao watapata nguvu ya wananchi na maandalizi mema ya kuchukua nchi 2015.

Uko sawa kabisa mkuu. Hapa ndo patakuwa ni mahali pazuri pa kujua nani mnafiki na nani yupo kwa interest za wananchi. Chadema wao wapeleke hoja binafsi bungeni kuitaka serikali iondoke halafu tuone hao wabunge wengine watareact vipi. Kulingana na jinsi hali ya maisha ilivyo ngumu nawahakikishieni, wananchi wote watakuwa nyuma ya CHADEMA, iwapo itaamua kuchukua uamuzi huo.
 
Naunga mkono hoja kwa 100%, hili litakuwa somo zuri kwa watawala wetu!! Lakini ni nani atakayethubutu kufanya hayo? Si CDM wala si CCM bado tuna zile siasa za kuoneana aibu.
 
CHADEMA walianzishe liungwe mkono na wabunge wote
Haswa na hata kama wabunge wengine hawataunga mkono, angalau itaonekana kwamba katika historia ya siasa za tanzania chadema wamethubutu. Na wananchi watawaona chadema wapo serious zaidi na kile wanachokipigania. Lakini kama wataendelea kupiga kelele bila kuchukua hatua wataonekana hawana tofauti na CCM.
 
Chadema wahakikishe wanapeleka hiyo hoja haraka iwezekanavyo maana hata CCM sasa hivi wanatambia wingi wao tu bungeni lakini wanafahamu kabisa wanaoungwa mkono na wananchi walio wengi ni chadema hivyo itabidi na wabunge wa ccm japo najua hawatakuwa wote wataunga mkono hoja hiyo. Na chadema watambue kuwa 2015 ni lazima wachukue nchi hivyo ni wakati wao wa kuanza kuiwajibisha serekali iliyoko madarakani ili wakute nchi iko wangalau kwenye mwelekeo hiyo 2015
 
Naunga mkono hoja kwa 100%, hili litakuwa somo zuri kwa watawala wetu!! Lakini ni nani atakayethubutu kufanya hayo? Si CDM wala si CCM bado tuna zile siasa za kuoneana aibu.
Hapa ndipo ambapo busara inahitajika sana kwa CHADEMA. Wao ni wapinzani, wanamwonea aibu nani. kama kweli nia yao ni utumishi kwa umma na si nafasi zao za ubunge basi wajitose kupeleka hoja hii. Watachukiwa na viongozi lakini wataungwa mkono na jamii. Hii ni karata mhimu sana kwa CHADEMA hivi sasa.
 
Tangu jana nasikiliza bunge nikitarajia CHADEMA watafikia hatua ya kutoa tamko la kupeleka hoja binafsi inayomtaka Kikwete ajiuzulu, badala yake naona wanaendeleza tu siasa, na kutoa kauli ambazo zinaruhusu mhusika ajifanyies self assessment. Hapa ilitakiwa CHADEMA watumie lungu la wabunge wengi kuipinga serikali, kama tiketi yao ya kuiondoa serikali madarakani. sasa wanalalamika tu, na hawafikii uamuzi.

lukolo,
wenye uwezo wa kufanya hivyo ni wabunge wa ccm sbb wako wengi kuliko wa cdm. nadhani hadi hoja hiyo ikubaliwe na bunge inahitaji theluthi mbili ya wabunge wakubali. ccm wako zaidi ya theluthi mbili bungeni. ila hizo guts za kufanya hivyo hawana.
 
Naunga mkno hoja, sina imani na serikali iliyopo madarakani akiwemo rais waziri mkuu na mawaziri kwa ujumla. Niwazi wapo madarakani kwa manufaa yao na si kwaajili ya taifa hili na vizazi vijavyo.

Japo wabunge CCM wataungana kuhakikisha hawaiachi serikali ianguke lakini ujumbe wa haki na utawala bora utawafikia wananchi na wezi watarajiwa wanaweza kuacha nia yao mbaya.

Ustawi wa nchi na mabadiliko yapo mikononi mwa watakao dhubutu. Nani adhubutu kwa sasa kama sio wabunge wa CDM?
 
Kupeleka hoja bungeni si lazima ikubalike, mwisho wa siku nadhani itakuwa juu ya kamati husika kufanya mamauzi.

Lakini iwapo Chadema itafikia hatua hiyo itakuwa ni alama nzuri ya kuonesha kukomaa kwa demokrasia hapa nchini.
 
Wazo lako ni la msingi sana mdau.hata hivyo naamin hata wao wamekwisha liona lakin naamin hawa jamaa ni watu makini sana na kabla hawajafanya jambo wanashauriana.labda kuna kitu wanakipanga ili kizae matunda mazuri zaidi.kwanza mpaka hapo wenyewe kwa wenyewe ccm wamegawanyika na wameonekana live wacha waumane kwanza wakubali kwamba wenyewe ni mafisadi kama ilivyojitokeza jana,ili waendelee kuahbika.nakwambia hawana pa kwenda na serikali yao kwa sabab kila kona pameoza.mwenye macho haambiwi tazama.
 
kwa hakika wapinzani na wanaccm bungeni wasikubali siasa za kila siku za serikali kutaka eti kuyafwatilia nasema hivi wakati ni sasa wala si kesho kama tume zimeshaundwa sana riport ya mkaguzi mkuu inatosha kabisa kuwawajibisha watu.
wabunge wawawajibishe na wasisubiri kesho wala kuundwa kwa kamati teule wala tukufu.
iwe fundisho wa walaji wa mali za watanzania huku watanzania hao wakifa na njaa wakikosa maji dawa na miundombinu bora kwa maisha yao na maendeleo ya jamii.
 
na hiki ndio kipimo cha wana ccm kwa jamii kama kweli wapo serious tutaona kama walikuwa wanasema wasikike tutaona jambo lazima lifanyike la muhimu na haraka tumechoka na wizi huu kila leooooooooooooooooo
sasa iwe mwanzo wa uwajibikaji unaoonekana na kueleweka.
shen....................................... zao mafisadi wauwaji hawa
 
Back
Top Bottom