Chadema ni Sauti ya Watanzania.

Gudlucky

Member
Feb 9, 2011
22
1
Ndugu wana JF, naomba nivunje ukimya kwa kusema kuwa, Tanzania ni nchi inayokaliwa na watu wenye macho (hivyo wanaona), wenye masikio (wanasikia) lakini pia wenye uelewa (wanaelewa jema na baya). Ndugu zangu, watanzania si 'robots' hata wasisikie maumivu pindi mambo mabaya yanapo waumiza! Ni muda murefu sasa watanzania wakiwa hawaoni mambo yakienda sawa, sauti za faraja na maneno matamu ya kubembeleza yenye ahadi zisizotekelezwa yamekuwa yakisika masikioni mwao kila mara. Mioyo yao imejawa na uchungu ulotokana na matatizo rukuki hasa ktk eneo la kiuchumi. Wamedanganya kuwa matatizo yataisha tu. Wamesubiri na sasa wamechoka ikiwa ni pamoja na mimi. Sasa tumeelewa, tunataka mabadiriko. Tumefumbua vinywa vyetu kutoa sauti zetu, si sauti za vilio vya kuomba msaada wa magunia ya mahindi, au chandarua, au pengine misaada mbalimbali. HAPANA!!! Tunataka utawala bora utakao badirisha maisha ya kila mtanzania kwa vitendo na si kwa kaulimbiu zisizo tekelezeka. Sauti yetu ni moja tu, nayo ni sauti ya watanzania wote. CHADEMA ndiyo sauti ya watanzania, sauti ya Ukombozi wa watanzania na nchi yao.

Tutasema, tutatafuta haki kwa gharama yoyote mpaka tutakapofikia hatima ya taifa hili. Tunapigania haki ya mtanzania kwa kizazi cha sasa na kijacho!!

People... Power...
Hii ndio sauti yetu watanzania.
 
Back
Top Bottom