CHADEMA na tishio la Tendwa kukifuta Chama kisa Maandamano/M4C

Kauli ya msajili wa vyama John Tendwa ni ya hatari sana serikali inatakiwa ijiepushe na kauli kama hizi. Hizi kauli hazina tofauti na kauli cha uchochezi ambazo zinaweza kusababisha nchi isitawalike. Nawaasa viongozi kama Tendwa wazisome alama za nyakati, watu sasa hivi wameerevuka sio kama zamani za fikra sahihi za mwenyekiti baba wa taifa. Watu hawana woga wa kijingajinga, kama alilijua ana uwezo wa kukifuta chama chochote cha siasa angefanya hivyo mapema kwa sasa amechelewa CDM ik Tendwa kama msajili na mlezi wa nyama vya siasa ana uchaguzi huu tu... ama aendelee kukilinda CCM ambacho kinakufa na ni sawa na kiegemea nguzo ya mpapai siku ikianguka atanguka nayo au akatae kufanywa mjinga kwa kujiuzulu nafasi hiyo maana hatakuwa na chakuporeza. namsihi asijaribu kukubali kupakwa damu ya wanyonge na watawala hawa ambao wanaikataa sauti kuu YA UMMA ambayo pia ni SAUTI YA MUNGU
 
Huyu anayejiita 'mlezi' wa vyama vya siasa kisha waandikia CDM barua ngapi za onyo kutokana na vifo anavyosema vilitokea katika mikutano ya CDM? Atafutaje vyama bila mawasiliano ya 'onyo' ya muda mrefu?
 
Kwamba mwanaharakati wa LHRC alisema jambo na kukataa jina lake kutajwa? Naamini ni uongo mkubwa kuliko ule wa Pinda bungeni kuhusu issue za arusha. Sijamuona mwanaharaka wa LHRC muoga hivyo na aliyepwaya hivyo.
Nawafahamu wanaharakati wa LHRC. Hakuna mwoga hata mmoja. Huyo mwandishi wa Daily News ndo mwongo kabisa; Tendwa ni mwana CCM na hategemewi kutetea chama kingine isipokuwa chake. hivi; yeye ni mahakama yenye uwezo wa kutafsiri sheria na kukonclude kuwa kuna uhaini katika harakati za CDM? Tendwa ni feki, period!
 
Sept 07, 2012

TUMEZOEA kumsikia Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa akitoa kauli zenye utata na za kukanganya. Kauli zake mara nyingi huwa kali na hulenga kujenga hofu kwa viongozi wa vyama vya upinzani. Kama tulivyosema hapo juu, kauli zake zimezoeleka kiasi cha walengwa kuzibeza, kuzipuuza na kuziita za kutishia nyau.

Ni kauli ambazo mara nyingi hutolewa kwa kukurupuka na pengine ndiyo maana huwa hazifuatiliwi, kwa maana ya kutekelezwa.

Ni mara ngapi ametoa vitisho vya kufuta usajili wa baadhi ya vyama kwa sababu ya kutoonyesha uhai na kushindwa kufanya kazi za kisiasa kama mikutano ya hadhara, kufungua matawi, kushiriki katika chaguzi, kutafuta wanachama, kufanya maandamano, makongamano na kadhalika? Ni mara ngapi ametoa kauli zenye hisia kali dhidi ya vyama visivyokuwa na ofisi au visivyoitisha mikutano ya wanachama au kuendesha chaguzi kwa njia za kidemokrasia, kwa maana ya kuwaweka au kuwaondoa viongozi madarakani kwa mujibu wa katiba za vyama hivyo?

Kama tulivyosema hapo juu, kauli hizo hubezwa kwa sababu hazifuatiwi na utekelezaji. Ndiyo maana miaka 20 tangu uanzishwe mfumo wa vyama vingi nchini, asilimia kubwa ya vyama vilivyosajiliwa havina ofisi, havifanyi chaguzi za viongozi, kwa maana ya vyama hivyo kuwekwa mifukoni na viongozi kama mali zao binafsi. Vyama hivyo havifanyi kazi za kisiasa, haviko hai na havina wanachama wa kuitwa wanachama. Ni vyama vilivyoanzishwa kwa mategemeo kwamba Serikali ingetoa ruzuku kwa kila chama kilichosajiliwa kwa muda au chenye usajili wa kudumu.

Inawezekana kwamba hutoa kauli kwa hisia kali, tena kupitia vyombo vya habari ili kuonyesha na kuuthibitishia umma na mamlaka iliyomteua kwamba anafanya kazi yake vizuri na kwa ufanisi mkubwa. Lakini pia hufanya hivyo pengine kuonyesha umuhimu wa kuwapo kwa ofisi hiyo ya Msajili wa Vyama vya Siasa. Hicho ni kitu gani kama siyo kuidhalilisha Ofisi ya Msajili?

Kwa njia hiyo, amefanikiwa kuzima kelele za watu ambao wamekuwa wakitoa hoja kwamba msajili huyo hafai kwa kuwa amejidhihirisha kwamba ni ‘simba wa karatasi’ na kwamba ofisi hiyo ifutwe kwa sababu haina manufaa yoyote kwa vyama vya siasa. Yapo madai mengine mengi kuhusu msajili huyo, ikiwa ni pamoja na kusajili vyama mamluki ili kuvidhoofisha vyama makini na kukisaidia chama tawala wakati wa chaguzi mbalimbali.

Hata hivyo, pamoja na msajili huyo kuendeleza kauli zake za vitisho, vyama makini vya kambi ya upinzani vimeshtushwa na kuichukulia kwa uzito mkubwa kauli iliyotolewa juzi na Msajili Tendwa. Wakati wananchi bado wanaomboleza kifo cha Mwandishi Daudi Mwangosi aliyeuawa kikatili na polisi mwishoni mwa wiki mkoani Iringa, msajili huyo alitia chumvi kwenye kidonda alipotishia kuvifuta vyama alivyodai vinakaidi amri ya polisi ya kutofanya mikutano na maandamano, akidai kwamba mikutano hiyo inakuwa na matukio ya vurugu na kusababisha vifo.

Tendwa ambaye amekuwa akitishia kuvifuta vyama visivyofanya kazi za kisiasa kama kufanya mikutano ya hadhara, juzi aligeuza kibao na kutishia kukifuta Chadema, akidai kushangazwa na operesheni zake mikoani wakati huu ambapo hakuna kampeni za uchaguzi. Tendwa yuleyule aliyetishia vyama vilivyokuwa vinasubiri chaguzi ndipo vifanye kazi za kisiasa ndiye yuleyule anayesema sasa hakuna kufanya kazi za kisiasa kama hakuna shughuli za uchaguzi.

Huyo ndiye John Tendwa anayezuia vyama vya upinzani kufanya shughuli za kisiasa kwa kisingizio cha kuwapo Sensa, huku akikaa kimya siyo tu wakati chama tawala kikiendelea na kampeni za uchaguzi katika Jimbo la Bububu, bali pia kikiendelea na mchakato wa uchaguzi wa viongozi wake nchi nzima kwa wagombea wake kuchukua na kurudisha fomu kwa nderemo na bashasha. Huyo ndiye Tendwa aliyesema juzi baada ya mauaji ya Mwandishi Mwangosi kuwa, polisi wanaporusha mabomu hawakusudii kuua watu, isipokuwa hivyo ndivyo vitendea kazi vyao.

Huyo ndiye John Tendwa.

Source: Mwananchi
 
Mhariri umenena vyema; Tendwa ni mbumbu na kibaraka wa CCM! Kama anao uwezo aifute CHADEMA! Maana hilo ndo lengo lao, vyombo vya dola vinashirikiana kusababisha mauji kwenye mikutano ya chadema ili kutafuta sababu ya kuifuta chadema.
 
Huyu hana jipya mwenzake nchimbi alisema alimuuliza Mkama kuhusu mikutano yao lkn kwa slaa alituma vikosi bla kuuliza. Sasa huyu tendwa anajidhalilisha mwenyewe haiwezekani chama alichokisajili yeye kiitwe cha kidini, au kikanda achilia ukabila ilihali alijua. Kipo nchi nzima na bado hajatoa karipio kwa wanadanganya wananchi huyu hajui yupo wapi.
 
Huyu mzee mshirikina huyu. Ni mara nyingi nimemuona katika TV akitoa hizo kauli za kufuta vyama mfu, visivyofanya mikutano n.k.
Leo bila aibu anaibuka na kusema hakuna haja ya mikutano ya kisiasa kwa sababu hakuna uchaguzi.

Ni lazima wahamanike maana plani yao imeshindwa, na siyo kushindwa tu, imewalowesha damu kuliko walivyotarajiwa. Ni lazima wakurupuke na kuongea hata yale ambayo hawakuwa nayo kabisa, lazima wahewuke, maana walitegemea wafungue shampeni kupongezana kutokomeza chadema.
 
Katibu Mkuu wa CHADEMA amemshangaa msajili wa vyama vya siasa Bw. Tendwa kwa kutishia kuvifuta vyama vya siasa ambavyo vinasababisha vifo vya raia na kudai kama ana ubavu huo basi akifute kwanza CCM kwa kuwa polisi wake wamehusika kuwaua raia wengi katika mikutano ya siasa ya vyama vya upinzani!

"Tendwa ni vuvuzela! alidandia mambo asiyoyajua Arumeru na sasa Iringa," amesema Dr. Slaa.

Dr. Slaa amemuelimisha Tendwa kuwa kinachoweza kufuta vyama vya siasa ni sheria na si matakwa yake yeye Tendwa.

Source: Radio One Stereo.

MAONI YANGU: Kama ilivyo kwa mapolisi kujipendekeza kwa watawala ili kupata hisani ya kupandishwa vyeo au kujiwekea mazingira mazuri kujiunga na siasa baada ya kustaafu, Tendwa naye anajitengenezea mazingira ya kuingia katika ulingo wa siasa kupitia CCM!
 
Huyu katibu wa cdm ni janga la kitaifa, si wana kikao kinachotarajiwa kutoa maamuzi na tamko la tendwa litajadiliwa?

hiki chama mbona kila mtu msemaji? Naendelea kutafakari kauli ya 6.
 
Hivi kuna mtu alitegemea kauli ya maana kutoka kwa Bw Tendwa? La hasha! Jamaa hafai kuwa pale basi kwa vile mfumo wetu wa vyama/siasa unapendelea kila kitu CCM. Huwezi kupambana na CCM huku msajiri wa vyama vya siasa ni mteule wa CCM, M/Kiti NEC ni mteule wa CCM, Mahakama na majaji wake ni wateule wa CCM, the list go on!!
 
Ukijiuliza kauli ya WASIRA na hii ya TENDWA unapata picha gani? ati chama kinachoua, inamaana CDM ndo wanaua na sio Polisi sio? Conclusively IT IS A BATTLE AGAINST CDM FROM ALL ANGLES.

If CDM survives this time, They will take over.........
 
Back
Top Bottom