CHADEMA na FALSAFA ZA WAARABU

Acha CDM wapoteze muda wewe jali kazi zako na ujineemeshe. Siku zaja utajua kwa nini CDM walipoteza muda. Na huu utaratibu unaousema wa kupokezana madaraka walipokezana na nani kwa takriban miaka 50?
 
Hili ni tatizo la KULA VYAKULA VYA KUKU WA KISASA!!! Inaonyesha labda umezaliwa mwezi wa kwanza mwaka huu na kwa kula misosi na madawa ya kuku wa kisasa umekuwa haraka mno!!! Hujui Chadema wameanza kwenda lini kwa wananchi wala hujui waarabu wameanza kuangusha serikali zao lini??! Au wewe ndo wale waliozoea kukaririshwa tu bila kujali kama unachokaririshwa ni cha kweli au uongo??? Yaani hujawahi kuona/kusikia/kusoma habari za maandamano dhidi ya serikali ktk nchi zisizo za kiarabu??? Haya ndugu kawaambie wakubwa zako kuwa umepost waliyokukaririsha. si umefurahi eeh?
 
Mwalimu Nyerere aliisha wahukumu wapinzani siku nyingi sana, mnazoona zote hizi vurugu za CDM ni laana ya huyu mzee

Siioni laana ya CHADEMA hapo ila ya CCM inayomkejeli Mwalimu na sera zake kila kukicha. CCM imeshafanya "Kufuru" katika kila fundisho jema la mwalimu. Kwa hakika viongozi wa sasa wa CCM wanamwaibisha Mwalimu kwa kuishi tofauti na mifano yake; hebu tazama, katika maisha yake alijishughulisha sana kuipiga vita Rushwa, lakini viongozi waliomrithi wameikumbatia rushwa kuanzia Rais hadi tarishi, aliwaasa dhidi ya fikra za kibaguzi; sasa tunasikia wenyewe kwa wenyewe, walewale waliokuwa wanafunzi wateule wake wakishutumiana huyu si Mtanzania halisi, huyu si mtu wetu! Na sasa kiranja wa CCM yuko bize kuhamasisha watu kufuata siasa za kidini; analia kuna udini.... udini.... ili apate wajinga wa kumwitikia. Ni Nyerere alilaani ikulu kutumika kama pango la kibiashara, lakini CCM ya sasa ni rasmi ikulu ni pango la biashara za kifisadi na wezi, vibaka, matapeli, majambazi na viruka njia wa kisiasa wana ngome yao ikulu. Enzi za Nyerere kina Chenge, EL, RA, Karamagi na wengine wangeisikia ikulu redioni au kuitazama kwenye video; lakini sasa ndiyo walioshika "hatamu" za uongozi wanaingia na kutoka ikulu wapendavyo. Enzi za Nyerere hata fundi seremala, Mkulima wa kawaida kabisa aliweza kugombea udiwani, ubunge na kuupata bila ya kutumia rushwa, lakini leo hii kila nafasi ya kugombewa ndani au kupitia CCM ina bei yake. Nyerere aliufananisha ubaguzi na mchawi aliyewahi kula nyama za watu ambaye hupata "kiu" ya kuila kila siku; na sasa yametimia. Walianza kubaguana kikabila ndani ya CCM, baadae ki-nchi (Huyu Mwarabu sisi watanzania halisi, huyu Msomali sisi watanzania halisi, sasa wanaimba huyu Mkristo sisi waislamu n.k. Si kosa lao; ni laana ya Mwalimu. Kinachoipata CCM na Kikwete wao sasa ni laana ya Mzee huyu aliyetangulia mbele ya haki. Na bado kuna makubwa zaidi yatawakuta labda watubu na kujirekebisha. Mwisho nasema Bravo CHADEMA. Go CHADEMA Go! Baraka za Nyerere na wazee wote waliopigania nchi yetu waliotutangulia ziwalinde hadi kurudisha hadhi ya nchi yetu na kuikomboa toka makucha ya manyang'au waliokiteka nyara chama alichoasisi Baba wa Taifa.
 
Kufanya maandamano katika vitongozi mbalimbali vya mji wa Mwanza na kisha leo kuhamia Musoma ili kupinga kuongezeka kwa gharama za maisha, malipo ya dowans nk ni kufuata philosophy isiyofahamika. Warabu ni watu makini sana, wao wamefanya maandamano kudai matango tu baada ya miaka mingi ya utawala na hali isiyombaya ya uchumi.
Chadema wanachofanya sasa ni kuiga falsafa ambayo haiwezi kufanya kazi bongo. Tanzania ni nchi iliyojiwekea utaratibu wa kukabidhiana madaraka kila miaka 5.
Nawashauri CDM wasubiri 2015 vinginevyo watapoteza MVUTO.

Ndugu yangu, hizi ni harakati za kisiasa kuwaamsha wananchi wazijue na kuzidai haki zao. Pia, baada ya hayo ni kujijinga kwa kukieneza chama, kupata wanachama na wapenzi wengi zaidi na kuuza sera zao kwa wananchi.

By the way, wakati wanatangaza mpango huu wa maandamano ya nchi nzima, vuguvugu la ARABUNI lilikuwa bado kuanza. Hivyo, labda tuseme kuwa Waraabu walichukua kutoka cdm basi.
 
Charityboy,,,think of your name......
Siasa si uchaguzi tu,siasa ni maisha ya kila siku,ni uchumi,na chadema tunatambua hilo,ni wajibu wa chadema kufanya siasa bila na kupinga upandaji hovyo wa gharama za maisha,ushauri wako ni batili na kamwe chadema hawatakubali....
Chadema hawakurupuki,na wanachofanya ni sahihi bila kujali wewe charityboy utasemaje
ni swala la muda tu
saa ya ukombozi ni sasa

kwanza wewe ni nani katika chadema mpaka unaandika utumbo huo?

Pili kamuulize mzee wako, kuwa maisha ya sasa na ya wakati wao ni sawa? na je kama nawao wangeandamana kupinga mabadiliko yanayotokana na kubadilika kwa nyakati situngekuwa tunaishi kama maisha aliyoishi wazee wetu miaka 70 iliyopita?
Tatu chadema ilipatwa na mtihani mkubwa kuwa wanachama wake wengi ni masela masela yaani watu ambao maadili yao katika jamii ni mabovu, hawa hawawezi kuwa na future na fikira sahihi ya kulinda amani ya nchi, mfano mwepesi piga taswira kwa umakini viongozi wako wa chama wanajishirikisha kwenye maandamano.wabunge wa chadema wenye maadili mazuri na ambao kweli nia zao ni safi hata siku moja hutowaona kwenye maandamano ya slaa ambae anatafuta jinsi ya kutoka baada ya kujikuta aliuziwa mbuzi kwenye gunia.

Mwisho nasema chadema wanakurupuka, kwani hata isue ambazo zinahitaji wao kama viongozi wenu waifate serikali eti wao wanaanza kwa masela.Huyo slaa wakati bunge linavunja mkataba sialikuwepo bungeni? na je si haohao wabunge wa chadema walilikomalia la kuvunja mkataba? ivi walikuwa hawajui madhara ya kuvunja mkataba? slaa aseme wakati bunge linapitisha mswaada wa kuvunja mkataba hakuunga hoja? muwekezaji wa dowans kawekeza kwenye jimbo ambalo mbunge ni wa chadema muulizeni kama alienda kuongea nae DOWANS, au kwenye sera zenu mbunge haruhusiwi kuonanan na muwekezaji aliyewekeza kwenye jombo lake?
 
Back
Top Bottom