CHADEMA MUST now Reform and Restructure!

"

Who is the clever people then? You? me or? Please advice so that we search for that person because i thinkd we need that person more than we have never needed anything before. Tanzania is sinking and yet people are discouraging others who are showing at least some effort to show us the way to go, even if they might have their personal agenda, but so far i will go for them rather than just seat and say "haiwezekani"
:sick:.
we need changes regardless wheather you are ccm or cdm member. Tanzania is regarded as one of the richest nation on earth in terms of natural resources but look at our pace of development when compared to other neughboring leave a lot to be desired.what is requred is completely overhaulong of the governance system of our beloved country.
 
Ni chama cha wachaga aka majambazi.

Duh!
Do you Believe in Democracy or Communocracy?

If the truth were to be told,it's like you lack African Moral values and Intellectual capacity in Discussing issues .
Now people are working against each other and trying to sabotage one another so that this person from this tribe can be in power or that person from that tribe doesn't have the opportunity to steal as opposed to the thief from our tribe.Tuna tatizo kubwa kuliko tunavyofikiria,hata tupate katiba mpya ,kama hatutabadilisha mentality za watu tuna kazi
 
Jeshi na polishi limesha wasoma CDM siku nyingi, CCM haitaleta vurugu Tanzania ni chama cha majambazi ndio kitaleta vurugu, je huoni hao viongozi wenu wanavyo ropoka kwenye mikutano? Narudia tena hiyo lugha yenu nyie viongozi wa CHAMA CHA MAJAMBAZI ndio inawapeleka kwenye virungu.


mnaambiwa muende shule mnang'ang'ania madrasa sasa hayo ndo matatizo yake
 
Kwa mwendo huu wa maandamano wala cdm hamtafika popote.

Swali: mkimaliza kufanya maandamano mikoa yote mtafanya nini ukizingatia ccm haitabadilisha msimamo wake wa kutowajibisha mafisadi. Kwa kuwa kuwawajibisha mafisadi sie wananchi wenye kusoma situation tumeishaona haitawezekana.

Fisadi anawajibishwa kwa kufilisiwa na siyo kufanya maandanao kama chadema. Na natumai ni Rais wa nchi tu ndio anaouwezo wa kuwafilisi hao mafisadi.

Hivyo chadema hizi ni mbio za sakafuni. Ni bora kama kweli mnaipenda tz mngeanza juhudi kuwasemea na kuwaanika kwa vidhibiti mafisadi na kufuatilia vijisenti wanavyoweka mabenki ya huko ulaya na america ili msaidie intel ya kushinikiza kuwafilisi vizuri.

Just to advice u.

And don't think you are the most clever pple to talk for this nation, no, you are just pple who have ambition to shout against CCM and doubtly not for the nation's benefit.

do you know what happened after operation sangara?muulize gamba mkuu atakusimulia!
 
Mpaka sasa katiba inawaruhusu kuongea ovyo ovyo kama hivo.Lakini kwa miondoko hiyo CDM haiwezi kuwaunganisha watanzania, na kwa sababu hiyo ndio maana chadema haiwezi kuingia Ikulu hata kwa miguvu.Siku zote kitu ambacho huwa kinaonekana haraka huwa ni matatizo na si mafanikio.Viongozi wasiokuwa waadilifu wao wenyewe hawawezi kuwa viongozi wasafi.Mtu muovu hawezi kuongoza mapambano ya kuleta Haki hata siku moja
 
mnaambiwa muende shule mnang'ang'ania madrasa sasa hayo ndo matatizo yake

kwahiyo wewe umeenda Shule?!!! Kama mtu aliyeenda shule ana akili kama za kwako basi wewe hukutakiwa kusoma maana akili zako ziko kama za mtu ambaye hajaenda shule. Si kila siku mnasema nyinyi mmesoma na watu wa madrasa hawajasoma sasa imekuwaje? mbona nyinyi ambao hamjapitia madrasa mnaandamana nawakati nyinyi ndio mmeishika nchi? waswahili wasema "Masikini akipata ****** hulia mbwata" which means nyinyi mlijiona mmesoma kumbe ni wajinga tu na haya ndiyo matokeo yake
 
mbowe atakubali kuachia?unajua sometimes namwona mbowe kama anapenda madaraka,anyway tuone watafanyaje manake 2015 ipo karibu kuliko tunavyowaza
 
Wazo zuri sana! sasa umeongea kitu kwani mimi hupenda zaidi kusikia sababu kubwa ya kufanya mabadiliko mnayotahitaji. Lakini pia tukumbuke tu kwamba bungeni hawa watu hukaa sio zaidi ya siku 100 na pale ndipo wananchi wengi hutazama mwelekeo wa chama. Haya tazama JK ni mwenyekiti wa CCM na muda mwingi yuko nje ya nchi sijui labda niseme siku 236 kwa mwaka huwa nje ya nchi na hakika binafsi sikumbuki kabisa toka mwalimu Nyerere kuna mwenyekiti wa CCM ambaye aliongeza au kuongoza ufanisi wa chama hiki ktk ushindi au matokeo ya maagizo yake kwa wananchi, isipokuwa makatibu wakuu ndio wamekuwa chachu ya chama hiki.. Hizi ndio siasa za Bongo hivyo Dr.Slaa ktk nafasi alonayo akipambana na kina Makamba au kinana nadhani hapo kuna raha zaidi. Wananchi hawajali sana mwenyekiti isipokuwa wanachama wenyewe ndio wanajua yupi anaweza kuwashawishi kichama na ktk nafasi gani.


Binafsi niseme ukweli sikupenda Mbowe achukue kiti cha uongozi wa Upinzani bungeni zaidi ya yeye kuendelea kuwa mwenyekiti wa chama kwani kaifanya kazi nzuri sana ndani ya chama. Bungeni kinachotakiwa ni safu wa wabishi kama kina Mkandara hapa maadam unalishwa data za kutosha kuweka pingamizi. Watu wasioogopa na wenye kiburi cha kuulizwa maswali magumu pamoja na kuwakilisha zaidi matakwa ya wananchi. Tukumbuke tu nguvu ya Chadema mwaka huu imetoka bungeni na Dr.Slaa kama msemaji mkubwa ndiye amekuwa kiungo kikubwa zaidi kwa wananchi kupata chachu ya Ufisadi na kadhalika. Sina uhakika kama Mbowe anaweza kuendeleza pale alipoachia Dr.Slaa, lakini nina hakika kwamba kumweka Dr.Slaa kama mwenyekiti kunaweza kuleta matatizo mengine ambayo hayana sababu kabisa kuyaendeleza. Na ukumbuke tu wananchi wanachotazama sio mabadiliko hayo kulingana na picha yako, wao wanayaona matatizo ya Chadema ktk sura mbili za Ukabila na Udini na ndicho pekee Chadema wanatakiwa kuondosha dhana hiyo (watu na Mazingira).

Zakumi,
Mkuu wangu nimepiga makelele sana hapa JF kuhusiana na ubaguzi wa aina yeyote ile lakini ndio kwanza nilikuwa nachochea vitu hivyo. Maadam sisi hatukuzaliwa kwa kupenda kuwa kabila gani basi nasi tusiwapitishe viongozi wetu kwa kufuata vigezo hivyo kwani wajinga wengi hataweza kuona tofauti. Mimi naweza kabisa kukubali Mbowe alikuwa na kila sifa ya kuwa mwenyekiti lakini ni wangapi wanaokubaliana nami?..Hivyo kuna wakati ili kuepuka lawama kama hizi unatakiwa kuchukua maamuzi mazito ambayo hukutaka kuyafanya..
Amini maneno yangu kwamba Chadema ilipofikia leo haihitaji kuendlelea kufikiri kisomi zaidi ktk nchi ya wajinga.. kuna wakati mwingine inabidi nawe uwe mjinga ili upate ku mingle na society unayoiongoza, ukitumia elimu na exposure yako sana mahala hapastahili utaitwa mwizi tu.

Ulinganifu wako na mfumo wa CCM wa kuwa na katibu imara lakini mwenyekiti siyo lazima awe na uthabiti siyo sahihi katika mazingira ya chama chenu hiki. CCM ni chama dola na mfumo huo ni sustainable for as long as bado kinaendelea kushikilia dola. Kwa chama kama Chadema survival yake inategemea sana uimara wa institutions zake, na umahiri wa uongozi wake kujenga institutions zake na kubaki kuwa relevant kwa wananchi. Ni lazima wananchi waji-identify na chama hicho kama kinataka kuwa imara na hufanya hivyo kwa kujua mahitaji ya wananchi na ku-articulate yale matarajio (kwa mfumo wa sera). Haya tumeyajadili jana lakini kama kawaida kukawa na disruptions na hoja ile ikageuzwa kuwa malumbano yasiyo na tija kwani wengi wa wachangiaji ni walevi wa euphoria badala ya kuangalia posterity ya chama na nchi kwa ujumla.

Sina hakika kama mpaka hapa tunapoongea Chadema wamefanya postmortem ya uchaguzi uliopita na kubaini kwa nini mahudhurio ya watu kwenye rallies hayaku-translate into votes na wafanyeje kuhakikisha hilo halijirudii. Inawezekana bado wengi wako busy kujadili kuchakachuliwa kwa matokeo (kama wanavyodai) bila hata kujiuliza kama kweli uchakachuaji ulikuwepo nini kilisababisha na wafanyeje ili sasa lisijirudie. Lakini typical of our opposition parties, wakarukia kwenye agitation ya katiba na kujikita huko bila hata kupata fursa ya tathmini hiyo na bila hata kuwa na mapendekezo ya kile ambacho kingekua ni rasimu ya katiba kwa maoni yao. Hata sasa wanapofanya mikutano yao, huelewi kama lengo la mikutano ni kuwashukuru wananchi (kama Slaa alivyosema Songea), au kuhamasisha wananchi kuchangia katiba (japo hatusikii muongozo wowote kwenye mikutano yao kuhusu namna wananchi wanavyotaka wachangie), au ni kuwaeleza wananchi (alleged) failure ya CCM kuleta maisha bora, au kuwataka wajiandae kumuondoa Kikwete kabla ya 2015 (kama walivyoahidi Songea). Chama kina-bank on euphoria na hasira za wananchi kutokana na kupanda kwa gharama za maisha bila kufanya mipango madhubuti ya kuwapa matumaini ya namna watakavyotatua shida hizo au namna ya ku-take advantage ya mdodoro huu kuwa na mfumo wa enrolment ya wanachama na kutoa elimu ya uraia kwa ujumla.

Kuna hili la reputation binafsi ya baadhi ya viongozi na tuhuma kwamba baadhi ya viongozi wanatumika kuwasafisha watuhumiwa wa ufisadi na hata kupokea vibahasha kama vichocheo vya misimamo yao ndani na nje ya bunge. Haya ni mambo ambayo yamekuwa yakiitia doa CCM na yakibainika kuwepo ndani ya Chadema, watu wataona kwamba wote ni wale wale lakini ikubwa ni kupoteza moral authority ya kukemea maovu yanayotendwa na chama kilichopo madarakani. HATA HIVYO KUJIREKEBISHA KUNAHITAJI KUYAKUBALI KWAMBA MATATIZO HAYA YAPO NA NI KIKWAZO KWA USTAWI AU HESHIMA YA CHAMA NA YANATAKIWA KUREKEBISHWA!
 
mnaambiwa muende shule mnang'ang'ania madrasa sasa hayo ndo matatizo yake

Hii ni kashfa na kuchochea hasira pasipo na sababu. Kwa mchango huu, kweli unaweza kuwaambia watu kwamba wewe umewahi kuliona hata jengo la shule? Hivi hoja huijui mpaka unaanza side issues. Hovyoo!
 
Zitto, Azimio la Arusha is our blue print as Taifa. Tatizo ni kila mtu kuonanisha kushindwa kwetu kujiendesha na hata kukimbilia soko huru kama ndio kigezo ch aAzimio kuwa baya.

Mimi narudi kwenye kule kuwapa Watanzania nguvu na msukumo wa kuwa ni watu wanaojitegemea. Hata tukizungumzia Ujamaa, si ule wa mantiki ya kikomunisti au jinsi CCM walivyofanya. Ama kuna mengi ya kuhakikisha viongozi hawawi tabaka la pekee na kinyonyaji jinsi CCM ilivyo.

Dr. Slaa was a popular figure just after Uchaguzi, Lwakatare is a technocrat who could spend time to carry over party responsibility.

My suggestions were based on freeing all the elected Chadema MPs who happen to be party leadership from the party day to day running and focus more into Serikali as Serikali kivuli.

Mimi nakubaliana na wewe kimsingi on Azimio la Arusha. Lakini haiwezekani tukachukua azimio kama lilivyo. Kuna mambo mengi ya kusahihisha kwa mfano haiwezekani 'all major means of production by state'! Inaweza kuwa all strategic major means na tukadefine hizo kama umeme, reli, bandari etc.
Nikilisoma azimio nakubaliana na code of ethics for leaders na Misingi ya 'kila mtu anastahili heshima, na ule wa binadamu wote ni sawa. Ule wa Ujamaa na kujitegemea ndio njia 'PEKEE' ya kujenga jamii sikubali. Tuboreshe kuwa ujamaa na kujitegemea ni njia bora ya kujenga jamii ya watu walio sawa na huru. Azimio sasa ni kama myth! Maana hata waliokuwa wanalipinga ie petty bourgousie sasa wanalizungumzia. Nadhani Azimio kwa maana ya leadership code (ambayo nchi zote za kibepari zinayo code wakiita 'conflict of interest code') tuichukue.

On kutofautisha kazi za chama na za kibunge naona sense. Kitila pia amekuwa akilisemea hili sana kwenye vikao vya chama. Kuna haja ya kufanya mabadiliko makubwa ya muundo wetu ili kuwa tofauti na CCM. Mfano wakati tunapinga Spika kuingia kwenye vikao vya CC ya CCM, katiba yetu inasema Spika anayetokana na CHADEMA atakuwa mjumbe wa CC! Tumeanza mchakato wa kuangalia upya katiba yetu na hili wazo lako tutaliangalia kwa kina.
 
Zitto

Mimi naunga mkono kutenganisha ubunge na uongozi wa chama lakini ama kwa tahadhari kubwa au kwa kupembua faida na hasara zake.

Najua wabunge wana fursa zaidi za rasilimali na hivyo kuweza kutekeleza majukumu ya chama kwa ufanisi zaidi kuliko wasio wabunge.

Baadhi ya wabunge ni popular hivyo wanavuta umma kwenye mikutano.

Utendaji wa kila siku wa kazi za chama ndio inahitaji kutenganishwa, siyo uongozi wa chama. Kwangu mimi nafasi kama ya Mkiti, katibu na manaibu wao ni za uongozi na zibaki kushikwa na wabunge walio imara na popular, ambao pia wana easy access na serikali
 
Mimi nakubaliana na wewe kimsingi on Azimio la Arusha. Lakini haiwezekani tukachukua azimio kama lilivyo. Kuna mambo mengi ya kusahihisha kwa mfano haiwezekani 'all major means of production by state'! Inaweza kuwa all strategic major means na tukadefine hizo kama umeme, reli, bandari etc.
Nikilisoma azimio nakubaliana na code of ethics for leaders na Misingi ya 'kila mtu anastahili heshima, na ule wa binadamu wote ni sawa. Ule wa Ujamaa na kujitegemea ndio njia 'PEKEE' ya kujenga jamii sikubali. Tuboreshe kuwa ujamaa na kujitegemea ni njia bora ya kujenga jamii ya watu walio sawa na huru. Azimio sasa ni kama myth! Maana hata waliokuwa wanalipinga ie petty bourgousie sasa wanalizungumzia. Nadhani Azimio kwa maana ya leadership code (ambayo nchi zote za kibepari zinayo code wakiita 'conflict of interest code') tuichukue.

On kutofautisha kazi za chama na za kibunge naona sense. Kitila pia amekuwa akilisemea hili sana kwenye vikao vya chama. Kuna haja ya kufanya mabadiliko makubwa ya muundo wetu ili kuwa tofauti na CCM. Mfano wakati tunapinga Spika kuingia kwenye vikao vya CC ya CCM, katiba yetu inasema Spika anayetokana na CHADEMA atakuwa mjumbe wa CC! Tumeanza mchakato wa kuangalia upya katiba yetu na hili wazo lako tutaliangalia kwa kina.

Pamoja sana Mkuu! Umma Uko Nyuma yenu.

Napenda sana CHADEMA iliyo Creative na Ndiyo Maana naamini sana Katika BAVICHA iliyo na Nguzu. Zitto as Leaders you all have chance to reform the party ili kiwe na Mvuto Zaidi na Hili mnaweza kulifanya kwa Kuanza kuwajenga Vijana waweze kupambana na Changamoto ya siasa za Kisasa najua Mna Vijana wengi ambao wako well Groomed cha Msingi msiwakatishe Tamaa
 
Tunatumiaje Azimio CHADEMA Rev? We are a centre right party in the family of Concervative party of UK and Canada, the Republican party, CDU of germany etc.

Sijaelewa reforms unazopendekeza are informed with what? Unaposema Lwakatare awe Katibu Mkuu unazingatia nini? Unaposema Slaa awe mwenyekiti una maanisha nini pamoja na majukumu uliyoweka.
Mbowe afanye kazi gani? Zitto? Halafu Lwakatare akiwa mbunge tutafute KM mwingine? Can you suggest reforms without names?

Zitto,

Kukiweka Chadema in the family of Concervative party of UK and Canada, the Republican party, CDU of Germany etc, ni rahisi. Whether Chadema will succeed like those centre right parties is another issue. Hivyo vyama vime-operate kwenye mazingira tofauti kabisa na ya kwetu. Wakati hivyo vyama vimekuwa vikioperate kwenye mazingira ya kibepari, kwa muda mrefu mazingira yetu yamekuwa kwa kiasi kikubwa ya kijamaa. Japokuwa hatufuati tena siasa za kijamaa, bado practice za kijamaa zimejikita sana kwenye mioyo mingi ya Watanzania. Kwa mfano, the way Watanzania wanavyobehave ni tofauti kabisa na Wakenya. Labda hili ndilo lililomfanya JK kusema kuwa siasa za kijamaa zimewafanya Watanzania waogope ubepari.

Chadema identifies itself as a centre right party. But what is the Tannzanians' understanding of rightness? At the end of the day is not whether you are centre right party or centre left party. A party can identify itself as a centre right party, lakini bado ikafuata siasa za mlengo wa kushoto kabisa. It is all about how you address the need of the voters.

I think whether or not Chadema will succeed as a centre right party should be addressed in the context of the success and failure of centre-right parties in post-communist states in Eastern Europe to which we have similar communist backgrounds. We are much related to that environment than the British, American, Canadian or Japanese one. My understanding is that some centre-right parties in these post-communist states have been successful but others have also failed for a number of reasons. Badala ya kuji-compare tuu na centre right party in the West, has Chadema done its homework on the success and failure of centre right parties in the post-communist states? Success I mean the the ability to construct a broad and durable political party.

So far Chadema has focused on macro-institutional explanations that focus on executive structures and electoral system design. However, these have limited explanatory power and it is often difficult to separate out analytically the processes of cause and effect. Although CCM historical-structure and legacy can be used to explain Chadema's ideological positioning as a centre-right party, they do little to explain whether Chadema will succeed as a centre right party.

Elite characteristics and capacity are needed to supplement the shortcomings currently exists in Chadema. I think that is what Rev. Kishoka is talking about. Chadema needs cohesive elites able to act as the nucleus of new centre-right formations and the ability of such elites to craft broad integrative ideological narratives that can transcend diverse ideological positions and unite broad swathes of centre-right and right-wing activists and voters.
 
EMT and Zitto could'nt be more analyitical and sensible and this is what other supporters of Chadema should strive to emulate, rather than calling each other names and deviating from the discussion. Chadema is trying to identify itself as a an institution that will transform the country and and a vehicle that carries peoples' hopes and aspirations. To be able to do this alot of things will need to be enlisted and the moral standing of the party leaders and operating above board rank the highest. The party has to do alot to shed the tag of a family enclave and things like that.
 
kimsingi uchambuzi wako ni mzuri na una lengo la kukijenga chama zaidi kwa kulenga kupata mvuto mpya mbele ya macho na masikio ya watanzania. ila kabla ya hayo mabadiliko hayo unayoyapendekeza ni vyema kufanya tadhmini ya mafanikio na mapungufu yaliyofanywa na viongozi wa wakati huu na kujiridhisha kwanza. nimependa sana ushauri wako wa vijana wa chuoni kutumika kueneza falsafa, madhumuni na malengo ya chama huko wanakotoka ila kuwe na mfumo mzuri wa upashanaji habari utakaowezesha kutoa picha ya haraka ya party networking hasa sehemu za vijijini. Thumb up, comrade!
 
Rev. Kishoka ume andika mambo mengi ya ushauri kwa CDM kutokana na mtazamo wako lakini sio utafiti/research na omba ni toe angalizo chama hiki kime pitia uongozi wa Mzee Mtei, Mzee Bob Makani na sasa Mbowe unaweza uka angalia ni wkatigani chama hiki kimeonekana na mtazamo wakitaifa zaidi na kuku balika kwa watu wengi zaidi.Hivyo kusema mbowe hafai kuwa mwenyekiti wa chama hiki eti hana mvuto nisigefurahi kabisa kuona zina rudiwa rudiwa na wana jamvi.Tatizo sio mbowe na wala sio chadema na wala sio upinzani tujaribu kuwa scientific na realistic ni kitu gani ambacho mbowe kafanya hadi umeona anakiangusha chama,hakika huna jambo lolote la msingi juu ya hilo na unatoa ushauri kabisa kwamba aondoke madarakani ampishe Dr. Slaa kwa uchaguzi upi? Kumbuka hiki nichama cha demokrasia kama kinavyo jipambanua.Acheni kabisa kutoa ushauri usio nautafiti kabisa kwani huu ni upotoshaji.

Unasema CDM iungane na vyama vingine kama CUF hivi nikweli unashauri kwania njema au una mpango gani Mchungaji,hawa CUF mkono wakulia ni CCM mkono wa kushoto ni wapinzani labda Mchungaji ndoa ya CCM na CUF huitambui, vyama vya namna hii huwezi kushirikiana kwasababu hawa eleweki na mtazamo wao hautabiliki.

Hawa wengine kama TLP unajua kabisa ni matawi ya CCM, mwenyekiti wake msimamo wake umesha onekana kweli CDM tunahitaji kufanya kazi na vyama vya namana hii,NCCR mageuzi nao ni wale wale kutwa wako mahakamani na vitisho kwa CDM hivi tuungane tunavyo taka kufanya nini hapo sija kuelewa.au mchungaji unataka vyama viungane halafu viitwe vimeungana kwa hiyo vina umoja, huo umoja kwa ajili ya kufanya nini? mara ngapi CDM haijaweka mgombe uraisi na kime waunga mkono hao unaotaka leo wa ungane nao nini kimetokea baada ya hapo? majibu utakuwa nayo mchungaji

Mchungaji una shauri chama kiwe na mshina toka kijijini hadi mkoani hivyo umeona kama hiyo ndio njia pekee yakuondoa ufisadi katika nchi hii? umefanya utafiti liability ya kumaintain huo mfumo?au una shauri bila kuwa na scietific research! Unafikiri kuondoa ufisadi nchi hii ina hitaji chama chenye wanachama wangapi? jaribuni kuwa logical jamani CCM ina wanachama wangapi naime pata kura ngapi pamoja na uporaji wa waziwazi ulio fanyika na tume au huelewi kilicho tokea?

Angalieni mnapo toa ushauri base yenu nini hasa!acheni kupotosha uma Please! huna utafiti unatoa ushauri wakubadirisha uongozi wa CDM baada yakuona nini eti kiongozi hana mvuto samahani mchungaji naomba nikukosoe mvuto hapo hapo anatafutwa mchumba hapo? tunahitaji uwezo wakuleta mabadiliko maisha yetu yawe safi.Nyie hamueleweki kwakuangalia sura ndio mnasema kiongozi mzuri mwaka 2005 wengine walisema eti mgombea wa chama fulani nichaguo la mungu leo wako wapi uliza kama wanajibu au watarudia tena kauli zile.

Nakataa kabisa ushauri wako

Nashukuru kwa uchambuzi mahiri angalizo wengine humu jamvini wako si kwa kujenga bali kuandikiza migogoro. Jamma anasema mbowe hana mvuto ni hoja gani ya kipuuzi namna hii.
 
Back
Top Bottom