CHADEMA msimpokee Makonda

Akaribishwe ila aishie kufanya mikutano majukwaani kuwaambia wananchi waikatae ccm. Huu ndio uwe mpaka wake hata kama itabidi iwe kwa miaka 30 hadi hapo itakapoamiwa kua anafaa. Asipate nafasi ya kuchangamana na viongozi wa chama na kupata siri na mikakati ya chama kwa muda wowote. Kazi yake iwe kuhubiri tu wananchi waikubali cdm.
 
Mpaka sasa CCM na intelejensia yake wameshindwa kudhibiti kasi ya CHADEMA kukubalika kwa wapiga kura wengi, hivyo CCM kwa kusaidiwa na wataalam wa kijasusi wameandaa mbinu kadhaa za kuidhoofisha CHADEMA kwa kutengeneza mitafaruku ndani ya CCM ili makada wa juu watimkie CHADEMA kwa kazi maalum.

CCM inakufa, hivyo CHADEMA jipangeni vyema kushika dola.

Hii hii intelijensia ya Ulimboka na Kova?
 
Binafsi sisemi asipokelewe kabisa; inaweza ikatokea wakapokelewa kama wanachama kama ulivyosema kwa kuwa wanayo haki kikatiba, lakini chadema wasifanye haraka kuwaingiza watu kama hawa kwenye vyombo vya maamuzi ya chama. Ikiwa ni pamoja na kuwatumia kwa uangalifu majimboni mwaka 2015. Maana nina uhakika CCM wataweka mamluki wengi wa kuja kuchukua form za kugombea majimboni na baadaye kutangaza kujitoa ili kuwasafishia njia CCM.
hili naliunga mkono.ndg.cdm wana takiwakuwa makini sana.awa jamaa watatumia kila mbinu kuakikisha wanaidhibiti cdm kwa mfano kwenye nafasi za ubunge wanajua watapoteza sana kwaiyo watajidai kufukuza watu wakubwa.katika chama.watajiunga na cdm alafu bila cdm kujua watawa simamisha katika majimbo wakidhani ni wakwetu.na jamaa watauza majimbo.na kuwa kosesha cdm majimbo mengi ya uchaguzi.ushauri wangu kwa ndg mbowe.chama kijipange sawa sawa kuwadhibiti masalia ndani ya chama.nanje ya chama.kisikimbilie kupokea watu kutoka ccm.kwa sasa maana mipango yao kwa sasa juu ya cdm ni mikubwa sana na watatumia kila mbinu kuakikisha cdm.inakosa nguvu 2015 pesa zitamwagwa na wenye njaa watachukuliwa ndani ya chama.
 
Napingana na wewe, CHADEMA wampokee na awe mwanachama wa kawaida kama wengine.
Na ajishughulishe na maisha yake au marufuku kugombea uongozi ndani ya chama mpaka baada ya 2015.
 
Hakuna sababu ya kumkataa. Apewe kazi ya kuwa mwanacha mtiifu wa chadema na pale inapobidi apewe zile kazi ngumu za kupambana na kina nape. Kwa kufanya hivyo hakuna ubishi lazima tutamjua tu. Sidhani hata kama ni mchezo wa kuigiza kuna mtu atakubali alishwe sumu huku akijua ni sumu na akainywa kwa kuwa tu ni mchezo wa kuigiza. Hivyo hivyo kwa makonda akiingia chadema kwa hila atagundulika tu kama ambavyo shibuda ameufyata baada ya kumshtukia. Unafikiri shibuda yuko tayari tena kujichafua kwa wananchi wake kwa kukitumikia chama ambacho kinamtumia na mwishowe kimtupe kama kondomu iliyokwisha tumika? Chezea CCM wewe? Tusubiri tuone, muda utaamua....
Ingawa ana haki ya kikatiba kujiunga na chama chochote cha siasa, lakini CHADEMA wana haki kumkubali ama kumkataa.

Sasa kinachotakiwa ni kujenga kada mpya ya viongozi ambao hawana nasaba na CCM ili kuepusha madudu ya chama tawala kuendelea kutesa umma.
 
ni vema chama kiongozwe kwa misingi sheria kanuni na taratibu kilichojiwekea. hisia, hofu na woga ni adui mkubwa katika jamii au chama katika kufikia malengo yake. mimi naona hakuna haja ya kuwa na hofu wala wasiwasi kwani mwanachama mpya haingii kwenye chama kwa ajili ya kubadilisha sheria kanuni na taratibu zake kilichojiwekea. kama wanachama wapya wanakuwa na nguvu ya kuaamua nini kifanyike na kwa namna gani katika chama chake kipya basi hicho si chama makini na hakitakiwi kuaminiwa na kupewa ridhaa ya kuongoza nchi. chama makini huwapokea wanachama wowote na kuwafunda kuziishi taratibu zake kwa maslahi ya umma, kinyume chake mwanachama anaadhibiwa kwa taratibu chama kilichojiwekeana hii ni kwa wanachama wote: wapya na wa zamani.
kuhusu suala la makonda kujiunga na chadema au la si hoja ya msingi kwani chadema kilipata funzo zuri kutoka uchaguzi mkuu wa 2010 nadhani kuliweka kanuni zitakazowabana watu wanaoingia chadema kwa maslahi ya uongozi na kujenga makundi au kuleta mifarakano. milango iwe wazi kwa yoyote anayetaka kujiunga na chochote na kuwa tayari k heshimu taratibu zake. wasalaam!
 
ni vema chama kiongozwe kwa misingi sheria kanuni na taratibu kilichojiwekea. hisia, hofu na woga ni adui mkubwa katika jamii au chama katika kufikia malengo yake. mimi naona hakuna haja ya kuwa na hofu wala wasiwasi kwani mwanachama mpya haingii kwenye chama kwa ajili ya kubadilisha sheria kanuni na taratibu zake kilichojiwekea. kama wanachama wapya wanakuwa na nguvu ya kuaamua nini kifanyike na kwa namna gani katika chama chake kipya basi hicho si chama makini na hakitakiwi kuaminiwa na kupewa ridhaa ya kuongoza nchi. chama makini huwapokea wanachama wowote na kuwafunda kuziishi taratibu zake kwa maslahi ya umma, kinyume chake mwanachama anaadhibiwa kwa taratibu chama kilichojiwekeana hii ni kwa wanachama wote: wapya na wa zamani.

kuhusu suala la makonda kujiunga na CHADEMA au la si hoja ya msingi kwani chadema kilipata funzo zuri kutoka uchaguzi mkuu wa 2010 nadhani kuliweka kanuni zitakazowabana watu wanaoingia CHADEMA kwa maslahi ya uongozi na kujenga makundi au kuleta mifarakano. milango iwe wazi kwa yoyote anayetaka kujiunga na chochote na kuwa tayari k heshimu taratibu zake. wasalaam
 
Kufuatia taarifa za kufukuzwa kwake UVCCM ambapo ni wazi kwa hatua hiyo anaweza akachukua uamuzi wa kujitoa kutoka chama chake cha CCM na kutaka kujiunga na CHADEMA.

Mpaka sasa CCM na intelejensia yake wameshindwa kudhibiti kasi ya CHADEMA kukubalika kwa wapiga kura wengi, hivyo CCM kwa kusaidiwa na wataalam wa kijasusi wameandaa mbinu kadhaa za kuidhoofisha CHADEMA kwa kutengeneza mitafaruku ndani ya CCM ili makada wa juu watimkie CHADEMA kwa kazi maalum.

CCM inakufa, hivyo CHADEMA jipangeni vyema kushika dola.
Mkuu CHADEMA ni chama cha wananchi wote an ni haki ya kila mwananchi kujiunga nacho pale anaporidhia.nadhani hatuna sababu ya kushuku mambo ambayo hayatuhusu.wapinzani aw CHADEMA Hawatoki CCM pekee hata ndani ya chama kunawezekana kukawepo wapinzani pia.uingozi aw chadema una utaratibu wake wa kufanya mambo yake.kama kingekuwa ni chama legelege kisingekuwepo Leo hii.mamluki walikuwepo na wataendelea kuwepo lakini naamini chama kinda utaratibu wake jinsi ya kudeal nao.lakini sio haki kunyima watu kujiunga na chama eti tu kwasababu wametokea CCM. CCM nao wana majukumu Mengi mengine zaidi ya kufikiria kupandikisha mamluki CHADEMA.pia mamluki hawapandikizwi public namna Hiyo. Be blessed
 
Mnajisumbua bure kabisa Paul hawezi kutoka CCM kwani unafikiri kutoka umoja wa vijana ndio kuvuliwa uanachama kama CHADEMA? Makonda ni kijana mtiifu wa chama cha mapinduzi na ni kiongozi bora tutakayefanya nae kazi ya kujenga nchi mwaka 2015 kupitia serikali ya CCM itakayoshinda kwa kishindo.Poleni sana.
 
Mnajisumbua bure kabisa kufikiria Paul atahama CCM.Kumbukeni kuwa huyu ni mwana CCM na ni kiongozi wa miaka ijayo ktk kuitumikia serikali ya CCM.Makonda hapelekwi na upepo,sisi ndio vijana wa CCM tunaojitambua kwani baada ya 2015 wanaharakati wote watasambaratika yetu macho.Mwenye macho haambiwi tazama.CCM JANA-LEO-NA KESHO.
 
huwa napenda sana kuona watu wa humu JF mnavojipa moyo kuhusu kufa kwa CCM, mtasubiri sana
 
Mkuu karatta kila dalili ya kufa kwa CCM ipo wazi, na kibaya ni kwamba ikishatimia andiko lile basi hata wale waliokula na kunywa pamoja kwenye hili dubwasha watakimbiaana na kusalitiana.

Ni suala la muda tu.

Ila twajua kwamba mtaua wengi sana ktk kufikia mwisho wenu na mwisho kabisa HAKI itawatenda
 
Last edited by a moderator:
Wataumia kigezo gani kumkataa?
Unajua kwanini USA inaiunga mkono Israel kwa nguvu zake zote?
What goes around comes around, kigezo watakachokitumia kumkataa Makonda ndicho kitakachokuja kutumika kumkataa mtu mnayemtaka na hapo ndipo kitachimbika.
Wakati mwingine ni bora kuweka hisia pembeni na kufuata sheria na kanuni...

Sheria na kanuni zipi unazo ziongelea wewe masalia? Sheria hizi hizi zinazowalinda mafisadi na kuwakandamiza wanyonge? au kanuni azitumiazo Bi-kiroboto kulipoteza bunge kutoka kwenye wajibu wake wa msingi?
 
Nakuunga mkono asilimia milioni moja,CCM kwa sasa wanakaa kutafuta mbinu nyingi sana za kukizoofisha chama cha CHADEMA,Wameanza na kusema kuna ukabila,wameshindwa,wameanza kusema kuna ukanda=WAMESHINDWA,wameingia kwa kusema mara UDINI=Wameshindwa.SASA STAIL WANAYOKUJA NAYO SASA HIVI NI YA KUTULETEA MAMLUKI NDANI YA CHAMA.Nalo hilo watashindwa tu.NADHANI IFIKE HATUA SASA WATANZANIA WASEME WAMECHOKA.
 
hakuna nafasi ya makapi ya ccm kama kina shibuda.japo pia si kila anayetoka ccm huwa kapi kama shibuda.wapo kama kinamawazo wanaopiga kazi kwenda mbele.
 
Back
Top Bottom