Baada ya ripoti ya tume ya jaji Manento ambayo ndio tume halali yenye mamlaka ya kisheria yanatakiwa yafanyike maandamano ya yasiyo kuwa na kikomo mkoani Iringa kuhakikisha kuwa Kamanda Kamuhanda,Mwema, chagonja na Nchimbi wanang'oka kwenye nafasi zao. Kuna mambo viongozi wetu wa chama wanatakiwa kuongozwa na busara lakini sio hili ambalo mara baada ya tukio chama kikapakwa matope kupitia vipindi vya kupika kwenye runinga.
1. Dr slaa.
2. Mbowe
3. Lissu
4. Zitto
Popote mlipo, amkeni mhamasishe umma wa wana Iringa ili kumtendea haki marehemu Daudi Mwangosi,ally zona na wengine wengi walio uwawa mikononi mwa Polisi, ile kauli ya hakuna kulala mpaka kieleweke ndio inatakiwa kutumika hapa kuwaondoa mabaradhuri walio sababisha vifo vya watanzania wenzetu! Chama kitatuangusha kama kitanyamaza baada ya kutolewa ripoti yenye nguvu za kisheria.
Tusisubiri kesho, tuanze sasa maana ukimya wetu ni mauti kwa wengine, 'hakuna kulala mpaka haki ipatikane, na ikipatikana wahusika wawe wameshapoteza nafasi zao'
Ninachojua ni kuwa M4C inaendelea mkoani Iringa muda si mrefu, tuwe na subira kidogo nadhani mziki wake utakuwa mzito sana, watu wa iringa wana hasira ya kufa mtu.