Elections 2010 CHADEMA: Mbinu Ya Kuchelewa Kuanza Kampeni - Mkakati Wa Mohamedi Ali?

Superman

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
5,695
1,696
Kwa wanaopenda Masumbwi, bila ya shaka mtamkumbuka bingwa wa zamani wa uzito wa Juu Mohamed Ali ambaye umahiri wake umeacha historia.

Bondia huyu anapokua ulingoni, huwa raundi za mwanzo harushi makonde mengi, badala yake hujitahidi sana kukwepa maakonde ya mpinzani wake mpaka hapo anapoona ameshaanza kuchoka ndipo hufungulia mvua ya makonde kwa kasi ya ajabu na hivyo kuwashinda wapinzani wake wengi kwa knock Out!

Kuchelewa kuanza kampeni kwa CHADEMA kunaweza kuwa na faida kwao kwani wanapata muda wa kuwasoma ni nini hasa wapinzani wao wanafanya na wapi wanakosea. Nimeona pia katika vijiwe vya walalahoi wa kawaida hapa DSM kwamba habari za Slaa zenye uzito zinasomwa sana ingawa bado hawajaanza kampeni. Ni kama vile watu wana hamu ya kusikia CHADEMA ni nini kinaendelea lakini unfortunately bado hakuna habari nyingi hasa kutoka kwa Slaa ambaye amekuwa kama nyota njema.

Je, hii ni dalili njema kwa CHADEMA kuwa mbinu wanayotumia ya kuchelewa kuanza Kampeni itawafanya watu wawe excited mara tu Kampeni Zitakapoanza?

Je hii ina maana yoyote katika suala zima la kupata ushindi?

NB: Mwandishi wa thread hii si mwanachama wa chama chochote. Na hana itikadi ya kutofungamana na Chama Chochote ingawa kura yake ni siri yake.
 
Politics na Boxing zina tofauti kubwa..nadhani kila mmoja ana mbinu zake za kushinda mchezo so haitakuwa sahihi sana kulinganisha vitu hivi viwili japo kimtazamo ni kuwa vyote lengo lake ni ushindi...inaweza kuwa na faida na inaweza isiwe na faida kwa kuchelewa au kuwahi kampeni...la msingi ni chama kimejipanga vipi...inawezekana ukapata ushindi siku ya kwanza unapotia mguu mahali au siku ya mwisho unapoondoka eneo fulani...la msingi ni jinsi gani utafanya kampeni zako na kuweza kuwashawishi wapigakura...mbinu ziko nyingi kama nilivyosema awali so unaweza kutumia hii ya kuwahi/kuchelewa kampeni na nyingine nyingi kushinda mchezo kwani ukiwahi/kuchelewa na kusema umeshinda itakula kwako....so hii ni mbinu moja tu ya mchezo hivyo huwezi kusema kama ina faida au la kwa chama chochote.
 
Kunaweza kuwa na Mantiki katika hoja zako . . . Let us wait and see . . . .
 
Chema chajiuza kibaya chajitembeza.

Nani alikwambia Chadema hawajaanza kampeni, kitendo cha CCM juzi kutomalizia kutangaza ilani yake ni kampeni tosha ya Chadema, kuna magoli mengine ya kujifunga lakini linahesabika ni goli la mpinzani.
 
Kwa nini Mkuu?
Unamuuliza huyo kwani anajua chochote yeye ni kama roboti limesetiwa liseme Chadema hoi lakini ukimuuliza how haelewi hata kwa nini amesema hivyo, ni sawa na wanaosombwa bure kwa magari kwenye mikutano ya CCM nauli yao ni kusema CCM OYEEEEE.
 
Jana niliona kwenye taharifa ya habari(sikumbuki ni chanel gani)
Mgombea wa ubunge wa CHADEMA jimbo la Mbeya mjini, Mr II Sugu anajinadi mbele ya umati wa watu.
Sasa Unaposema CHADEMA hawajaanza kampeni unamaanisha ya Urais au?
Ya Wabunge je sio kampeni?
 
You are right . . . Nilikuwa Namaanisha kampeni ya Kitaifa. Nilisoma mahali kuwa Wanaanza tarehe 28 August.
 
Mkakati wa kuchelewa na kusikilizia wenzako wanasemaje wakati mwingine unaweza kuwa counter-productive; naona wanapanga kujibu hoja ambazo CCM wamenadi kwenye kampeni zao na hii itawapunguzia muda wa kuuza sera zao wenyewe.

Tungependa kuona wakitangaza alternative policies na kama wananchi watazielewa kuna uwezekano wa kupata mabadiliko ya kweli. Negative campigning kwa ku-focus kwenye makosa ya kiutendaji yanayofanywa na chama tawala haisaidii wapiga kura kuelewa sera mbadala na badala yake unawapa CCM nafasi ya kutayarisha propaganda za kujisafisha.

We eed alternative policies, we need a second REVOLUTION!
 
Wa Kitaifa?
Uwe mkweli kwenye post yako ya kwanza hujasema kampeni ya kitaifa, watu wanarespond kama ulivyouliza. Na kutosikia habari nyingi si kuwa hakuna kinachoendelea, kumbuka kipindi kabla ya Slaa kuteuliwa kugombea watu walianza kuuliza kulikoni Chadema,

lakini baada Slaa kuanza kutafuta wadhamini walewale wakanza kulia lia eti kaanza kampeni mapema. Kumbuka mambo mazuri hayahitaji haraka. Kuanza mapema kwa CCM ni dalili ya kutojiamini wanaona muda hauwatoshi ukizingatia na afya ya mgombea wao.
 
Si Chadema pekee walioamua kuchelewa kuanza kampeni,hata wapinzani wengine kama CUF /TLP n.k bado hawajaanza.Nadhani hii strategy ni nzuri kwani wanasubiri kibaya kijitembeze kwanza halafu walete mapigo ya knock out huko mbele.Nasubiri kuona hali itakavyojitokeza.
 
Mkakati wa kuchelewa na kusikilizia wenzako wanasemaje wakati mwingine unaweza kuwa counter-productive; naona wanapanga kujibu hoja ambazo CCM wamenadi kwenye kampeni zao na hii itawapunguzia muda wa kuuza sera zao wenyewe.

Tungependa kuona wakitangaza alternative policies na kama wananchi watazielewa kuna uwezekano wa kupata mabadiliko ya kweli. Negative campigning kwa ku-focus kwenye makosa ya kiutendaji yanayofanywa na chama tawala haisaidii wapiga kura kuelewa sera mbadala na badala yake unawapa CCM nafasi ya kutayarisha propaganda za kujisafisha.

We eed alternative policies, we need a second REVOLUTION!
Umesema kweli Chadema wasifanye negative campaign wawe na positive campaign yaani watafanya nini, wawaache CCM wajikaange kwa mafuta yao kujibu walifanya nini kuliko Chadema kuanza kusema CCM hawakufanya nini.

Wanatakiwa waseme Chadema itafanya 1.....2.....3........, halafu nashauri wasiwe na mambo mengi ya kuahidi wachague vitu muhimu kama 10 tu ambavyo watakuwa wanaviimba kila siku hadi viwaingie watu. Mafano 1. Chadema tutabadirisha katiba 2. Mshahara kima cha chini laki mbili na nusu 250,000= ndani ya miezi minne, 3.....................nk nk.
 
uCHELEWAJI NAFIKIRI ITASAIDIAA SANA KWANI ALIYEHARIBU AKIANZA KUJITETEA WAPINZANI WANALAKUWAAMBIA WANANCHI UKWELI.

Bora ccm wameanza kwani JK anazidi kudanganya kuhusu issue ya wafanyakazi na maisha bora kwa kila mtanzania.

Nasubiri CHADEMA waje watuambie ukweli kwani CCM ni uongo na propaganda tu.
 
Back
Top Bottom