CHADEMA 'Lowassa siyo fisadi', CCM 'Lowassa ni fisadi'

Kwa jinsi mambo yalivyo CHADEMA kwa kumwacha SLAA asigombee uraisi na kumwachia Lowasa ni wakati muafaka kwa wana CHADEMA kuonyesha mshikamano na SLAA kwa kuitisha kura ya kutokuwa na Imani na Mwenyekiti wa CHADEMA Mbowe ili mpate mwenyekiti mwingine makini zaidi katika uendeshaji chama.Omeni pia mchakato wa uraisi usimame hadi suala la kutokuwa na imani na Mwrnyekiti Mbowe likamilike.

Tangu lini mwana'ccm akashauri watu wa chadema? Nyinyi mmeshindwa kumshauri mwenyekiti wenu asimkate jina Lowasa?
 
Waziri Mkuu wa Uingereza aitwaye Harold Wilson aliwahi kusema, A week is a long time in politics.

Watanzania tumejaliwa kila kitu cha kidunia mpaka unafiki na usahaulifu!

Septemba 15, mwaka 2007, Dk. Slaa alisimama jukwaani na kutangaza orodha ya mafisadi 11 katika mkutano ulioitishwa na vyama vya upinzani kwenye viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam. Mojawapo katika majina hayo lilikuwepo jina la Edward Lowassa.

Baada ya kutangaza, WanaCCM wengi walipinga kwa nguvu zote wakidai huo ulikuwa ni udaku huku wakitaka vielelezo vya ufisadi kuonyesha ukweli wa kile CHADEMA walikuwa wanakisema.

Miaka minane baadaye, wale wale waliosimama kwenye majukwaa na kudai Lowassa ni fisadi, kwa sasa wameanza tena kupiga kelele kuaminisha Watanzania wakidai Lowassa siyo fisadi, wakati huo huo, CCM nao wamebadilika na kuanza kupiga kelele wakidai Lowassa ni fisadi. CHADEMA nao kwa sasa wanaomba vielelezo vya ufisadi wa Lowassa.

Watanzania wengine wanajiuliza, what's going on?

Wanaopiganiwa kwa sasa wako kimya huku nyasi zikiumia!

This is more than political flip-flop!

Waingereza wanasema, money talks and money alone sets the entire world in motion!

Ama kweli, a flag follows the direction of the wind!

Siasa za aina hii zitaendelea kulitafuna taifa wakati wachache wakifaidika kwa unafiki na ufisadi.

Mkuu inawezekana uko sawa kabisa labda unisaidie tu swali moja - Dr Slaa aliposema Mh Lowasa ni fisadi - CCM na serikali ilijibu nini?
 
Kama unaweza kumkuta mwanamke bar na ukatangaza ndoa kabla hjakaa nae ujuwe we n klaza wa ngono

Mkuu bar mbali sana,suppose nina mke, halafu kila siku unaniambia shemeji yako malaya,then nikagundua kweli shemeji yako ni mcharuko nikamuacha. Kesho yake nakukuta unamtambulisha kwa majirani, umemuacha mkeo umeoa wangu niliyemuacha.
 
Kila mara nasema hapa, Watanzania tumeichoka mno ccm hakuna anaeipenda ccm Hata kama anaipigia kura, lakini tumpe nani mwingine? Upinzani wa nchi hii ni wa kipuuzi kuzidi ccm yenyewe, ndio maana unaona Watanzania wanaamua tu kupiga kura kwa hasira kuwapa hao hao ccm, Leo hii fisadi namba 1 ndio anakuja kuwa rais wa nchi, group lake lote linajulikana ndio mchwa wanaotafuna nchi, yeye kishakuwa rais huyo mbowe atakuwa na sauti gani ya kumdhibiti? Au nani atakuwa juu yake? Wataburuzwa kama mateka,
Mkuu hakika mawazo haya ni ya mtu aliye hai na ubongo wenye afya......njema
 
Tanzania na Watanzania tunapitia katika kipindi kigumu nafikiri kuwai kutokea katika taifa letu. Ni kipindi ambacho tunajiuliza kuwa tumwamini nani? Mbona wale tuliojua kuwa ni watu wa kuwaamini nao wamebebwa na nguvu ya fedha??? Tunapitia kipindi ambacho sio kwamba sie ni wa kwanza kukipitia la hasha hata wenzetu wa Italy na Thailand walishawai kukipitia ila tofauti ni kuwa hizi nchi ni za tofauti sana na Tanzania kuanzia kiuchumi hata kisiasa.

Kwanini nasema hivi?
Kutokana na hali halisi kuwa Tanzania ni nchi ambayo kimaendeleo tunaweza kusema kuwa ni kama ndege iliyo kwenye njia yake kuelekea kuruka, yaani ni nchi ambayo inafunguka zaidi kifursa kiasi ambacho kwa watu wakubwa wa ndani na wa nje imegeuka kuwa sehemu wanayoiangalia sana. Hii imetokana na fursa za maliasili, madini ambayo inasemwa hadi leo yaliyochimbwa ni asilimia 10 tu na mafuta na gesi.

Kwa matajiri na watu wenye nguvu ya kifedha ambao wanataka waendelee kumaintain status quo yao au wanataka waendelee kukua zaidi na zaidi wanajua kuwa wakiweza kuikamata Tanzania leo basi watakamata hizi fursa zote na siku ya mwisho Forbes itawatambua.

Matajili ni watu wenye akili sana na wanajuaga sana mahali popote pale, ukitaka kula mema ya nchi basi kikubwa ni kwa gharama yeyote ile muwekeni mtu wenu kwenye top post ya hiyo nchi. kwa nchi zingine top post kiserikali ni waziri mkuu kama italy na Thailand ila kwa Tanzania ni RAIS. Ukishamuweka tu malengo yako yote ya kibiashara yatatimia.

Kama nilivosema hapo juu kuwa yanayotokea leo Tanzania sio yameanzia hapa la hasha yameanzia huko mbele na mfano mzuri ni italy ambapo kulikuwa na Bilionea ambaye sasa yuko jela anajulikana kama Silvio Berlusconi na Thailand kulikuwa na bilionea anayejulikana kama Taksin Shinawatra. Kwa msio wafahamu hawa watu hawa ni matajili wakubwa sana na walitumia sana nguvu yao ya pesa kutengeneza ushawishi wa kisiasa kwenye nchi zao, kwa Thailand ilibidi jeshi(system) iingilie kati kumuondoa Shinawatra ila kwa italy ilibidi wapate msaada wa nje ili kuweza kuiharibu syndicate ya bwana Silvio Berlusconi na hata leo hii wanashukuru ni bora ameondoka na yuko jela.

Hali ilivokuwa Tanzania sasa:
Kwa hapa Tanzania kuna syndicate ilishajipanga tangu mda kuwa lazima mwaka 2015 tuweke mtu wetu. N i kundi kubwa lenye nguvu ya pesa tena sio kawaida ni sana ambalo lilijipanga kisawa sawa kuwa lazima tuikamate CCM na tuiforce imuweke mtu wetu. Walijipanga vizuri sana kuanzia makanisani, misikitini, bodaboda hadi vyuo vikuu. KWA KIFUPI walimpa mtu wao fedha nyingi sana ili ajenge ushawishi kwa sababu walijua weakeness kubwa ya watanzania/waafrika(na binadamu kwa ujumla) ni fedha. Zilitolewa hela zisizo za kawaida makanisani, misikitini na hata meeneo mengi kama bodaboda na vyouni, walitafutwa wahariri wa vyombo vya habari wakaongwa fedha nyingi sana na kwa kifupi hawa watu waliweza kununua asilimia 90 ya vyombo vya habari.

Walivofika dodoma walikuwa na uhakika kuwa iwe isiwe lazima nguvu ya fedha itatamalaki kiasi ambacho mtu wao atapita ambaye ni EL. ila hamadi kilichotokea dodoma kila mtu anakijua kwa sababu CCM walishtuka kuwa tunakoelekea tutakuja kulaaaniwa na vizazi vyote vijavyo vya watanzania kwa sababu hawa watu sio watu wazuri na hawana nia njema na mama Tanzania ikabidi kutokana na hali ilivokuwa waseme inatosha na lazima kweli ya haki ishinde dhidi ya fedha chafu.

Wakamkata na wakaamua kumchukua mtu aliyekuwa hana makundi, hajawekwa na wenye fedha na hana wa kumlipa fadhila wakati atakapokuwa anaendesha nchi yaani John Pombe Magufuli mambo yakatulia.;

Kwa upande wa hawa watu kibaya zaidi hawakuwa na plan b kwa upande wa CCM, walitawanyika ila kiongozi wao na mtu wao kwa sababu yeye nia yake kuu ni kuingia magogoni tu wakasema lets go the other side. Walijua wanayo pesa na wanayo pesa na kiukweli kwa upande huo hamna anayeweza kushindana nao, wakaenda kuwashawishi viongozi wa upinzani. Kuna taarifa zinasema kuwa walikubaliana kugharamia kampeni yote kuanzia uraisi hadi ubunge ya upande wa pili, walikubaliana kuwawezesha upande huo kifedha na viongozi wa upande huo waliwekwa sawa kifedha.

Ukiliangalia hili suala juu juu unaweza kufikiri ni jambo la kawaida sana ila hapana. Kuna kitu hapa ambacho watanzania lazima waamke na wakione nacho ni hadi hawa wameweza kuingiliwa na fedha???????

Katika dunia ya leo mwanasiasa anatakiwa awe mtu predictable na asiwe mnafiki kiasi ambacho mtu aliyempa kura anatakiwa awe na uhakika nae kuwa nilimpa kura huyu mtu kwa sababu anaamini katika A, B, C na hizo ndo zilizonishawishi mie kumuamini na kumpa nafasi kwenye akili yangu.

Mwaka 2007/8 Chama kilichojijengea sifa kubwa nchini Tanzania Chadema kilitoa kile kilichoitwa The list of Shame ambapo walitoa majina ya watu 11 wao waliowataja kuwa ni mafisadi, wanaolitafuna taifa na kuliangamiza taifa. Walisema kuwa wana ushahidi kamili usio na shaka juu ya hawa watu na kama hawa watu wanabisha waende mahakamani. Walisema hawa watu hawastahili kuwa mitaani sehemu wanayostahili kuwa ni jela. Na hiki ni kitu kilichowapa public trust ya kiwango cha juu kabisa, hiki ni kipindi ambacho chadema ndo ilianza kujijenga mioyoni mwa watanzania kuwa ni wakombozi wa kweli, watu wanaongea ukweli, sio waongo na yote wanayosema ni kweli tupu kwa hiyo ndo watu wanaostahili kupewa nchi.

Chadema hawakuishia hapo walizunguka nchi nzima kwenye mikutano na kampeni mbalimbali wakiendelea kuitaja iyo THE LIST OF SHAME, ambayo no 9 alikuwapo Edward Lowassa.

Sio huyo tu washirika wa Lowassa yaani mzee wa vijisenti na the Kings Maker Rostam Azizi washawai kutajwa na Chadema kuwa ni watu mafisadi na wasiofaa.

Kichwa cha mada kinasema ni ulaghai, unafiki na uzandiki kwa sababu pamoja na hiki chama kumtaja huyu mtu ila viongozi wao wamekula matapishi yao wenyewe na leo wamempokea huyu Lowassa na wanamnadi kuwa ni mtu safi, mwenye weredi na anayefaa.

Kuna kitu kimekuwa kikiendelea kwa hawa viongozi kutoa majibu mepesi eti siasa ni dynamics na sio static eti mtu unaweza kubadirisha gia angani wakifikiri watanzania ni mambumbumbu sana kiasi ambacho hawawezi kuhoji na hawafuatilii mambo yanayofanyika duniani huko.

Napenda kuwaambia viongozi wa Chadema kuwa katika siasa za 21st century mwanasiasa akisema jambo alafu ikitokea otherwise au ikitokea tofauti na alivosema au kuuaminisha umma uwa anajiuzuru. Mfano wa haya ni kama ilivotokea juzi Scotland pale waziri mkuu na kiongozi wa chama cha Scotish National Party alipojiuzuru nafasi zake zote baada ya kile kitu alichokuwa akiwaaminisha wascotland kuwa nchi yao inafaa kujitenga kufeli kwenye referundum. Sio huko tu hata England Ed Milband nae baada ya chama chake kushindwa kwenye kushawishi kitokana na sera zake alibidi ajiuzuru. Huu ndo ustaarabu mpya kwenye siasa kwa kifupi siasa za dunia ya leo ni kuwa endapo mwanasiasa ukisema jambo fulani lile jambo likija tokea tofauti na ulivouaminisha umma au chama chako inabidi ujiuzuru.

Sasa kwa Chadema na ukawa what thet were supposed to do ni kuwa kabla Lowassa hajatambulishwa rasmi au soon after kutambulishwa wale viongozi wote waliokuwa wanauaminisha umma na kudai wana ushahidi juu yake kuwa ni fisadi walitakiwa kula matapishi yao kwa wao kujiuzuru nyadhifa zao zote ndani ya chama chao na kuomba msamaha kwa jamii ya Tanzania kwa upotoshaji mkubwa walioufanya.

Ila kwa majibu mepesi wanayoyatoa kama aliyatoa jana Mchungaji Msigwa kwenye kipindi cha Madamoto, kama aliyoyatoa Lema au kama aliyoyatoa Lissu na ziadi na zaidi kama aliyoyatoa mwenyekiti wao Freeman Aikael Mbowe wakati anamkaribisha Lowassa basi its obvious kuwa HUU NI ULAGHAI, UNAFIKI NA UZANDIKI ULIOTUKUKA.

Nakataaa kudharauliwa na viongozi wa ukawa kuniona mie siwezi kufikiri ila wao ndo wanaweza kufikiri kwa niaba yangu.....

Tukutane Oktoba.

MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATANZANIA.
 
Kuna msemo humu ndani unasema "....You can't fool all the people all the time". Tupishe na stori zako hizo.

CCM imekuwa madarakani kwa kipindi gani? Wamefanya nini? Wajerumani walitutawala kwa kipindi kifupi mno! Mpaka sasa hivi tunaona investement walizowekeza. Ukoloni wa CCM ni mbaya mno.. Imetosha!

Tumeweka pamba masikioni hatutaki kusikia chochote kuhusu umalaika wa CCM. CCM must go. CCM must go. TUMECHOKA.
 
Kwa asili hakuna binadamu anayezaliwa akiwa mwovu, fisadi, n.k. Mifumo "huumba" watu; mifumo ya kifisadi huzaa mafisadi. CCM ni mfumo wa kifisadi hivyo huzaa mafisadi; ukiwa ndani ya CCM (mfumo) ni lazima utaishi sawasawa na mfumo ulivyo.

Ukiachana na mfumo unakuwa umeachana na mambyo ya mfumo ule; unakuwa umezaliwa upya kuishi sawa sawa na mfumo mpya ulioingia. Wanachopambana nacho UKAWA ni mfumo fedhuli na wa kifisadi; uliojaa ubabe wa kila namna; viongozi wakipiga na kuumiza watu hadharani bila aibu kisa - watalindwa na mfumo. Viongozi wanafanya ufisadi bila aibu simply kwa sababu mfumo unawalinda.

Sio Lowasa tu, bali yeyote ambaye angependa "kuzaliwa" upya anakaribishwa as long as yuko tayari kubadilika na kuishi maisha mapya yasiyo ya kifisadi. Kisichoeleweka hapo ni kipi unless umeamua kujitia ujinga.

Kwahiyo ikitokea mfano mwanao akaiba simu ya mtu utaita wizi wa mwanao ni wa mfumo? hapa elewa tabia zote inazozisikia hapa duniani zimeumbiwa watu lakini si kweli kwamba watu sote tuna tabia zote zilizoko hapa dunianai ...ni bora CCM hii tunaypifahamu ikaendelea kutawala kuliko kuwakaribisha hawa waliotwambia ni wasafi wakati wa uchumba kumb kwenye kuingia ndoa ni hatari zaidi ya ibirisi mwenyewe
 
Achia watoto wako waendane na mabadiliko. Wazee kama wewe hawakubali mabadiliko. CCM Must go. TUMECHOKA.
 
Waziri Mkuu wa Uingereza aitwaye Harold Wilson aliwahi kusema, A week is a long time in politics.

Watanzania tumejaliwa kila kitu cha kidunia mpaka unafiki na usahaulifu!

Septemba 15, mwaka 2007, Dk. Slaa alisimama jukwaani na kutangaza orodha ya mafisadi 11 katika mkutano ulioitishwa na vyama vya upinzani kwenye viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam. Mojawapo katika majina hayo lilikuwepo jina la Edward Lowassa.

Baada ya kutangaza, WanaCCM wengi walipinga kwa nguvu zote wakidai huo ulikuwa ni udaku huku wakitaka vielelezo vya ufisadi kuonyesha ukweli wa kile CHADEMA walikuwa wanakisema.

Miaka minane baadaye, wale wale waliosimama kwenye majukwaa na kudai Lowassa ni fisadi, kwa sasa wameanza tena kupiga kelele kuaminisha Watanzania wakidai Lowassa siyo fisadi, wakati huo huo, CCM nao wamebadilika na kuanza kupiga kelele wakidai Lowassa ni fisadi. CHADEMA nao kwa sasa wanaomba vielelezo vya ufisadi wa Lowassa.

Watanzania wengine wanajiuliza, what's going on?

Wanaopiganiwa kwa sasa wako kimya huku nyasi zikiumia!

This is more than political flip-flop!

Waingereza wanasema, money talks and money alone sets the entire world in motion!

Ama kweli, a flag follows the direction of the wind!

Siasa za aina hii zitaendelea kulitafuna taifa wakati wachache wakifaidika kwa unafiki na ufisadi.
Tungeumia hivi wakati jina lake limeondolewa kimizengwe ingekuwa poa.Politics is a matter of dynamics;change according to the conditions.
 
Sasa kama Lowasa ni fisadi ni kwa nini hiyo serikali ya CCM haijamchukulia hatua yoyote hadi sasa?

Acha kujitoa akili mkuu. .aliyemrushia tuhuma ni chadema au serikali? Yaani umtuhumu wewe alafu nimpeleke mahakamani mimi? ...tumia akili kabla ya kucomment ...usikariri comments za wasiofikiri na kuzifanya zako
 
Waziri Mkuu wa Uingereza aitwaye Harold Wilson aliwahi kusema, A week is a long time in politics.

Watanzania tumejaliwa kila kitu cha kidunia mpaka unafiki na usahaulifu!

Septemba 15, mwaka 2007, Dk. Slaa alisimama jukwaani na kutangaza orodha ya mafisadi 11 katika mkutano ulioitishwa na vyama vya upinzani kwenye viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam. Mojawapo katika majina hayo lilikuwepo jina la Edward Lowassa.

Baada ya kutangaza, WanaCCM wengi walipinga kwa nguvu zote wakidai huo ulikuwa ni udaku huku wakitaka vielelezo vya ufisadi kuonyesha ukweli wa kile CHADEMA walikuwa wanakisema.

Miaka minane baadaye, wale wale waliosimama kwenye majukwaa na kudai Lowassa ni fisadi, kwa sasa wameanza tena kupiga kelele kuaminisha Watanzania wakidai Lowassa siyo fisadi, wakati huo huo, CCM nao wamebadilika na kuanza kupiga kelele wakidai Lowassa ni fisadi. CHADEMA nao kwa sasa wanaomba vielelezo vya ufisadi wa Lowassa.

Watanzania wengine wanajiuliza, what's going on?

Wanaopiganiwa kwa sasa wako kimya huku nyasi zikiumia!

This is more than political flip-flop!

Waingereza wanasema, money talks and money alone sets the entire world in motion!

Ama kweli, a flag follows the direction of the wind!

Siasa za aina hii zitaendelea kulitafuna taifa wakati wachache wakifaidika kwa unafiki na ufisadi.

Team of Rivals: The Political Genius of Abraham Lincoln is a 2005 book by Pulitzer Prize-winning American historian Doris Kearns Goodwin, published by Simon & Schuster. The book is a biographical portrait of U.S. President Abraham Lincoln and some of the men who served with him in his cabinet from 1861 to 1865. Three of his Cabinet members had previously run against Lincoln in the 1860 election: Attorney General Edward Bates, Secretary of the Treasury Salmon P. Chase and Secretary of State William H. Seward. The book focuses on Lincoln's mostly successful attempts to reconcile conflicting personalities and political factions on the path to abolition and victory in the American Civil War.
Goodwin's sixth book, Team of Rivals was well received by critics, and won the 2006 Lincoln Prize and the inaugural Book Prize for American History of the New-York Historical Society. US President Barack Obama cited it as one of his favorite books and was said to have used it as a model for constructing his own cabinet. In 2012, a Steven Spielberg film based on the book was released to critical acclaim
 
utafuteni kwanza ufalme wa mbingu,na hayo
yote mtazidishiwa.Itoeni kwanza ccm madarakani
na mengine mtazidishiwa.Binafsi mi nataka ccm
watoke,haijalish ukawa watamsimamisha
nani,hata shetani

Unaitoa CCM madarakani ili umkabidhi nani?
 
Back
Top Bottom