Kama lengo pekee la Upinzani ni kwenda Ikulu kwa walichofanya ni sawa kabisa. Ikulu ndo target hata Taifa zima wafe, waingie Ikulu kilichofanyika ni sahihi kabisa. Ila kama upinzani ni kuwasaidia wananchi, kupigania haki zao, kuonyesha madhaifu ya chama Tawala hapo watakuwa wamecheza mchezo mbaya sana. Jingine kubwa wajue wanaweza kushika Dola na kwa kawaida alieko nje ya dola huona makosa mengi sana mabaya yalioko kwenye dola. Tusubiri na tuone. Mungu ibariki Tanzania.