CHADEMA kwa hili Mmechemka

Kishongo

JF-Expert Member
May 4, 2010
932
64
ALHAMISI ya wiki iliyopita wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) walimkamata Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Bi. Fatma Kimario kwa
madai kuwa walimkuta akifanya kikao na viongozi wa vijiji na kata ndani ya ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Isakamaliwa.

Kwanza kabisa kwa mtazamo wangu CHADEMA walichofanya ni makosa lisha ya kwamba walimdhalilisha kiongozi wa wananchi kwa kumvuta huku na huko huku wakitambua wazi kwamba kufanya hivyo ni kosa la jinai.

Kosa ambalo ama hakika bila ushabiki wowote wahusika wote wanapaswa kushtakiwa na kuchukuliwa hatua za kisheria haraka iwezekanavyo.

Ni hoji kwanza, hivi hawa wahuni wanaojiita makomandoo wa CHADEMA wameenda Igunga kwa misingi ya kumnadi mgombea wao ama kumdhalilisha kiongozi aliyewekwa madarakani na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Awali nilikuwa ninawakubali CHADEMA kutokana na sera zao za kuleta maendeleo lakini kwa uhuni huu uliofanywa na wanachama hao Igunga katu siwezi kusita kutamka kwamba wakipata nafasi ya kutawala nchi hii awachelewi kuwanyanyasa Watanzania kijinsia.

Tuzingatie kwamba, Bi. Kimario ni kiongozi wa nchi hawakustahili kumdhalilisha kiasi hicho, tena kibaya zaidi wanaume ndio waliohusika kumvuta mama huyo huku na huko kama mwizi.

Haiwezekani hizi ni vurugu ambazo zinatakiwa kupigwa vita na kukemewa kwa nguvu zote ina maana kiongozi ana mipaka ya kufanya mikutano?

Huyu ni kiongozi ana haki ya kufanya kikao mahali popote muda wowote na wananchi wake bila kubuguziwa ili mradi asivunje sheria.

Ina maana wakati huu kampeni za uchaguzi mdogo unaoendelea Igunga kiongozi yoyote wa serikali hatakiwa kufanya kikao na wananchi wake kwa kuhofia kuwa anapanga njama za ushindi wa chama fulani.

CHADEMA sasa mnakoelekea ni kubaya mlikuwa mnakwenda vizuri sasa vurugu zenu na ubabe wenu ndio utakaowakosesha kura na wala si vinginevyo.

Kwani mkifanya siasa na kampeni za ustaarabu hamtaonekana ndani ya jamii ama hadi kila siku muwe na jambo jipya linaloonesha udhalilishaji kwa ili nidhiriki kutamka kwamba wapumbavu siku zote huwa wanajitwalia makaa ya moto wenyewe hivyo siwafichi kwa stahili hii mnajiangusha wenyewe na mnajiua wenyewe.

Vurugu hazipendezi hata kidogo, huyu Mkuu wa Wilaya ana haki ya kufanya mkutano au kikao na viongozi wake kwa sababu kwa ni haki yake ya msingi ili kuharakisha maendeleo ya wananchi.

Katika suala hili hakuna ubishi ni lazima mchukuliwe hatua, watu waliomkamata na kumdhalilisha ni lazima sheria ichukue mkondo wake huu ni ukosefu wa nidhamu.

Hii ni hatari kwa maana hiyo kiongozi yoyote wa serikali wa Wilaya ya Igunga asifanye chochote kwa kuhofia vyama vya upinzani, jamani tuacha mawazo mgando huu ni uhuni kama siyo ujinga katika vichwa vya watu walioelimika.

Hata kama huyo mama alikwenda kinyume, lakini hakustahili kufanyiwa kitendo hicho hata kidogo ni udhalilishaji.

Source: GAZETI MAJIRA
 
Back
Top Bottom