CHADEMA kuunguruma Musoma mjini

mgeni wenu

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
3,664
1,730
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)kitafanya mkutano wa Hadhara katika Shule ya Msingi Mkendo,katika mkutano huo wa Hadhara utakaohutubiwa na Meya wa Mji wa Musoma(Alex Malima)pia atakuwepo Mbunge wa Jimbo hilo(Vincent Nyerere)na Mbunge wa viti Maalum(Ester Matiko) mbali na salam za Mwaka mpya na Ufafanuzi wa katiba pia wataelezea Mafanikio ya Maendeleo ya Jimbo Hilo tangu waingie Madarakani
 
Hongereni, lakini mjue kuwa mijini CDM imesha jenga mizizi, kwa sasa ni kukita mizizi vjijini. AMKENI CDM
 
thanks for infomation ila kumbuka kuleta feedback ya mkutano wote na usilete habari nusunusu au kuleta misifa isiyo na mpangilio leta hoja uwe balanced

kila la heri mkuu tupo pamoja sana
 
Agizo limezingatiwa mkuu
 
hii cdm vipi sasa mi nataka wakaungurume vijijini wao bado wanaunguruma mjini,by the way nieleze kitakachojiri na nataka kujua huyo meya ni wa chama chetu au ni magamba?
 
Huyu meya(Alex Malima)ni meya anayetokana na nguvu ya Umma(Chadema)na ni meya pekee wa Chadema aliyepita bila kupingwa Tanzania ambaye ni CHADEMA.....na ndiyo mwenye Halmashauri inayofanya vizuri bila kelele
 
Tunaomba kupewa mrejesho baada ya mkutano,na itafaa kukiwa na actualities mkuu.kila la heri
 
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)kitafanya mkutano wa Hadhara katika Shule ya Msingi Mkendo,katika mkutano huo wa Hadhara utakaohutubiwa na Meya wa Mji wa Musoma(Alex Malima)pia atakuwepo Mbunge wa Jimbo hilo(Vincent Nyerere)na Mbunge wa viti Maalum(Ester Matiko) mbali na salam za Mwaka mpya na Ufafanuzi wa katiba pia wataelezea Mafanikio ya Maendeleo ya Jimbo Hilo tangu waingie Madarakani

Hii ni habari nzuri,

Kwakuwa wabunge wa ccm na mawaziri wanapita pita wilayani nchi nzima wakijaza watu propaganda za uzuri wa sheria ya mapitio ya katiba mpya, basi limekuwa jambo la kheri sana kwa chadema nayo kwa kuwatumia wabunge wake pamoja na viongozi wake wa kitaifa/mikoa na wilaya wakaendelea kutoa elimu ya uraia kwa wananchi, hasa juu ya sheria ya mapitio ya katiba mpya.

Kwa kufanya hivi upotoshaji wowote unaofanywa na ccm na serikali yake utakuwa umedhibitiwa na wananchi watapata elimu ya ukweli juu ya sheria ya mapitio ya katiba mpya.
 
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)kitafanya mkutano wa Hadhara katika Shule ya Msingi Mkendo,katika mkutano huo wa Hadhara utakaohutubiwa na Meya wa Mji wa Musoma(Alex Malima)pia atakuwepo Mbunge wa Jimbo hilo(Vincent Nyerere)na Mbunge wa viti Maalum(Ester Matiko) mbali na salam za Mwaka mpya na Ufafanuzi wa katiba pia wataelezea Mafanikio ya Maendeleo ya Jimbo Hilo tangu waingie Madarakani
Ningependa Meya na mh mbunge na cabinet yake inayoongoza Municipal ya Musoma wajikite katika masuala yafuatayo:
Ukosefu wa maji katika maeneo ya Buhare kigera Nyasho. Ziwa Viktoria lipo jirani sana na maeneo hayo si haki yukose maji.
Piganieni Chuo cha Buhare kiwe chuo kikuu ili mji uweze kupanuka. Uwepo wa vijana wengi wasomi utasaidia mzunguko wa fedha kuwa mkubwa Nyumba zitapata thamani, daladala zitafanya kazi, stationeries zitapata wateja, hata mama ntilie watauza vyakula.
Fufueni viwanda vya samaki, maziwa, Mutex ili vijana wapate ajira za kudumu. BODABODA, gutas,sio, mji mdogo sana gaweni viwanja vya makazi kuanzia zerozero. nendeni Makoko hadi mmahare. watu wajenge kusiwe na mizengwe ya kugawa ardhi.
Alex Kisurula Malima Kyamba, Vincent Joseph Kiboko Nyerere, Ester Mwita matiko na wenzenu wa CDM akina Bwire Nyamwero umizeni vichwa Musoma ibadilike. Angalieni Mwanza kwa akina Manyerere, Kiwia, Wenje mji unaongezeka kwa kasi. Naunga hoja kufanyika mkutano huo.
 
Hoja imeungwa Mkono
Ningependa Meya na mh mbunge na cabinet yake inayoongoza Municipal ya Musoma wajikite katika masuala yafuatayo:
Ukosefu wa maji katika maeneo ya Buhare kigera Nyasho. Ziwa Viktoria lipo jirani sana na maeneo hayo si haki yukose maji.
Piganieni Chuo cha Buhare kiwe chuo kikuu ili mji uweze kupanuka. Uwepo wa vijana wengi wasomi utasaidia mzunguko wa fedha kuwa mkubwa Nyumba zitapata thamani, daladala zitafanya kazi, stationeries zitapata wateja, hata mama ntilie watauza vyakula.
Fufueni viwanda vya samaki, maziwa, Mutex ili vijana wapate ajira za kudumu. BODABODA, gutas,sio, mji mdogo sana gaweni viwanja vya makazi kuanzia zerozero. nendeni Makoko hadi mmahare. watu wajenge kusiwe na mizengwe ya kugawa ardhi.
Alex Kisurula Malima Kyamba, Vincent Joseph Kiboko Nyerere, Ester Mwita matiko na wenzenu wa CDM akina Bwire Nyamwero umizeni vichwa Musoma ibadilike. Angalieni Mwanza kwa akina Manyerere, Kiwia, Wenje mji unaongezeka kwa kasi. Naunga hoja kufanyika mkutano huo.
 
Huyu meya(Alex Malima)ni meya anayetokana na nguvu ya Umma(Chadema)na ni meya pekee wa Chadema aliyepita bila kupingwa Tanzania ambaye ni CHADEMA.....na ndiyo mwenye Halmashauri inayofanya vizuri bila kelele
Alex Malima kupita bila kupingwa that was obvious, kwanza ni mzaliwa wa musoma mjini, anaufahamu mji, anawafahamu kaka baba dada shangazi, bibi, hata vijana wenzake anafahamu matatizo yao hata kabla hajaingia ktk siasa. Ni kijana msikivu mpenda watu mpenda maendeleo ya kweli. Mcha mungu. Wana Musoma mkimtumia vizuri atawasiadia kuwatoa ktk lindi zito la umaskini unaowakabili. mpeni sapoti acheni u musoma. Nawatakia mkutano mwema wenye mafanikio.
 
Tuko pamoja ila madiwani wafwatao tunaomba wajirekebishe la sivyo nguvu ya uma itatumika kuwatoa madarakani naibu mea diwani wa kamunyonge sodbi diwani wa bweri na diwani wa makoko acheni tamaa mjirekebishe.
 
kila laheri wana musoma na mungu awatangulie kwenye mkutano huo.

By the way juzi siku ya Jumamosi tarehe 07/01/2012 Mh.Tundu Lisu mbunge wa Singida Mashariki alifanya mkutano wa hadhara ktk viwanja vya stand ya zamani mjini Singida pamoja na maovu mengine ya serikali aliozungumzia, muda wake mwingi alitumia kumshambulia mkuu wa mkoa kuhusu "conflict of interest" akidai kwamba kampuni ya mkuu wa mkoa imepatiwa kazi na manispaa isivyo halali ya kuzoa takataka mjini sgd.Waandishi wa habari wa singida hawajaripoti taarifa hizi kwenye vyombo vya habari huenda ni kwa ajili ya woga au wamezibwa midomo.Hebu waliokuwepo huko na wenye taarifa kamili wamwage data.
 
Ujumbe umefika mkuu kwa kuwa na wao ni member humu nadhani wanasoma

Back
Top Bottom