CHADEMA kupata majimbo mapya mengi zaidi ila itapoteza machache ya sasa

msambaru

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
245
109
Wana JF wenzangu napenda kukishukuru CDM kwa chachu kiliyoleta ndani ya Bunge na serikali iliyo likizo ya CCM, Lakini ninakuwa na hofu juu ya utendaji ama uwajibikaji wa baadhi ya wabunge wetu majimboni, tunaenda mwaka wa pili sasa lakini kwenye majimbo hali bado ni tete sio kwa wananchi kupewa zawadi, michango au misaada ya mtu mmoja mmoja, ila katika kuwapanga wananchi kutumia japo raslimali kidogo zilizopo kwenye maeneo yao. Juzi niliwasikia vijana wasukuma matoroli yenye bendera ya CDM wakiuza maji wakisema mbunge wao ni mbunge wa Taifa, kwamba yuko makini sana kwenye mambo ya kitaifa ila jimboni anakuja kusalimia ndugu zake. Je kama hali ndo inaanza kuaw hivi Taswira ya chama na imani yake kwa umma wa maskini wa kitanzania itabaki wapi?
 
Kweli ndugu hii ninchangamoto sio kwa CDM tu bali vyama vyote vya upinzani wanatakiwa wawe wabunifu majimboni kwao watekeleza ilaini za vyama majimboni kuibua fursa zilizopo za kuondoa umaskini kuwashirikisha na kuwaongoza wapiga kura wao kujiletea maendeleo na kuondokana na matatizo kama njaa, maradhi, shule na elimu duni, miundo mbinu mibovu. Wasitegemee tu serikali ifanye maana ni kweli serikali ipo bisased sana kwa majimbo ya upinzani, hivo wawe wabunifu kutumia michango ya wananchi na kutafuta wafdhali toka nje kama alivowahi kufanya Dr.Slaa jimboni kwake ili mwisho wa siku tofauti ionekane kati ya majimbo ya upinzani na yale ya ccm na hii itavuta wapiga kura zaidi na mwisho kushika dola!!
 
Kuna wabunge wasiopenda kukosolewa na hili litawagharimu pindi watakapotaka kutetea viti vyao si kwa kupambana na vyama vingine tu bali hata chaguzi za ndani ya chama zinaweza kuwaangusha..
 
CCM tutachukua majimbo yote ya Chadema mwaka 2015, CHADEMA hawatafikisha hata majimbo matano TANZANIA nzima.
 
Mbona bado ni mapema sana kuja na hizi tathmini. Siasa ni mchezo wenye trick nyingi sana. Karata fulani fulani zinaweza zikageuza mtizamo wa wananchi kwa chama fulani. Lolote linaweza kutokea kwenye uwanja wa mapambano, lakini si vibaya kujipa moyo kwani inawajenga watu kwa spirit ya ushindi
 
Je tunahitaji kuwatrik waTZ au kuwa na nia ya dhati ktk kuwapanga kujiletea maendeleo? Yana mwisho jipe moyo.
 
Wana JF wenzangu napenda kukishukuru CDM kwa chachu kiliyoleta ndani ya Bunge na serikali iliyo likizo ya CCM, Lakini ninakuwa na hofu juu ya utendaji ama uwajibikaji wa baadhi ya wabunge wetu majimboni, tunaenda mwaka wa pili sasa lakini kwenye majimbo hali bado ni tete sio kwa wananchi kupewa zawadi, michango au misaada ya mtu mmoja mmoja, ila katika kuwapanga wananchi kutumia japo raslimali kidogo zilizopo kwenye maeneo yao. Juzi niliwasikia vijana wasukuma matoroli yenye bendera ya CDM wakiuza maji wakisema mbunge wao ni mbunge wa Taifa, kwamba yuko makini sana kwenye mambo ya kitaifa ila jimboni anakuja kusalimia ndugu zake. Je kama hali ndo inaanza kuaw hivi Taswira ya chama na imani yake kwa umma wa maskini wa kitanzania itabaki wapi?

Hakika kabisa uliyosema. Ninafikiri ifike wakati sasa kuwe na mikakati ya kitaifa ya maendeleo kwa kila jimbo katika kila chama cha upinzani chenye wabunge (haswa CHADEMA) ambacho ni chama rasmi cha upinzani bungeni. Mikakati hiyo iwekwe na wahusika katika kila jimbo kulingana na mahitaji ya maendeleo katika eneo husika, nakala ipelekwe makao makuu kwa ufuatiliaji. Pesa ni muhimu sana kwa maendeleo, lakini ninadhani rasilimaliwatu ni zaidi ya pesa haswa kama wamehamasishwa na kuelekezwa ni nini cha kufanya katika kujiletea maendeleo yao.
 
Naona kama kichwa cha habari hakiendani na maudhui yaliyomo. Ila kichwa cha habari kimenilazimu nikuulize swali lifuatalo" wewe ni sheikh Yahya Hussein au??"
 
Usemayo i kweli tumewatuma kufanya yote ya kitaifa na ya kwetu majimboni. Naishi Mbeya (jiji) barabara hazipitiki na tunaambiwa Wachina watakuja zijenga lakini lini? Sugu atembelee Ituha, Isyesye, Uyole na sehemu nyingine hakuna badiliko lolote. Tunao RC Mkurugenzi dynamic lakini hataki kumtumia. We are just too patient but we can not wait too much kimbembe 2015 tutamwondoa tuweke mwingine
 
Aige ukerewe na Musoma mjini mbona wao wanafanya kazi za Taifa na JiMboni ?
Usemayo i kweli tumewatuma kufanya yote ya kitaifa na ya kwetu majimboni. Naishi Mbeya (jiji) barabara hazipitiki na tunaambiwa Wachina watakuja zijenga lakini lini? Sugu atembelee Ituha, Isyesye, Uyole na sehemu nyingine hakuna badiliko lolote. Tunao RC Mkurugenzi dynamic lakini hataki kumtumia. We are just too patient but we can not wait too much kimbembe 2015 tutamwondoa tuweke mwingine
 
naamini sera za kitaifa ndizo zilizowapa ushindi wabunge wa cdm,sidhani kama cdm imewageuka wananchi katika kusimamia masuala ya kitaifa.mwananchi wa kawaida anaelewa kwamba mbunge hawezi kumletea ugali mezani bali kwa kupitia mbunge anaweza kutokea mabadiliko ya kimfumo ambayo yatamuhakikishia kupata ugali mezani kwa kitumia vipawa alivyojaaliwa na mwenyezi.hivyo ni vyema wabunge wa cdm wakaendelea kushughulikia maswala ya kimfumo na wananchi wataichagua tu.kazi ya mbunge ni kuwakilisha na sio kujenga majosho na barabara.
 
Kuna wabunge wasiopenda kukosolewa na hili litawagharimu pindi watakapotaka kutetea viti vyao si kwa kupambana na vyama vingine tu bali hata chaguzi za ndani ya chama zinaweza kuwaangusha..

Sasas demokrasia imekua....hii ni dalili njema
 
Ni hivi nenda ukawaambie waliokutuma CDM haitapoteza jimbo hata mmoja badala yake tutaongeza majimbo mengine mengii tuu, kwa ufupi wananzengo wameamka hawataki ubabaishaji wala ujanja ujanja na tena hata kwa mtutu wa bunduki jimbo la Arusha mjini halimpati ng'ooo
 
Nilichosema ni kwamba CDM tutapoteza majimbo ya sasa na kupata mengine mengi mapya, hebu kuwa na akili chanya kimaendeleo, suala sio uCDM ila maendeleo ya jamii kupitia wawakilishi wao. we bibi vipi?
 
Nikiuangalia vizuri kabisa ktk '3 dimension' huo uzi wako ninauona una 'hidden agenda' najua ndio wakati wa wamagamba kuanza kumwaga sumu kimtindo..... anyway nimeamua kuepusha shari vinginevyo ningekushukia kisawa sawa mithili 'drone apache'
 
Shuka kama unaelewa unachofanya, Mi mwanaCDM hai sio shabiki kama wewe na hapa najaribu kuweka mambo sawa kama mwanachama, ila kwa wewe mpiga porojo endelea. Nipo kwa ajili ya kujenga chama sio kukishabikia kama wewe.
 
Back
Top Bottom