CHADEMA kupata majimbo mapya mengi zaidi ila itapoteza machache ya sasa

Shuka kama unaelewa unachofanya, Mi mwanaCDM hai sio shabiki kama wewe na hapa najaribu kuweka mambo sawa kama mwanachama, ila kwa wewe mpiga porojo endelea. Nipo kwa ajili ya kujenga chama sio kukishabikia kama wewe.

Japo si mwanaCDM imemjibu vizuri sana na kwa busara ya hali ya juu japo bado naamini hatakuelewa si tu kwa sababu labda ya uelewa mdogo bali kwa kuwa kwanza hajajua hoja vizuri na hata kama hajajua kashindws kupambanua na hata kama kaweza au kashindwa ushabiki hautampa afikie lengo.

Kuna watu wengine Mungu awarehemu tu manake they are just waiting to praised hawataki kabisa kusikia kasoro sasa binadamu au Chama kisicho na kasoro ni kipi hicho
na kasoro hizo zisiposemwa watu watajirekebisha vipi! Ulofa mbaya sana' pole sana kaka
ila toa mawazo yako achana na watu wa vijiweni.....
 
Ni hivi nenda ukawaambie waliokutuma CDM haitapoteza jimbo hata mmoja badala yake tutaongeza majimbo mengine mengii tuu, kwa ufupi wananzengo wameamka hawataki ubabaishaji wala ujanja ujanja na tena hata kwa mtutu wa bunduki jimbo la Arusha mjini halimpati ng'ooo

You are almost right. Kabla ya uchaguzi wa 2010 CDM ilikuwa na majimbo mangapi? Ilipoteza mangapi na kuongeza mangapi!!!
 
sitaki nikupinge katika hili maana hta katika jimbo langu ambalo lina mbunge kutoka chadema ninaona kama vile amejisahau na sioni kama ana mpango mkakati katika kuinua maisha ya wananchi wa jimbo letu... ila ninachoamini ni kuwa kila mbunge atahukumiwa kulingana na aliyoyafanya
 
Mabadiliko ya kimaendeleo hasa kijimbo kwa speed ya miaka 2 sidhani kama ni kigezo sana cha kutolea huku kulinganisha na miaka 35
ya ssm ...Think twice before judgement
 
Humu ndani ya JF kuna haja ya kuwapima watu wengine akili. Huyu Kadakabikile ni mmojawapo kwani hajui hata mazingira anayoishi kwa sasa. Kama anafuatilia upepo wa siasa hawezi kuja na ***** kama huo. Haya wamepewa chochote ili wararuke tu chochote ambacho hakina mashiko. Moto ulioko sasa kwa nchi nzima ni kufanya replacemrnt ya chama cha magamba. Gharama ya kutowajali wananchi kama ilivyotokea juzi kwa madaktari ni kubwa. Nadhani kuna tatizo la shule pia kwa wana JF. Tunawasihi msome alama za nyakati: hivi katika mazingira haya ya sasa mtu anakereketwa na magamba? Watu wanaoota mchana wapishe watu wajenge nchi yao.
 
CCM tutachukua majimbo yote ya Chadema mwaka 2015, CHADEMA hawatafikisha hata majimbo matano TANZANIA nzima.
Umetumwa au unaota mkuu? lakini ni aibu sana kwa mwanaume kuota mchana. utakuwa unataka kuolewa
A%20S%20embarassed.gif
 
Kuna umuhimu wa kuanza kuvinyoosha kisawa sawa hivi vi magamba vidogo vidogo vinavyo tumwa kimtindo na akina Nnape kabla havija leta madhara mbele ya safari!
 
CCM tutachukua majimbo yote ya Chadema mwaka 2015, CHADEMA hawatafikisha hata majimbo matano TANZANIA nzima.

Kama ni kauli hiyo mbona hata Mzee Makamba alitamka tena alisema CDM watapata Labda jimbo moja tu japo hakusema jimbo gani! NIKUFAHAMISHE KUWA CDM NI PROGRESSIVE PARTY,JIULIZE KWA NINI 1995/2000 hawasimamisha mgombea urais halafu comment maoni yangu.
 
...ndugu yangu Newvision mbona vitongoji vyote ulivyovitaja hapo Mbeya kuwa Sugu hajashughulikia barabara ni vya Mbeya-vijijini? Sugu ni mbunge wa Mbeya-mjini nduguyangu,siyo huko unakosema sijui Ituhe,Uyole,Isyonje,nk. ENDELEA KUWAUNGA MKONO CHADEMA,NA 2015 MBEYA ITAONGEZA WABUNGE WA CHADEMA NA MIMI MWENYEWE MUNGU AKIPENDA NTAMNG'OA PROFESSOR MMOJA KATI YA MWANDOSYA AU MWAKYUSA HUKO RUNGWE MASHARIKI AU MAGHARIBI RESPECTIVELY.
 
Vi hoja vya wamagamba utavijua tuu, yaani huwa wanaanza vizuri tuu as if tuko pamoja nao ktk ukombozi wa nchi, lakini mwishoni wana li attack jeshi letu la wabunge tena kwa nia mbayaa kabisaa. mbona wao na wabunge kwa miaka 40 hivi hawajafanya lolote si majimboni mwao wala kitaifa, kimataifa kazi kulilia posho tuu, na kuuchapa usingizi bungeni, alafu wakikulupuka ni kupiga makofi na kuvituma vimagamba kutuzubaishaa zubaisha! alooooo bahati yenu sijabahatika kumiliki AK-47.....
 
CHADEMA ina wabunge wachache ambao wanafanya kazi kubwa kulea majimbo yao na majimbo yasiyo yao ili uchaguzi ukifika waweze kushinda nchi nzima
 
CCM tutachukua majimbo yote ya Chadema mwaka 2015, CHADEMA hawatafikisha hata majimbo matano TANZANIA nzima.

Hizi kauli mbiu; "tanzania yenye neema inawezekana" na "maisha bora kwa kila mtanzania" zimetusaidia kiasi gani? Maana kila siku iendayo ni heri ya jana.
 
Wana JF wenzangu napenda kukishukuru CDM kwa chachu kiliyoleta ndani ya Bunge na serikali iliyo likizo ya CCM, Lakini ninakuwa na hofu juu ya utendaji ama uwajibikaji wa baadhi ya wabunge wetu majimboni, tunaenda mwaka wa pili sasa lakini kwenye majimbo hali bado ni tete sio kwa wananchi kupewa zawadi, michango au misaada ya mtu mmoja mmoja, ila katika kuwapanga wananchi kutumia japo raslimali kidogo zilizopo kwenye maeneo yao. Juzi niliwasikia vijana wasukuma matoroli yenye bendera ya CDM wakiuza maji wakisema mbunge wao ni mbunge wa Taifa, kwamba yuko makini sana kwenye mambo ya kitaifa ila jimboni anakuja kusalimia ndugu zake. Je kama hali ndo inaanza kuaw hivi Taswira ya chama na imani yake kwa umma wa maskini wa kitanzania itabaki wapi?

Kaka nikweli tunahitaji kuwajibika kwa wananchi na kuwa support hasa kimawazo ili waweze kutumia fursa zilizopo kujiendeleza nikweli hatuwezi kutegemea serikali maana iko biased kwa majimbo ya chadema! Wabunge wetu wanahitaji kufanya ziara kwenye majimbo na kusikiliza kero za wananchi, kero nyingine zinahitaji mawazo tu ya mbunge ili zitatulike wala si fedha!
 
CCM tutachukua majimbo yote ya Chadema mwaka 2015, CHADEMA hawatafikisha hata majimbo matano TANZANIA nzima.
No and yes. Inategemea wabunge wa pande zote watakavyoperform majimboni. Wabunge wa Chadema wakifanya kazi majimboni kama alivyokuwa akifanya Dr. Slaa, wataendelea kupata majimbo kadhaa, lakini wakiendekeza ujana wao kwenye majukwaa tu ya kelele za siasa na ndani ya Bunge (Hata ubishi wa vifungu vya sheria Bungeni wa Tundu Lissu havina tija sana kwa wapiga kura wa jimbo lake) bila kujikita kwenye kero za wananchi - maji, mbolea na pembejeo, umeme, barabara za vijijini, dawa mahospitalini, elimu duni, unyanyasaji wa wananchi na rushwa, hakika CCM watawashangaza CHadema. Lakini na wabunge wa CCM lazima pia wajikite kwenye kero za wananchi majimboni ili wasalimike.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom