Chadema kuna ushauri hapa!

sasa subiri uone negative comments toka kwa wana cdm,nafikiri hawajui maana ya siasa na opposition party wao ni kupinga tuuu hata yale mema! Hata nyerere aliongea" mnaacha yale mazuri na kuongelea ya kijinga" karibuni wan cdm tusikie pumba zenu na kutoa negative comments kuhusu hii topic
kwahiyo ndo defence mechanism uliyochagua au?
 
Umeme,Dowans,Bei za bidhaa juu,Rushwa,Katiba nk na hizi ndizo pumba unazosema wee mchangiaji mada na isitoshe leo mawaziri wamekaa kujadili ati wabadilishe sheria ya manunuzi na iruhusu serikali kununua used parts hii inaingia akilini?

ili mitambo ya dowans ipiti kwenye manunuzi. serikali kununua vitu vilivyotumika na sheria hii ikipita hapa hatuna serikali kwa uzoefu private sector ndizo zinaweza kununua used material kutokea serikalini na si serikali, sasa unataka chadema iubiri nini?

kati ya hayo yapi yamepitwa na wakati wee mchangiaji kwanza serikali jibu hayo then tutajua chadema wanatoa porojo. Watanzania wa sasa sio wajana
 
Umeme,Dowans,Bei za bidhaa juu,Rushwa,Katiba nk na hizi ndizo pumba unazosema wee mchangiaji mada na isitoshe leo mawaziri wamekaa kujadili ati wabadilishe sheria ya manunuzi na iruhusu serikali kununua used parts hii inaingia akilini? ili mitambo ya dowans ipiti kwenye manunuzi. serikali kununua vitu vilivyotumika na sheria hii ikipita hapa hatuna serikali kwa uzoefu private sector ndizo zinaweza kununua used material kutokea serikalini na si serikali, sasa unataka chadema iubiri nini? kati ya hayo yapi yamepitwa na wakati wee mchangiaji kwanza serikali jibu hayo then tutajua chadema wanatoa porojo. Watanzania wa sasa sio wajana

Nimesahau hapa spika wa bunge lelo anahutbia na kusema ati tanzania uchumi umekua na umeboreka embu wanatakwimu tuchambulieni kwa hili? uchumi wakati wanapoteza mabilioni kwa ajili ya umeme?

vipi mfumuko wa bei kila kukicha ndio uchumi umeboreshwa so, wanataka chadema wawasifie kwa yapi?
 
sasa subiri uone negative comments toka kwa wana cdm,nafikiri hawajui maana ya siasa na opposition party wao ni kupinga tuuu hata yale mema! Hata nyerere aliongea" mnaacha yale mazuri na kuongelea ya kijinga" karibuni wan cdm tusikie pumba zenu na kutoa negative comments kuhusu hii topic

Wewe naye pumba tupu! Kwa akili yako unadhani serikali ikijenga uwanja wa ndege inakuwa imefanya mazuri?

Huo ni wajibu kwa kuwa watendaji wote wa serikali wanalipwa na kodi za wananchi. Miradi yote inagharamiwa na kodi pia. Au hujui kama unalipa kodi kibao kwa kuwapo ndani ya nchi tu bila kujali una mali kiasi gani? Unatumia kauli kali kuwaponda CDM wakati wewe mwenyewe zoba la mwisho.

Kwa mawazo yako mgando utamsifu Mbunge wako kwa kuhudhuria vikao Bungeni au kwa kupanga vizuri hoja zake tofauti na wengine wajinga kama wewe wanaojua kuzomea tu? Mpuuzi kweli wewe!
 
hhahahaa pumba zilezile... yaani CCM na serikali haijawahi kuisifia CHADEMA zaidi ya kuitukana na kuidhalilisha halafu wategemee mkono wa pole kutoka CHADEMA pale wanapoumia...sahauini kabisa...!!

Ukiwa kwenye siasa hata amerika unaona republicans wanavyompinga Obama kila mahali.

Upinzani ni kumpinga mwenzako ili awekwe pembeni wewe uingie na sio kumwangalia tuu na kumsifia kama CUF na NCCR wafanyavyo... kufanya hivyo utakuwa ni ndoto kwa maana ya chama cha siasa kushika dola...!!!
 
sasa subiri uone negative comments toka kwa wana cdm,nafikiri hawajui maana ya siasa na opposition party wao ni kupinga tuuu hata yale mema! Hata nyerere aliongea" mnaacha yale mazuri na kuongelea ya kijinga" karibuni wan cdm tusikie pumba zenu na kutoa negative comments kuhusu hii topic

Unaonyesha namana gani unafanya mambo kwa maslahi ya watu fulani...nani kakwambia kuwa wa-CDM watapinga kila kitu?
 
kulingana na muda na walichokifanya ni sawa na hakuna CCm wanachokifanya ni kuharibu watoto wake kama vile mama anavyomuharibu mwanae akijua mwanae ananyonya ndio CCM wanalazimisha kulipwa kwa fedha kubao kwa Dowans hali ya kuwa wananchi wanapata mlo mmoja na ww unaandika upumbavu
 
Hivi ambacho huwa unafanya wewe kina tofauti gani? Wewe hupinga ya wanaCDM nao hupinga ya wanaCCM. Tofauti ni nini ee Kashaga na Ngekewa?
Du! Ikiwa tunakalia kupinga tu basi mwisho wake tutashindwa kujua tunazungumza nini. Nafikiri mara zote huwa nachangia pale CHADEMA wanapofanya sivyo.

Nafikiri nanyi hamtaki kuwa kama CCM kujidanganya kuwa kila mnalofanya na kusema ni sahihi au lina maana kwa Taifa.
 
Habari leo!kumbe walikuwepo kwenye mkutano wa Sugu,mbona hawajaandika mengine aliyoyasema,wamechukua moja tu,kwel kuna waandish vilaza
Usiwatukane waandishi kwani hiyo ndio kazi yao kila mmoja kumtumikia Bwana wake na hili si kwa CCM tu bali hata kwa CHADEMA.
 
Umeme,Dowans,Bei za bidhaa juu,Rushwa,Katiba nk na hizi ndizo pumba unazosema wee mchangiaji mada na isitoshe leo mawaziri wamekaa kujadili ati wabadilishe sheria ya manunuzi na iruhusu serikali kununua used parts hii inaingia akilini? ili mitambo ya dowans ipiti kwenye manunuzi. serikali kununua vitu vilivyotumika na sheria hii ikipita hapa hatuna serikali kwa uzoefu private sector ndizo zinaweza kununua used material kutokea serikalini na si serikali, sasa unataka chadema iubiri nini? kati ya hayo yapi yamepitwa na wakati wee mchangiaji kwanza serikali jibu hayo then tutajua chadema wanatoa porojo. Watanzania wa sasa sio wajana
Una uhuru wa kutafsiri unavyotaka lakini lililokusudiwa limeshasemwa.
 
Nimesahau hapa spika wa bunge lelo anahutbia na kusema ati tanzania uchumi umekua na umeboreka embu wanatakwimu tuchambulieni kwa hili? uchumi wakati wanapoteza mabilioni kwa ajili ya umeme? vipi mfumuko wa bei kila kukicha ndio uchumi umeboreshwa so, wanataka chadema wawasifie kwa yapi?


Kwani haukukuwa? Waulize wazee wako wapi tulikotoka?
 
kulingana na muda na walichokifanya ni sawa na hakuna CCm wanachokifanya ni kuharibu watoto wake kama vile mama anavyomuharibu mwanae akijua mwanae ananyonya ndio CCM wanalazimisha kulipwa kwa fedha kubao kwa Dowans hali ya kuwa wananchi wanapata mlo mmoja na ww unaandika upumbavu


Unajuwa kuambizana kuko lakini kila mtu ana uhuru wa kuamuwa anavyoona. Sijawahi na wala sitapigia debe CCM lakini nitampinga yeyote anaetumia njia zisizo sahihi kuondosha mabaya ya CCM.

Na huo ndio msimamo wangu daima, sitasema eti iondoke Amani kwasababu ya demokrasia kwani lengo la demokrasia halijawahi kuwa ni kuondowa Amani.
 
CHADEMA INAFAA KUKOMAA KISIASA

KAULI kuwa kumalizika kwa uchaguzi ni mwanzo wa maandalizi ya uchaguzi ujao, ingawa si mpya, lakini hivi karibuni imetumika sana katika vyombo vya habari na majukwaa ya kisiasa tena ikipewa maana tofauti na iliyokuwapo hapo awali.

Kauli hiyo ambayo mara kwa mara imekuwa ikitumiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) hasa baada ya uchaguzi wao wa ndani ya chama, sasa inatumiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuhalalisha maandamano na tunaona huenda ndio sababu ya kubadilishwa maana yake.

Katika maana ya awali, CCM waliitumia kauli hiyo kuponyesha makovu ya baada ya uchaguzi kwa kuwataka walioshindwa kushikana mikono, kupendana na kushirikiana kukiimarisha chama chao ili kishinde Uchaguzi Mkuu na kuongoza Dola.

Lakini maana ya sasa ya Chadema iliyojitokeza kwa vitendo ni kuhamasisha hisia za kutengana, kuharibu mshikamano na kuzuia Serikali isipate fursa ya kutekeleza majukumu yake ya kuiletea nchi yetu maendeleo.

Mifano iko dhahiri, kilichotokea mkoani Arusha na hata yaliyofanyika kwa mfululizo katika Kanda ya Ziwa ambako wabunge wa chama hicho, licha ya kuwa na majukumu katika majimbo yao, walifuatana na viongozi wenzao kusambaza propaganda kuwa Serikali haifanyi kitu chochote.

Tunaona kuwa zilikuwa propaganda zenye nia mbaya kwa kuwa pamoja na kuwa walitumia usafiri wa anga na barabarani, wakapata huduma zote muhimu, hawakusikika wakisifia kazi ya Serikali katika kuboresha mazingira ya upatikanaji wa bidhaa na huduma au uboreshaji wa miundombinu kama viwanja vya ndege, ukiwemo wa Mwanza walioutumia.

Hawakusikika, wakisifia na kuhamasisha wananchi kushirikiana na Serikali katika kuboresha miundombinu mingine kama ya barabara walizozitumia; zaidi ya kusema maneno yasiyopendeza kuhusu Serikali kuanzia mwanzo mpaka mwisho kuonesha hakuna jema linalofanyika.

Hatua hiyo ya Chadema, tumeiona kuwa ni ya uchanga inayoonesha kutokukomaa kisiasa, kwani baadhi ya mambo waliyokuwa wakihamasisha katika jamii, yanatokana na mabadiliko ya siasa na uchumi wa kimataifa au ya hali ya hewa ambayo hakuna Serikali yenye uwezo wa kuyadhibiti.

Kwa mfano, wanapigia kelele kupanda kwa gharama za maisha ambazo katika uchumi wa Tanzania, husababishwa zaidi na hali ya upatikanaji wa chakula na bei ya mafuta katika soko la kimataifa.

Pamoja na Chadema kufahamu hilo, hatukusikia wakiwaelimisha wananchi kuwa hata mgogoro wa Libya unaoongeza bei ya mafuta na mabadiliko ya hali ya hewa yaliyosababisha ukame, si Tanzania, Serikali wala Rais Jakaya Kikwete wanaohusika.

Lakini juzi, tuliwasikia wabunge wawili wa Chadema, Tundu Lissu wa Singida Mashariki na wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, wakitoa kauli za kuisaidia Serikali na kuisifu jambo lililoonesha wanakaribia kukua kisiasa.

Lissu akiwa jimboni kwake, sio katika Operesheni Sangara, alihamasisha uongozi wa vijiji katika jimbo hilo kufanya tathmini ya haraka ya hali ya upungufu wa chakula katika maeneo yao na kupeleka taarifa mapema wilayani.

Kwa kauli zao za Operesheni Sangara, Lissu alitarajiwa aseme njaa imesababishwa na Serikali iliyopo madarakani, lakini alitoa kauli ya kiutuuzima, kama kiongozi kusaidia Serikali ipate taarifa mapema ili izuie njaa na huo ndio ukomavu tunaoona umeanza kujitokeza.

Naye Mbilinyi akiwa jimboni kwake, alisikika akiipongeza Serikali kwa kujenga Uwanja wa Ndege wa Songwe, akisema ameridhishwa na hatua za ujenzi zinazoendelea baada ya kuutembelea na kuwataka wananchi wajipange kunufaika nao ifikapo Agosti mwaka huu ndege zitakapoanza kutua katika uwanja huo.

Kauli kama hiyo inapingana na kauli nyingine walizosikika wakisema kuwa kazi yao si kuisifu Serikali na kwa hili, tunawapongeza wabunge hao kwa kuanza hatua zinazoonesha wanaelekea kukua kisiasa.

Tunawashauri Chadema, kutafakari changamoto za kiuchumi, kisiasa na kijamii na kuanza kuhamasisha wananchi namna ya kushirikiana na Serikali yao kukabiliana nazo.

Tunatarajia ukomavu huo ukifikia penyewe, tutaisikia Chadema ikiimba Kilimo Kwanza, kuhamasisha wananchi waongeze uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara, si tu ili wajipatie kipato, lakini pia wasaidie kupungua kasi ya kupanda kwa gharama za maisha.

Tunatarajia Chadema ihamasishe vijana shuleni, kujikita zaidi katika masomo ya sayansi, ili Tanzania ijayo iwe na wanasayansi wa kutosha watakaosaidia kupaisha ndege yake ya kiuchumi na kijamii na sio kukimbia nchi yao baada ya kupotea kwa amani.

GAZETI LA HABARI LEO

i never knew that we still have people with black minds at this age!
 
Back
Top Bottom