CHADEMA kujazana mahakamani ili kurekodi mwenendo wa kesi kwa lengo la kupotosha jamii na kutengeneza chuki dhidi ya mahakama siyo sawa

comte

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
8,210
5,966
Mbona mwandishi anarukaru. Hii hapa iko mwananchi ila hapa hamna

Taarifa ya Uchunguzi:

Shahidi: 13/8/2020 Maabara ya uchunguzi wa Kisayansi ikipokea barua na vielelezo simu nane pamoja na simu card zake kwa ajili ya uchunguzi kubaini Mawasiliano kupitia mitandao ya kijamii Kama vule Whatsapp, Telegram, unumbe mfupi na kupiga nakupigiwa katika namba za simu zilizotangulia, usajili wa namba hizo na Mawasiliano mengine

Kisha shahidi anasoma matokeo ya uchunguzi wake.

Shahidi: Katika uchunguzi huo shahidi anabainisha jinsi namba za simu hizo ambazo amebainisha usajili wake kuwa ni za baadhi ya washtakiwa, hususan Mbowe pamoja na shahidi mtarajiwa wa Jamhuri, Luten Denis Urio, wakijadiliana kuhusu kuwapata vijana ambao wengine wametajwa miongoni mwa washtakiwa.

Shahidi: Ripoti ya uchunguzi huo inabainisha muda wa mawasiliano hayo kupitia mitandao ya kijamii, zote ujumbe mfupi wa maneno, kupiga na kupokea simu na miamala ya fedha huku mmoja akimtahadharisha mwingine kuwa asiwe anatumia namba yake binafsi kwa masuala ya pesa

Wakati Shahidi anaendelea kusoma taarifa hizo, Jaji anahoji kama kuna kusoma taarifa zote hizo na hasa viambatanisho. Anashauri isomwe ripoti ya uchunguzi na wakili Hilla anamuongoza kwenye maneo muhimu ya uchunguzi.

Shahidi anabainisha mawasiliano Kati ya Mbowe na Denis Urio kuanzia Januari 2020 jinsi walivyotafutana kwa njia ya ujumbe wa mitandao na ujumbe na call kupitia telegram na ujumbe wa maneno

Shahidi: 20/7/2020 saa 1:59 asubuhi kupitia telegram Mbowe anasema kaka wale mtu tatu au nne ni muhimu sana siku zimekwisha.

Shahidi: Baadaye alipiga simu kwa telegram

Shahidi: Saa 1:45 asubuhi Denis alimpigia Mbowe

Shahidi: Saa 1:47'46 Mbowe alimpigia Denis

Shahidi: 20/7/2020 saa 2;20 Denis amtumia Mbowe ujumbe, bro kuna memba wawili mmoja yuko Tunduma anashughulika na mabasi ya safari za nje na mwingine yuko Dodoma

Shahidi:Mboye baadaye simu siyo salama

Shahidi: Baadaye Mbowe atuma ujumbe hao wawili kuanzia siyombaya na hawawezi kutelekezwa wameshakwanbia mahitaki yao

Shahidi: Denis anamtumia Mbowe ujumbe mmoja kazaliwa 1980

Shahidi: Baadaye Denis ujumbe kwa Mbowe nitumie nauli ya kwenda nao Moro

Shahidi: Mbowe anajibu hakuna tatizo, kiasi gani

Shahidi: Denis anajibu laki 5

Shahidi: Saa 2:21:48, Mbowe anajibu sawa kaka

Shahidi: 2:22:29 Denis kwa Mbowe Nashukuru nitakujibu jioni

Shahidi: Denis usiwe unatumia namba yako binafsi kutuma pesa tumia wakala au mtu mwingine

Shahidi: Mbowe Ok

Shahidi: 27/7/2020. Denis yule jamaa anayefanya kazi Yard ameshafika

Shahidi: Yule mtu wa Tunduma anakaribia Moro

Shahidi: Denis Ila Kuna maswali wanauliza kuhusu malazi na mishahara yao.

Shahidi: Baadaye Denis ampigia Mbowe

Shahidi: 22/7/2020 : 6:26 Denis ampigia Mbowe

Shahidi: 2/7/2020 saa 6: Denis Shikamoo mkuu wale vijana tayari niko nao nimekutana nao na wako tayari kwa kazi

Shahidi: Denis naomba unipe utaratibu wao

Shahidi: Mbowe 7:38 Denis amtumia Mbowe kuwa wamekuja Dar anaomba nauli na mahali pa kukutana

Shahidi: 22/7/2020 saa7:51 Denis kwa nauli na chakula kwa wote ni Sh200.000

Shahidi: Mbowe natuma namba gani

Shahidi: Denis 0787555200

Shahidi: Mbowe ni namba ya nani?

Denis: Namba yangu

Shahidi: Denis uliyotumia juzi

Shahidi: Denis Lakini wewe usitumie namba yako

Shahidi: Mbowe: Ok

Shahidi: Mbowe wakiwa around Mlandizi watume sms wanafika muda gani nitatuma gari kuwapokea Ubungo

Shahidi: Denis: niwape namba gani muweze kuwasiliana?

Shahidi: Siku hiyo 3 Mbowe namba ninayotumia unumbe ni ya dereva wangu wamtafute yeye

Shahidi: Denis sawa, nitumie hiyo namba baadaye Denis

Shahidi: Tayari nimeipata

Shahidi: Denis: Nashukuru nimeelewa nitawapa hiyo namba.

Shahidi: Saa 12:20 jioni Denis: Tayari wameshaondoka wanakaribia Ruvu

Shahidi: Denis wale vijana wengine nimewapata Mwanza, Mtwara na Dodoma

Shahidi: Denis: Naomba kushauri uwe unanitumia fedha za kutosha kwa ajili ya ku-mobilize

Shahidi: Mbowe: kaka bado niko kamati kuu tuma ujumbe please.

Shahidi: Denis: Kuna MSG nilizokutumia kuhusu wale vijana wengine ambao wako tayari.

Shahidi: 13/7/2020 Denis: Naomba rejea msg zangu za jana usiku

Shahidi: 23/7/2020 saa 1:03 jioni Urio anapokea ujumbe wenye jina la Mohamed Abdillahi Ling'wenya

Shahidi: Urio: Mbona hujatuma majina na picha ya Adamoo ( Adamu Hassan Kasekwa, mshtakiwa wa pili?

Shahidi: Baadaye Urio apokea picha nyingine Kisha ujumbe usemao Adamu Hassan Kasekwa

Baada ya shahidi kumaliza kusoma ripoti hizo wakili Hilla anaomba ahirisho.

Jaji Tiganga anaahirisha kesi hiyo hadi saa 7:55 mchana huu ili upande wa mashtaka uendelee kumuongoza shahidi wake kutoa ushahidi wake.

Mahakama imerejea kwaajili Shahdi kuendelea kuhojiwa na wakili wwa serikali Piusi Hilla.

Shahidi: Baada ya kumaliza kufanya uchunguzi vielelezo hivi nilivifunga na kufihifadhi sikuviona tena hadi jana Ijumaa Januari 17.

Shahidi: Ijumaa iliyopita nilipigiwa simu na Inspekta Swilla kutakiwa kuja kutoa ushahidi kuhusiana na uchunguzi niliofanya.

Shahidi: Nilienda kuangalia kwenye register ya maabara ili kufahamu na Jumatatu tuliwasiliana aliniletea vielelezo.

Shahidi: Vielelezo hivyo ni simu nane na kwakuwa nilizifanyia kazi kwa kuangalia stika zilizokuwa kwenye simu zile…..

Shahidi: Hali ya vielelezo hivyo niliona jina langu na juu ya bahasha ilikuwa imeandikwa kwa makapeni.

Shahidi: Nilivihifadhi kwenye begi langu kwaajili ya usalama na kuja navyo mahakamani kwa ajili ya kuvitolea ushahidi.

Shahidi: Lakini jana kutokana na changamoto ya kiafya, nilirudi navyo na kwenda kuvihifadhi ofisini Kitengo cha uchunguzi wa kisayansi katika makao Makuu ya Polisi ya zamani na leo
 
Mbona hii imerushwa sehemu nuingi Sana Bwana mkubwa. Yaani hata Mimi namlaumu aliyerusha Jamii Forum ambaye alilalamika kuna mahali alikuwa hasikii vizuri. Kati ya ushahidi unaomtoa Mbowe bila kesi ya kujibu ni huu wa Inspekta wa IT. Msg pekee yenye ushahidi ni "Nitaambatana nao Kila mahali"?

Kwenye hizo msg umeona popote kuna mipango ya ugaidi? Kiujumla umeleta ushahidi wa kumsafisha Mbowe kabisa. Sisi wengine tumeupata mitandaoni Tangu Jana SAA 9 sijui mwenzetu Jana ulilala?
 
Mbona hii imerushwa sehemu nuingi Sana Bwana mkubwa. Yaani hata Mimi namlaumu aliyerusha Jamii Forum ambaye alilalamika kuna mahali alikuwa hasikii vizuri. Kati ya ushahidi unaomtoa Mbowe bila kesi ya kujibu ni huu wa Inspekta wa IT. Msg pekee yenye ushahidi ni "Nitaambatana nao Kila mahali"?
Kwenye hizo msg umeona popote kuna mipango ya ugaidi? Kiujumla umeleta ushahidi wa kumsafisha Mbowe kabisa. Sisi wengine tumeupata mitandaoni Tangu Jana SAA 9 sijui mwenzetu Jana ulilala?
JUMBE fupi za maneno (meseji), zinazodaiwa kuwa za Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na baadhi ya washtakiwa wenzake, katika kesi ya ugaidi inayowakabili, zimesomwa kwenye Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Dar es Salaam. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Meseji hizo zinazodaiwa kutumwa katika mitandao ya kijamii ya Telegram na WhatsApp, zimesomwa leo Jumanne, tarehe 18 Januari 2022 na Mchunguzi wa Kitengo cha Uchunguzi wa Kisayansi cha Jeshi la Polisi, Inspekta Innocent Ndowo wakati akitoa ushahidi wake mahakamani hapo, mbele ya Jaji Joachim Tiganga.

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine katika kesi hiyo yenye mashtaka ya ugaidi, ni waliokuwa makomandoo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Halfan Bwire Hassan, Adam Kasekwa na Mohammed Abdillah Ling’wenya.

Shahidi huyo wa 10 wa Jamhuri, amesoma meseji hizo baada ya kukabidhi mahakamani hapo taarifa za uchunguzi wa kisayansi za simu, alioufanya kwenye simu zinazodaiwa kuwa za kina Mbowe.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Pius Hilla, Inspekta Ndowo, alianza kusoma mawasiliano yanayodaiwa kufanyika kati ya Julai hadi Agosti 2020, katika mtandao wa Telegram, kati ya namba inayodaiwa kuwa ya Mbowe, 0719933386 na 0754612518, inayodaiwa kuwa ya Denis Urio.

Kwa mujibu wa ushahidi wa Inspekta Ndowo, meseji hizo zinaonesha namba za Mbowe alizotumia kuwasiliana na Urio, kwa ajili ya kumtafutia watu wa kumfanyia kazi pamoja na namna alivyotumia fedha za kufanikisha zoezi hilo.

Ushahidi uliowahi kuletwa mahakamani hapo na Jamhuri, unadai kuwa Mbowe alimuomba Urio amtafutie waliokuwa makomandoo wa JWTZ, kwa ajili ya kumsaidia kupanga njama za vitendo vya kigaidi, ambapo inadaiwa alitoa zaidi ya 600,000 kufadhili mipango hiyo.

Inspekta Ndowo alisoma mawasiliano hayo kama ifuatavyo:

Kuanzia tarehe 20 Julai 2020, muda wa saa 1 asubuhi, mmiliki wa kielelezo hiki (Urio), kupitia akaunti ya Telegram alipokea ujumbe kutoka kwa mmiliki wa Telegram ambayo ni ya namba ya Free (Mbowe), ujumbe unasema, “kaka wale mtu tatu au nne ni muhimu sana na siku zimekwisha.”

Inspekta Ndowo aliendelea kusoma, akidai siku hiyo hiyo Free alipiga simu kwa kielelezo hicho (Urio), wakaongea sekunde 54. Mnamo siku hiyo hiyo saa 1 asubuhi wakaongea duration (kipindi) ya sekunde 55.

Tarehe 20 Julai 2020, muda wa saa 2 asubuhi kupitia Telegram, Urio alituma ujumbe kwenda kwa Free, ambao unasomeka “Broo kuna members wawili hadi sasa, mmoja yuko Tunduma anafanya kazi katika kampuni inayosafirisha magari nje ya nchi na mmoja anafanya kazi zake.”

Tarehe 20 Julai 2020, muda wa saa 2 asubuhi, Urio anadaiwa kutuma meseji “sio salama sana niwezeshe.” Tarehe hiyo hiyo kuna ujumbe kutoka kwa Urio kwenda kwa Free uliosomeka “kikubwa ilikuwa hizo shughuli wanazofanya waziache, sasa hivi waje waelekezwe.”

Inspekta Ndowo aliendelea kusoma meseji hizo akidai, siku hiyo hiyo saa 2 asubuhi, Free alituma ujumbe katika kielelezo hicho (Urio), unaosema “hao wawili kwa kuanzia sio mbaya wanaweza kuelekezwa kuwa na mimi full time, wamekwambia wanataka nini na una maoni gani.” Saa 2 asubuhi Free alituma tena ujumbe uliosema ” sema tu kaka nitasemaje.”

Inspekta Ndowo alidai, siku hiyo muda wa saa 2 asubuhi, Urio alituma ujumbe kwenda kwa Free, unaosomeka “mmoja kazaliwa 1984 na mwingine 1986.”

Kwa mujibu wa Inspekta Ndowo, siku hiyo hiyo asubuhi, Urio alituma ujumbe kwenda kwa Free, unaosema “naomba unitumie nauli kumobilize kwenda nao Moro.” Ambapo Free alijibu akidai “no problem kaka, kiasi gani na kwa simu ipi.”

Urio alijibu ujumbe huo akisema “500,000.” ambapo Free alijibu akisema “sawa kaka tayari.

Inspekta Ndowo aliendelea kusoma akidai, Urio alimtumia Free ujumbe uliosomeka “nashukuru nimeupata, nitakupa majibu jioni.” Urio alituma tena meseji kwa Free iliyosomeka “usiwe unatumia namba binafsi kutuma pesa, tumia wakala au wasaidizi wako.” Ambapo Free alijibu “ok.”

Inspekta Ndowo anadai kuwa, kesho yake tarehe 21 Julai 2020, muda wa saa 5 asubuhi, Urio alituma ujumbe mwenda kwa Free, unaosomeka “shikamoo bro, habari ya kuamka.” Kisha akatuma tena “jamaa anayefanya kazi Yard ameshafika ninafanya mazungumzo naye.”

Shahidi huyo wa Jamhuri, amedai siku hiyo hiyo Urio alituma ujumbe mwingine kwenda kwa Free, uliosomeka “yule wa Tunduma yuko njiani anakaribia kufika Moro. Ila nina maswali wanayouliza kuhusu utawala, malazi yakatakuwaje pamoja na mshahara wao.”

Siku hiyo hiyo ya tarehe 21 Julai 2020 muda wa saa 2 jioni, Inspekta Ndowo anadai Urio alituma ujumbe kwenda kwa Free ukisema “Mkuu.”, kesho yake 22 Julai 2020 alimtumia tena meseji “mkuu shikamoo, habari ya asubuhi.” Alituma tena “vipi maendeleo ya mgonjwa wako.”

Urio alimtumia tena Free ujumbe “shikamoo mkuu, vijana wako tayari tunasubiri maelekezo yako. Nimekutana nao wote wako… niko nao na wako tayari kwa kazi.”

Siku hiyo hiyo, Urio alimtumia ujumbe Free akisema “naomba unipe utaratibu wao.” Ambapo Free alimjibu akisema “naendelea vizuri kaka.”

Inspekta Ndowo aliendelea kusoma meseji hizo akidai, Urio alituma meseji “wamekuja Dar, naomba uwatumie nauli na wapi watakapofikia.”

Inspekta Ndowo amedai, tarehe 22 Julai 2020, Free alituma ujumbe kwa Urio unaosomeka “kwa maana ya Sh. ngapi” kisha akatuma tena “tutakuwa na safari ya kwenda Hai leo usiku au kesho asubuhi.”

Shahidi huyo wa Jamhuri amedai kuwa, siku hiyo hiyo Urio alituma ujumbe kwenda kwa Free, uliosema “nauli na pesa ya kula 200,000 kwa wote wawili. Hakuna shida wako tayari.” Free anadaiwa kujibu ujumbe huo akisema “natuma kwa namba gani?” Urio alijibu akiandika namba “0787555200”.

Free alimjibu akisema “ni namba ya nani.” Urio alijibu akisema “namba yangu.” Baadae Urio alimtumia ujumbe Free uliosema “niliwatumia juzi. Lakini wewe usitumie namba yako” Free akajibu “ok”.

Inspekta Ndowo amedai kuwa, siku hiyo hiyo Free alituma ujumbe mwingine uliosema “wakiwa around Mlandizi watumie WhatsApp, wapo na basi gani? Wanafika Dar es Salaam saa ngapi, nitatuma gari kuwapokea Ubungo.”

Urio alimtumia ujumbe Free uliodai “niwape namba gani ili muweze kuwasiliana, ya WhatSApp.” Baadae akatuma tena “bado vijana wako safarini.” Ambapo Free akajibu ” namba ninayokutumia fedha ni ya dereva wangu wamtafuta yeye, yeye ndiye mwenyeji atakayewapokea.” Urio akajibu “Ok. Sawa nitumie hiyo namba ya driver.” Kisha akatuma tena “tayari mashukuru nimepata.”

Inadaiwa kuwa, Free alituma ujumbe “namba niliyotuma fedha.” Ambapo Urio akajibu “nashukuru nimeelewa nitawapa hiyo namba.” Mbowe alijibu “hope wameondoka.”

Siku hiyo hiyo muda wa saa 12 jioni, Urio alituma ujumbe “Yah tayari wameshaondoka, wanakaribia Ruvu sasa.”

Denis aliendelea kumtumia ujumbe Free uliosomeka “wale vijana wengine watatu nimewapata, Mwanza, Dodoma na Pwani. Ndio wako njiani.” Alituma tena ujumbe “nilikuwa naomba ushauri kama ikikupendeza uwe unanitumia pesa ya kutosha kuwa mobilize na kuwaleta. Hao wawili wako tayari hata kusafiri usiku.”

Inspekta Ndowo anadai kuwa, tarehe 22 Julai 2020 muda wa saa 2 usiku Urio alimpigia simu Free, kisha Free akatuma meseji “bado niko kamati kuu, tuma meseji please.” Kisha Urio akajibu “kuna msg nilizokutumia kuhusu wale vijana wengine ambao wako tayari.”

Kesho yake tarehe 23 Julai 2020, Urio alituma ujumbe kwa Free uliosomeka “naomba ujibu msg zanghapo juu za jana usiku.” Tarehe 24 Julai 2020, kisha akatuma tena “shikamoo mkuu, habari ya jioni. Wale vijana walishaondoka ni matumaini yangu kuwa kuna mtu wa kuwapokea.” Free alijibu “helo Bro nilishindwa kupokea simu yako, naamini umenielewa.”

Mbali na meseji hizo zinazodaiwa kuwa za Mbowe kwenda kwa Urio, Insepkta Ndowo alisoma meseji za Ling’wenya na Urio, zilizotumwa kupitia mtandao wa WhatsApp, kama ifuatavyo;

Tarehe 23 Julai 2020, muda wa saa 1 jioni baadhi ya ujumbe unaosomeka kuwa ni wa Mohammed uliotumwa kwa Urio kutoka kielelezo hicho ulisomeka hivi,” mbona hujatuma majina na picha ya Adam.” Ambapo alijibu kwa kutuma picha ya mwanaume na ujumbe uliosomeka Adam Kasekwa.

Siku hiyo hiyo, muda wa saa 1 usiku, Mohammed alituma ujumbe kwenda kwa Urio uliokuwa na picha yake.

Tarehe 24 Julai 2020, Mohammed alimtumia ujumbe Urio uliosomeka “bro kwema”, kisha Urio akajibu “poa dogo niaje, uko poa?”.

Siku hiyo hiyo, inadaiwa Mohammed alimtumia ujumbe Urio uliosema “mambo?” Ambapo alijibiwa “fresh, mambo yaanaendaje” Mohammed akajibu “Mungu anasaidia mpaka sasa hakuna mbaya bro.”

Urio aliendelea kumtumia ujumbe uliosomeka “hakuna lolote kutoka kwa hao jamaa.” Mohammed akajibu “tumeongea kuhusu malipo ya kuajiriwa ila bado hayajakamilika.”

Kisha Urio akajibu “yaani mlivyoongea mlikubaliana nini na kwa muda gani.” Mohammed alijibu “alidai katuajiri kabisa na mshahara kila mwezi.”

Baada ya kusoma mawasiliano hayo, Inspekta Ndowo aliiomba mahakama hiyo izipokee simu nne kati ya nane alizozifanyia uchunguzi, kama sehemu ya ushahidi wake ambapo Jaji Tiganga alizipokea.

Shahidi huyo anaendelea kutoa ushahidi wake.

Mohammed na mwenzake Kasekwa, walikamatwa tarehe 5 Agosti 2020, maeneo ya Rau Madukani, Moshi mkoani Kilimanjaro.

Mbowe na wenzake wanakabiliwa na mashtaka sita ya ugaidi, ikiwemo ya kupanga njama za ugaidi, kudhuru viongozi wa Serikali akiwemo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya. Pia wanadaiwa kutaka kulipua vituo vya mafuta na maeneo yenye mikusanyiko ya watu, ili kuonesha Serikali imeshindwa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2020.

HUO HAPO USHAHIDI WAKO!
 
Mbona hii imerushwa sehemu nuingi Sana Bwana mkubwa. Yaani hata Mimi namlaumu aliyerusha Jamii Forum ambaye alilalamika kuna mahali alikuwa hasikii vizuri. Kati ya ushahidi unaomtoa Mbowe bila kesi ya kujibu ni huu wa Inspekta wa IT. Msg pekee yenye ushahidi ni "Nitaambatana nao Kila mahali"?
Kwenye hizo msg umeona popote kuna mipango ya ugaidi? Kiujumla umeleta ushahidi wa kumsafisha Mbowe kabisa. Sisi wengine tumeupata mitandaoni Tangu Jana SAA 9 sijui mwenzetu Jana ulilala?
Mkuu sisi tunafatilia tu mwenendo wala siyo kazi yetu kuhukumu ILA tunalohoji ni kwa nini huyo msamalia mwena aliyejitolea kuacha kazi ya kutafuta riziki atumpe mwenendo nusu nusu?! Lengo lake ni nini? Kwa maoni yangu lengo ni kuyumbisha mtazamo wa jamii kuwa upande wa mashitaka hauna ushahidi dhidi ya Mbowe na wenzake
 
Mkuu sisi tunafatilia tu mwenendo wala siyo kazi yetu kuhukumu ILA tunalohoji ni kwa nini huyo msamalia mwena aliyejitolea kuacha kazi ya kutafuta riziki atumpe mwenendo nusu nusu?! Lengo lake ni nini? Kwa maoni yangu lengo ni kuyumbisha mtazamo wa jamii kuwa upande wa mashitaka hauna ushahidi dhidi ya Mbowe na wenzake
Leo naomba nikujibu kistaarabu maana umeuliza kistaarabu. Kati ya watu wanaotakiwa kupongezwa ni Mtu anayeleta updates za kinachoendelea mahakamani. Maana inahitaji Kasi na utimamu wa akili Muda wote kuweza kurekodi Mambo mengi kiasi kile lakini mengine lazima yampite. Hata baadhi ya vielelezo vinaposimwa Jaji anakubaliana na mawakili, Jamani Shahidi asome heading to au reference tu kama Mambo ni mengi. Yaani kaweka hapa caution statements ambazo serikali inaamini ndo Kila kitu halafu aache makusudi Kuweka hizo msg ambazo hazina uzito wowote?
 
Mkuu sisi tunafatilia tu mwenendo wala siyo kazi yetu kuhukumu ILA tunalohoji ni kwa nini huyo msamalia mwena aliyejitolea kuacha kazi ya kutafuta riziki atumpe mwenendo nusu nusu?! Lengo lake ni nini? Kwa maoni yangu lengo ni kuyumbisha mtazamo wa jamii kuwa upande wa mashitaka hauna ushahidi dhidi ya Mbowe na wenzake
Basi unapoona pamepelea ongezea wewe na siyo kulalamika lalamika kama mwanaume bila solution. Be positive
 
JUMBE fupi za maneno (meseji), zinazodaiwa kuwa za Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na baadhi ya washtakiwa wenzake, katika kesi ya ugaidi inayowakabili, zimesomwa kwenye Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Dar es Salaam. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Meseji hizo zinazodaiwa kutumwa katika mitandao ya kijamii ya Telegram na WhatsApp, zimesomwa leo Jumanne, tarehe 18 Januari 2022 na
Yule aliyeleta updates humu jana- hakuweka kabisa alichosoma shahidi baada ya vielelezo kupokelewa. REASON?
 
Basi unapoona pamepelea ongezea wewe na siyo kulalamika lalamika kama mwanaume bila solution. Be positive
Mkuu sasa ninaongezea kutoka wapi? maana siko mahakamani? Hebu nielekeze HOW DO I DO IT?
 
Leo naomba nikujibu kistaarabu maana umeuliza kistaarabu. Kati ya watu wanaotakiwa kupongezwa ni Mtu anayeleta updates za kinachoendelea mahakamani. Maana inahitaji Kasi na utimamu wa akili Muda wote kuweza kurekodi Mambo mengi kiasi kile lakini mengine lazima yampite. Hata baadhi ya vielelezo vinaposimwa Jaji anakubaliana na mawakili, Jamani Shahidi asome heading to au reference tu kama Mambo ni mengi. Yaani kaweka hapa caution statements ambazo serikali inaamini ndo Kila kitu halafu aache makusudi Kuweka hizo msg ambazo hazina uzito wowote?
Nakubaliana na wewe ila sidhani kama alichofanya bwana Nyendo ni sawa(!) NI KUSUDI NA NI HATARI
 
Yule aliyeleta updates humu jana- hakuweka kabisa alichosoma shahidi baada ya vielelezo kupokelewa. REASON?
Tumpe credits zake Kwa kazi nzuri anayofanya, ukiona kuna kitu hakipo vyanzo viko vingi maana wanaoleta updates wako zaidi ya watatu.
Hata hivyo nyie CCM Wenye Nia ya kumfunga Mbowe hamjakatazwa kwenda mahakamani mtuletee Yale ambayo hayaletwi na wale mnaoona ni watetezi wa Mbowe.
 
Yule aliyeleta updates humu jana- hakuweka kabisa alichosoma shahidi baada ya vielelezo kupokelewa. REASON?
Kwa akili ndogo kabisa, unadhani ni possible kuandika document yote anayosoma shahid? unafakiri hata jaji huwa anaandika mambo yote yanayosomwa kwenye hyo document wakati nakala anayo? kikubwa ni mtiririko wa cross examination baada ya document kusomwa?.Just be logical
 
Tumpe credits zake Kwa kazi nzuri anayofanya, ukiona kuna kitu hakipo vyanzo viko vingi maana wanaoleta updates wako zaidi ya watatu.
Hata hivyo nyie CCM Wenye Nia ya kumfunga Mbowe hamjakatazwa kwenda mahakamani mtuletee Yale ambayo hayaletwi na wale mnaoona ni watetezi wa Mbowe.
Kwa vile Nape karudi Habari tumuombe aiOmbe mahakama kesi iwe live TBC- NATOA HOJA
 
Mkuu sasa ninaongezea kutoka wapi? maana siko mahakamani? Hebu nielekeze HOW DO I DO IT?
Sasa kama huna taarifa sahihi na zilizokamalika kwa wakati,hoja yako inasimamia miguu ipi? Sababu hilo ni jukumu lako kama mleta mada
 
Back
Top Bottom