CHADEMA kufungiwa kwa uchochezi?

Hathubutu mtu kwa sasa kuifungia CHADEMA hata CUF...
hivi mandamano ya amani ni uchochezi ? kwani wamesema wanataka kufanya fujo?.......ni maandamano ya amani kupinga ishara za kidicteta nchini...na haya ni kwa faida ya kila mtu..tunahitaji bunge huru..
Lugumi limezimwa hivihivi na wabunge wa CCM walinywea kimyaaa, naamini hata wao moyoni kwao wanaunga mkono haya maandamano
 
Hivi kwa mfano, Serikali ikaamua kuwaacha chadema wakaandamana na kufanya mikutano ya siasa nini kitatokea? Dunia itaisha au uchumi utayumba? mm nadhan Serikali ingewaacha then ikajibu hiko ambacho wao wataongea, ila kwa wote kujifanya wababe na watemi mwisho wa siku wanainchi ndio wanaumia

Nakuhakikishia hakuna wananchi watakaoumia. Isipokuwa watu wasio na akili timamu hasa BAVICHA ndio watajiumiza kwa kumfuata . Yeye hata siku moja kwenye maandamano haonekani. Si yeye, Lowassa wala Sumye wataonekana hapo Sept. 1.
 
Kwani kila amri ya Rais ni halali? Hata kama ina kiuka sheria na katiba?
Hivi Rais akiagiza atakaye kila atakaye pitisha contena bandarini achinjwe tutasema ni amri halali?
Nchi ya kidemokrasia na inayofuata utawala wa sheria hata Rais akikiuka amapingwa hadharani

BAVICHA jaribu tu kupinga amri ya Rais uje ututhibitishie kama ni halali au siyo. Usijifiche nyuma ya keyboard na kuchakaza screen kwa maneno matupu.
 
BAVICHA jaribu tu kupinga amri ya Rais uje ututhibitishie kama ni halali au siyo. Usijifiche nyuma ya keyboard na kuchakaza screen kwa maneno matupu.
Jibu swali la msingi sio kuleta nadharia za kufikirika. Jee ni kila kila tamko la Rais ni la kisheria?
Hivi unadhani kwa dunia ya Leo mkutano unao tambulika kisheria ukifanyika na Polisi kwa amri ya mkuu wakauvamia na kuua watu hata 20 tuu nini kitatokea?
Muulize AlBashiri wa Sudan anaishi kama digidigi kwa nini?
 
Usiwe bendera fuata upepo. Anayeweza kusema hili ni halali au haramu katika mabishano ya wawili au zaidi ni MAHAKAMA.
CHADEMA inaongozwa na watu wasio na akili sana!
Kwenda mahakamani kupinga tamko la Rais ndiyo ingekuwa hatua ya kwanza.
 
Jibu swali la msingi sio kuleta nadharia za kufikirika. Jee ni kila kila tamko la Rais ni la kisheria?
Hivi unadhani kwa dunia ya Leo mkutano unao tambulika kisheria ukifanyika na Polisi kwa amri ya mkuu wakauvamia na kuua watu hata 20 tuu nini kitatokea?
Muulize AlBashiri wa Sudan anaishi kama digidigi kwa nini?

Al-Bashiri anaishi vipi kama digidigi? BAVICHA unachanganyikiwa kabisa. Hivi kwa akili yako ya kushikiliwa na Mbowe, mtaruhusiwa mvunje sheria na vyombo vya usalama vinawatazameni tu? Mbona huo mkutano wa CCM Dodoma umefanyika na wenzenu sasa hivi wana kesi hapo Mahakama ya Wilaya ya Dodoma kwa kutaka kuleta fujo? Hata kwenda kuwajulia hali tu mmefyata mikia.

Sasa nyie andamaneni hiyo Sept. 1 muone kama amri ya Rais ni halali au siyo halali.
 
Nilidhani msajili angekuwa kati ya ccm Na chadema kujua tatizo ni nini kwani mbona hiyo hali haikuwepo hapo awali? Msajili hajatoa ufafanuzi wa kisheria Juu ya zuio la serikali kuhusu mikutano
 
Nchi inaongozwa wa utawala wa Sheria, Kila kiongozi hapa nchini hawezi kuongoza anavyofikiri yeye. CDM haijaletwa na Mbowe - IPO KISHERIA.
Unasahau kuwa CDM kuwepo kisheria ni pamoja na kuheshimu sheria zenyewe.
Mbowe atatiwa hatiani kwa kifungu kifuatacho:
Sheria ya Vyama vya Siasa no 5 ya mwaka 1992 Kifungu 9(2)(c) na (f), kinachosema aidha vyama haviruhusiwi kutumia nguvu kufikia malengo ya kisiasa na kutotumia lugha za matusi, kashfa na uchochezi.
 
Al-Bashiri anaishi vipi kama digidigi? BAVICHA unachanganyikiwa kabisa. Hivi kwa akili yako ya kushikiliwa na Mbowe, mtaruhusiwa mvunje sheria na vyombo vya usalama vinawatazameni tu? Mbona huo mkutano wa CCM Dodoma umefanyika na wenzenu sasa hivi wana kesi hapo Mahakama ya Wilaya ya Dodoma kwa kutaka kuleta fujo? Hata kwenda kuwajulia hali tu mmefyata mikia.

Sasa nyie andamaneni hiyo Sept. 1 muone kama amri ya Rais ni halali au siyo halali.

Ndio maana Mwenyekiti wenu kawafananisha na ng'ombe! Huna ujualo
 
Kumbe hujui kuwa chama chako kimeenda mahakamani halafu unashauri tena mahakama iseme kuwa ni halali au la

CDM siyo chama changu. Sina chama, Popote watakapo tetea kuimarika kwa democrasia na utengamano na sheria nitawaunga mkono
 
Nchi inaongozwa wa utawala wa Sheria, Kila kiongozi hapa nchini hawezi kuongoza anavyofikiri yeye. CDM haijaletwa na Mbowe - IPO KISHERIA.
Ipo kisheria !!?
Nisheria ipi imeitaja CDM?
Au nisheria ipi inaipa nguvu CDM kufanya ujinga nchini?
 
Back
Top Bottom