Chadema kuchukua kata jimbo la Januari Makamba

Mbelwa Germano

JF-Expert Member
May 7, 2011
789
289
Ni ukweli usiopingika kwamba Mkoa wa Tanga ni ngome ngumu kwa CDM lakini ukweli huu unakwenda kugeuka kuwa uongo.Kadri siku zinavyozidi kwenda ni dhahiri kwamba upepo wa mabadiliko unazidi kushika kasi na ukweli huu utaanza kudhihirika kwenye uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Tamota Jimbo la Bumbuli.

Nimepata fursa ya kuzunguka jimbo la Bumbuli, jimbo la Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia ndugu January Makamba na kujifunza mambo mengi tofauti na unavyoweza kumsikia na kumsoma kwenye magazeti, he deserve to be called Media Boy kwasababu hakubaliliki kwa namna ambavyo watu wengi wanaweza kufikiri zaidi ya kujenga jimbo kwenye magazeti na mitandao ya kijamii. Ukweli ni kwamba ni mwepesi mno silaha kubwa anayotumia ni nguvu ya fedha basi.

Kata ya Tamota ni moja kati ya kata 29 (moja ya kata mbili kwa Mkoa wa Tanga) nchi nzima ambapo kutakuwa na uchaguzi mdogo wa udiwani, kwa hali halisi ya kisiasa ilivyo ni dhahiri kwamba CHADEMA inakwenda kushinda na kuhesabu kata ya kwanza mkoa wa Tanga. Ni ukweli uliowazi kwamba ushindi wa kata hii utakuwa na maana kubwa kwa chama na hasa katika kueneza fikra za mabadiliko mkoa wa Tanga. Ni STAMINA Amir Sheshe anayetegemewa kutangazwa kuwa diwani wa kwanza wa CDM mkoa wa Tanga mnamo tarehe 28/10/2012.

Tusubiri ushindi!
 
asante kwa taarifa, lakini pia muonekano wa january si wa mtu makini kisiasa na pia hajawahi kupigiwa kura so hana mzani mzuri, ngoja tuone kama atatetea hiyo kata kwa ushiriki wake kwa mara ya kwanza kuomba/kumuombea kura mgombea wa udiwani
 
Kama ulivyosema kinyume chake pia inaweza kuwa kweli kwamba CDM inakubalika katika kata hiyo kupitia mitandao na siyo kupitia wananchi ambao ndiyo wapiga kura, tusubiri tuone nani anakubalika kwa wananchi na nani anakubalika kwenye mitandao.
 
hapa dar nilikutana na mzee m1 namnukuu, .''hiki chama tulivyokichoka hata atayejifanya kugombea atakuwa na roho ngumu''

Mkuu isije ikawa mzee ni wewe menyewe na uliyekutana naye ni wewe mwenyewe unajua humu JF watu wengi wana vichwa viwili viwili na mara kadhaa wamekuwa wakitengeneza maneno kama haya upange mmoja wa kichwa na kuufanya upande mwingine siyo yeye na kuuita mzee mmoja.
 
asante kwa taarifa, lakini pia muonekano wa january si wa mtu makini kisiasa na pia hajawahi kupigiwa kura so hana mzani mzuri, ngoja tuone kama atatetea hiyo kata kwa ushiriki wake kwa mara ya kwanza kuomba/kumuombea kura mgombea wa udiwani

Wilaya ya Lushoto ni potential sana kwa CDM as a reference target ya kueneza fikra za mabadiliko mkoa wa Tanga tofauti na Tanga mjini, pangani, Kilindi n.k. Ukitazama jimbo la Lushoto kwa mfano uwepo wa Chuo kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa, Chuo cha usimamizi wa Mahakama (IJA) na Chuo cha ustawi wa jamii- Mabughai kumechangia kwa kiasi kikubwa uwepo wa muako mkubwa wa kisiasa hasa kwa CDM, lushoto ni wilaya yenye proptional linganifu kati ya Wakristo na waislamu hivyo hakuna udini kwa upande wa kisiasa kutokana na propaganda na maneno rahisi ambayo yamesanbazwa kipindi cha nyuma dhidi ya CDM, ni moja ya wilaya ambayo ina mchanganyiko na mwingiliano wa watu toka sehemu mbalimbali za Tanzania, n.k.
 
asante kwa taarifa, lakini pia muonekano wa january si wa mtu makini kisiasa na pia hajawahi kupigiwa kura so hana mzani mzuri, ngoja tuone kama atatetea hiyo kata kwa ushiriki wake kwa mara ya kwanza kuomba/kumuombea kura mgombea wa udiwani

Kwani Januari makamba anagombea udiwani?
 
Tusubiri tuone....

safi sana kamanda hebu simamaia hiyo show, ni kweli siku hizi January kawa Media Boy, imagine issue ya kijiji cha maisha Plus- Mama shujaa inahusika nini na wizara yake kama siyo kujipendekeza na kutaka media coverage ka ZZK,
 
mkuu tupe indicator zilizokufanya utabiri ushindi kwa mgombea wa CDM

1. Wananchi wamechoka na utawala wa CCM
2. Mgombea wa CDM anakubalika sana na wananchi wa kata ya Tamota
3. Ubovu wa barabara za kata ya Tamota umejenga hasira kubwa kwa wananchi dhidi ya CCM
4. Hamasa kubwa kwa wanawake, ikiwa ni pamoja ni kikundi cha uhamasishaji cha siku nyingi cha CCM jimbo la Bumbuli kuhamia CHADEMA na kujitolea kuhamasisha wananchi wa kata ya Tamota kuunga mkono CDM ni ishara kubwa ya matumaini ya ushindi
5. Mkakati kambabe wa kampeni kata ya Tamota ni ishara ya ushindi ikiwa ni pamoja na uwepo wa viongozi kutoka mkao mkuu ya chama.
6. Vijana wa kata ya Tamota wamejitoa vilivyo kukabiliana na hujuma zozote za CCM n.k.

Hizi ni baadhi ya indicator...
 
Ayaaa!! sa kwanini unamwamsha aliyesinzia? au ili anywe dawa ya usingizi?

Silaha kubwa ya CCM ni fedha (kuhonga, kununua shahada za kupigia kura, kuhujumu wagombea wa upinzani n.k.), Makamanda wamejipanga vilivyo, kambi imara ipo kata ya Tamota kukabiliana na hujuma yoyote ile, kata hii inatafutwa kwa udi na uvumba, ina maana kubwa sana kwa CDM,makamanda wapo mstari wa mbele...
 
Mkuu nilioona thread yako imebdi nimuombe jamaa mmoja ambaye alishiriki kumsaidia kijana J.Makamba kuzunguka kupata watu wa kumsapoti kupitishwa na chama.Ameniambia kuwa ulivyosema ni sahihi kabisa na yeye alikuwa huko Bumbuli jana ameona Cdadema wakifanya kazi yao lakini pia mwitikio wa watu ni mkubwa sana ikizingatiwa mambo ya kisiasa kwa eneo hilo ni kama ulikuwa chini sana japo wanamabadiliko ni wengi.
Kikubwa kabla ya kwenda kufanya uchaguzi ni vema mkajenga network ya uhakika na mawakala wasio na njaa na ambao they truly committed kupata mabadiliko.Wapeni elimu ya kuwajenga kiraia,kidemokrasia na kimabadiilko,wakumbusheni mateso wanayoyapata yanatokana na matumizi mabaya ya kura zao.
Jamaa hapa pia amenieleza kuwa maji ni tatizo japo vyanzo vipo huko huko bumbuli kama Mlalo- Bumbuli.Mkuu tunawatakia mpanmbano mema na mshikamane kweli kweli ili kuweza kuchukua kata hiyo.
 
Back
Top Bottom