CHADEMA: Kawambwa amebakiza siku kumi

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,244
103,937
KAULI ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa kwamba hawezi kujiuzulu, imeamsha hasira ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambacho kimesisitiza kwamba maandamano ya kumng'oa yako pale pale na sasa amebakiza siku kumi. Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, John Mnyika wakati alipotakiwa kueleza msimamo wa chama chao, hasa baada ya kauli ya Waziri Kawambwa jana kwamba hawezi kujiuzulu.

Akizungumza na gazeti hili(Tanzania Daima) jana, Mnyika ambaye ni Mbunge wa Ubungo, alisema kauli aliyoitoa Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Freeman Mbowe kwamba anampa siku 14 Waziri Kawambwa ajiuzulu, vinginevyo atang'olewa kwa maandamano bado ipo pale pale.


Alisema majibu ya Waziri Kawambwa yameonesha dharau kwa Watanzania, hasa walalahoi ambao ndio watoto wao wengi wamepata ziro katika mitihani yao ya kidato cha nne.


"CHADEMA tunaendelea kusisitiza kwamba Waziri Kawambwa ang'oke, awajibike, ameshindwa kazi na hili tunamaanisha," alisisitiza Mnyika. Alisema CHADEMA inaangalia namna ya kuitisha maandamano hayo kwa kuwashirikisha vijana waliofeli kwani wanaamini wamehujumiwa.


Mnyika aliwataka Watanzania na wengine wenye uchungu na udhaifu wa elimu ya Tanzania, hasa wazazi wajitokeze kwani fedha walizowekeza kwa watoto wao kwa ajili ya elimu, zimeteketea.


Mh. Zitto Kabwe
Naye Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe, alimtaka Waziri Kawambwa na Naibu wake, Mulugo, kuwajibika na kupisha katika wizara hiyo. Pia alimtaka Rais Kikwete aichukue wizara hiyo na kuwa chini ya ofisi yake. Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Zitto alisema kuwa ni muhimu viongozi wanaosimamia wizara hiyo wakawajibika. Alisema uwajibikaji huo unapaswa kufanyika kuanzia kwa katibu mkuu wa wizara hiyo pamoja na kamishna.


Zitto alisema kuwa rais anapaswa aelezwe kuwa iwapo matokeo yatabaki hivi mwakani, na yeye atatakiwa kuondoka katika nafasi hiyo.

Chanzo: Tanzania Daima

SWALI: NAMBA ZA SIMU ZA DR.KAWAMBWA NA AMIM AUGUSTINO ZITATOLEWA KWA WANANCHI?
 
Kawambwa alitakiwa kupelekwa ile wizara ya Sofia Simba at first place. Elimu sio mahala la kufanyia majaribio ya uwaziri kwa kuwaweke Amim Ahustino (Mulugo) na Kawambwa. Wakijiuzulu itampa pressure waziri atakayefuata kurekebisha kasoro maana naye akichemsha atakwenda na maji. Ndio maana ya uwajibikaji
 
Waondoke ,tena mara moja, hatutaki mambumbu ndani ya uti wa mgongo wa taifa letu...mbatia alipeleka hoja bungeni mkamkejeli kwa wingi wenu BUNGENI leo yamewakuta..chezea elimu wewe!!!!!!!!!!!!!!!!

NB.TATIZO KUBWA LA UONGOZI WA NCHI YETU NI KUBEBANA NA KULIPANA FADHILA.KWA STAILI HI HATUTAFIKA
 
Tuliyarajia na tunataka yatimie.MIMI NI MZAZI MMOJA WAPO NILIYEMSOMESHA MWANANGU NA WA DADA YANGU KWA GHARAMA KUBWA NA WOTE WAMEANGUKIA PUA.
 
Polisi pigeni haoooo

hivi watanzania wapo katika msiba mkubwa,alafu wewe,unaleta ushabiki,katika mambo mazito ya mstakabali wa taifa letu,katika hili hata mjinga kiasigani hataiunga chadema mkono,taifa haliwezi kuendelea bila kuwa namsingi mzuri wa elim,mwlm nyerere,alisema hivi,tanzania tunamaadui wa tatu[1]ujinga[2]maradhi[3]umaskini]na serikali yake ili weka nguvu nyingi,katika mambo,haya[3]sasa wewe ,huwezi kujua kwa sababu inaelekea,hukuwepo,sisi tulisoma bure,tulitibiwa bure maosptalini,helim ilikua bora walimu,serikali iliwajali watumishi,wake,sababu chama,kweli kilikua ni chama cha wakulima,wafanyakazi,leo jiulize ccm,ni chama cha nani,wenye,akili watajua,wapi wametoka na wapi wanakwenda,
 
Kumbukeni kuwa hawa watoto waliofeli sio watoto wa wanachama wa Chadema peke yao bali watoto wa waTanzania wote wake kwa waume; hivyo hoja ya kutaka Kawambwa ajiuzuru sio ya Chadema bali ya wananchi wa Tanzania wote ili kulinusuru Taifa hili! Inawabidi wananchi muoneshe hasira yenu kwa kudorola huku kwa elimu kwa vitendo hivyo jitoikezeni kwenye maanadamano siomnakalia kulalamika tu!
 
KWANI UNAWEZA KUPANDA MAHINDI UKAVUNA MAHARAGE?

CCM MLIIWEKA MADARAKANI MNATEGEMEA NINI?
Shukuru kawambwa ata-eliver nini!
Wasira ?
Lukuvi?
Yule waziri wamaji Prof. ..ataifanyia nini nchi!
karia maziri wote akiwemo rais wao hamna kitu!
 
hivi watanzania wapo katika msiba mkubwa,alafu wewe,unaleta ushabiki,katika mambo mazito ya mstakabali wa taifa letu,katika hili hata mjinga kiasigani hataiunga chadema mkono,taifa haliwezi kuendelea bila kuwa namsingi mzuri wa elim,mwlm nyerere,alisema hivi,tanzania tunamaadui wa tatu[1]ujinga[2]maradhi[3]umaskini]na serikali yake ili weka nguvu nyingi,katika mambo,haya[3]sasa wewe ,huwezi kujua kwa sababu inaelekea,hukuwepo,sisi tulisoma bure,tulitibiwa bure maosptalini,helim ilikua bora walimu,serikali iliwajali watumishi,wake,sababu chama,kweli kilikua ni chama cha wakulima,wafanyakazi,leo jiulize ccm,ni chama cha nani,wenye,akili watajua,wapi wametoka na wapi wanakwenda,


Ni kweli kwa matokeo yaliyotangazwa Tanzania tuko kwenye msiba mkubwa. Tuko kwenye maombolezo na sijui kama Mjomba anajua hili maana kila jambo linalotokea Mjomba anachukulia masihara. Sisi walala hoi tutafunga mikanda mpaka lini? lazima wawajibike..
 
Sishangai haya madudu katika elimu, mawaziri wenyewe ni wababaishaji; mnategemea mti wa mnazi utatoa maembe? Hii wizara ya elimu inahitaji watu makini kama vile akina magufuli na mwakyembe. Waziri asyejua hata document za ofisi yake kama vile mitaala, asiyeona kosa lake hata akiambiwa, majukwani wanasimama na kusema walimu hawaongezewi mishahara hata wafanyeje. Nimekerwa sana na matokeo ya form 4. Mawaziri waondoke tu madarakani.
 
Watoto walifeli kwa sababu ya njaa - Shukuru Kawambwa (hapa ndio ametumia za kuambiwa akachanganya na za kwake, angetumia za kwake peke yake sijui ingekuwaje?)

Hivi Kawambwa na Mulugo walipata nini form IV na VI? Tunataka tujue kama na hawa ni wale vihiyo wa CCM wanaofeli then wana-fluke na kupata PhD za kuandikiwa.
 
wangeandamana waislamu hapo watu mngesema waisalamu wanapenda fujo, tulipotaka wajiuzulu hao mwanzo mkatuona sisi akili hatuna leo hii kwa sababu chadema ndio wanataka kuandamana kwa kutafuta political gain na nyie ndio mnaona sawa, kweli mkuki kwa nguruwe tu, sasa sijui na haya maandamano polisi watazuia au kanisa litabariki
 
Polisi pigeni haoooo
Polisi si ndio wale waliotaga mayai mashuleni, na ndio CCM wanaowataka, watu wasiotumia akili, wao ni kama dogs, akiambiwa shh kamata, na yeye anakimbia kukamata hata bila kuuliza kosa la anaekamatwa.
 
CCM tumewachoka,..Elimu duni,Afya duni,Maji duni,mnajua UFISADI na KULINDANA tu..
 
Back
Top Bottom