CHADEMA inahitaji viongozi wa aina gani nyakati hizi?

Oct 5, 2015
88
476
CHADEMA INAHITAJI VIONGOZI WA AINA GANI KWA SASA?

(Andiko hili lina chembe za ushetani ndani yake)

Haya ni maoni yangu binafsi juu ya aina ya viongozi wanaohitajika kwa faida ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, kwa kutazama mfumo wa utawala uliopo nchini Tanzania kwa sasa, lakini pia kwa kutazama mwenendo wa siasa za ulimwengu wa leo.

Maana ya uongozi.
Kwa tafsiri fupi ya kileo, uongozi ni ule uwezo wa kushawishi watu wengine watende vile anavyotaka huyo kiongozi. 'KUSHAWISHI" ndio siri ya uongozi. Mtu yeyote mwenye uwezo wa kushawishi ni kiongozi, iwe kwa maneno, kwa vitendo, kwa maandiko au kwa mbinu zingine. Haijalishi mtu huyo ana nafasi gani serikalini, au kwenye chama, au popote, isipokuwa tu kama ana uwezo wa kuwashawishi watu watende vile anavyowashawishi basi huyo ndio kiongozi.
Kushawishi maana yake kuwafanya watu waamue kwa hiari yao kutenda vile anavyotaka huyo mshawishi. Kwa maana hiyo, kama watu watalazimishwa au watawekewa mazigira ya kulazimika kufanya jambo fulani bila hiari yao, hao watu hawajashawishiwa au hawajashawishika. Hao watu, wanaweza kubadilisha maamuzi wakati wowote, au hata kuasi kwa sababu hawakuamua kwa hiari yao kufanya hayo wafanyayo.

Na ikiwa mtu atashindwa kuwashawishi watu, basi huyo mtu sio kiongozi hata kama ana nafasi kubwa kiasi gani serikalini. Uongozi ni ushawishi, na kiongozi anapofikia ukomo wake wa kushawishi basi kama ana hekima anawapisha wengine kwa kujiuzulu. La! Wapo wengi wanaong'ang'ania nafasi zao kwa mabavu, wengine kwa kutengeneza mbinu za kupata ufuasi, wengine kwa uongo na ulaghai...yote hayo ni kwa lengo la kutaka kujionesha wana ushawishi na wanakubalika.

Uongozi wa kisiasa unaweza kuwa moja ya kazi ngumu sana kwa kiongozi mwenye nia ya dhati, lakini yaweza kuwa kazi rahisi sana kwa kiongozi ambaye lengo lake ni kushawishi tu bila kujali anashawishi kitu gani, hasa kwenye nchi kama Tanzania ambapo wananchi wengi bado hawana fikra na misimamo huru, pia hawana taarifa na hawajisumbui kuzitafuta taarifa. Wananchi wa aina hiyo ni rahisi kuwadanganya na kuwalaghai na kwa hiyo ni rahisi kwa kiongozi asiye na nia ya dhati kudumu katika nafasi yake.

Ni wakati gani uongozi wa kisiasa unakuwa mgumu sana?
Uongozi wa kisiasa unakuwa mgumu kwenye jamii zenye makundi makubwa ya watu wenye itikadi tofauti za kisasa, kiimani, utamaduni nk. Itahitaji kiongozi mwenye ufahamu juu ya imani, mitazamo na misimamo ya makundi hayo ili aweze kuwashawishi. Na ugumu unaongezeka zaidi ikiwa watu hao wameelimika na hivyo wana uwezo kuhoji na kuhitaji majibu ya kuridhisha kabla hawajashawishika kufuata jambo fulani. Ni vigumu kuongoza jamii ya watu walioelimika ambao miongoni mwao kuna wanaofahamu kwa undani mambo mengi kuliko anavyofahamu kiongozi.

Kwa Tanzania, wananchi wengi hawajaelimika na hata wanaofikiriwa kuwa wameelimika ni watu waliokaa masomoni kwa muda mrefu na hiyo haina uhusiano na kuelimika. Pia, wasomi wengi ambao ni watumishi wa umma au taasisi binafsi 'hawapotezi muda wao kushiriki kwenye siasa' na hivyo kutoa nafasi nyingi kwa watu ambao ni mashabiki wa siasa tu, na watafuta chochote, huku wananchi nawo wakisubiri kudanganywa na kulaghaiwa ili washabikie mtu au chama fulani.

Ni vigumu kwa wasomi wanaojitambua kushiriki siasa za Tanzania, na baadhi yao wanaojiingiza kwenye siasa wanalazimika kujitoa ufahamu ili wadumu ndani ya siasa, au wakishindwa kujitoa ufahamu wanajikuwa nje ya ulingo wa siasa za Tanzania. Ni kwa sababu jamii ya Watanzania inaweza kushawishiwa hata kwa uongo wa wazi kabisa bila shaka yoyote, ali mradi roho ya ushabiki ilishapandwa ndani yao. Wasomi wachache wenye ufahamu hawana athari; kwanza kwa sababu ya uchache wao, pili kwa sababu hawajihusishi na siasa, tatu kwa sababu ya woga wa kushughulikiwa na wanasiasa wenye madaraka walioyapata na wanayoyatunza kwa kutumia 'ujinga' wa watanzania.

CHADEMA inahitaji viongozi wa aina gani?
1. Kazi kubwa ya maana iliyofanywa na Chadema ni kutoa elimu ya uraia kwa wananchi. Kwa kipindi cha miaka ya 2005 hadi 2015 Chadema kikiongozwa na Dr. Wilbroad Slaa kilijikita sana kwenye kutoa elimu ya Uraia, na hiyo ilisaidia wananchi wengi kuanza kufuatilia siasa za nchi yao. Siasa ikapokelewa kwa kasi mitaani, vyuoni, makazini na hata mashuleni. Kumekuwa na faida kubwa, lakini pia kumekuwa na hasara baada ya watu kuipokea siasa na kuifanya ndivyosivyo. Lakini kwa ujumla wake ni kazi nzuri.
Kitendo hiko cha kutoa elimu ya uraia kwa mtindo wa kushawishi wananchi wakubaliane na sera za Chadema kilipelekea Chadema kujizolea ufuasi mkubwa wa watu katika kila pembe ya nchi. Tuliozunguka kwenye kampeni mwaka 2015 tuliona Chadema ilivyoenea hadi vichochoroni kwa wasiojua kiswahili. Kazi yetu haikuwa kushawishi tu, bali pia kutoa elimu ya Uraia na kwa hiyo wananchi wanapoelewa mambo ambayo hawakuwa wakiyajua hapo kabla, basi wanajikuta wakishabikia upande wa yule aliyewaelimisha - Chadema.

1. Kutokana na uzoefu huo mdogo, naweza sema Chadema inahitaji viongozi wenye ufahamu mkubwa katika siasa na elimu ya uraia, na hata ufahamu wa mambo mengine, ambao wanapohutubia basi watu wanajifunza vitu vya msingi na 'automatically' wanakuwa na mapenzi na Chadema. Kutoa elimu au tarifa muhimu kwa watu, na kwa namna inayoteka husia za watu ni mbinu nzuri ya kuvuna ufuasi. Dr. Slaa, Mh. Zitto Kabwe, Prof Kitila Mkumbo ni baadhi ya watu wenye uwezo wa kushawishi kwa namna hii. Nimewataja hao makusudi kwa kuwa sasa hawapo Chadema ili isionekane napigia watu kampeni. Hata Sasa wapo wengine wengi wenye uwezo huo ndani ya Chadema.

2. 'CCM bila dola ni karatasi nyeupe'. Ni ukweli kwamba vyama vya upinzani nchini Tanzania havishindani na CCM, bali vinashindana na dola. CHADEMA inashindana na Serikali, Polisi, Bunge, Usalama wa Taifa (hii ni bahati mbaya kwa nchi), na kwa wakati fulani mahakama na Jeshi (hii ni bahati mbaya zaidi). Ni kazi ngumu kwa chama cha siasa kupata nguvu kubwa ya ufuasi hali kikiwa na 'maadui' wa haiba hizo, si rahisi. Lakini Chadema kimepata ufuasi.
Kwa sasa **** nguvu kubwa inayotoka kwenye vyombo hivyo ikiwa na lengo la kuidhoofisha Chadema, nguvu hiyo ni kubwa kiasi cha kuweza kusababisha mauti kwa watu watakaopingana nayo. Huo ni ukweli mtupu na ushuhuda unatosha hata sioni haja ya kueleza hapa. Ni ukweli kwamba kazi ya kukosoa ambayo ni moja kati ya kazi za upinzani, inaweza kupelekea mtu kutekwa na hata kupotezwa kabisa. Kwahiyo ni sawa kusema kila mkosoaji wa serikali hii ya Magufuli, yupo katika hatari ya kupotea.

CHADEMA inahitaji viongozi ambao, kama ilivyo ada ya majukumu ya upinzani watalazimika kuwa wakosoaji wa baadhi ya mambo yanayofanywa na serikali ya CCM, na kwakufanya hivyo watajiweka kwenye hatari kubwa, hata kupoteza maisha. Wanachama wa Chadema wanaoendelea kufanya uchaguzi wajue hilo, na wagombea wa nafasi mbalimbali wajue hilo. Nawashauri wanachama wa Chadema wanaotafuta kipato kupitia uongozi ndani ya chama waende CCM, lakini Chadema ni mateso matupu kwa mtu anayetafuta kipato. Viongozi wanaohitajika Chadema kwa sasa ni wale wasiohitaji uongozi kwa ajili ya kipato. Na hiyo simaanishi watu masikini, la! Bali watu waliojitosheleza na ambao wamejaribiwa na wamekuwa na misimamo, bila kujali hali zao za kiuchumi. Uongozi wa Chadema ni wito.

3. Siasa za Tanzania hasa kipindi cha Magufuli, ni siasa za uadui. Ni siasa za damu. Ni siasa za chuki. Ni siasa za uhasama, uongo, ukatili, ulaghai, ukomoaji, dhuluma, ujinga nk. Na mambo hayo yanafanywa hadharani bila aibu yoyote na hupokelewa na wafuasi wa CCM ambayo kwa kutumia nyenzo za dola imekuwa ndio bingwa wa siasa hizo. Idadi ya viongozi na wanachama wa Chadema waliouawa kikatili kwa silaha za jadi na wengine kumiminiwa risasi hadharani, kwa sababu za kisiasa, inatosha kusema tupo kwenye siasa za uadui wa kifo.
Kwa sababu ya mazingira hayo, baadhi ya watu wanadhani Chadema inahitaji kiongozi 'machachari' atakayekwenda sawa na mazingira hayo. Kwa lugha nyingine, watu hao wanaamini kwamba Chadema inahitaji viongozi vijana, viburi, wenye kauli hamasishi, 'wenye jazba' na wanaochukua hatua papo hapo. Kwa muono wangu hilo si sawa.
Katika mazingira ya sasa, Chadema ikipata viongozi wa aina hiyo itapoteza sana. Watakamatwa zaidi kuliko sasa, watapewa kesi nyingi na mbaya zaidi kuliko sasa, watafungwa au hata kuuawa.

Ni viongozi wa aina gani sasa wanaohitajika?
Kwa mazingira yaliyopo Tanzania, Chadema inahitaji viongozi wenye akili na hekima kubwa, lakini pia wajue kuwa siasa za sasa ni siasa za damu Kama nilivyosema hapo juu. Viongozi watakaojua kuwa hakuna ushindani wa maana kati ya upande unaopoteza na upande unaopata, bali ushindani wa maana ni kwa pande mbili zinazopoteza au zinazopata.

Hakuna maana kama viongozi na wafuasi wa Chadema tu ndio wanaotekwa na kuuawa kwa silaha za jadi na risasi, huku viongozi wa CCM na wafuasi wao wakijifanya kutoona au wakati mwingine kutengeneza stori za kuchukiza zaidi. Ilipaswa kuwa, pande zote mbili zipoteze - hapo ndipo kuna suluhu.
Hata hivyo, si rahisi kwa Chadema kufanya yale wanayofanyiwa na CCM kwa sababu hawana dola ya kuwalinda. Ikiwa utekaji unaofanywa na CCM unaratibiwa na baadhi ya watumishi wa usalama wa Taifa, Chadema wakitaka kufanya hivyo watafanikishaje? Watumie vijana wao wasio na ujuzi wa masuala ya intelijensia ili wakamatwe na kupewa kesi mbaya? Hapo ndipo panahitajika viongozo wenye akili kubwa na hekima ya kutosha. Pointi ya msingi ni kuwa, bila kuwashughulikia CCM kama wao wanavyoshughulikia wapinzani huku wakiamini eti ni 'michezo ya kawaida kwenye siasa' basi hakutakuwa na kusonga mbele. Ni lazima CCM ilazimike yenyewe kutafuta suluhu, na hilo litawezekana kama wataanza kupoteza kama wanavyowapoteza wengine. Bila CCM kupoteza, mambo yataendelea kama yalivyo.

Hekima na akili za viongozi wa Chadema zitasaidia wao na wafuasi wao kuepuka mkono wa sheria na kuepuka kuchukiwa na jamii wakati huohuo wakiwatia adabu CCM kwa siasa za damu zilizoanzishwa na CCM yenyewe. Viongozi hawapaswi kuchochea chuki hadharani, hawapaswi kuhamasisha vurugu hadharani, hawapaswi kutangaza vita hadharani, badala yake wahubiri upendo, amani, msamaha na umoja wa kitaifa. Lakini wasiruhusu damu za wafuasi na viongozi wao zimwagike bila majibu.
Hakimu atakayemuhukumu kifungo kiongozi wa Chadema kwa kesi ya kisiasa, asamehewe hadharani, na kumwachi Mungu. Huku wafuasi wakipozwa wasifanye chochote. Lakini siku chache baadaye hakimu huyo au jaji huyo 'avamiwe' na majambazi, au 'ajirushe' chini kutoka ghorofa ya saba, au 'ajinyonge' au 'ajilishe sumu' au apate ajali mbaya...hivyo yani.
Wakuu wa wilaya au mikoa wanaonea viongozi wa Chadema na wenyewe wasamehewe hadharani, waombwe waache uonevu kwa maneno ya hekima na busara...lakini wakizidi basi 'Mungu' afanye kazi yake. Wapigwe rungu na mtu kichaa, au 'wajipige' risasi, au 'wadondoke' bafuni na kuvunjika kiuno, wavamiwe na 'vibaka'. Hayo yote yawe kazi ya Mungu - maana yake yasiwe na ushahidi. Ndio maana yangu ya Hekima na Akili.
Kwa matukio kumi tu ya hivyo yakiwatukia watu wenye ushawishi ndani ya CCM yatasaidia sana kurejesha siasa za kuheshimiana.

4. Chadema inahitaji viongozi wenye ushawishi ndani na nje ya mipaka ya Tanzania angalau kwenye nafasi za juu; Mwenyekiti, Katibu mkuu, makamu wao na viongozi wa mabaraza hasa baraza la wanawake 'Bawacha' na baraza la vijana 'Bavicha'. Viongozi wenye ushawishi nje ya mipaka ya nchi watasaidia kuitangaza Chadema na kupata kuungwa mkono kutoka kwenye taasisi za kimataifa na kwahiyo kujiongezea ushawishi na heshima ya ndani. Sio kazi rahisi kupata ushawishi kimataifa lakini ni Jambo linalowezekana kwa watu wenye ufahamu wa diplomasia na mahusinao ya kimataifa ikiwa watazitumia vema jumuia za kimataifa.

5 (i) Uvumilivu, Ustamihilivu na Ujanja. Viongozi wavumilivu watavumilia misukosuko kutoka ndani na nje ya Chama na kuchukulia kama sehemu ya maisha yao. Lakini pia wanahitaji kuwa wajanja wa kuwagundua na kuwashughulikia wanachama wenye nia ovu bila kusababisha madhara kwa chama.

(ii) Ugatuzi, Urithishi na Uandaaji wa viongozi.
Chadema inahitaji viongozi watakaogawa madaraka kwa viongozi wa ngazi za chini na pia kuwarithisha uwezo wa kuongoza. Viongozi wanaofahamu kwamba hawatakaa madarakani kwa kipindi chote cha maisha ya Chadema, na kwahiyo waandae warithi watakaoendeleza kazi nzuri iliyofanywa na waasisi wa Chama. Hii ndio mbinu bora kabisa ya kuwashinda wanaokesha wakipanga kuiua Chadema - kuandaa viongozi.
Nawasilisha.
 
Nimekusoma vizuri. Point imetulia. hasa hiyo 3. ila mchezo uwe mtamu lazima watu wa system wawepo ndani kuwatambua mamluki system. Hii ccm wanaianzisha wenyewe mfano mimi siamini mpaka sasa mzee Kingunge eti kafa kwa kuumwa na mbwa home kwake. ilikuwa ajari ? NO. siafiki
 
Mnapotoa mawazo ya aina hii muangalia na mwenendo wa siasa kwa nchi hii ulivyo,siamini kama Chadema hawafanyi kama walivyokuwa wanafanya kabla ya Awamu hii.Awamu hii wote tumeshuhudia Mikutano ya hadhara imezuiliwa kwa vyama vya upinzani,mikutano ya ndani nayo kwa vyama vya upinzani ni tatizo,Viongozi wa vyama vya upinzani hasa Chadema wote wana kesi katika Mahakama mbalimbali,viongozi wa vyama vya upinzani wengine wamefungwa kwa kuonewa Wabunge na madiwani wa vyama vya Upinzani wanarubuniwa na kuvihama vyama vyao na kisha, kurudishwa na kuwa wa chama tawala,ili mradi ni misukosuko kwa vyama vya upinzani.Je hayo ukiyoyaandika yatatekelezeka kwa aina hii ya siasa?
 
Maelezo mengi point chache hivyo humchosha msomaji
But kazi nzur

Y
 
Toka nimejiunga jamii forums leo ndio mara ya kwanza nimekutana na mada iliyoenda shule. Hii ni mada yenye nguvu ya ajabu na ukweli usioacha shaka. Kwa kiwango fulani umeendana na mawazo yangu. Nimewahi kusema zaidi ya mara moja, nchi hii hakuna chama cha siasa kinachoitwa ccm, bali kuna kikundi cha dola kinachotumia ccm kufanya siasa. Ukitaka kuamini kuwa ccm sio chama cha siasa angalia uchaguzi wa juzi, watu wengi waligoma kujiandikisha kupiga kura, ila ccm ikakazimisha kushinda kwa asilimia mia moja. Angalia viongozi wote kabla ya kujiunga ccm au wakitoka wanachoongea, na wakiwa madarakani ndani ya ccm wanaongea na kutenda nini. Sasa ni dhahiri kabisa kuwa dola ndio inafanya siasa kwa mgongo wa chama cha siasa.
 
Back
Top Bottom