CHADEMA imeng'ara kwenye Uchaguzi na Itashinda 2015

Ushindi wa CHADEMA ni nguvu ya Umma. CCM ni kama timu za Uarabuni. Wao kushinda kwa mabavu, hila na fitina ni kawaida sana kwao!
Tume ya Uchaguzi inawabeba; Polisi inawabeba. Lakini yote yana mwisho. Na mwisho wa hila ni adhabu ya kusambaratika vipande vipande!

Hivi sasa kuna ccm tatu, ipo ya kikwete, ya lowasa na ipo ya wajiitao wapinga ufisadi,
 
Hujakosea herufi, umekosea maana nzima.
Yaani mantiki yote haieleweki ... labda ulitaka kufafanua LOCAL POLITICS na kusema kuwa kuna geographical "issues" na general "issues"?

Lazima utakuwa ni mgambile enough maana ndio wenye kujifanya mnajua kizungu.
 
Inawezekana kauli yangu isiwaingie watu masikioni mwao kabisa, lakini nitawaeleza japo kwa kifupi.

Katika siasa kuna kitu kinaitwa siasa za jumla (general politics) na siasa za kijiografia (geography politics)

General politics inahusu mambo yanayohusu siasa za kitaifa bila kuchagua chama au itikadi na hizi mara nyingi husimamiwa kwa katiba, kanuni na sheria za nchi, hapa inahusiana pia na daftari la wapiga kura na tume ya uchaguzi,

Geography politics inahusu siasa za eneo husuka, kuna international gp, na domestic gp,

Katika hayo Chadema ime win kwenye Gp-D kwa asilimia zaidi ya 90%, hili linatokana na chama kushiriki uchaguzi kwa miaka yote huku mambo muhimu yanayopaswa kufanywa kwenye General Politics yakiwa doro kabisa, mambo hayo ni kama tume kuwa huru, daftari la wapigakura kuboreshwa, na dola kuvuruga chagizi nyingi kwa maslahi ya ccm.

Takwimu za chaguzi hizi zinatoa sura stahiki ya ubora wa domestic political ya Chadema,

Mathalani uchaguzi huu Chadema ilikuwa ikitetea kata 3, za Nyaisura, Kiborloni na Mikol.. Kigoma.

Tumepoteza Nyaisura, na Kigoma, na Tumeipoka ccm kata za Sombetini na Njombe.

Tamani ya kata ilizoshinda chadema nikubwa kuliko ccm, kubeba kata ya njombe ni turufu kubwa, vivyo hivyo kata ya sombetini. CCM hawajaongeza thamani yoyote ya kata,

Kwa lugha nyingine nikuwa CHADEMA 0-0 CCM, lakini CHADEMA wananafasi ya golden goal kwakubeba kata ya Njombe ambayo kwanza inafuta propaganda za ccm yakuwa chadema ni chama cha ukanda, sasa tunashuhudia Chadema sio chama cha ukanda tena bali chama cha kitaifa na kila pembe ya jamhuri hii.

Izingatiwe kuwa oparesheni Pamoja Daima haikuwa maalumu kwaajili ya uchsguzi huu bali sehemu ya ratiba ya chama katika kutoa elimu ya umma kudai/kuhimiza uboreshaji wa daftari la wapiga kura.

Naamini hapo mmenipata ndugu zangu mnaojenga hoja dhaifu kuwa kama dhana ni daftari la wapiga kura na polisi why kwingine chadema imeshinda?
Kuna watu kama wewe unaweza ukadhani unaisaidia sana CHADEMA katika ukuaji wake kumbe propaganda zako ndizo zinazoididimiza kabisa hasa pale unapochukua nafasi ya mmojawapo wa watu walio karibu na jiko la maamuzi ya CHADEMA (false position).

Kwanza hoja yako hii hapa juu ina matobo mengi ya kisayansi katika siasa kwa ujumla achilia mbali hali ya ksiasa nchini Tanzania bila hata kugusia maneno uliyotumia katika hoja yako.

Ukiangalia katika nchi nyingi zenye vyama vya kisiasa ambavyo ni mbadala halisi wa chama tawala kidemokrasia utaona kuwa chaguzi ndogo huwa ni mwiba kwa chama tawala kutokana sababu nyingi lakini sababu kuu huwa ni mbili.

1) Wapiga kura kuanza kukata tamaa kutokana na ahadi kupitia ilani ya uchaguzi kusua sua au kutokutimizwa na chama tawala huku muda uliobakia wakiona kama hautoshi kuzitimiza. Kwa maana nyingine, ile euphoria inayopatikana baada ya uchaguzi huwa inakumbana na political reality.
2) Chama pinzani kuwa na fursa ya consolidate uwezo wao katika human resources (human capital) and fund kutokana na uchache wa maeneo ya chaguzi yanayofanyika.

Kunapotokea hali ambayo chama mbadala hata chaguzi ndogo kinashindwa kukitikisa chama tawala lazima kutakuwa na maswali mengi sana ambayo yanataka majibu halisi ili kuweza kuondoa sababu zilizosababisha kushindwa kutoa mtazamo chanya katika chaguzi kuu ijayo.

Kwa kutumia mifano yako hiyo, Ningekuelewa kama ungesema CHADEMA kwa sasa bado haijafikia nafasi ya kuongoza nchi, kwa maana nyingine, iko kwenye mkakati wa pili wa kisiasa kwa vile haijakuwa chama cha kitaifa ndiyo maana imeanza kupata maeneo mengine ya nchi kama kwenye Kata ya Njombe. My goodness, this is 2014.

CHADEMA kwa vile kimeingia kwenye chaguzi na kinajinasibisha kama ni chama ambacho kiko tayari na kinasubiri muda kisheria kupewa nchi kuongoza, basi kilitakiwa angalau kishinde nusu ya kata zilizofanya uchaguzi au zinazofanya chaguzi ndogo bila kujali ziko pande gani ya nchi.

Kukaa hapa na kuanza kujipongeza kwa mtazamo wa chama kama ndiyo kinaanza kujijenga ni kufurahisha jukwaa lakini hakuondoi uharisia wa kuwa kilichofanyika ni total failure bila hata kuangalia nguvu iliyotumika katika kuzitafuta hizo kata.

Ukiangalia zaidi, utagundua kuwa hoja uliyojitahidi kuijenga hapa inapingana kabisa na hoja iliyoijenga kwenye thread hii,

Tatizo lako unajitahidi kutetea swala ili kufurahisha macho ya wapenda kusikia mazuri tu ya chama badala ya kuangalia mabaya yake kwa faida ukuaji wa chama ndiyo ukasahau hata ulichokiandika na kukiweka saa 10:39, yaani masaa 7 tu kupita, ukawa tayari umebadilisha mtazamo. Hata hueleweki unasimama kwenye nguzo gani kisiasa katika matokeo haya ya uchaguzi. Hapo hapo unasema chama kinayumba na hapo hapo unasema chama kimefanya vizuri sana!.

Hebu soma ulichokiandika hapa saa 10:39,

Nimeshiriki hatua zote za uchaguzi katika katika kata 27 nchini, nasema nimeshiriki kwa 100%, sijasimuliwa, wala kusikia tu,

Uchaguzi wa udiwani katika Kata 27 umemalizika kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kujinyakulia ushindi.

Hata hivyo, ushindi wa chama hicho katika uchaguzi huu ulitarajiwa kwa sababu nyingi zikiwemo zile zilizozoeleka nyakati zote za uchaguzi kama, kutumia vyombo vya dola, na serikali kwa ujumla kuwadaidia wao.

Hoja ya msingi hapa ni je haya yametokea katika uchaguzi huu tu ama yalikuwepo katika chaguzi zote??

Kuna wanaoamini kuwa Chadema kuwaadhibu wanachama wake waliovunja katiba ya Chama Zitto, Killa, Mwigamba eti ni "Mgogoro" uliochangia kwa 100% kushindwa uchaguzi huu.

Nikubaliane nao wale wafikirio hivyo akini niwape shule ya falsa ya siasa kidemorasia,

Niwakumbushe kuwa, mwaka 1958 chama cha TANU kikiwa kwenye vuguvugu kali la kupigania Uhuru, kiliwafukuza kabisa uanachama Katibu Mkuu wake Mr Mtevu, na Mwenyrkiti wa Baraza la Wazee ndugu Seleiman Bin Amir aliyekuwa na nguvu ya ushawishi hasaaa, walifukizwa waliposhindwa uchaguzi mkuu uliofanyika katika ukumbi wa shule ya wavulana ya Tabora pale kanda ya Magharibi Tabora na Julius Nyerere akawa rais wa TANU, baada ya uchaguzi ule wao walianzisha uasi kwakuanzisha chama ndani ya chama, chama hicho kilikuwa cha kidini. TANU iliyumba kwa mwaka kamamoja hivi lakini mwaka 1961 ikaingia katika uchaguzi na kushinda.

Kwanza niwaambie kuwa Chama cha siasa kilichokomaa na chenye wanachama wenye nguvu ya kitaifa kinapotokea kumuwajibisha mwanachama yeyote mwenye nguvu ya kitaifa, kovu lake huwa halizibwi kwa miezi mitatu au sita tu, kisayansi itachukua mwaka kuirejesha nguvu ya chama katika mizani stahiki ya kisiasa.

Hivyo Mwanachadema yeyote na mwanamageuzi ni lazima atambue kuwa uchaguzi wa Udiwani huu kwa kata 27 nchini, sio kipimo cha kufuta pengo la akina Zitto. Labda kwa mchambuzi wa siasa asiejua sayansi ya siasa tu na mwenye agenda ya kipropaganda ndie ataamini kufukuzwa akina Zitto ni chanzo cha kushindwa uchaguzi huu.

Athari za kufukuzwa kwa Zitto na wenzie ndani ya chama zitapimwa baada ya Mwaka mmoja kutoka sasa hii ikiwa na maana uchaguzi mkuu ujao, kwa sasa yanayotokea nikuwa yalitarajiwa kwa 100% na yalipita kwenye chekecho la kimkakati kisha yakaamuliwa iwe hivyo.

Kosa kubwa kwa Chadema ni kosa la kimkakati na hili ni lazima lifanyiwe kazi haraka iwezekanavyo,

Kwanza ieleweke kuwa daftari la wapiga kura ndio rungu lililoibeba ccm, ni lazima liboreshwe ikiwa ni pamoja na uingizaji wawapiga kura wapya, idadi kubwa ya wapiga kura hawakupiga kura kutokana na sababu mbalimbali kama kuuza shahada zao.

Wanamikakati tukae chini tuwafanyie utafiti wa kisayanzi viongozi wa majimbo, mikoa na kanda, nilazima tuwapime kwa nyuzi 360 kiutendaji kwakuwa hizi chaguzi ndogo za kata na serikali za mitaa zinatakiwa wao wasimamie na kuonyesha uwezo wao na sio hivyo tu bali lipo ndani ya uwezo wao kikatiba,

Ni lazima tufanye utafiti wa kimkakati usio na unafiki wala haya,

Tukiyatekeleza haya yote, uchaguzi wa serikali za mitaa utaanza kutupa majibu ya mkakati huu.

Yote kwa yote Chadema haijapoteza uchaguzi huu, kimkakati ni ccm ndio imepoteza,

Propaganda zenu ziko too much biased kiasi kwamba mnawaamisha wapiga kura wenu kuwa everything is rosy na kama kuna lawama basi wa kulaumiwa ni chama tawala.

Yetu macho na masikio.
 
Kuna watu kama wewe unaweza ukadhani unaisaidia sana CHADEMA katika ukuaji wake kumbe propaganda zako ndizo zinazoididimiza kabisa hasa pale unapochukua nafasi ya mmojawapo wa watu walio karibu na jiko la maamuzi ya CHADEMA (false position).

Kwanza hoja yako hii hapa juu ina matobo mengi ya kisayansi katika siasa kwa ujumla achilia mbali hali ya ksiasa nchini Tanzania bila hata kugusia maneno uliyotumia katika hoja yako.

Ukiangalia katika nchi nyingi zenye vyama vya kisiasa ambavyo ni mbadala halisi wa chama tawala kidemokrasia utaona kuwa chaguzi ndogo huwa ni mwiba kwa chama tawala kutokana sababu nyingi lakini sababu kuu huwa ni mbili.

1) Wapiga kura kuanza kukata tamaa kutokana na ahadi kupitia ilani ya uchaguzi kusua sua au kutokutimizwa na chama tawala huku muda uliobakia wakiona kama hautoshi kuzitimiza. Kwa maana nyingine, ile euphoria inayopatikana baada ya uchaguzi huwa inakumbana na political reality.
2) Chama pinzani kuwa na fursa ya consolidate uwezo wao katika human resources (human capital) and fund kutokana na uchache wa maeneo ya chaguzi yanayofanyika.

Kunapotokea hali ambayo chama mbadala hata chaguzi ndogo kinashindwa kukitikisa chama tawala lazima kutakuwa na maswali mengi sana ambayo yanataka majibu halisi ili kuweza kuondoa sababu zilizosababisha kushindwa kutoa mtazamo chanya katika chaguzi kuu ijayo.

Kwa kutumia mifano yako hiyo, Ningekuelewa kama ungesema CHADEMA kwa sasa bado haijafikia nafasi ya kuongoza nchi, kwa maana nyingine, iko kwenye mkakati wa pili wa kisiasa kwa vile haijakuwa chama cha kitaifa ndiyo maana imeanza kupata maeneo mengine ya nchi kama kwenye Kata ya Njombe. My goodness, this is 2014.

CHADEMA kwa vile kimeingia kwenye chaguzi na kinajinasibisha kama ni chama ambacho kiko tayari na kinasubiri muda kisheria kupewa nchi kuongoza, basi kilitakiwa angalau kishinde nusu ya kata zilizofanya uchaguzi au zinazofanya chaguzi ndogo bila kujali ziko pande gani ya nchi.

Kukaa hapa na kuanza kujipongeza kwa mtazamo wa chama kama ndiyo kinaanza kujijenga ni kufurahisha jukwaa lakini hakuondoi uharisia wa kuwa kilichofanyika ni total failure bila hata kuangalia nguvu iliyotumika katika kuzitafuta hizo kata.

Ukiangalia zaidi, utagundua kuwa hoja uliyojitahidi kuijenga hapa inapingana kabisa na hoja iliyoijenga kwenye thread hii,

Tatizo lako unajitahidi kutetea swala ili kufurahisha macho ya wapenda kusikia mazuri tu ya chama badala ya kuangalia mabaya yake kwa faida ukuaji wa chama ndiyo ukasahau hata ulichokiandika na kukiweka saa 10:39, yaani masaa 7 tu kupita, ukawa tayari umebadilisha mtazamo. Hata hueleweki unasimama kwenye nguzo gani kisiasa katika matokeo haya ya uchaguzi. Hapo hapo unasema chama kinayumba na hapo hapo unasema chama kimefanya vizuri sana!.

Hebu soma ulichokiandika hapa saa 10:39,

Propaganda zenu ziko too much biased kiasi kwamba mnawaamisha wapiga kura wenu kuwa everything is rosy na kama kuna lawama basi wa kulaumiwa ni chama tawala.

Yetu macho na masikio.

Ninatambua vema wapi nimesimama na imani yangu ipo palepale,

Kwanza umeanza kwakupotosha maana ya andiko langu, andiko hili ni la Yericko Nyerere na sio la chadema, hivyo halihitaji muongozo wa msemaji wa Chama.

Dhana yako kuu katika hoja hii nikuwa chama kinachojiandaa kushika dola ni lazima sura halisi injionyeshe kwenye chaguzi hizi ndogo,

Hilo nakubaliana na wewe kabisa, hasa katika anga la siasa pembuzi.

Siasa za kiafrika ni tofauti na matakwa ya siasa za vitabuni za muono wa akina Karl Max, hapa lazima tutohoe siasa zetu ambazo ndizo hizi tunazoziishi kwamfano wa Uhuru Kenyatta, Michael Satta, Alasanei Wattara nk,

Hivyo acha nadharia ya kitabuni kisha njoo unakili falsafa ya kibantu
 
Last edited by a moderator:
- Chadema mmeshindwa uchaguzi huu kwa sababu za msingi sana nazo ni kushindwa kwenu kutatua matatizo ya ndani ya chama chenu na kupata muafaka kabla ya huu uchaguzi, mnoanekana kumu-underestimate sana Zitto lakini ana mchango mkubwa sana kwenye kushindwa kwenu,

- Mlikuwa salama sana kuishi na Zitto, sawa Chama kinatakiwa kuwa kikubwa kuliko Zitto lakini kwenye kumtishia kumfukuza hamkukisaidia chama chenu hakuna chama Duniani kimeweza kushinda chaguzi za aina yoyote ile na matatizo kama mliyonayo sasa hivi, na kama hamkumaliza hayo matatizo yenu na Zitto kwa amani mjue 2015 itakuwa aibu zaidi,

- Kama nilivyomwambia Mwenyekiti wenu wa Taifa majuzi tulipokutana uso kwa uso ni kwamba Zitto hataingia CCM, wala vyama vilivyopo vya upinzani labda kianzishwe chama kipya, na in the end atakapofanya uamuzi huo atakuwa ameshawamaliza wote viongozi wakuu huko kisiasa,

- Ushauri wa bure ni lazima mfanye uchaguzi sasa tena ulio huru na ifike pahali Mwenyekiti mpya awe sio kutoka Kaskazini kama kawaida yenu, yamalizeni kwa amani na Zitto, kuwepo kwake kwenu huko kunawasadia sana na public relations kwamba angalau mnaheshimu Demokrasia, lakini kumfukuza hamukisaidii chama chenu in the longrun,

- Jana mmeshindwa goli moja linatosha sana haihitaji magoli mengi tena mmeshindwa under expenses za Helikopta, how do you recover from that tena that quick na uchaguzi wa 2015 upo ukiongoni? Panahitajika mabadiliko makubwa sana huko na serious kurudisha kale ka-credibility kalikokuwepo kabla ya kugombana na Zitto, uchaguzi huru na wa haki will do na Zitto aruhusiwe kugombea ama sivyo mnacheza ngoma ya wachawi tu!!, na yule Mzee Mtei kila anapoongea anawaharibia sana in the Public eyes it is about time mkamuomba awe anayamaza maana huwa hana jipya zaidi ya kurudia kuunga mkono maamuzi ya mkwe wake public haipendi hilo!!

poleni sana na kipigo cha jana haikuhitaji kuwa na PhD kujua kwamba mtapigwa tu na helikopta zenu, sasa tuambieni mmetumia hela ngapi kupoteza jimbo moja?

Le Mutuz

ImageUploadedByJamiiForums1392060013.693649.jpg

Acha unafiki
 
Inawezekana kauli yangu isiwaingie watu masikioni mwao kabisa, lakini nitawaeleza japo kwa kifupi.

Katika siasa kuna kitu kinaitwa siasa za jumla (general politics) na siasa za kijiografia (geography politics)

General politics inahusu mambo yanayohusu siasa za kitaifa bila kuchagua chama au itikadi na hizi mara nyingi husimamiwa kwa katiba, kanuni na sheria za nchi, hapa inahusiana pia na daftari la wapiga kura na tume ya uchaguzi,

Geography politics inahusu siasa za eneo husuka, kuna international gp, na domestic gp,

Katika hayo Chadema ime win kwenye Gp-D kwa asilimia zaidi ya 90%, hili linatokana na chama kushiriki uchaguzi kwa miaka yote huku mambo muhimu yanayopaswa kufanywa kwenye General Politics yakiwa doro kabisa, mambo hayo ni kama tume kuwa huru, daftari la wapigakura kuboreshwa, na dola kuvuruga chagizi nyingi kwa maslahi ya ccm.

Takwimu za chaguzi hizi zinatoa sura stahiki ya ubora wa domestic political ya Chadema,

Mathalani uchaguzi huu Chadema ilikuwa ikitetea kata 3, za Nyaisura, Kiborloni na Mikol.. Kigoma.

Tumepoteza Nyaisura, na Kigoma, na Tumeipoka ccm kata za Sombetini na Njombe.

Tamani ya kata ilizoshinda chadema nikubwa kuliko ccm, kubeba kata ya njombe ni turufu kubwa, vivyo hivyo kata ya sombetini. CCM hawajaongeza thamani yoyote ya kata,

Kwa lugha nyingine nikuwa CHADEMA 0-0 CCM, lakini CHADEMA wananafasi ya golden goal kwakubeba kata ya Njombe ambayo kwanza inafuta propaganda za ccm yakuwa chadema ni chama cha ukanda, sasa tunashuhudia Chadema sio chama cha ukanda tena bali chama cha kitaifa na kila pembe ya jamhuri hii.

Izingatiwe kuwa oparesheni Pamoja Daima haikuwa maalumu kwaajili ya uchsguzi huu bali sehemu ya ratiba ya chama katika kutoa elimu ya umma kudai/kuhimiza uboreshaji wa daftari la wapiga kura.

Naamini hapo mmenipata ndugu zangu mnaojenga hoja dhaifu kuwa kama dhana ni daftari la wapiga kura na polisi why kwingine chadema imeshinda?

CC
Mwita Maranya
 
Last edited by a moderator:
Ninatambua vema wapi nimesimama na imani yangu ipo palepale,

Kwanza umeanza kwakupotosha maana ya andiko langu, andiko hili ni la Yericko Nyerere na sio la chadema, hivyo halihitaji muongozo wa msemaji wa Chama.

Dhana yako kuu katika hoja hii nikuwa chama kinachojiandaa kushika dola ni lazima sura halisi injionyeshe kwenye chaguzi hizi ndogo,

Hilo nakubaliana na wewe kabisa, hasa katika anga la siasa pembuzi.

Siasa za kiafrika ni tofauti na matakwa ya siasa za vitabuni za muono wa akina Karl Max, hapa lazima tutohoe siasa zetu ambazo ndizo hizi tunazoziishi kwamfano wa Uhuru Kenyatta, Michael Satta, Alasanei Wattara nk,

Hivyo acha nadharia ya kitabuni kisha njoo unakili falsafa ya kibantu
Vyama vya siasa ambavyo ni makini lazima viwe na washauri wa mambo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ambao wamesoma siyo kwa maono ya yaliyotokea na yanayotokea nchini (political experiance) bali kwa kiwango kikubwa ni wale ambao wanatumia ushauri unaochagizwa na vitabu vya kisiasa, kiuchumi na kiajamii.

Unaponiambia niweke pembeni ujenzi wa hoja za maono ya vitabu, ni sawa na kuniambia nijenge hoja giza.

Sitaki kuamini kama huelewi kuwa vitabu ni chimbuko la upembuzi na vinasaidia sana katika kupanua uwigo wa fikra na mitazamo na pia katika ukuaji wa siasa kwa faida ya kimaendeleo katika taifa endelezi.

Utazifahamu vipi siasa kwa mapana na marefu bila vitabu na hasa ikichukuliwa kuwa our political system emenated from ideas za watu kama hao uliowataja ambao maandiko yake unayapata kwenye vitabu. Pale unapoyaingiza haya maandiko kwenye hali halisi ya kisiasa, utapata njia mbadala ya kupambana na vizuizi vya kisiasa kwa faida ya maendeleo katika chama na taifa kisiasa.

Yangu macho na masikio.
 
What chadema has gained in this by-election could be rightly termed as modest success. No need for panic.

Of course, for a party that is on decline, like CCM, it is huge relief to temporarily stop this political hemorrhage (losing seats). But for a growing party, like chadema, there is no pride in achieving draw: 2 - 2.
 
Labda sikueleweka vema niliposema usinakili ya vitabuni,

Hapa nilimaanisha kuwa kwanza nilazima uijue siasa kwa mapana yote tena siasa ya kitabuni kbisa, lakini nimeonya mitazamo ya wanasiasa wa kimagharibi kwakuwa haiakisi viunga vya afrika, hivyo imefanya afrika kutohoa falsafa zake.
 
What chadema has gained in this by-election could be rightly termed as modest success. No need for panic.

Of course, for a party that is on decline, like CCM, it is huge relief to temporarily stop this political hemorrhage (losing seats). But for a growing party, like chadema, there is no pride in achieving draw: 2 - 2.

wewe ndiye mwanaccm mwenye akili ! Unasubiri nini huko , hivi huoni aibu kuwa ccm ?
 
Chaguzi hapa Tanzania zinakuwa ngumu sana kwa opposition parties sababu tume ya uchaguzi na polisi ni taasisi zisizo huru. Tume ya uchaguzi ina namna nyingi za kisayansi kuiba kura. Polisi hao tumewazoe.

Lakini, mleta mada ujue kwamba vijana wetu wengi hawana ajira wala kipato kinacho eleweka. Ndiyo maana wengi wao wamewekwa na CCM kupinga kila hoja humu ndani ya JF. Hawa nao ni kazi ya Chadema itakapo twaa dola kuwasaidia wawe na ajira ili wasiendelee kuuza utu wao. Ni mizigo yenu hiyo, hivyo muwapende na muwavumilie.

Hata wakati wazee wetu wanapigania uhuru, siyo watu wote walikubaliana na hizo harakati. Lakini nchi ilipopata uhuru nao walifaidi matunda ya uhuru kama msemo usemao " a rising tide lifts all boats"

Mapambano na yaendelee.
 
nakubaliana na wewe mkuu, tatizo la umasikini ni mojawapo nyenzo itumiwayo na chama tawala.
 
Back
Top Bottom