CHADEMA imekiri kufadhiliwa kutoka nje ya nchi katika shughuli zake za kujijengea uwezo

Status
Not open for further replies.
Hebu jaribuni kumuelewa Dr. Slaa. Hakusema kuwa KAS ni wafadhili wa CDM bali wanawawezesha katika seminars kwa kuleta wataalamu wa kutoa mada.

acha ujinga ww kuna sehemu amesema ni kawaida kwa vyama vyenye mrengo mmoja kuwa na ushirikiano kwa hiyo chadema ni chama cha kikristo
 
Imagine CUF ikiri kupokea misaada kutoka chama kimoja cha Kiislamu IRAN! JF pasingekalika na magezeti yao pia! Mungu hawafich wanafiki! Wadini wakubwa nyie!
 
Mimi nina wasi wasi na elimu tunayopewa watanzania, kwanini mnapandikiziwa udini nanyi mnakubali? Hivi sabodo alipowafadhili CHADEMA yeye ni mkristu? mbona hamkusema kuwa CHADEMA ni chama cha waislam kwa kuwa sabodo ni Mwislam?
mkuu wala usihangaike nao,ni uoga wa kupoteza nyadhifa walizonazo,sasa wanahaha,bahati nzuri wa tz na udini hatupo.angalia viongozi wa kiislam wanavyogombana,lakini waamoni wao wala hawana huo mda wapo kimya busy na majukumu,ndo watanzania tulivyo hatuongozwi na dini sie.
 
kiukweli chadema sasa msitaje hawa wafadhili hadharan coz mtapoteza wanachana wenu.hawa wazungu tena wakristo kwa nchi km tanzania c nzur sana kupublish.halafu mzungu cku zote ana kamsemo kake anasema "no economic aid without political interest" sasa hapa watanzania tuwe macho zaid kuliko tulivyokua macho kwenye tukio la mwangosi.kila hatua lazma tulifuatilie icje ikawa heri ya ccm walivyouza nchi yetu kuliko watakavyokuja kugawa hawa cdm.

Yani wewe ndiye bure kabisa, hao hao unaojaribu kuwapinga ndio unatumia avatar yake.
Ungekuwa na akili nzuri usingeandika hiki ulichoandika hapa.
 
Mimi naona tungeanzia kwa mfadhili huyu hapa kwenye picha.
Angalia vizuri picha hii ambayo JK yuko na mfadhili. JK anashirikiana na mfadhili huyu !!
Unamfahamu vizuri mfadhili huyu ?? Basi hebu angalia vizuri hapo kwenye maandishi ya rangi ya blue !!
Hapo vipi ?? (Hii kauli ya "Hapo Vipi ??" ni kwa hisani ya Edward Lowassa !!

Huyo mfadhili namuogopa sana, naona yeye kila akiona wanaume wenzie anatamani kuwadandiadandia mgongoni, hata kupiga nae tu picha yahitaji ujasiri!
 
CDM yafaa kukumbuka kwamba wazungu wanasema ''there is no free lunch'' haya misaada yao ya nini wakati tunapigania raslimali zetu zituendeshe? kwanini CDM muendelee kukumbatia na kukodolea macho misaada ya hao jamaa badala ya kukomaa na kuendesha kampeni kabambe kwa raia kuchangia chama chao? itakua kama hii serikali yetu kusubiri kapu la wahisani!
 
Imagine CUF ikiri kupokea misaada kutoka chama kimoja cha Kiislamu IRAN! JF pasingekalika na magezeti yao pia! Mungu hawafich wanafiki! Wadini wakubwa nyie!

Nakaa kimya kuchelea BAN!
 
Nape kisha shinda kesi, hilo hamkwepi hata mseme nini.


Haya ni marudio tu kwani Anthon Komu afisa wa fedha wa CDM alikuwa katika interview na Channel 10 kipindi nape alipoanza kyatoa hayo matamshi na aliyaongea hayo na walimpigia Nape simu naye akakubali na wao wanaasasi na vyama kama hivyo vinavyosapoti DEMOCRASIA penginge kwa kutoa fedha au mafunzo
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimekiri kufadhiliwa kutoka nje ya nchi katika shughuli zake za kujijengea uwezo.

Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt Willibrod Slaa alisema hayo jana katika semina iliyoshirikisha baadhi ya viongozi wa chama hicho na wageni kutoka shirika la Chama cha Kikristo cha Ujerumani (CDU) la Konrad Adenauer Stiftung (KAS).

Kwa mujibu wa Dkt. Slaa, CHADEMA na KAS, wamekuwa na ushirikiano wa karibu kwa miaka sita sasa na ushirikiano huo umelenga zaidi kukuza demokrasia nchini.

Dkt. Slaa alidai kuwa CHADEMA ni chama chenye uwazi kwa kila mtu na katika uhusiano wao na KAS, hakiletewi fedha moja kwa moja kwa ajili ya operesheni au maandamano, ila kujijenga kiuwezo.

"Kwa sasa kumekuwa na propaganda zinazoenezwa kwamba CHADEMA wanapata mabilioni ya fedha kutoka kwa wafadhili, hii si kweli, ila wanatujengea uwezo na si kutufadhili kampeni. Napenda kusema propaganda za aina hii zimepitwa na wakati na wote watakaozifanya tutawafungulia kesi," alisema Dkt. Slaa.

"Wanaosema kwamba CHADEMA wanapokea mabilioni nao wanashirikiana na mashirika ya aina hiyo yenye mrengo mmoja na ni utamaduni duniani kote, vyama vyenye mrengo mmoja kushirikiana, hivyo hii dhana isipotoshwe," alidai.

Pamoja na kusema kuwa KAS haitoi fedha moja kwa moja kwa CHADEMA kwa ajili ya maandamano na kampeni, lakini Dkt. Slaa alidai kuwa shirika hilo huwasaidia wastani wa Sh milioni 60 kwa mwaka kwa ajili ya machapisho na kutoa elimu.

Pia alisema kipo chama cha Uholanzi ambacho hakukitaja jina, lakini akakiri kuwa huwafadhili Sh milioni 20 kulingana na idadi ya wabunge walio bungeni.

Pamoja na kusema kuwa ni kawaida kwa vyama vya mrengo mmoja kusaidiana duniani, Dkt. Slaa alisema chama hicho cha Uholanzi kinachowasaidia, pia hufadhili CCM fedha zaidi ya zinazopelekwa CHADEMA kutokana na chama hicho tawala kuwa na idadi kubwa ya wabunge.

Nape ashitakiwa

Dkt. Slaa alidai kwamba kwa kuanzia wameamua kumshitaki Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.

Kwa mujibu wa madai ya Dkt. Slaa, tayari CHADEMA imefungua kesi namba 186 ya mwaka 2012, katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam dhidi Nape, ambaye anadaiwa alitamka CHADEMA kufadhiliwa kutoka nje.

Dkt. Slaa alidai kuwa kesi hiyo itakapokuwa ikiendelea, wataongeza watu wengine walioeneza kauli hiyo.

Semina ya KAS

Akizungumzia semina ya kujenga uwezo iliyotolewa jana kwa makada wa CHADEMA, Dkt. Slaa alisema imelenga kuangalia wanavyoweza kuleta uchumi wa soko utakaoshirikisha watu walio katika ngazi za juu na chini.

Lengo la kushirikisha watu hao wa tabaka mbalimbali kwa mujibu wa Dkt. Slaa, ni ili raslimali za nchi zitumike kwa faida ya Watanzania wote ambapo pia mgeni kutoka KAS ambaye alipata kuwa Naibu Waziri wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani, Klaus-Jurgen Hedrich atatoa mada.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe alisema ili uchumi uwe endelevu, lazima wananchi wapewe haki na kuruhusu sekta binafsi kusimamia uchumi na si rahisi kusimamia uchumi kwa sera za kijamaa.

via HabariLeo

Source: wavuti - wavuti




My VIEWS!
Kila mtanzania anaefuatilia siasa za Tanzania anamfahamu ndugu NAPE NNAUYE tangu alipokua UVCCM na hatimae ukuu wa wilaya. Mabadiliko yake hasa alipokua mkuu wa wilaya ilibidi mtambue kua kelele alizokua akipiga UVCCM ilikua ni kutokana na kutaka kutimiza ndoto flani aliokua nayo, na pindi alipoona mwanga (Baada ya kua m/wilaya) mtazamo ukaanza kuota kutu. Hii ni kwa kua anajaribu kuonyesha ukweli ulio nyuma ya pazia tangu enzi za waliomlea (CCM).

Kukimbizana na mtu kama huyu mahakamani ni kupoteza muda kwani mi ninamfahamu kama mtu wa maneno mengi hasa linapokuja suala la FEAR OF THE UNKNOWN.......
CHADEMA endelezeni kile mnachoamini kitatutoa katika hali hii tuliyonayo na Watanzania wataamua katika sanduku la KURA katika chaguzi, CCM sera ni ileile iliyomtoa Rostam katika siasa(MAJI TAKA) japo si muumini wa kigezo hiki.

... need to say more!??? ahsante Slaa!
mi nikisema naambiwa mdini!
 
Imagine CUF ikiri kupokea misaada kutoka chama kimoja cha Kiislamu IRAN! JF pasingekalika na magezeti yao pia! Mungu hawafich wanafiki! Wadini wakubwa nyie!
Hata nchi yetu inapata misaada mingi na pona yetu ni kutoka kwa nchi za hao wakristo...tafakari!
 
Mimi nina wasi wasi na elimu tunayopewa watanzania, kwanini mnapandikiziwa udini nanyi mnakubali? Hivi sabodo alipowafadhili CHADEMA yeye ni mkristu? mbona hamkusema kuwa CHADEMA ni chama cha waislam kwa kuwa sabodo ni Mwislam?

sabodo kaingia choo cha kike
 
Imagine CUF ikiri kupokea misaada kutoka chama kimoja cha Kiislamu IRAN! JF pasingekalika na magezeti yao pia! Mungu hawafich wanafiki! Wadini wakubwa nyie!

kaka we n noma.yaan hii comment yko n thread tosha.uko juu.
 
Yani wewe ndiye bure kabisa, hao hao unaojaribu kuwapinga ndio unatumia avatar yake.
Ungekuwa na akili nzuri usingeandika hiki ulichoandika hapa.

unaonekana una akili chakavu km chuma za gerezan kariakoo.kwan kutumia avatar yao ndio nn.unataka kuniambia watu wanaotumia avetar ya mbwa ama nyani nao wakoje.tatizo lenu hamjadili hoja mnapenda kurukia matukio.hoja iliokuwepo n ufadhili wa cdm na kanisa na co avatar ya yaser.
 
Imagine CUF ikiri kupokea misaada kutoka chama kimoja cha Kiislamu IRAN! JF pasingekalika na magezeti yao pia! Mungu hawafich wanafiki! Wadini wakubwa nyie!

Kwa nini umeandika comment kama hii ?? Au kwa sababu umesoma kwenye vyombo vya habari kuwa Chadema inashirikiana na taasisi fulani ya Ujerumani ??

Sasa, kabla ya kuandika hii comment, ungeendelea kusoma kwenye vyombo hivyo hivyo vya habari kuhusu swala hili kama ifuatavyo:- Angalia vizuri hapo kwenye maandishi ya red, halafu uache unafiki mara moja !!

Kauli hii hapa chiniimetolewa na Dr. Slaa na kunukuliwa na vyombo vya habari ambavyo wewe umevisoma habari zake.

"CHADEMA tumeamua kumfikisha Nape mahakamani, ili atuthibitishie hayo mamilioni tunayopokea kwa wafadhili wa Ujerumani na kesi hii, itawaunganisha na wale waliowahi kusema kauli kama hiyo. Hapa mnaona kuna wageni, hawa ni viongozi kutoka Ujerumani na baadhi yao ni watumishi wa Serikali ya nchi hiyo, sasa tumekutana hapa kwa makusudi, ili kuwaeleza wazi jinsi wenzetu wanavyosema kutokana na ushirikiano wetu na wao.

Tunashangaa sana, yaani CHADEMA ikishirikiana na watu kutoka nje ya nchi wanasema na kuzusha mambo ambayo yanaweza kuleta utengano kati ya nchi na taifa jingine. Kwa mfano, sisi CHADEMA tunashirikiana na Taasisi ya Korrad Adenauer Stiftung ya Ujerumani, CCM inashirikiana na FES, CUF inashirikiana na FNF zote za Ujerumani, sasa tunataka Nape atueleze mbele ya Mahakama juu ya jambo hili," alisema Dkt. Slaa.

Source: wavuti - wavuti
 
Kweli Dr slaa kazeeka anaanza kuropoka sasa, tujiandae tutashuhudia mengi, imedhihirisha udini wa chadema kwa Mahusiano na Christian Democratic union, wadini wa kikristo wataendelea kumtetea! Ss atatueleza Mahusiano na vyama vyenye mrengo wa ushoga kule uingereza.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom