Mngoreme wa pili
Member
- Feb 22, 2024
- 8
- 8
Takriban wiki mbili sasa Makamu Mwenyekiti wa Chadema Taifa,Tundu Lissu amekuwa akizunguka na kutoa tuhuma za rushwa zinazoendelea katika uchaguzi wa ndani wa Chama hicho.
Lissu ameenda mbali zaidi nankudai baada ya kutuhumu suala la rushwa,baadhi ya wanachama wenye ukaribu na viongozi wa juu wa Chama hicho wamemjia juu na kumuonya kwanini anakituhumu Chama hadharani badala ya kwenye vikao vya Chama
Kwamba kama Kuna rushwa wangeambiana ndani na wamakize kimya kimya badala ya kufedheheshana.
Kwa maoni yangu Mimi Mngoreme,kitendo Cha kumlaumu Lissu na kukaaa kimya Kwa Chama hicho bila kuchukua hatua yoyote hata ya kuunda Tume ya kuchunguza uhalali wa kauli hiyo ya Makamu Mwenyekiti inaiondolea Chadema Uhalali wa kukosoa kitendo chochote Cha rushwa au ufisadi unaofanywa na taasisi nyingine ikiwemo Serikali.
Lakini pia inawaondolea viongozi hao uhalali wa kukemea uhalifu wa aina yoyote ndani ya nchi Kwa kuwa kila watakaponyoosha vidole watu watawauliza juu ya fedha za Abdull zimetoka wapi na nimefanya kazi gani ndani ya Chama hicho.
Ni vema sasa wakakaa chini na kuacha kumshambilia Lissu na kujielekeza kutoa majibu ya tuhuma zilizopo