CHADEMA, huu ni wakati wa kufanya maamuzi magumu...

Status
Not open for further replies.
Hata hapa Stein amependekeza uchunguzi wa kina kufanyika kuhusu kwanini wanaoueneza ukanda wa kaskazini watokee Kigoma?
Kwanini Vijana wa juzi tu kwenye siasa watake uongozi wa juu kwenye vyama vyao? (zitto na kafulila)
ni akina nani wanawatumia vijana hawa machachari kuitaka kuivuruga chadema?
Uchunguzi huru na wa kina ufanyike kubaini hawa wahuni, before consodering serious and critical action to be taken kama alivyopendekeza Stein kwamba maamuzi magumu yachukuliwe sasa kabla madhara hayajatokea hapo baadaye!
No research no right to speak, mimi nakaa kimya! Ila if you think you have evidences toeni hapa then watu wadiscuss siyo kwa heresay!
 
Habari yako ni angalizo zuri ila umeficha taarifa hapo mwanzoni Kwa kusema kuna vijana wa juzi tu (2005) leo wanataka nafasi za juu. Kwa nguvu kazi inayohitajika CDM, hata Vijana wanachama wazalendo watakaojiunga leo (hasa wasomi) wanahitajika Kwa wingi Kwa ajili ya kuongoza chama na serikali. Mfano Madiwani,wenyeviti na majaribio ngazi mbalimbali, bado kunahitajika kufungua matawi sehemu nyingi. CDM inawapenzi wengi sana hapa nchini, na wengi wangependa kujiunga kuwa wanachama. Nihitimishe kwa kusisitiza: Vijana bado ni nguzo muhimu sana ya kuiongoza CDM/ serikali.


Katika hilo nadhani unaona CDM ndiyo ya Kwanza maana hadi vijana walioko Chuo kikuu wanshiriki as long as ni wanachama lakini inapofika wanaanza kupinga maamuzi ya vikao halali vya Chama na wanapoanza kufanya harakati za Ukanda aua udini ndani ya CDM ndipo tunapowashangaa. Pengine tunajiuliza wanafanya hayo kwa interest za nani jibu liko wazi.

Vile vile kuna vipandikizi vya Magamba na CCM vina anza ku mature kwa hiyo ni wakati wa kuwachunguza na kujua nani Kondoo inje ndani chui na kumtenganisha na Kondoo.

CCM inaiandama sana CDM kwa mafanikio kwa hiyo kuna vijana naona wameshindwa kujizuia na kuonyesha tamaa yao ndani ya Chadema.

Embu fikiria Nchi nyingi zilizoendelea zimefanikiwa kwa kufanya Research ambayo inatoa directives za nini kinatakiwa kifanyike na kwa vipi, wanakuja watu tena wasomi wakubwa wanahoji sababu za CDM kutenga pesa kwa ajili ya huo utafiti.

CCM na serikali yake wamekuwa na mazoea ya kufanya hata mambo ya kitaalamu bila utafiti ndiyo wametufikisha hapa leo hii CDM wanafanya utafiti eti kuna wasomi wanahoji... Hawa ni waganga njaa tu, haijalishi CDM umeisaidia vp lakini kama malengo yako yanapinga na malengo ya CDM bora uchingiwe baharini tu.

Mfano Mzuri wa Utafiti uliofanywa na CDM na kuleta mafanikio ni.

1. Dr W. Slaa kugombea Urais 2010, wote tumeona, kama uchaguzi ungekuwa huru na haki leo hii tungekuwa tunazungumza mengine.

2. Uteuzi wa Wabunge viti Maalum, Kila mwana CDM mkweli anajua Kazi aliyofanya Dr Mkumbo inavyowatesa CCM huko majimboni kwani mfano Kilombero, Hanang, KIGAMBONI etc ni kama kinaongozwa na wabunge wa CDM na Bila kusahau mchango wa Wabunge hawa kwenye kura za Urais.

3. Recently tumeona Uchaguzi wa Arumeru na Chaguzi Ndogo za Udiwani.

Mifano ipo mingi ni basi tu watu hawataki kufikiria.
 
NAMPENDA SANA ZITTO KABWE...NAJUA WAZI SANA KUWA ANA UWEZO MKUBWA SANA WA KIUONGOZI..HILO SIPINGI!!!!
LAKINI UKWELI NI KWAMBA ZITTO KABWE HAYUKO PAMOJA NA CHADEMA!!!!!
ISHU YA Arumeru, alishiriki ila sio kikamilifu! najua CHAMA kilimpangia kazi nyingine Mwanza! Lakini! Tumezoea kuona matamko yako online, iwe FB,TWITTER, kwenye blog YAKE AU JF(mara chache, siku hizi haipendi JF), lakini zitto mara nyingi hakupenda kuizungumzia Arumeru( sababu ya kushabikia ukanda na udini.) ile ishu ya Polisi kuua watu Arusha haikuingia akilini mwa zitto..likaja suala la LEMA...Zitto akapiga kimya kikali mpaka kesho!!!!
Kifupi ZITTO ni kichwa sana ila mienendo yake ndani ya CHADEMA inaleta maswali mengi saaana..kuliko majibu!!!!
Hapo naona sense kwa uliyosema. Sina hakika kutoa misimamo binafsi inayoweza kikigawa chama kama ina maana gani hasa inapotoka kwenye kinywa cha kiongozi kama Zitto. Anaposema siendi Arumeru kwani nna sababu zangu, watu wa kawaida watamuekewaje? Anaotoa matamko kadhaa kwenye twitter yake, nini maana yake? Siasa si ugomvi wala uadui ila viongozi wanaojenga pamoja wanapaswa kuscreen yale wanayotoa kwenye public kwa faida ya chama. Ningetamani zaidi kusikia Zitto akitoa misimamo ya chama kuliko ya kwkae binafsi na hasa pale anapojionyesha kutofautiana na wenzake hadharani. Nadhani anakisa sense ya collective accountability ka chama na viongozi wake
 
Mkuu, nimekuomba matokeo ya kura ya jimbo la Zitto. Ukishaona matokeo hayo ndiyo utaona kuwa jamaa alishinda kibahati sana sana maana alikuwa kafukuzwa nyuma kama mashindano ya Formula 1.

Hata Mnyika na Lema walishinda kwa kura nyingi sana kwenye majimbo yao ila siyo Zitto.

Zitto wengi tunamfahamu na Mungu bariki hata yeye anafahamu kuwa tunamfahamu na nimeongea na watu wengi sana na wote wanasema wazi kabisa kuwa Zitto ni Handle With Care. Kama Arumeru CCM ingelishinda, basi hilo kundi lingelikuwa na nguvu sana ila kwa sababu Chadema wameshinda, hilo kundi la kina Tuntemeke limekuwa hoi.

CCM inavyozidi kuboronga, Chadema itazidi kusimama na soon hadi Tabora tutaanza kuipokea Chadema. Mengine yatabaki ni muda tu kuamuanini kitafuata. Zitto uzuri wake ameshajifahamu kuwa uaminifu kashauuza ila bado ni heri kuwa na Zitto kuliko kuwa na Shibunda na mwisho ni heri kuwa na Shibunda kuliko kuwa na CCM.

Nafikiri Zitto aliingizwa sehemu fulani ambayo hata afanyaje, hawezi kujinasua labda CCM ife na hao Wazee wanaomdai kumfikisha hapo nao wafe au wapoteze nguvu. Vinginevyo, wataendelea kumdai kukihujumu chama chochote ambacho yeye atakuwepo.

Pamoja na yote, Zitto ni Zimwi likujualo, milele haitakuja kutokea atule atumalize kama CCM inavyotula sasa.
Nina sababu kubwa kwaa nini namwingiza Zito, kwanza anawapa nguvu hawa wanaofanya harakati za ukanda ndani ya CDM, Pili nimeshangazwa sana na kitendo cha yeye kuwa kiongozi mwandamizi ndani ya CDM kupigiwa debe na wazee wa kutetea Magamba humu jamvini.

Nashidwa kuelewa kuna uhusiano gani kati ya Zito na hawa wahuni wa CCM humu ambao wamekuwa wakitetea mafisadi/ufisadi humu TZ.
 
Usimuhukumu mtu kwa kitu usichokijua hata mungu hapendi.Kumhisi mtu na kuanza kutoa shutuma ni kosa kubwa sana.
 
Zitto ni mtu wa karibu sana na Ally Mley aliyegombea Kigoma mjini na Wakamchakachua.

Hivi Zitto alishinda kwa kura ngapi vile? Hebu leteni data hapa na ndipo tuanze kumjadili Zitto.

Una pointi nzuri na muhimu sana kwa Chadema ila umeharibu tu kumuingiza hapa Zitto.
WILAYA YA KIGOMA
KIGOMA KASKAZINI
Candidate
Political Party
Number of Votes
Percentage Votes
ZITTO KABWE ZUBERI
CHADEMA
23,36648.57
LEMBO ROBINSON FULGENCE
CCM
18,35238.15
OMARY MUSSA NKWARULO
CUF
4,83910.06
CHONGERA HARUNA CHONGERA
CHAUSTA
2640.55
MFAUME HAMISI MFAUME
APPT - MAENDELEO
1080.22
AUGUSTINO PETER MBOLEGWA
SAU
880.18
GERMANI MAULIDI MLETE
DP
870.18
HAMISI FADHILI KISWAGA
NRA
470.1
MAUWA SHAURI KAMANA
JAHAZI ASILIA
190.04
TATU SAIDI HUSSEIN
UMD
80.02
SPOILT VOTES 927 1.93
TOTALS 48,105 100
 
Zitto ni mtu wa karibu sana na Ally Mley aliyegombea Kigoma mjini na Wakamchakachua.

Hivi Zitto alishinda kwa kura ngapi vile? Hebu leteni data hapa na ndipo tuanze kumjadili Zitto.

Una pointi nzuri na muhimu sana kwa Chadema ila umeharibu tu kumuingiza hapa Zitto.
Mkuu nadhani alishinda kwa kura 450 kama sikosei....alikuwa ukingoni kabisa
 
Niliwahi kuambiwa na mtu wangu kutoka Kg kask. kwamba Zitto alikabiriwa na upinzani na kura zake kuporomoka baada ya wanakigoma kukosa imani na misimamo yake ndani ya CDM na kuanza umbayuwayu ...

Nendeni Kg huko naamini hata wapiga kura wake watakuwa na la kusema kwa usahihi.
 
Usimuhukumu mtu kwa kitu usichokijua hata mungu hapendi.Kumhisi mtu na kuanza kutoa shutuma ni kosa kubwa sana.

Wadau wanachokisema ni Ukweli, Chakujiuliza ni kwamba Mrema aliungwa mkono na CCM, na yeye alimkampenia JK Leo tunaona hata kanuni za bunge zilitenguliwa ili kulipa fadhila kwa usaliti alioufanya.

Leo hii kuna wapinzani wameona hilo ni dili sasa hatuwezi kukaa na kusubiri huko.
 
FEEDBACK, nina wasiwasi na hizo Data za NEC ya Tanzania.

Baada ya matokeo kutangazwa na kabla hayajawekwa NEC, Zitto alikuwa na kura chache sana kama Excellent hapo juu alivyosema. Hata mie mwanzoni sikufuatilia sana hadi Mtanzania wa JF aliposema kuwa Zitto ameshinda kwa tofauti ndogo sana. Naona NEC kama kawaida wamechemsha tena hayo matokeo yao.
 
Mkuu nadhani alishinda kwa kura 450 kama sikosei....alikuwa ukingoni kabisa

Zitto alishinda kwa kura 5014...Pro-Chadema JF bana uwa wanachekesha sana kama hawampendi mtu wanasema kashinda kwa tabu, kama mtu wanaompenda hakishindwa wanasema kaibiwa kura.

Mchungaji Peter Msingwa Iringa Mjini alishnda kwa kura 1000.

Mesharck Opolukwa wa jimbo la Meatu alishinda kwa kura 1500.

Hawa watasema wameibiwa kura na CCM lakini Zitto kashindwa kihalali.
 
zito ana udhaifu mkubwa sana na hayupo tayari kurekebishwa'ccm walishagundua hilo wanamtumia kwa gharama yoyote ile kuivuruga chadema kwa bahati mbaya sana hajui kama anatumiwa kwa nia mbaya'anafikiri ccm wanampenda'nini faida ya kuwa msomi kama unashindwa kugundua vitu vidogo kama hivyo'je kesho tukimpa uwaziri mkuu si atakuwa anazini ofisini?kwangu mimi future yake imekaa vibaya sana kisiasa
 
FEEDBACK, nina wasiwasi na hizo Data za NEC ya Tanzania.

Baada ya matokeo kutangazwa na kabla hayajawekwa NEC, Zitto alikuwa na kura chache sana kama Excellent hapo juu alivyosema. Hata mie mwanzoni sikufuatilia sana hadi Mtanzania wa JF aliposema kuwa Zitto ameshinda kwa tofauti ndogo sana. Naona NEC kama kawaida wamechemsha tena hayo matokeo yao.
Sikonge, hizo data ni za NEC hata mimi sijui kama ni za kweli ama la.

Tatizo la Zitto ni kufikiri umaarufu huwa haushuki, aelewe kwamba kwenye siasa umaarufu unashikiliwa na wananchi, wananchi wanaweza kukupa na kukunyang'anya siku yeyote. Ukilinganisha kura alizozipata 2005 (28,198) na zile za 2010 (23,366) ni almost pungufu ya kura 5,000, tujiulize hawa wamekwenda wapi wakati wapigakura waliongezeka na umaarufu wa Chadema ulikuwa maradufu. Kwa trend hii naweza kusema kama next election 2015 CDM itasita kuonyesha ushirikiano na Zitto wa wazi kura zinaweza zisitoshe, kwa sababu umaarufu wa Zitto haushuki tu kitaifa inaonyesha hata jimboni kwake ameshuka.
 
nina sababu kubwa kwaa nini namwingiza zito, kwanza anawapa nguvu hawa wanaofanya harakati za ukanda ndani ya cdm, pili nimeshangazwa sana na kitendo cha yeye kuwa kiongozi mwandamizi ndani ya cdm kupigiwa debe na wazee wa kutetea magamba humu jamvini.

Nashidwa kuelewa kuna uhusiano gani kati ya zito na hawa wahuni wa ccm humu ambao wamekuwa wakitetea mafisadi/ufisadi humu tz.

ila hushangazwi na wale wasiotaka hata kusikia mwenyekiti au katibu akitajiwa maovu yake?
 
Zitto alishinda kwa kura 5014...Pro-Chadema JF bana uwa wanachekesha sana kama hawampendi mtu wanasema kashinda kwa tabu, kama mtu wanaompenda hakishindwa wanasema kaibiwa kura.

Mchungaji Peter Msingwa Iringa Mjini alishnda kwa kura 1000.

Mesharck Opolukwa wa jimbo la Meatu alishinda kwa kura 1500.

Hawa watasema wameibiwa kura na CCM lakini Zitto kashindwa kihalali.
nijibu swali moja..hivi kwanini nyie watu wa magamba huwa mko tayari kumtetea ZITTO kwa ghrama yeyote ile?
mbona sio LEMA aliyefukuzwa ubunge ? mbona sio mzee mpendazoe? mbona sio LISSU anayetaka kupigwa chini huko jimboni kwake? yaani hiyo kitu inaumizia akili sana!!! kwanini zitto na magamba????
 
zitto alishinda kwa kura 5014...pro-chadema jf bana uwa wanachekesha sana kama hawampendi mtu wanasema kashinda kwa tabu, kama mtu wanaompenda hakishindwa wanasema kaibiwa kura.

Mchungaji peter msingwa iringa mjini alishnda kwa kura 1000.

Mesharck opolukwa wa jimbo la meatu alishinda kwa kura 1500.

Hawa watasema wameibiwa kura na ccm lakini zitto kashindwa kihalali.

kwa mitazamo ya kibaguzi hiki chama ni balaa sana!
 
nijibu swali moja..hivi kwanini nyie watu wa magamba huwa mko tayari kumtetea ZITTO kwa ghrama yeyote ile?
mbona sio LEMA aliyefukuzwa ubunge ? mbona sio mzee mpendazoe? mbona sio LISSU anayetaka kupigwa chini huko jimboni kwake? yaani hiyo kitu inaumizia akili sana!!! kwanini zitto na magamba????
Mkuu hata mi sielewi,hawa magamba wanamtetea na kumsifia sana zitto,mbona hawasifii wengine...inaonekana kuna maslahi flani
 
nijibu swali moja..hivi kwanini nyie watu wa magamba huwa mko tayari kumtetea ZITTO kwa ghrama yeyote ile?
mbona sio LEMA aliyefukuzwa ubunge ? mbona sio mzee mpendazoe? mbona sio LISSU anayetaka kupigwa chini huko jimboni kwake? yaani hiyo kitu inaumizia akili sana!!! kwanini zitto na magamba????

Hata John Mnyika namkubali sana.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom