CHADEMA, huu ni wakati wa kufanya maamuzi magumu...

Status
Not open for further replies.

STEIN

JF-Expert Member
Aug 29, 2010
1,770
553
Ndugu wana CDM,

Sasa umefika wakati wa kufanya maamuzi magumi kuliko kipindi chochote, Kina sisimizi wanafanya mapambano ya chini kwa chini kutataka kuonekana wao ndiyo wana haki ya kuwa viongozi wa wananchi.

Nasikita kuona kuna vijana wa juzi tu 2005 leo wanataka nafasi za juu ile hali uadilifu wao si wa kuridhisha hata kidogo na kinachotokea hawa vijana wamekuwa wanashambulia ile hali Chama kimewafichia siri zao nyingi.

Hawa vijana wanafanya harakati za kutaka nchi hii iendelee kuwa mikononi mwa mafisadi sijui hadi lini I think hadi wananchi watumie nguvu ya Umma.

Rai yangu kwa Mwenyekiti na Katibu mkuu wa CDM Taifa kujaribu kuwahoji hawa vijana na ikiwezekana ni kuwa subject kwenye mazingira magumu ili hawa vijana ikiwezekana waondolewe kwenye chama maana ndiyo nimeiona wanaojihangaisha kuigawa Chama kwa Ukanda na Udini ambao hauna Msingi wowote.

Embi fikiria hata Ushindi wa Nasari wanasema ni kwa sababu ya Ukanda, Mbona hatukusikia wakati wa Charles Mwera wa Tarime?

Mbona CDM kina Nguvu sana Kanda ya Ziwa na Nyanda Za juu kusini, Mbona CDM kimeshika Nafasi ya pili Uzini, Igunga na Sehemu Karibu Zote isipokuwa Kigoma ambako Kimehujumiwa na Zikto Kabwe ambaye alikuwa na anawapigia Debe NCCR na JK katika Kampeni Zake?

Mimi naomab Uchunguzi huru ndani ya Chama ufanyike ni kwa sababu gani CDM kilishindwa kigoma na NCCR wakati Zito N/K anatoka ukanda ule?

Nawasilisha.

UPDATES:

December 20, 2012
Guys:

Kama CCM wakaamua leo kulipuana Mitandaoni kama Mnavyofanya nyie wana CDM, It will be completely Dead.

Siamini kama ni haki kwa nyie viongozi vijana na tegemeo kwa Chadema kuanza kulimbana na kulipuana mitandaoni tena mtandao maarufu kama Huu.

Sidhani kama hii ni busara hata kidogo. Tunaomba hayo mambo yenu ya ndani malizieni kwenye vikao. Kuna wengine tulishaona ukombozi ukija kupitia CDM. ila kwa haya yanayojitokeza sasa naomba nikiri kukosa Imani na CDM. na kwa mwendo huu niseme tu hiki Chama hakifai kupewa Dola.

Nguvu zote, Gharama zote zilizotumiaka kwenye M4C zimekua Bure? hivi mnajua kuna watu wamepoteza maisha kwaajili ya kuitetea Chadema? ni raia wangapi wamepigwa risasi kwenye mikutano ya CDM?

Leo hii kula kitu kimekua bure? hivi haya malumbano mnayaleta huku jamvini kwa faidi ya nani? Kwahiyo tumeshajua yote hayo, mnataka tuchukue hatua gani?

Kumbukeni sisi hatuna la kufanya zaidi ya kufanya maamuzi ya Binafsi kuhusu CDM. Hivi nikisema haya malumbano yameshusha umaarufu wa CDM nitakua nimekosea?
Vijana wa CHADEMA na Uongozi wa Taifa wa CHADEMA wanakatisha tamaa na wanasikitisha pamoja na kuudhi kulikopitiliza; na hapa nazungumzia wa kambi zote zinazokinzana katika mjadala unaoendelea. Wanakatisha tamaa kwa sababu wanarudisha nyuma juhudi zote za yote tuliyoyafanya kufikia hapa tulipofikia.

Maana sasa inaonekana wanashindanisha nani ana akili zaidi kichwani, nani mjanja zaidi na nani anaweza kugundua unafiki wa mwingine.

It is pathetically shameful and somebody need to do something vinginevyo wengine tutaingilia kati kama kwenye mjadala wa "Urais na Ujana vs. Uzee".

If you guys can't we will help you. It is absolutely pathetic.

MMM
Tik Tak Tik Tak
 
Hii hoja inamashiko.

Iringa, Mbeya na Kanda ya ziwa, Rukwa, Songea kuna madiwani wa chadema kwanini Arumeru iwe ukanda?

Kigoma inahitajika uchunguzi wa kina ufanyike
 
Tulishalishalizungumzia hapa jùu ya Intelensia ya Chadema inatakiwa ipanue wigo badala ya ya kuishia kwenye kulinda kura na ulinzi wa RED BRIGADE ifanye kazi ya kiuchunguzi kubaini hawwasaliti ambaoinaonekana wamejipanga, hawapaswi kudharauliwa kwani huenda madhara yake yakawa mabaya sana hapo bàadaye.
 
Hii hoja inamashiko.
Iringa, Mbeya na Kanda ya ziwa, Rukwa, Songea kuna madiwani wa chadema kwanini Arumeru iwe ukanda?
Kigoma inahitajika uchunguzi wa kina ufanyike

Uko sahihi kabisa, maana hata wanaopaisha ukanda ndani ya CDM wengine wanatoka Kigoma kwa hiyo tunatakiwa kufahamu ni kwa sababu gani?

Tuanatakiwa tujiridhishe kuna uhusiano gani kati ya waajiriwa wa Nape humu JF na Kigoma, Je wanatoka huko au wameoma wakipitia Kigoma wanaweza kupenya ndani ya CDM?


Vile vile tunatakiwa kujua ni kwa nini kipindi fulani hata Zita kwanini alitaka kugombea Geita/Shinyanga/Kawe dar etc na si kugombea jimbo la K/Kaskazini jimbo lake?

Lazima tuwe very clear katiaka hili.
 
Habari yako ni angalizo zuri ila umeficha taarifa hapo mwanzoni Kwa kusema kuna vijana wa juzi tu (2005) leo wanataka nafasi za juu. Kwa nguvu kazi inayohitajika CDM, hata Vijana wanachama wazalendo watakaojiunga leo (hasa wasomi) wanahitajika Kwa wingi Kwa ajili ya kuongoza chama na serikali. Mfano Madiwani,wenyeviti na makatibu katika ngazi mbalimbali, bado kunahitajika kufungua matawi sehemu nyingi. CDM inawapenzi wengi sana hapa nchini, na wengi wangependa kujiunga kuwa wanachama. Nihitimishe kwa kusisitiza: Vijana bado ni nguzo muhimu sana ya kuiongoza CDM/ serikali.
 
Zitto ni mtu wa karibu sana na Ally Mley aliyegombea Kigoma mjini na Wakamchakachua.

Hivi Zitto alishinda kwa kura ngapi vile? Hebu leteni data hapa na ndipo tuanze kumjadili Zitto.

Una pointi nzuri na muhimu sana kwa Chadema ila umeharibu tu kumuingiza hapa Zitto.
 
Hilo ndio jambo muhimu mi huwa nasema kuwa chadema inatakiwa ifanye ustadi mkubwa ktk ku-scan virus wote ndani ya chama pasipo kuja kuleta mgawanyiko kama ulotokea kwa CUF, pia njia moja ambayo CDM wanatakiwa waifanye ni kuhakikisha ktk chaguzi zote za chama hadi 2015 ktk kuteua flag-barriers wa chama kwenye ubunge wanatakiwa wachaggue viongozi ambao sio mamluki wala wenye element za undumikuwili ili kukijenga chama vizur ktk kuelekea uchaguzi mkuu.
 
Mawazo yako mkuu ni muhimu yakafanyiwa kazi mara moja ili tuweze kuzuia hizo mbinu chafu zinazoweza kutugarimu hapo baadae.

Unajua Kinachotokea kuna kikundi fulani cha vijana wenye njaa wanataka nchi hii iendelee kuwa mikononi mwa CCM hadi ardhi yote ichukuliwe na Wakenye, waganda maana wazungu washachukua sehemu wanazohitaji sasa wanataka, huu si muda wa mzaha.

maana naona sasa hadi wanafanya Personal attack kwa Mwenyekiti na Katibu Mkuu wa CDM.. Mimi nafikiri lazima hawa jamaa iju;likane moja ama tunawakosa kwenye chama au wanajirekebisha.

Wameanza hizi harakati tangu 2008 sasa 2010 tumewavumilia hatuwezi kuendelea kuwalea hadi 2015..

Ukitaka kujua rejea magazeti ya Mwanahalisi kipindi cha Uchaguzi na Baada tu ya uchaguzi...

Ndiyo utaelewa tunamaanisha nini.
 
Hii hoja inamashiko.
Iringa, Mbeya na Kanda ya ziwa, Rukwa, Songea kuna madiwani wa chadema kwanini Arumeru iwe ukanda?
Kigoma inahitajika uchunguzi wa kina ufanyike

jamani zitto kashapata alichokitaka so cdm msimwamini kabisa.
 
Mkuu STEIN, chokochoko ndani ya CHADEMA chama makini, wakati wote huanzisha na usalama wa ccm. Lakini wakati wote nimekuwa nafurahishwa na msimamo wa viongozi wetu Ku-focus kwenye vipaumbele vya chama kuliko chokochoko. Shibuda kama zinamtosha mkichwa atakuwa anajuta.
 
Zitto ni mtu wa karibu sana na Ally Mley aliyegombea Kigoma mjini na Wakamchakachua.

Hivi Zitto alishinda kwa kura ngapi vile? Hebu leteni data hapa na ndipo tuanze kumjadili Zitto.

Una pointi nzuri na muhimu sana kwa Chadema ila umeharibu tu kumuingiza hapa Zitto.

Nina sababu kubwa kwaa nini namwingiza Zito, kwanza anawapa nguvu hawa wanaofanya harakati za ukanda ndani ya CDM, Pili nimeshangazwa sana na kitendo cha yeye kuwa kiongozi mwandamizi ndani ya CDM kupigiwa debe na wazee wa kutetea Magamba humu jamvini.

Nashidwa kuelewa kuna uhusiano gani kati ya Zito na hawa wahuni wa CCM humu ambao wamekuwa wakitetea mafisadi/ufisadi humu TZ.
 
STEIN una hoja, lakini elewa kumchinja kobe kunahitaji timing. Hata hivyo baada ya mbinu zao ku-prove failure Arumeru Mashariki kuna baadhi yao nimewaona wameanza kujirudi. Tuipe muda intelligensia ya CDM ifanye kazi yake najua itakuja na solution wakati mwafaka ukifika, kwa sababu wanajulikana na hawajafikia stage ya kusababisha madhara makubwa kama unavyofikiri ingawa si wa kupuuza.
 
NAMPENDA SANA ZITTO KABWE...NAJUA WAZI SANA KUWA ANA UWEZO MKUBWA SANA WA KIUONGOZI..HILO SIPINGI!!!!
LAKINI UKWELI NI KWAMBA ZITTO KABWE HAYUKO PAMOJA NA CHADEMA!!!!!
ISHU YA Arumeru, alishiriki ila sio kikamilifu! najua CHAMA kilimpangia kazi nyingine Mwanza! Lakini! Tumezoea kuona matamko yako online, iwe FB,TWITTER, kwenye blog YAKE AU JF(mara chache, siku hizi haipendi JF), lakini zitto mara nyingi hakupenda kuizungumzia Arumeru( sababu ya kushabikia ukanda na udini.) ile ishu ya Polisi kuua watu Arusha haikuingia akilini mwa zitto..likaja suala la LEMA...Zitto akapiga kimya kikali mpaka kesho!!!!
Kifupi ZITTO ni kichwa sana ila mienendo yake ndani ya CHADEMA inaleta maswali mengi saaana..kuliko majibu!!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom