Idimulwa
JF-Expert Member
- May 27, 2011
- 4,503
- 1,722
Timu ya kampeni ya chadema iliyo piga kambi katani Lwenzera chini ya mwenyekiti wa jimbo kamanda Mabula Kachoji kwa takribani wiki 2 sasa,imesababisha ccm kupotezana na kukoswa mwelekeo na kumwacha njiapandamgombea wao bwana Misango asijue la kufanya.
Wakati chadema wakiendelea na mikutano yao ya kampeni katani humo wakimnadi mgombea wao anayekubalika sana kamanda Ibuga,huku wakiendelea pia kutoa elemu ya uraia,kupokea wanachama wapya na wale wanaotokea ccm,ccm wameshindwa hata kuzindua kampeni zao na mstakabali mzima juu ya uchaguzi haujulikani.
Uwezo mkubwa wa kujenga hoja unaoonyeshwa na timu nzima ya kampeni katika mikutano yao umekuwa gumzo na kivutio kwa wakazi wa kata hii, na wengi wamekwenda mbali zaidi kwa kuhoji ni wapi chadema imekuwa ikipeleka watu wake kujifunza mambo ya siasa,hali hii imechagizwa pia na uwezo mkubwa wa kujibu maswali ya papo kwa papo ambao umekuwa ukionyeshwa na mgombea wa chadema.
'.........IBUGA(mgombea wa cdm) tunamfahamu sababu kazaliwa nakukulia hapa na hakuwa muongeaji, kaingia tu cdm sasa anaongea mbele ya halaiki kubwa ya watu, kwa hisia, tena kwa kujiamini....huko nyuma kabla ya mambo haya ya uchaguzi alikuja kijana anaitwa ALPHONSE MAWAZO akafanya mikutano mingi tu.....na hivi majuzi tulishuhudia sura ngeni kabisa kwenye uzinduzi wa kampeni zao lakini uwezo wa watu hawa katika kujenga hoja,kushawishi na kujieleza uko juu........HIVI HAWA CHADEMA CHUO CHAO CHA MAFUNZO YA SIASA KIKO WAPI NA WALIMU WANAWATOA WAPI.....?' Ni mazungumzo kati ya wazee wawili(mmoja akiwa ni mwalimu wa s/msingi) niliyo yanasa nilipokuwa jirani nao wakati tunafuatilia mkutano wa kampeni kule Membe(eneo maarufu sana kwa uvuvi wa samaki aina ya kamongo.
Nawasilisha.