CHADEMA Arusha kuweni makini na haya

hiyo ni uhakika mkuu nanyaro,hapa kata ya themi watu wa ccm kama kina lobora wanaweka vikao usiku kupanga hayo mambo.

Usitishike na vikao, uchaguzi ukiitishwa ndiyo utajua Arusha inaongozwa na akina nani? Yaani utafurahi na kuchekelea wewe wenyewe baada ya kujiuliza mbinu za vile vikao zimeishia wapi baada ya hali kuwa mbaya.
 
Sumu na wenzako nawajulisha kuwa hapa Arusha CHADEMA ni zaidi ya chama. Tunaifananisha na dini mpya ambayo waumini wake wana msimamo. Kama huamini njoo muda wa uchaguzi mdogo wa madiwani uta-prove.

BTW habari za hapo LUMUMBA vipi? Ushapata posho?

Hapa Lumumba mambo ni shwari kabisa na unakaribishwa sana CCM mkuu Arushaone. CCM ndiyo chama pekee ambacho kipo Tanzania nzima bila ya kubagua maeneo, kina mashina kila kona ya nchi, CCM ndiyo chama pekee ambacho hadi mtu wa chini kabisa anasikilizwa, CCM ndiyo chama pekee kisichokuwa na mmiliki wake, CCM ndiyo chama kilichofanikisha umoja wa nchi tulionao leo hii. Maendeleo unayoyaona leo hii ni jitihada za CCM.

Karibu sana.
 
Last edited by a moderator:
Hapa Lumumba mambo ni shwari kabisa na unakaribishwa sana CCM mkuu Arushaone. CCM ndiyo chama pekee ambacho kipo Tanzania nzima bila ya kubagua maeneo, kina mashina kila kona ya nchi, CCM ndiyo chama pekee ambacho hadi mtu wa chini kabisa anasikilizwa, CCM ndiyo chama pekee kisichokuwa na mmiliki wake, CCM ndiyo chama kilichofanikisha umoja wa nchi tulionao leo hii. Maendeleo unayoyaona leo hii ni jitihada za CCM.

Karibu sana.

naona huwezi kutofautisha kati ya TANU na CCM!!!!!!!!!So sad
 
CCM Arusha wamebakiwa na yale majengo ya chama yanayokodishwa kwa wafanyabiashara wanajilia kodi tu lakini siasa ilisha kufa na mwaka 2015 atabaki chatanda kama mama mwenye nyumba wa majengo
 
Mh. Mwigulu amewashika pabaya kwa kweli. Mkisinzia ni Mwigulu, mkilala ni mwigulu, mkiamka ni Mwigulu, mkikaa ni Mwigulu, mkisimama ni Mwigulu, mkitembea ni Mwigulu, mkichuchumaa ni Mwigulu, mkila ni Mwigulu, mkinywa ni Mwigulu.

Na huu ni mwanzo tu! Bado mengi yanakuja. Kuliko kuendelea kuwalaghai wananchi ni bora muingie msituni mkashike bunduki ili tujue kabisa kwamba chama chenu ni kikundi cha waasi.

Dr. Slaa amewashika pabaya kwa kweli. Mkisinzia ni Dr. Slaa, mkilala ni Dr. Slaa, mkiamka ni Dr. Slaa, mkikaa ni Dr. Slaa, mkisimama ni Dr. Slaa, mkitebea ni Dr. Slaa, mkichuchumaa ni Dr. Slaa, mkila ni Dr. Slaa, mkinywa ni Dr. Slaa.

Na huu ni mwanzo tu! Bado mengi yanakuja. Kuliko kuendelea kuwalaghai wananchi ni bora muondolewe madarakani ili nchi isiendelee kufisidiwa na kuwa na umasikini endelevu uliotufikisha pabaya na kuleta hatari ya vita. Mmeshindwa kila kitu na hatimaye mmeleta mambo ya udini, ukabila nk. katika kuweweseka na kutaka kung'ang'ania madaraka.


Hata hivyo mwisho wenu umefika. Yatatimia.
 
Kwa kuishabikia kwako CHADEMA, umeshindwa kutofautisha chama cha Siasa na kikundi cha waasi.
kikundi cha uasi chenye usajili wa kudumu serikalini?, kama ndivyo hivyo basi tatizo sio la kikundi tatizo ni la wenye serikali,na kama ni hivyo kikundi hakina uasi wowote ila mnaona kinataka kuwaharibia ulaji ndiyo maana mnakitungia hadithi
 
Ni kweli kabisa uchaguzi umenukia, hapa kwetu arusha kata ya Themi ccm wameanza kuomba kura kijanja.
Nina kuhakikishia chadema tunachukua viti vyote 5.
Mchakato wa kupata wajumbe wa mabaraza ya kata umedhihirisha kuwa ccm wana agenda ya kuendelea kuhujumu demokrasia.
Tutatoa adhabu kali kwa ccm kupitia kura za madiwani hawa.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Kwangu ni kata ya Elerai Chadema ni jimbo letu asikuambie mtu hata yule mamluki Bayo anajui hii maneno! time will tell.
 
Pamoja na aliyekua diwani wa kata ya Elerai Bayo kua ni mwenzetu katika kata hii tunamshauri atupigie debe japokua nasikia kahama mtaa kahamia Sanawari small house aje atuunge mkono Chadema tunashinda.
 
Mkuu gagonza probabaility ya hayo kutokea ni kubwa mno; ni vyema viongozi wa chama chetu, Makamanda, Wapiganaji, Wapambanaji, na Wapenda mabadiliko kote duniani kila mmoja wetu akatimiza wajibu wake kwa mda muafaka ili kufanikisha safari hii ya ukombozi tunayokaribia kuikamilisha.

Rai yangu kwa wapenda mabadiliko wote nchini; Tusiruhusu hata kidogo huu utamaduni wa mamluki na usaliti dakika za mwisho. Endapo tumemchagua mgombea miongoni mwetu ili apeperushe bendera ya CHADEMA na dakika za mwisho akatusaliti kinyume cha matarajio yetu "Huyo mtu hatufai, na hatakiwi kuonekana katika jamii" ; Hivyo basi ni lazima apotezwe kwa gharama zozote zile ili liwe fundisho kwa wenye mawazo potofu kama hayo.
 
Ndallo ile small h ya Bayo ni CDM so jamaa hana jinsi lazima ajipendekeze kwenye kampeni ili nyumbani mambo yasiharibike
 
Maendeleo gani yameletwa na ccm. Wee ni ushamba tu unakusumbua. Tembea nchi za watu uone kinachoitwa maendeleo

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom